Michuzi,
Naomba wadau wanisaidie, ninahitaji kusafirisha vitu(vitabu, cds, na research papers n.k) kutoka USA kwenda bongo Sasa nimekwama njia ya kutumia.
Nikitumia posta kwa maximum size ya box linalokubaliwa na posta USA kama package naona nitatumia mabox mengi sana. Pia nikisema niweke kwenye box kubwa na nitume kwa meli naona nitalazimika kupitia process gumu ya kuclear mzigo huo bandarini wakati hivi ni vitu nilivyokuwa natumia katika masomo yangu huku (USA) na sasa nimemaliza masomo nataka nirudi nyumbani.
Pia siwezi kusafiri navyo maana pound zinazoruhusiwa kwenye ndege ni kidogo.Wahenga walisema kwenye wengi hariharibiki neno naamini wadau watanipa mawazo ambayo yatakuwa ya msaada kwangu.
Asante
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. kwanz ahongera kwa kumaliza, kama umeishi miaka miwili nje na unarejea unaruhusiwa kuingia na vitu ulivyokuwa ukitumia na hawatakutoza ushuru, computer, gari ni ruksa hivyo usikonde kwa hilo.

    ReplyDelete
  2. kwani huko USA hakuna kampuni zinazo safirisha mizigo by container(cargo). Nadhani hizo kampuni ziko nchi zote. Jaribu kutafuta information zaidi huko huko usa. Nchi kama ukelewe makampuni ni mengi tu sasa sijui huko USA

    ReplyDelete
  3. Kwani ni mabox mangapi ya vitabu? Hata kama ni matano ukitumia media mail havitakucost hela sana. Nenda posta waambie unataka kutuma kwa media mail otherwise tumia air cargo. Nayo haina usumbufu.


    That is the only solution

    ReplyDelete
  4. uza kwenye garage sell

    ReplyDelete
  5. kama unaona gharama kusafirisha kwenye flight,tumia UNGO NI RAHISI NA FASTER.MBONA USAFIRI HUO UPO WA KUMWAGA

    ReplyDelete
  6. Tumia ndege za mizigo.. its cheap and fast. kama hujui ndege gani.. tumia serach engines mazee..google itamaliza mambo.
    I hope hii itakusaidia..
    http://www.shipping-worldwide.com/

    All the best, na maisha mema Nyumbani.

    ReplyDelete
  7. Tuambia upo State gani hapa USA na tupe namba yako ya simu ili tukusaidie au e-mail yako. Container la futi 20 toka Eastern part of USA ni $ 3200 ambamo waweza kuweka gari moja na vitu vingine vingi vingi tu ukitokea NY, NJ Baltimore na bandari zingine zilizoko Mashariki. Linatumia miezi miwili kufika Dar. Haya weka simu ili tukupigie.

    ReplyDelete
  8. Hongera kw amaamuzi yako ya kurejea nyumbani. Kama una vitu vingi tafadhali tumia njia rahisi kabis aya kufikisha m zigo wako. Tuna bahati ya Mungu kwamba tupo katika eneo la bahari.Chagua shipper mzuri na hakika vifaa vyako vitafika na sheria ya nchi hii imewekeza neema kwa watu sehemu kubwa ya vifaa vyako vitaingia bure kwa kuwa tayari umekaa miaka miwili nje na vitu vingine ni kawaida tu ya custom usiwe na hofu bado nakutakia kila la heri .Nilikuwa Uingereza na nilisafirisha mizigo yangu kwa kontena, sikuw ana fedha na hata mkweche wanguj niliusafirisha kwa roll off roll on na kila kitu nilikipata ni suala tuj la msafirishaji.karibu Home

    ReplyDelete
  9. Tumia Courier wa ndege. Kuna ndege za mizigo zinazosafirisha mizigo na kwa bei ya chini kulinganisha na utakaposafiri na box lako.Either mzigo utafika mapema au kuchelewa kidogo kuliko wewe. La muhimu ni wewe mwenyewe kuushughulikia utakapofika hapa bongo.Kama ni vitabu na vitu vyako ulivyokuwa unavitumia wakati wa masomo hautachajiwa hata shilingi kwa upande wa kodi.Utachajiwa processing fees tu za airport.Hakikisha unashughulikia wewe mwenyewe airport kwani kuna jamaa wengi hapo airport from clearing agents wanaweza wakakucharge fedha nyingi kwa shughuli ambayo unaweza kuifanya tu kwa muda mfupi.Mimi nilisafirisha kama kilo sitini za vitabu na vitu vyangu vingine vidogo vidogo nilivyokuwa natumia Sweden kwa kutumia SKY Transport. Sijui kama huyu wakala yupo marekani lakini nafikiri hatakosekana.Sikuchajiwa kodi kabisa ila TRA walikagua na kuona ni vitu nilivyokuwa navitumia shuleni.Nafikiri maelezo hayo yatakuwa yamekupa mwanga kidogo.Big up kwa kukumbuka nyumbani!!Kuna kazi nzuri tu!!Njoo tujenge taifa.

    ReplyDelete
  10. Wewe mbeba box, una nini zaidi ya nguo zako na viatu.Haiwezekani mtu ambaye amekaa USA asijue namna ya kusafirisha mzigo.Google ipo, yahoo search. Na kwanini usiulize hata kwa watu DHL, au bandari. WEWE unataka tu kujifagilia huna lolote mbeba box wewe.Umeota kibiongo kwa sababu ya kubeba box

    ReplyDelete
  11. Sasa haya ya kashfa yamekujaje wewe annon wa 10.43 AM? Au umeamka nazo asubuhi asubuhi? Mtu ameuliza asaidiwe mawazo na watu wanamsaidia na ndio kazi ya kijiwe hiki sio kukashifiana na kutukanana bila sababu za msingi. Ukiona ya humu uyawezi hamia JF huko ndiko utakuna na mambo hayo!

    Hata mie nimenufaika na mawazo yaliyotolewa humu na wengi tu wamenufaika nayo ingawa wengine hawakuuliza. Kutumia google kusearch haitakwambia credibility ya kampuni lakini kwa waTZ wenzio utapata uzoefu wao kama walivyoeleza hapo juu. Shukrani wote mliotoa ushauri umenisaidia hata na mie ambaye sikujua nianzie wapi.

    ReplyDelete
  12. Jamani msimkatishe tamaa kijana wa watu. alichoomba ni kutafuta unafuu wa kusafrisha vitabu hivyo ambavyo vitawasidia na wengine huko nyumbani. Dollar yake haiwezi kugharamia usafiri wa raslimali hizo zote ukizingatia alikuwa masomoni. usihofu sana kijana kama umekaa zaidi ya mwaka kuna tax exemption itakusaidia, pia unaweza kupata marafiki walio na kilo pungufu za mizigo ambao wamekuja huko kwa siku chache tu labda kutembea wanaweza kukupa tafu wakapunguza baadhi ya kilo zako. achana na hao wasiosoma wanakaa nje kazi kubeba mabox tu bila kufikiria elimu na kukatisha tamaa wenzao.

    ReplyDelete
  13. Emirates na Northwest through KLM wana ndege za mizigo ambazo ni cheaper. Nimeshawahi kusafirisha mabox kwa bei ambayo ni reasonable kwa kutumia Northwest. Nenda Northwest cargo kwenye internet site yao. Tatizo ni kuwa ndege zao zinashukia Kilimanjaro International Airport hivyo itakubidi ukaikomboe mizigo yako huko (KLM). Hii hapa website yao. http://www.cargo.nwa.com/ I hope this will help. Jaribu pia Emirates.

    ReplyDelete
  14. Watu wengine bwana sijui wana matatizo gani kazi lakini sishangai sana najua ni jinga tu siku moja ataacha. Pole kaka lakini kama upo USA najua wanafunzi wengi wanaomaliza shule wanataka kurudi nyumbani wanachangia container na kuweka vitu vya wanapotaka kurudi nyumbani ebu jaribu maana hii ingekusaidia wewe hata kama huna gari yako na vitu vingine ungeweza kusafirisha kwa bei rahisi kidogo maana mie ndio njia niliyotumia wakati nilipomaliza masomo na kufanikia kurudi na vitu vyangu vyote.

    All the best.

    ReplyDelete
  15. funga kwenye mabox usiseal lakini then peleka moja kwa moja kwenye office za emirates wao wako cheap zaidi kuliko mawakala na klm then watakucharge ukifika bongo nenda pale swiss port air port ya zamani suijiangaishe kuna vijana wanashunghulika pale ukifanya mwenyewe utajichosha sana si unajua bongo kwa urasimu kuna dogo anaitwa farouq 0754815530 yeye elfu ishirini tu anakutolea anpitia sehemu zote wewe unafuata tu akimaliza utachajiwa kama shs 50,000 kwa box zote cos una exeption ya return resident,hlf make sure kama utatumia mawakala wasikufanyie consolidation maana wakikufanyia hivyo utalipa some extra charges

    ReplyDelete
  16. sisi huku bongo hatuna haja na vitabu magazeti ya sani, majira kasheshe, na mengine mengi tu yanatutosha

    ReplyDelete
  17. Mdau Tumia pikipiki maana utaweza hata kukwepa foleni ukiwa na mabox yako!!

    ReplyDelete
  18. Asanteni wadau wote mliochangia hapa,mawazo yenu yatanisaidia sana kupata njia bora ya kusafirisha mizigo yangu. Asanteni sana
    Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...