Mwakilishi wa Mheshimiwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Maajar, anatarajiwa kuja Ireland hivi karibuni ili kushughulikia passport za Watanzania waishio Ireland.

Watanzania wote waishio Ireland ambao wanahitaji passport mpya au wana tatizo lolote kuhusu passport zao watumie fursa hii.

Tafadhali kama unahitaji kutatuliwa matatizo yako jiandikishe kabla ya tarehe 20/02/2008 kwa kutumia namba hii 0857368751.
Asanteni
Mwakilishi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Nampongeza Balozi kwa jitihada hizo zilizojaa maamuzi ya kibusara kuhakikisha kila Mtanzania aliyeko nje anayehitaji Passport ya TZ anapata bila ya kipingamizi chochote.Lakini jitihada hizo zisiishie hapo tu.Pawepo na utaratibu utakao wawezesha Watanzania wote walioko nje wanashiriki kupiga Kura kila Uchaguzi Mkuu utakapo wadia ili kumchagua Rais wao wa nchi.Siyo hapo tu.Watanzania hao wajengewe mazingira yatakayo waruhusu na kuwavutia kuleta huku nyumbani Tanzania sehemu ya Akiba yao ya kila mwezi(monthly savings) ili wawekeze katika kuinua na kuimarisha uchumi wa nchi yao na wakati huohuo wao wenyewe kujiwekea misingi imara ya maisha pindi watakapo amua kurejea huku nyumbani kama wenzao wanavyofanya katika nchi zingine.Pia wataziwezesha Familia zao (extended families) zilizopo huku nyumbani ziweze kuwa na maisha bora zaidi.Wasikatwe kodi kwa fedha zote watakazo zituma nyumbani azawaiz hakuna mtu atakayetuma pesa nyumbani Tanzania.Pia waelimishwe kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini kwa sasa.Keep it up Balozi.Sijui Balozi zetu ngapi zinafanya zoezi kama hili.Tungependa kupata habari zao pia ili Vijana wetu wasiwe watumwa huko ugenini kwa kutojua mabadiliko yanayo tokea huku nyumbani.YOURS ROVING AMBASSADOR AT LARGE IN TZ.

    ReplyDelete
  2. afadhali uko kuna huduma bora ya kupata passport, sehemu za huku america, tunapataga usumbufu sana, michuzi tafadhali usibane hii, yaani usumbufu kiasi kwamba mnakua hamna imani na ofisi ya serikali, hapa us wanazungusha sana watu.

    ReplyDelete
  3. afadhali huko kwenu .....marekani ni muozo mtupu...yaani inakatisha tamaa...I hope huyo balozi mpya atawabadilisha tabia wale pale ubalozini....

    My friend wameipoteza hata passiport yake sasa ni kusumbuana tu.

    ReplyDelete
  4. Sasa wewe kule marekani ya nini pasipoti ya kibongo???jamani si mnalenga girinikadi...si mko tayari kuvitenda vyovyote ili mpate haki huko...tuachie sie wazalendo tuwe na haki yetu hapo TZ!

    ReplyDelete
  5. Hamna lolote danganya toto tuu au sababu rais anakuja
    Watu kiba londo hawaja pewa pasipoti
    na raisi akija tuna lazima tufikishane mablil

    ReplyDelete
  6. @1:12 nenda shule kwani kuwa na green card ndio passiport ya bongo basi tena... elimikeni kidogo...mambo msioyajua waachieni wenyewe..

    Na ni kweli ubalozi wetu USA unanyodo sana...kila ukipiga simu ni subiri, subiri, na wakikwambia watakucall back ndio usahau...

    Halafu kwa kwenda lunch au kwenye meeting ndio wenyewe. Ukipiga simu pale ...unaambiwa ameenda lunch, mara yupo kwenye mkutano. Yaani mikutano yao haiishi... sijui wanafanya party time somewhere else au ndio kuitangaza Tanzania kwa nguvu hivyo.

    Ubalozi wetu UN pale NY city at least wako pro ukiwapigia simu watakupa information na kama ni simu wakikwambia tutakucall back ....wanafanya hivyo lakini DC wanahitaji a big wake up call.

    ReplyDelete
  7. Mie sijawahi fika Ireland kwahiyo sijui ukubwa wake ni kiasi gani mpaka watu wote wajiandikishe kwanza ndio mpewe huduma na pia siwezi m-judge huyu balozi kwa kua sijatumia huduma zao toka mama kapewa wadhifa huu.Ila ubalozi uliopita walini boa sana na huduma zao.Uingereza ina counties tofauti kama wanataka toa huduma ya kutoa passport basi kwa nini wasi tangaze kua mwezi fulani tuta tembelea county fulani kwahiyo watanzania wote wenye kuishi katika miji inayo share the same county wanajikusanya wanapata huduma zao,kuliko walivyo tufanyia miaka ya nyuma ya kwenda kwenye mji mmoja halafu watu wote wa miji mingine waende kuwafata kwenye hicho kijimji walichokichagua.Ukikosa kwenda siku hiyo ndio imetoka inabidi utafute safari ya London(Bond St).I hope huyu mama kaleta mabadiliko.

    ReplyDelete
  8. ulaya, marekani tumechoshwa sana, bora hata blog ya kaka michuzi, niko florida yaani ubalozi wa usa, ni wa ajabu sana, wanajinufaisha wao tu, kama una shida ya passport wanakuzungusha mpaka basi, ni vizuri kama kikwete akifwatilia hili swala, kwani wananchi nje ya nchi wanakosa imani na serikali.

    ReplyDelete
  9. michuzi wewe ni kiboko, kwa blogu yako, maana hizi ofisi za serikali ulaya kikwete hajui mambo yao, ya kujuana juana, amefika dc lakini kashindwa hata kufuatilia ni vizuri kama akielekeza macho yake na uko pia.

    ReplyDelete
  10. nakubaliana na annon wa february 16th, kweli dc kikwete hajui mambo yao, ya kuzungusha zungusha.

    ReplyDelete
  11. ni kweli kabisa safari anazofanya us, hajui mambo wanayofanya watendaji pale, ni bora kama angekuwa anafuatilia kwa makini sana.

    ReplyDelete
  12. michuzi wewe ni kiboko sana, tupo ulaya lakini tunafaidika sana na blogu yako kaka, kikwete amefika london, washington lakini ameshindwa kujua kabisa urasimu kwenye hizo balozi, kwa kweli kikwete tafadhali fuatilia maoni ya watanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...