kunradi wadau. kuna mdau kauliza watu 'vegetarian' kwa kiswahili wanaitwaje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 53 mpaka sasa

  1. Waswahili hatuna watu wasiokula nyama labda awe kakatazwa na Daktari kwa sababu za kiafya. Hivyo basi sidhani kama kuna kiswahili fasaha cha kufupisha hilo neno la wasiokula nyama. Maana vegetarian kwa kweli ni majani tupu hasa ukimkuta vegan hata maziwa ya ng'ombe hawanywi sasa utamuitaje huyu wakati mswahili mila yake 'tonge nyama'. Au tuwaite mla majani? Mla mboga mboga? Asiyekula nyama ndilo linafaa zaidi.

    ReplyDelete
  2. na wee michuzi acha kutuchanganya hapa! mara ulete habari za ufisadi kabla hatujamaliza kutoa madukuduku yetu, mara unatuletea cjui tuzo za reds mara sasa hivi tena unaleta sijui mavejiteriani, aaaraaaaa... jijibu mwenyewe sasa na jibu nalifaham na sikupi sasa, aaraaaaaaa

    ReplyDelete
  3. anaitwa Ras

    ReplyDelete
  4. Natumaini wanaitwa wala-mimea!

    ReplyDelete
  5. Wasiokula nyama.

    ReplyDelete
  6. Easy...! "wambogamboga"

    ReplyDelete
  7. BANIANI!!!

    ReplyDelete
  8. wala mimea!!!

    ReplyDelete
  9. wala mimea!!!

    ReplyDelete
  10. Ni wale marastafari yani majah pipo ingawa jina zuri ni mbogajani au wamajani,ni hayo tu nasubiri kuteuliwa ktk post yoyote kwny cabinet ijayo.

    ReplyDelete
  11. wa mbogazamajani.

    ReplyDelete
  12. Wanaitwa wambogamboga au ukitaka wambogaterian

    ReplyDelete
  13. wala majani/ mboga

    ReplyDelete
  14. Nadhani vegetarian ni mtu asiyekula nyama

    ReplyDelete
  15. Nadhani vegeterian wanaitwa WALAMBOGA

    ReplyDelete
  16. VEGETARIAN ni WALAMBOGA


    Bob Tv

    ReplyDelete
  17. Vegeterian kwa kiswazi ni wasiokula nyama na vitokanavyo na nyama

    ReplyDelete
  18. kaka michuu haya mambo ni ya kizungu ,0hayapo kwenye kamusi yetu kwa sababu hakuna mswahili asiyekula nyama na kama wapo wana matatizo yao binafsi......so mimi naomba ku-suggest majina mawili matatu....maybe tuwaite
    1. wala majani au
    2. mbuzi !! ( na majina mengine ya wanyama kama huyu mpenda majani)
    ama wadau wenzangu mnaonaje ?

    Anyway Jamani kaka Michuzi Dodoma kunani?? hebu tupe news mana sie wa mbali huku hakukaliki kwa kihoro !!!!!!! TRUE DEMOCRACY WILL PREVAIL IN OUR GREAT NATION .........I love Tanzania with all its flaws its a great County and we should always be very proud of being wa-tz!! Mungu ibariki Tanzania na Rais wetu na watu wake , ONE LOVE always ......Ameen.

    ReplyDelete
  19. Simpo?!! MLA-MAJANI. Teh! Teh! Teh!

    ReplyDelete
  20. MAJANIAN!!

    nasubiri zawadi yangu ya £500 kwa kuwapa the best right answer ever!!

    Au kwa kiswahili fasaha mla majani!!tehe tihiiiii

    ReplyDelete
  21. wanaitwa " wala majani"....Asante sana bwana michuzi kwa Nyuzzzz moto moto....ubarikiwe

    ReplyDelete
  22. Watu vegeterian wanitwa walamboga mkuu! Nawasilisha.

    ReplyDelete
  23. wanaitwa MAJANI... au ukipenda wala Kisamvu aka. TIGO

    ReplyDelete
  24. Wala Mirungi.

    ReplyDelete
  25. WANAITWA MBUZI-MTU SIMPO.

    ReplyDelete
  26. Kweli wengi wetu tunaparamia mambo bila hata kufikiri kwa kina.VEGETARIAN kwa kuwa inatokana na Vegetables basi watu wana refers katika mbogamboga peke yake!Hapa maana yake ni NO ANIMAL AND ITS PRODUCTS-kwahiyo vilivyobakia vyoote Rukhsa kuliwa.Kwa maana hiyo- tafsiri yake siyo MLA MBOGA au MLA MIMIEA kwani huyu anaruhusiwa kula hata viazi,mihogo,nazi, kunde, matunda,na mazao mengine yote yatokanayo na mimiea.MIMI ningeomba kama hakuna jina la kiswahili mpaka karne hii basi napendekeza huyu Vegetarian aitwe:MlaMaMi ikiwa ni kifupi cha MLA MAZAO YA MIMIEA

    ReplyDelete
  27. WEE Myunani, Acha Komplikesheni!!!
    Wambogamboga is simple and good...teh teh teh!

    ReplyDelete
  28. Michu mimi nina mapendekezo mawili ya vegeterian in kiswahili

    1.ASIKUNYA - asiye kula nyama


    au

    2.ASIKUNYANASA - asiye kula nyama na samaki

    ReplyDelete
  29. Kuna maneno mengi huwezi ukayapatia maneno ya kizungu moja kwa moja.
    Sio kwa kiswahili tu hata maneno ya mengi ya kifaransa, kichina na hata kispanish hawana maana ya maneno yao kwa kiingereza hivyo hat atukiona ya kiswahili sio ajabu.

    Hivyo kama ulivyosema ni mtu asiyekula kitu chenye animal products. No one word for that

    ReplyDelete
  30. Neno sahihi ni MVIGA!

    Mla Mboga

    Mhindi

    Mpenda maharage

    ReplyDelete
  31. Kisamvu cha kopo

    ReplyDelete
  32. Mla nyasi!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  33. Nyie nyote hamjui anaitwa MLANYASI

    ReplyDelete
  34. Wanaitwa Mabwabwa teh teh teh teh

    ReplyDelete
  35. The comments are hilarious. Who said Wa-bongo have no sense of humour?

    ReplyDelete
  36. Hili swali linanikumbusha swali lingine .
    mwalimu aliuliza `Vegetarian is someone who eats vegetable.,What is the name of a person who eats humans?Wanafunzi wakajibu `Humanitarian;
    Mdau VA

    ReplyDelete
  37. sungura pori

    ReplyDelete
  38. Shee!!! kwanini mutu hakuli nyama? lasima takuwa naumwa, mwambie aje kule longido tapeleka yeye mahali iko dakitari.

    Haya taisere.

    ReplyDelete
  39. Mie naungana na Myunani: aitwe MlaMaMi = mlamami = mla mazao ya mimea.

    ReplyDelete
  40. ....kweli wabongo mmedata yaani hizo comment nimecheka sina mbavu!i love this blog.

    ReplyDelete
  41. Watu wanaokula mbo ga za majani!

    ReplyDelete
  42. wanaitwa CCM si unajua tena mambo ya kijanijani!!

    ReplyDelete
  43. Bw.Michu,nashukuru kwa kuwakilisha swali langu hilo kwa Wadau,na bila shaka Wabongo kweli ni Wabunifu,Majibu yanafurahisha sana,Kiswahili siyo Lugha Maskini Kama tunavyo dhani!!

    ReplyDelete
  44. Hahahahah ! Yaani wabongo tumedata sio siri !crazy people! yaani hizi comment zimeanza siku ambayo mlikuwa hamna selikali so to speak!! wenzenu wakenya walipigana visu nyie mnadiscuss maana ya wala-majani- walamami or whatever !! Anyway kaka Michuu mie suggestion yangu ni kwani i think kwki inabidi kamusi yetu itanuliwe kujumlisha tafsiri za kiswahili kwa majina kama haya.....mimi naona wamuombe Rais. mstaafu Mze Ruksa achangie mana alikuwa analonga Kiswahili cha hali ya juu sana........Kwa kwa wale mavegetable wa kibongo naombeni mukamuone dakitari!

    ReplyDelete
  45. kwa wale waliokuwa wakisoma Shule ya wavulana ya Songea maarufu kama Box 2 kati ya 1991 mpaka 1994 hivi wanafahamu vema jina hilo. tulikuwa na bwana mmoja ambaye leo hii ni mtu wa maana sana katika miradi ya serikali, wote tulimuita MC MBOGAMBOGA mwenyewe alilipokea vizuri na alienda nalo hadi UDSM.

    ReplyDelete
  46. ASANTENI SANA WOTE MNAOTUMIA MUDA WENU KUTOA MAONI,TUNAJIFUNZA NA MARA NYINGI MNAFURAHISHA SANA SANA, I LOVE MA COUNTRY TZ.THANKS YO.

    ReplyDelete
  47. Mimi ni mmoja wao, sili nyama nina miaka 11 sasa. Ni baada ya kusoma kugungundua madhara yapatikanayo kwa kula nyama. Napata tabu sometimes, ila watu wananiita mbogamboga. Nilipokuwa nasoma vitabu vya kitaalamu niligundua kwamba tunaitwa LACTO OVO!

    ReplyDelete
  48. WaTOSSao SALADi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...