Hi Bro Michuzi!

Kwanza kabisa napenda kutoa salamu zangu kwa Watanzania wenzangu wote!

Pili kutoa pongezi kwa waziri mkuu mpya kwa kuchaguliwa kwake. Namtakia mafanikio mema mengi katika shughuli zake.

Tatu pongezi kwa wanamziki wote wa Tanzania: kwakweli ni furaha kubwa kuwasikiliza.
Nimesikiliza kwenye mtandao nimekubali mwenyewe kwa mavituziii wanayo tuletea. Hasa pongezi zangu nyingi kwa kijana huyu MARLAW, kwa nyimbo yake nzuri kabisa ya RITA.


Pongezi nyingi sana kwako kijana kwa kazi nzuri uliyoifanya, endeleza juhudi zaidi na zaidi. Pia wanamziki wote wa huko kwetu hongereni sanaaaa!!!!!


Ni mimi Baraka F.Chibiriti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Bwana chibiriti safari hii watakukomaaa,hakuna maneno tena ohhh computer ohh niniii!!hiyo picha ulipigia kwa rafiki yako au umehama nyumba?maana ile computer yako siioni tena hapo..
    mdau Norway

    ReplyDelete
  2. Mungu wangu weee N'jomba CHIBIRITI unerudi tena humu,yale matuchi ulotunwa weee haukuchiba unataka mengine tena mimi chimo kabicha kwa yatayo kukuta tena.

    ReplyDelete
  3. Too much Chibiriti!!

    Hivi unakwenda shule/kazini wewe? naona unalala hapa kwenye blog ya MICHUZI.

    Chibiriti tafuta hobby nyingine

    ReplyDelete
  4. Muachenii ndugu yenu nyinyi watanzania, kwani nyinyi mmekatazwa kuweka picha zenu hapa?? hiyo ni roho mbaya inaitwa, na mwenye roho mbaya hufa kabla ya siku aliyopangiwa na mungu. Huyu kaka anaweka picha yake hapa kwa nia njema hajamtukana mtu, sasa nyinyi kashfa za nini wabongo nyiee? wekeni zenu basi tuwaone kama hampendi yeye aweke, la sivyo si mpite tuu kama hamja muona kwani lazima mpige domooo, Roho mbaya itawazeesha nyinyi waote wenye roho ya kwanini, mnatia aibu hapa hamuonyeshi roho ya upendo hata kidogo kwa watu wenu.

    ReplyDelete
  5. CHIBIRITI NIMEFURAHI SANA KUKUONA TENA, MZIMA? MTU WA WATU KAMA WEWE HUWA ANAFANIKIWA MWISHOWE. KEEP IT UP BROTHER!

    ReplyDelete
  6. Chibiriti, kwa mbaali unafanana na mheshimiwa Pinda.

    ReplyDelete
  7. we bwana wewe,

    upo tuuu???

    vile vitu vyako vilivyochakaa bado unavyo??

    naona umeamua kuchukua gheto la mshikaji na kupiga nalo picha,

    haya bwana kibatari

    ReplyDelete
  8. Lakini wewe Chibiriti unakaa Italy sehemu gani? Tibutina au Termine au wapi? Na hiyo kitambaa ya rangi nyekundu unajiandaa na Valentine? Hongera kwa kuficha sasa kale ka computerna Kiti cha wakati ule, kalikuwa kanatuaibisha!
    ciao amico!

    ReplyDelete
  9. Chibiriti aka. Chibatari aka. umeme wa Richmond, nakushauri pia ujaribu kutuma picha zako bungeni kwa kuwa umaarufu ulionao sasa unaweza kubahatika kuwa waziri mkuu. hongera maana naona kale ka lotion kameanza kukukubali.. usiache kukatumia

    ReplyDelete
  10. Mtu wa watu? Mh, mi simo!

    ReplyDelete
  11. U're back Chibiriti! Happy 2 c again! Karibu sana. Naona umechange room uliyopigia photo ya kwanza. Mie niliipenda ile ya mwanzo, it was great!

    ReplyDelete
  12. Hongera Chibiriti, maana umekuwa celebrity bila hata kuomba. Check ukipost ujumbe wadau wanavyohangaika! Keep it up brother!!

    ReplyDelete
  13. MTASEMA MTACHOKA. KWANZA MNGEJUA MICHUZI ASILI YAKE WAKE HALA NDIYO MNGEMLAUMU HUYO CHIBIRITI.
    NAKUMBUKA VIPINDI VYA SALAMU VYA REDIO TANZANIA DAR ES SALAAM (RTD) ENZI HIZO KULIKUWA KUNA MAJINA YA WATUMA SALAMU AMBAYO ULIKUWA HUWEZI KUKOSA KUYAKISIKIA NA WENGI WAO WALIKUWA WAMAKONDE.
    UKISIKILIZA KIPINDI CHA SALAMU ZA ASUBUHI NJEMA WAPO, MCHANA MWEMA WAPO, NA ZILE ZA JIONI NJEMA WALIKUWA HAWAPITWI.
    SIYO KWAMBA WALIKUWA WAKINUNUA POST CARD WINGI NA KUTUMIANA SALAMU, LA HASHA, BALI BAADHI YA WAFANYAKAZI WA RTD WALIKUWA WAKIGANGA NJAA KWA KUWAPATIA UMAARUFU WATU FULANI FULANI.
    WALIKUWA WANAJIFANYA WAPO SAFARINI DODOMA, MWANZA, ARUSHA, MTWARA, LINDI, MBEYA HUKU UKIPITA MITAANI DAR UNAKUTANA NAO.
    KWA HIYO SISHANGAI HUYU JAMAA NA WENGINE HUMU NDANI KUONEKANA MARA KWA MARA KWA KUTUMIA NJIA ZISIZO HALALI.
    WAPO KIBAO KAMA HUYU CHIBIRITI, JESSE, TWANGA PEPETA ILI MRADI TU UKIWEZA KUMRIDHISHA "BWANA LOWASSA".

    ReplyDelete
  14. Maskini Chibiriti. Inaonekana upo lonely kweli ndugu yangu. Huna watu wa kupiga nao story huko Italy? Maana kila kukicha wewe upo kwenye globu ya Michuzi.

    ReplyDelete
  15. Chibiriti, sai che cosa sta dicendo?. Non dire la bugia. anche noi qui a casa sapiamo che la vita in Italia e' dura. E meglio vivere qua che in Europa. Giusto????? Vivo in Chalinze e mi piace la vita in Tanzania

    Ti auguro una buona giornata.

    ReplyDelete
  16. We Chibiriti nini tena?KAMA UNATAKA KAMPENI ZA ABUNGE SI USUBIRI MUDA UFIKE.NAONA SAFARI HII UMEJITAHIDI SANA KUTAFUTA SEHEMU YENYE UNAFUU KWA AJILI YA KUPIGA PICHA.VIPI ILE COMPUTER YAKO ILIKUA NI YA MWAKA GANI, USIITUPE ITAKUSAIDIA SANA,

    ReplyDelete
  17. Khaaaaaaaaa jamani hii ni mara yangu ya pili kutuma maoni hapa, brooo usiibanie!
    Leo nimecheka sana hapo juu watu walivyomuandama Chibiriti wa watu, siku zile niliona walivyomnanga eti fenicha za bongo tena mbovu leo wanaanza kumkejeli jamani si vizuri ametuma salamu tu mnaanza ohhhhhhhhhh eheeee jamani muacheni!

    ReplyDelete
  18. Mwe mbavu zanguuuuu, nimecheka ile mbaya, mbona mnapenda kumnanga mwana wa mwenzenu

    ReplyDelete
  19. Your so sexy kibiriti,will you marry me please?.

    ReplyDelete
  20. Chibiliti i can thee the blingbling keep it up keeping the blog alive....

    ReplyDelete
  21. Pepe wa kale sio globu ni Blog Jamani na kuzamia Tanzania bado tu hajachangamka alafu tukiwafundisha oh box...

    ReplyDelete
  22. Kibiriti Kibiriti, achana nao hao waosha vinywa kama hoby yako kutoka kwenye globu toka tu. Fanya kitu ile roho yako inapenda. Tunashukuru kwa salamu ukikuta maneno mabaya huku usikasirike cheka sana, hata mie niko mahali huku watu weusi unawatafuta sasa nikiingia kwenye blogu angalau najisikia niko Kariakoo au Manzese kwa mfuga mbwa au Magomeni Mikumi kutokana na mipasho ninayokutana nayo. Wala safari hii usiwajibu acha wakupe raha waswahili wanasema raha jipe mwenyewe na wewe umeamua kujipa raha poa tu.

    Ciao

    ReplyDelete
  23. Kibiriti anatafuta mchumba jamani...singles mko wapiiiii.....

    manake watu kama hawa ndio wanakeep hiii blog alive.

    Nimefungua humu kumwona huyu mbavu sina. Ukiambiwa mtu ana thick skin ni huyu....

    ReplyDelete
  24. chibiriti,in professional terminology,suffers from chronic attention seeking syndrome,people of this nature end up committing suicide,if prevented,so michuzi keep on posting this guy or else you will ge liable

    ReplyDelete
  25. chibiliti mimi chichemi ng'o nikichema ooo chielewi...

    ReplyDelete
  26. Sikua na dhumunio la kutoa maoni,kilicho nifanya nije kwenye maoni ni furaha ya kuona picha ya Chilibiti,na idadi ya maoni yamezidi 20,nikaona nije nijifurahishe na wasuuza vinywa na huyu celebrity wetu,eeh bwana ee,nakusifu,either unatengeneza mazingira ya baadae au unapenda kutukanwa au kama anon hapo juu alivyo sema (CASS)Chronic Seeking Attention Syndrome,that your life depends on it.

    ReplyDelete
  27. ++++++++++++++++++++++++++++++++
    Anonymous said...
    Pepe wa kale sio globu ni Blog Jamani na kuzamia Tanzania bado tu hajachangamka alafu tukiwafundisha oh box...

    Monday, February 11, 2008 8:48:00 PM EAT
    +++++++++++++++++++++++++++++++

    .....Wewe bwege - Anonymous wa Feb 11 @ 8:48:00, yaonekana weye ni mgeni katika hii "GLOBU", yes, humu ndani sote tunajua hii ni BLOG lakini kutokana na uzoefu wetu tunaiita hii ni GLOBU na kama ungekua unapitapita humu kila siku kama wengi wetu tufanyavyo wala usingeona issue kwa mie kuandika "GLOBU" badala ya "BLOG". Ni lugha yetu maalum humu ndani. Ni sawa na kusema Ukerewe badala ya UK au Dumila badala ya Dubai. Braza Michu eee, hebu wafungulie shule ya hii "GLOBU" yetu hawa wageni.

    ReplyDelete
  28. Kibiriti usikonde hao wote ni ma homeboy wanapenda wakutibue nyongo kidogo, na washamirishe baraza wenye meno wacheke vibogoyo wagegede.

    ila uko jasiri kiasi inafurahisha we ukijiskia tu weka mdahalo wako kwa raha zako huku kwenu hugombwi mwenetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...