Mhandisi wa ujenzi Clemens Karokola akimweleza mam wa kwanza Salma Kikwete maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyamisati hukoa katika kata ya Salali wilaya ya Rufiji.Ujenzi wa shule hiyo ya bweni uko katika hatua za awali ambapo awamu ya kwanza inatarijwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu.Shule hiyo inajengwa kwa ufadhili wa Taaasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya Salali wilayani Rufiji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Huyu mama yetu kwa kweli anapiga kazi mpaka inatia raha.

    ReplyDelete
  2. Mama Salma Kikwete MUNGU akubariki, akulinde,akupe nguvu huendelee na kazi yako nzuri uliyoianza ya kutumikia taifa letu na maendeleo yake.

    ReplyDelete
  3. Mama yetu huyu anapiga kazi naungana na mdau wa kwanza. Mama Salma Mungu akubariki na akuzidishie utayari wako naomba uzidi kusaidia maeneo ambayo kupata hudumu ni ngumu kidogo. Mungu akubariki sana

    ReplyDelete
  4. Mama acha kudharau walimu wazalendo

    ReplyDelete
  5. Wewe anon hapo chini sasa huyu mama atadharau walimu ili nini amekuwa mwalimu pale mbuyuni miaka nenda rudi sidhani kama ataweza kufanya hivyo halafu tushukuru anafanya kazi sana kwa kweli yaani nadhani schedule tight sana

    ReplyDelete
  6. Sasa kama ukiingia kwenye blogu huna kitu cha kusema bora kupita kimya kimya, sasa kadharau walimu wazalendo, hapo kwenye picha yuko na walimu wageni au wazungu? Mwe mkiamkaga na mataputapu bora msiingie kwenye blogu!

    Mama hongera sana nina hakika huko Nyamisati tangu uhuru hawajawahi kuona sura ya first lady hata mmoja wewe ni wa kwanza bila shaka. Maana huko kwenye delta ya Rufiji mhuu sie tunaopajua tunakupa hongera kwa kusogeza elimu kwa watoto wa eneo hilo na itawasaidia watoto wengine wote wanaoishi kwenye delta ya Rufiji iliyo karibu na hapo.

    ReplyDelete
  7. Huyu mama alitamka kuwa hiyo shule itafundishwa na walimu toka nje kwani hapa kwetu hatuna walimu?

    ReplyDelete
  8. Huyo anony aliyesema kauli ya huyu mama kwamba ataleta walimu kutoka nje yuko sahihi amuangaliagi TV?

    Huyu mama alitamka hivyo wakati anatembelea huo ujenzi na hiyo ziara ilirushwa hewani na local TV station

    ReplyDelete
  9. Nyinyi mnaopinga kwamba huyo mama hakutamka hayo maneno inaonekana mko nje ya nchi

    ReplyDelete
  10. Afadhali aamke na mataputapu lakini anachoongea ni point wewe ambayo hujaamka na matapu tapu ona unavyoongea pumba

    ReplyDelete
  11. Mama Salma anashauriwa awe anaandika vitu halafu awe anahutubia kwa kusoma maana anaweza akawa anamuangusha mheshimiwa Rais kwa kuteleza ulimi hapa na pale kama alivyoonyesha kutowajali waziwazi walimu siku alipotembela ujenzi huu alisema hivi namnukuu

    "Na mimi nimekuwa nikitembea nchi mbalimbali huko tunaweza kupata walimu kuja kufundisha hii shule na wala sio walimu wa hapa"

    Unaona

    Kauli hii inadhihirisha wazi jinsi asivyothamini walimu wazalendo

    Mama Salma usimpe kazi Mheshimiwa ya kukutetea kila siku kama alivyokutetea pale alipotamka kuhusu suala la Ocean Road Hospital na vifaa vyake

    Andika hotuba au muombe husband wako akuandikie au kuedit kama huna wasaidizi wa kufanya kazi hiyo. Hii nafikiri itakuepusha na matamshi yenye mlengo wa kushoto

    ReplyDelete
  12. Ushauri kwa commentors wengine

    Usikurupuke kumshambulia na kumtukana commentor mwengine kama huna data, hatutaki ugomvi kwenye hii blog yetu.

    Mama Salma kweli alitamka maneno lakini tunamsamehe tunajua aliteleza hivyo tunaomba aufikirie ushauri huo hapo juu kama utamfaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...