Kaka michuzi,
Nahitaji msaada. Nimebishana sana na rafiki yangu kuhusu mambo ya ndoa. Swali linakuja hivi; je kati ya mwanamke na mwanaume yupi rahisi kupata mchumba kirahisi?
Nahitaji msaada. Nimebishana sana na rafiki yangu kuhusu mambo ya ndoa. Swali linakuja hivi; je kati ya mwanamke na mwanaume yupi rahisi kupata mchumba kirahisi?
Yeye anasema wao wanaume ni ngumu sana kwa sababu ndio wanaomtafuta msichana na ni lazima wawe wamejiandaa kimaisha.
Mimi nasema wanawake ni ngumu kupata mchumba kwa sababu ndio tunafuatwa kwa hiyo ni mpaka tusubiri.
Naomba naomba michango yenu wadau maana huyu nunda mbishi sana...
Mdau Marie
Bwana ehe integemea unatafuta mchumba wanamnagani. maana kila mmoja anajua ni nini anchotaka kwa hiyo ndio maana mnaona kama mmoja anachukua muda kupata mchumba hayo ni mawazo yangu
ReplyDeleteBi Marie unatafut mchumba nini? Anyway kwa kuwa tupo bize sana na mambo ya mzee kichaka, kwa sasa naweza tu kukwambia kuwa shida hiyo ipo pande zote,kwa wanaume na kwa wanawake. Maana kuna suala la vionjo anavyovitaka mhusika siyo bora mchumba au kuolewa/kuoa kutoa nuksi.Vionjo vyenyewe mi vingi kwa uchache ni kama Elimu,Tabia,umbile(yaani mlefu, mwembamba,mnene,mfupi n.k). Hivyo ndiyo husababisha ugumukwa anayejali vinginevyo ni simpo like ABC. tawile?
ReplyDeleteHaya yote yanategemea na mvuto tu. Kama binti analipa inakuwa sio tabu, kama kaka kasimama nae inakuwa easy.
ReplyDeleteBinti mrembo naomba nijaribu kujibu swali wasichana naona mtakuwa wa mwisho kupata uchumba kutokana na sifa zenu mbaya mliokuwa nazo wakati wakati wa maisha yenu maana utakuta umechezewa na watu kazaaa alafu unategemea utapata mchumba kwanza hakuna mwanaume anaetaka kuoa muozo atajaribu tu kuwa nawe ili kukufariji ila kiroho hayuko nawe tena mwanzoni huenda akawa anataka mtoto ila baadae atakuwa anaombea usishike mimba wakati huo maana wewe umechezewa sana na niaibu kwake. Hiyo ndio sababu kwani hawezi kusema mwanaume malaya ila utasema mwanamke malaya. Najua itakuchoma ila samahani umeyataka mwenyewe pole wee mrembo.
ReplyDeleteSwali la huyu muulizaji halina jibu la moja kwa moja. Mtu jinsia yoyote anaweza kupata mchumba haraka kama ana vigezo vizuri.
ReplyDeleteKwa MWANAUME- rahisi mno kupata mchumba kama ana pesa hata kama ana sura mbaya kiasi gani,
Kwa MWANAMKE- akiwa na sura nzuri na tabia nzuri haikawii kupata mchumba.
Wasivyo na vigezo tajwa hapo juu upataji wao wa uchumba ni bahati. Nawasilisha
mwanamke ndio rahisi kupata mchamba kwani yeye ndie anatafutwa.
ReplyDeleteunajua nini dadaangu! naungana mkono na wewe kwamba wanaume ni rahisi sana kupata wachumba kuliko wanawake.
ReplyDeletemwanamke ukifkisha umri flani hufatwi na kama ulikuwa huna mtu maalum asee unaweza akazeeka bila mume hadi MUNGU aingilie kati.
kwa wanaume ni tofauti, hata awe na miaka hamsini anaweza kuchumbia na akaoa,mwanamke ukifikisha arobain tu hujaolewa asee ndo umedoda hivoo..
So wanaume wao ndo wanafata watu,na anaamuua muda wowote kutafuta mtu..
Huwa najiuliza hiviiii... huyu niliyenayeeee nikimpotezaaa naoooo, si ndo basi tena mana sione kama naweza pata mtu tena etiii.. kwa umri huuu... mmmhhhh.. hii ngumuuu...
kwa mtizamo wangu, kama swala ni nani anataka kuoa, basi muoaji atakua na kazi ya ziada ya kutafuta mchumba anayemfaa. lakini kama swala ni kuoana; basi yeyote kati ya mwanaume au mwanamke anaweza kumtafuta mtu anaye dhani anafaakuwa mwenzi wake kimaisha.
ReplyDeleteshida inayo onekana hapa ni dhana iliyo jengeka ktk baadhi ya jamii kuwa lazima mwanaume aanze process ya kumtafuta msichana.Na hii hupelekea msichana kupata wakati mgumu wa kusubiri hadi afuatwe na mwanaume,ambapo kwa mtizamo wangu hili sio sahihi kwenu akina dada.
hivyo basi ushauri wangu ni hivi;maadam lengo ni kuanzisha familia mpya yenye furaha, basi hata nyie akina dada tafuteni mtu ambaye unaona mtashabihiana ktk baadhi ya mambo muhimu kijamii mwambie kama kweli unasikia chemistry ya mwili imebalance kwake. ila msisahau kuwa wanaume wa ndoto zenu mnaokuwa mkiwataka, labda muingie maabara[au kiwandani] mjitengenezee men of your dreams!
haya kazi kwenu kina dada!na kina kaka!
Kama wewe ndo unafuatwa then just pick one....very simple
ReplyDeleteni mada ngumu kidogo...kwani kulingana na tamaduni [ambazo ni mtazamo wa nje wa maisha], mwanaume ndio anaonekana kama ni rahisi kupata uchumba kwa maana ni yeye anayeanzisha "courtiship behavior. Lakini kutoka katika mtazamo wa ndani ya maisha, huwezi kuamini kuwa, ni wanawake ambao hufanya uchaguzi wa nani awe mchumba wake au mpenzi wake. kwa sababu kuna mambo mengi sana ambayo wanawake huwa wanajari kabla ya kukubali au kuukataa uchumba au upenzi...kwa mtazamo wangu naona wote mpo right ingawa kila mmoja anazungumza katika level tofauti.
ReplyDeleteANON February 17, 2008 10:13:00 THIS IS NOTHING TO DO WITH ME I WAS MARRIED 12YRS AGO,IAM BLESSED WITH MY 2 LOVELY CHILDREN&MY BETTER HALF.
ReplyDeletemadau
A-MARIE
Kweli mdogo wangu, Mimi naweza kukuunga mkono kuwa Wanawake/wasichana ndio huwa wanakuwa na wakati mgumu sana katika kupata mchumba or Mume kwani kwanza anakuwa akisubiria hadi Mwanaume ajitokeze ili amwambie kuwa anampenda na pia huyo anayejitokeza huju kama ni wakweli au anakudanganya kwani matapeli ndio wengi kuliko wale wanaosema ukweli.
ReplyDeleteSasa kama ulikuwa ushawahi kupata mmoja au wawili waliowahi kukudanganya akaja mwingine wa tatu basi tena unamwambia hauko tayari kwani hujui kama ni waukweli au atakuwa kama wale wa nyuma na hapo unakuta sasa huyo ndio alikuwa wa kweli so dear be care full kwani huwezi Jua who is rite person or roan g. Ni kumwomba tu Mungu sana ili akuonyeshe yeye mwenyewe.
Ahsante.
hapa tabu inakuwa kwa yeyote, awe mwanamke au mwaume ikiwa ataweka list ndefu ya vigezo anavyo vihitaji anye mtafuta awenavyo. na kwamtindo huo ataishia kukesha akitafuta hadi majogoo yawike.
ReplyDeleteshida ya pili ni tabia ya uongo iliyo jengeka kati ya pandezote,lakini hasa kw kina dada, wakificha historia za maisha yao yaliyopita. hivyo hata kama alikuwa na mchumba siku mchumba akigundua tu,akiuliza ukaanza kupinga chenga naye anakula kona.
mwisho nakuomba michuzi/au yeyote anaye weza kuanzisha blog ya kutafutana wachumba[dating singles] inaweza rahisisha kiasi fulani kitendawili hiki ambacho ni muhimu kwa sasa.
asee natafuta msichana hatamimi!!unaweza wasiliana nami kwa kupitia pstvm@yahoo.com
unasikia nyi wakina kaka,kuna mambo matatu sisi wanawake tunayo
ReplyDeletekwanza,unatakiwa kuwa na wanaume watatu,
1,mwanaume wa nje,yaani buzi kazi yake kila mkionana anakupa pesa ya kula na mambo ya wanja na mengineyo
2,unakuwa na buzi wa nje yaani endsome kazi yake kutoka nae nje na kujivinjali nae
3,huyu ni wa ndani yaani bwana mzee mwenye nyumba,
mimi dada kutoka bukoba
Kwa upande wangu kwa wasichana ni tabia nzuri period.Ukiwa na tabia nzuri halafu hauko too picky utaolewa in no time
ReplyDeleteKwa wanaume ni Pesa ukiwa bongo..Kama una hela nyingi bongo wachumba nao ni wengi tu wa kuchakua...
Ukiwa nje ya nchi kwa mwanaume ni akili....wanawake walio nje ya nchi wanapenda mwanaume mwenye akili.... Kama huna green card basi make sure hukuacha akili yako bongo...lakini kama unataka mchumba mbantu lakini kama unataka wazungu wala haina taabu kabisa. hela wala akili sio kigezo tena...
KAMA ILIVYOSEMWA HAPO JUU KABISA. VIGEZO VIKO VINATAWALA SEHEMU MBILI. ELIMU, UMBO,NA TABIA. NAFIKIRI KINACHOTANGULIA NI UMBO(First attraction),then MKIONANA AU KUKARIBIANA, UNACHUNGUZA TABIA(Ambayo ni rahisi wanaume kuiona katika kuongea) na mwisho ni ELIMU(Ambayo sometimes, wanaume hawajari, kama tu dada-etu ameshinda vigezo vilivyotangulia)ILA WAZUNGU HAWAJARI,SINCE THEY WANNA EXPLORE THE BLACK AFRICAN SKIN ILA UWE NA TABIA NZURI THOUGH! GOODLUCK KWA SUALA HILA, SABABU NAMI NATAFUTA MCHUMBA, WA KI-TANZANIA ILA TABIA BADO SIJAMPATA......
ReplyDeleteAnon wa Feb 17, 2008 10:13:00 akili zako changa...eti wanawake wanachezewa, na ni nani anayewachezea? hivi ni kuchezewa au kuchezeana? kwani mwanaume anapokuwa kwenye shughuli mwanamke anakuwa amekaa tu anamuangalia? na yeye si anamchezea? ingekuwa issue ni hiyo basi hata nyie msingeoa kwa sababu mnachezea wanawake..nyambaf kabisa!!
ReplyDeleteIssue ni nini unataka bwana, kwa mfano mie, nawapenda wakaka warefu, weusi, waliosoma ofcoz, hela ni sabuni ya roho kwa sababu ya kuendesha maisha ya kila siku mana hakuna kisichohitaji pesa, smile muhumu sana, ofcoz good looking ili hata akilala usije ukastuka usiku na kumuangalia anavyokoroma + sura ya ajabu = kutoka mkuku!!!
Wee kaka usianze kuponda wanawake eti wanachezewa, na kwa taarifa yako hakuna anayechezewa, mnachezewa nyie hapo.... tutakufanyia humu kwa michu mpaka uombe radhi!!!
mwambie shoga unaweza kukuta huyo kaka ni mfupi na sura kama anakunyawa ndimu au malimao,kama ameoa basi kaokota wale wachafu kama yeye muone kwanza mfupi nani atakupenda na kama uko ugaibuni basi ulifika kwasababu baba yako fisadi,mbeba mabox utakuwa mfupi zaidi
ReplyDeleteKweli akina dada tuna"china" kwa kungoja kuombwa uchumba. Lakini nadhani huo utaratibu ni wa kiafrika, Unatuumiza ila sidhani unatusaidia ila kutuumiza tu
ReplyDeletedu kazi ipo
ReplyDeletekwa upande wangu amara nyingi huona mwanamke hupata mchumba mara.
ReplyDeleteangalia kwenye blog hii kuhusu zaynab kisha pata wanaume wangapi waliomtumia e-mail.
mwanamke mara nyingi ni kivutio kikubwa mbele ya wanaume.