inafurahisha kuona vyakula vya asili vinaendelea kutayarishwa na kuliwa kama kawa. huu ni ugali kwenye sahani za majani ya mgomba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Wewe michuzi usinikumbushe huko kwetu Lushoto, maana siku za hitima au arusi sahani zinakua hazitoshi kwahio wanaweka kwenye majani ya mgomba, kisambaa [funge] hapo unaletewa na nyama ya ng'ombe au mbuzi iliyochinjwa siku hio. unafungua funge na nyama ya mbuzi.mmmmmh wewe bwana umenikumbusha nyumbani.

    ReplyDelete
  2. SAFI SANA LAKINI WAMECHANGANYA SOMO KIDOGO.
    UKITAKA KUFUATA UTAMADUNI BASI VEMA UTAFUTE KUUKAMILISHA INAVYOWEZEKANA (INGAWA HUTAWEZA KWA 100%).

    UGALI KUFUNGWA KATIKA MAJANI YA MGOMBA LAKINI UKAISHIA KUWA NDANI YA CHOMBO CHA ALUMINIUM AU STAINLESS STEEL N.K NI SAWA NA KUWAMBIA WATU WASINIITE STANLEY BALI WANIITE NYAKATAKULE- THE LAND SNIFFER BADALA YA KUKAMILISHA JINA LENYEWE KUWA NYAKATAKULE - UNYILISYA ECHALO!

    HUO UGALI NA MAJANI YAKE VINGEWEKWA KATIKA KISONZO (MUCHIBHO) AU KATIKA CHUNGU (MUNYUNGU) EWAAA!!

    ReplyDelete
  3. Huo ubwabwa ukila na mchuzi wa kambale...ahhh tena akichanganya na maharagwe...raha tupu mjomba,Kempinski mnasikiliza???

    ReplyDelete
  4. Huo ubwabwa ukila na mchuzi wa kambale...ahhh tena akichanganya na maharagwe...raha tupu mjomba,Kempinski mnasikiliza???

    ReplyDelete
  5. Mhhh michuzi ..
    Hiyo nguna inaonakana bomba sana lakini ujazo wake ni mdogo isije ikawa lile nguna la pale zamani gerezani mama ntilie ...wooops Mama Lishe walikuwa wanachanganya na hamira basi madude yakishajichanganya humo hukawii kuanguka na kupiga chini ...wellndio bongo yetu hiyo .
    kidumu ..
    mdau

    ReplyDelete
  6. kaka michuzi huo ugali ukiliwa na mchuzi tena nakualika wewe michuzi tuje kula pamoja nguna na mchuzi

    ReplyDelete
  7. Mr Nyakutule hata kuweka humo kwenye hizo besen ni kuweka kale kaustaarabu kapya kwani wakiweka kwenye hivyo vyombo ulivyovitaja vya asili ninashaka kama wangepitia humo kila mtu angeukwepa ila vile umewekwa kwenye mgomba nina shaka pia kama ulimalizwa, ila ungewekwa kwenye foil paper ewaaaaa wengi wangekua na imani nao

    ReplyDelete
  8. Michuzi hao waliofunga hizo funge washauri warudi lushoto japo kwa mwezi mmoja maana wamesahau namna ya ufungaji- funge.jani la mgomba ni Hotpot ya kisambaa kwa ugali, na ugali unatakiwa usionekane- shuti ufungwe vizuri kwa style yake, ili kuhifadhi joto na usafi kwa ujumla. hicho walichofanya hapo ni aibu. na sijui lengo lilikuwa nini!

    masamwei

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...