kunradi wadau. kuna mdau kauliza watu 'vegetarian' kwa kiswahili wanaitwaje?
Home
Unlabelled
msaada kwenye tuta
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Waswahili hatuna watu wasiokula nyama labda awe kakatazwa na Daktari kwa sababu za kiafya. Hivyo basi sidhani kama kuna kiswahili fasaha cha kufupisha hilo neno la wasiokula nyama. Maana vegetarian kwa kweli ni majani tupu hasa ukimkuta vegan hata maziwa ya ng'ombe hawanywi sasa utamuitaje huyu wakati mswahili mila yake 'tonge nyama'. Au tuwaite mla majani? Mla mboga mboga? Asiyekula nyama ndilo linafaa zaidi.
ReplyDeletena wee michuzi acha kutuchanganya hapa! mara ulete habari za ufisadi kabla hatujamaliza kutoa madukuduku yetu, mara unatuletea cjui tuzo za reds mara sasa hivi tena unaleta sijui mavejiteriani, aaaraaaaa... jijibu mwenyewe sasa na jibu nalifaham na sikupi sasa, aaraaaaaaa
ReplyDeleteanaitwa Ras
ReplyDelete= KISAMVU
ReplyDeleteNatumaini wanaitwa wala-mimea!
ReplyDeleteWasiokula nyama.
ReplyDeleteEasy...! "wambogamboga"
ReplyDeleteBANIANI!!!
ReplyDeletewala mimea!!!
ReplyDeletewala mimea!!!
ReplyDeleteNi wale marastafari yani majah pipo ingawa jina zuri ni mbogajani au wamajani,ni hayo tu nasubiri kuteuliwa ktk post yoyote kwny cabinet ijayo.
ReplyDeletewa mbogazamajani.
ReplyDeleteWanaitwa wambogamboga au ukitaka wambogaterian
ReplyDeletewala majani/ mboga
ReplyDeleteNadhani vegetarian ni mtu asiyekula nyama
ReplyDeleteNadhani vegeterian wanaitwa WALAMBOGA
ReplyDeletemboga-mtu
ReplyDeleteVEGETARIAN ni WALAMBOGA
ReplyDeleteBob Tv
Vegeterian kwa kiswazi ni wasiokula nyama na vitokanavyo na nyama
ReplyDeletekaka michuu haya mambo ni ya kizungu ,0hayapo kwenye kamusi yetu kwa sababu hakuna mswahili asiyekula nyama na kama wapo wana matatizo yao binafsi......so mimi naomba ku-suggest majina mawili matatu....maybe tuwaite
ReplyDelete1. wala majani au
2. mbuzi !! ( na majina mengine ya wanyama kama huyu mpenda majani)
ama wadau wenzangu mnaonaje ?
Anyway Jamani kaka Michuzi Dodoma kunani?? hebu tupe news mana sie wa mbali huku hakukaliki kwa kihoro !!!!!!! TRUE DEMOCRACY WILL PREVAIL IN OUR GREAT NATION .........I love Tanzania with all its flaws its a great County and we should always be very proud of being wa-tz!! Mungu ibariki Tanzania na Rais wetu na watu wake , ONE LOVE always ......Ameen.
Simpo?!! MLA-MAJANI. Teh! Teh! Teh!
ReplyDeleteMAJANIAN!!
ReplyDeletenasubiri zawadi yangu ya £500 kwa kuwapa the best right answer ever!!
Au kwa kiswahili fasaha mla majani!!tehe tihiiiii
wanaitwa " wala majani"....Asante sana bwana michuzi kwa Nyuzzzz moto moto....ubarikiwe
ReplyDeleteWatu vegeterian wanitwa walamboga mkuu! Nawasilisha.
ReplyDeleteMBUZI
ReplyDeletewanaitwa MAJANI... au ukipenda wala Kisamvu aka. TIGO
ReplyDeleteWala Mirungi.
ReplyDeleteWANAITWA MBUZI-MTU SIMPO.
ReplyDeleteKweli wengi wetu tunaparamia mambo bila hata kufikiri kwa kina.VEGETARIAN kwa kuwa inatokana na Vegetables basi watu wana refers katika mbogamboga peke yake!Hapa maana yake ni NO ANIMAL AND ITS PRODUCTS-kwahiyo vilivyobakia vyoote Rukhsa kuliwa.Kwa maana hiyo- tafsiri yake siyo MLA MBOGA au MLA MIMIEA kwani huyu anaruhusiwa kula hata viazi,mihogo,nazi, kunde, matunda,na mazao mengine yote yatokanayo na mimiea.MIMI ningeomba kama hakuna jina la kiswahili mpaka karne hii basi napendekeza huyu Vegetarian aitwe:MlaMaMi ikiwa ni kifupi cha MLA MAZAO YA MIMIEA
ReplyDeleteWEE Myunani, Acha Komplikesheni!!!
ReplyDeleteWambogamboga is simple and good...teh teh teh!
Michu mimi nina mapendekezo mawili ya vegeterian in kiswahili
ReplyDelete1.ASIKUNYA - asiye kula nyama
au
2.ASIKUNYANASA - asiye kula nyama na samaki
Kuna maneno mengi huwezi ukayapatia maneno ya kizungu moja kwa moja.
ReplyDeleteSio kwa kiswahili tu hata maneno ya mengi ya kifaransa, kichina na hata kispanish hawana maana ya maneno yao kwa kiingereza hivyo hat atukiona ya kiswahili sio ajabu.
Hivyo kama ulivyosema ni mtu asiyekula kitu chenye animal products. No one word for that
Neno sahihi ni MVIGA!
ReplyDeleteMla Mboga
Mhindi
Mpenda maharage
Kisamvu cha kopo
ReplyDeleteMla nyasi!!!!!!!!!!
ReplyDeleteNyie nyote hamjui anaitwa MLANYASI
ReplyDeleteWanaitwa Mabwabwa teh teh teh teh
ReplyDeleteThe comments are hilarious. Who said Wa-bongo have no sense of humour?
ReplyDeleteHili swali linanikumbusha swali lingine .
ReplyDeletemwalimu aliuliza `Vegetarian is someone who eats vegetable.,What is the name of a person who eats humans?Wanafunzi wakajibu `Humanitarian;
Mdau VA
sungura pori
ReplyDeleteShee!!! kwanini mutu hakuli nyama? lasima takuwa naumwa, mwambie aje kule longido tapeleka yeye mahali iko dakitari.
ReplyDeleteHaya taisere.
Mie naungana na Myunani: aitwe MlaMaMi = mlamami = mla mazao ya mimea.
ReplyDeleteBogaboga
ReplyDelete....kweli wabongo mmedata yaani hizo comment nimecheka sina mbavu!i love this blog.
ReplyDeletemamaalia
ReplyDeleteWatu wanaokula mbo ga za majani!
ReplyDeletewanaitwa CCM si unajua tena mambo ya kijanijani!!
ReplyDeleteBw.Michu,nashukuru kwa kuwakilisha swali langu hilo kwa Wadau,na bila shaka Wabongo kweli ni Wabunifu,Majibu yanafurahisha sana,Kiswahili siyo Lugha Maskini Kama tunavyo dhani!!
ReplyDeleteHahahahah ! Yaani wabongo tumedata sio siri !crazy people! yaani hizi comment zimeanza siku ambayo mlikuwa hamna selikali so to speak!! wenzenu wakenya walipigana visu nyie mnadiscuss maana ya wala-majani- walamami or whatever !! Anyway kaka Michuu mie suggestion yangu ni kwani i think kwki inabidi kamusi yetu itanuliwe kujumlisha tafsiri za kiswahili kwa majina kama haya.....mimi naona wamuombe Rais. mstaafu Mze Ruksa achangie mana alikuwa analonga Kiswahili cha hali ya juu sana........Kwa kwa wale mavegetable wa kibongo naombeni mukamuone dakitari!
ReplyDeletekwa wale waliokuwa wakisoma Shule ya wavulana ya Songea maarufu kama Box 2 kati ya 1991 mpaka 1994 hivi wanafahamu vema jina hilo. tulikuwa na bwana mmoja ambaye leo hii ni mtu wa maana sana katika miradi ya serikali, wote tulimuita MC MBOGAMBOGA mwenyewe alilipokea vizuri na alienda nalo hadi UDSM.
ReplyDeleteASANTENI SANA WOTE MNAOTUMIA MUDA WENU KUTOA MAONI,TUNAJIFUNZA NA MARA NYINGI MNAFURAHISHA SANA SANA, I LOVE MA COUNTRY TZ.THANKS YO.
ReplyDeleteMimi ni mmoja wao, sili nyama nina miaka 11 sasa. Ni baada ya kusoma kugungundua madhara yapatikanayo kwa kula nyama. Napata tabu sometimes, ila watu wananiita mbogamboga. Nilipokuwa nasoma vitabu vya kitaalamu niligundua kwamba tunaitwa LACTO OVO!
ReplyDeleteWaTOSSao SALADi.
ReplyDelete