MDAU, JE WEWE UNGEKUWA JK UNGEMCHAGUA NANI KUWA WAZIRI MKUU NA KWA SABABU GANI?
CHONDE CHONDE WADAU HILI SI SHINDANO WALA HAPA SI MAHALA PA KUONDOLEA DONGE. TUJADILI KWA KINA BILA YA KUCHAFUA HALI YA HEWA AMA KUMTIA MTU DOLE JICHONI..
NAWASILISHA ILI KUPOTEZA MUDA WAKATI TUKISUBIRI FAINALI...
Mizengo Pinda for PM post
ReplyDeleteau
Dr. Harrison Mwakyembe, hiki kichwa nakikubari toka enzi zake za UDSM
Professor Ibrahim Lipumba...in the interest of national unity!!!
ReplyDeleteNingekuwa JK ningemchangua Mwandosya kuwa waziri mkuu na Magufuri kuwa waziri wa nishati na madini.
ReplyDeleteMzee wa TBS
Mh Doctor Mch Askofu Mama Getrude Lwakatare:
ReplyDeleteSIFA
1.Ana mvuto
2.Hajidai
3.Mcha Mungu
4.Ana sauti yenye kujaa ushawishi(Kiongozi)
5.Ni tajiri (hatakuja kuwa fisadi)
6.Tangu aingie bungeni wabunge wote sasa wanamkumbuka wanamtaja Mungu ( Mfano:-Kilontsi Mporogomyi,Simbachawene,Mama Anne Killango,Maulida Komu,Ndesamburo na hata waliotuhumiwa ufisadi (LOWASSA,KARAMAGI NA MSABAHA)
Mpendakeroro@yahoo.com
ningekuwa mimi na kama katiba inaruhusu kufanya hivyo kwa kuteua wapinzani, basi ningempa mpenda nchi mmoja "Dr. Wilbroad Slaa" na madini ningemweka Zitto Zuberi Kabwe! nukta, hao wengine ningefumba macho na kutaja tu, lakini majina yao yote ningeyaandika kwa penseli ili iwe rahisi kuwafuta kazi pasipo kusubiri tume teule kama hivi!
ReplyDeleteNingemchagua Mark Mwandosya, nina imani kuwa atasaidia sana katika kuendesha serikali haswa katika kipindi hichi ambapo imekumbwa na matatizo. Na pia atakuwa amesoma kutokana na kilochotokea kwa hivyo atakuwa na tahadhari kubwa.
ReplyDeleteDuhh!! Hapo kazi ipo... Unaona sasa, Michuzi mimi nilikuuliza kwanini umeenda Zanzibar wakati kama huu! Wewe mdau wetu wa kijiweni, kura tayari zaidi ya mil.3 ungepita tu! au ndo utaunganisha boti mpaka Pemba kwa wajuzi? Sasa na vile spika 6 tena amemwaga hazalani ya kuwa watu wajisafishe mimi naona Mhe Lwakatare maana yeye tayari msafi au vipi, au hata Mhe Kilango-Malecela sababu yeye alikuwa tayari kumtosa hata mumewe kwaajili ya siasa. Nimeona badala ya wewe basi awe mwanamke maana katika ripoti nzima ya Richmonduli hakuna hata mwanamke wa kusingiziwa... Na hivi kule USA atashinda Mama, basi mwaka huu uwe wa wakinamama tu!!!
ReplyDeleteKinamama Oye!!!
Mimi nigekuwa JK ningemteua Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri(TAMISEMI) Mh.Mizengo Kayanda Pinda(MB) kuwa waziri mkuu mpya.Sababu ni hivi zifuatazo.
ReplyDelete1.Kitaaluma ni mwanasheria hivyo naamini anaweza kutumia taaluma yake kubaini mambo mengi ambayo yataonekana kuwa yanakinzana na sheria za nchi na hivyo kuepusha kuliingiza taifa kwenye matatizo yasiyokuwa ya lazima.
2.Amewahi kuwa afisa mwandamizi wa idara ya usalama wa taifa pale Ikulu kabla ya kwenda kugombea ubunge kwao huo Mpanda mwaka 1995.Kuwa katika idara hii ni imani kutamuweza kuwa upeo mkubwa wa kushushtua dili fekifeki mapema na kuchukua hatua haraka.
3.Alipochaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya kwanza 1995,Rais Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI chini ya waziri mzee Kingunge.Hapa ndipo wafuatiliaji wa mambo tulipogundua kuwa anaonyesha dalili za kuja kuwa kiongozi makini sana kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao katika kujenga hoja alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge.
4.Mwaka 2000 aliteuliwa tena kuendelea na nafasi yake hiyo hiyo chini ya Mh.Brig.Ngwilizi.Kwa kuwa tayari alishakuwa na uzoefu wa miaka 5 katika wizara hiyo,Mh.Pinda alizidi kuonyesha uwezo mkubwa sana kiasi ambacho wachambuzi wa siasa tuligundua kuwa alikuwa na uwezo hata kumzidi waziri wake.
5.2005 Rais JK kwakuwa alikuwa ameshauona uwezo wake kwa kipindi cha miaka 10,kama naibu waziri,akampandisha kuwa waziri kamili.
6.Sasa hoja yangu ni kwamba kwa wanaojua dhamana ya waziri mkuu katika mfumo wa serikali yetu,ni kwamba yeye ndiye msimamizi mkuu wa sera za serikali.Na sera za serikali zinatekelezwa kwa asilimia 90 na TAMISEMI.Kwa hiyomuhimu sana kuwa na mtu mwenye uzoefu na masuala ya serikali za mitaa na tawala za mikoa.Kwa lugha nyepesi,TAMISEMI ndio serikali yenyewe.Hakuna wizara isiyofanya kazi na TAMISEMIukiondoa,mambo ya nje,Ulinzi,na mambo ya ndani.
Naomba kuwakilisha,
Kada-Ohio
KAKOBE
ReplyDeleteKAKOBE
ReplyDeleteMkuu naona bora tu ampe mama Malecela maana hana mchezo na mafisadi hata kama angekuwa mshua wake mzee kilango angemkaanga..
ReplyDeleteBig Up mama zetu.
Ben Dar
Bro Michu
ReplyDeleteSamahani najua hii sio mwake hapa, ila nasikia na Hosea nae kapeleka barua ya kaachia ngazi? Taarifa za kweli hizi?
Kwa kweli ki haki lilah michu mi simuoni hasa ni nani mana nachelea kwa kuona wote ndo walewale walokunywa uji wa mgonjwa.
ReplyDeletekwa mbaaaali ingekua dr sheni si mgombea mweza ingekua afadhali yake mara kumi na mbili.
Hili swala ni zitto zitto mr michu kuamua
JOHN MAGUFULI.
ReplyDeleteHUYU AMEONYESHA UJASIRI MKUBWA KWENYE WIZARA ILIYOJAA UOZO YA ARDHI. PIA HAOGOPI KUSEMA PALE INAPOTAKIWA KUSEMA. KWA MFANO JUZIJUZI MBELE YA RAIS ALIWA-CHALLENGE MAWAZIRI WENZAKE WA MAJI NA MIUNDOMBINU JINSI AMBAVYO HAWATOI USHIRIKIANO WA KUTOSHA KWENYE UJENZI WA NYUMBA HUKO KARIBU NA CHALINZE
MAWAZIRI ALIO-WACHALLENGE WALILALAMIKA, LAKINI SISI WANANCHI(AMBAO SI WADANGANYIKA TENA) TULIMUUNGA MKONO NA TUNA MUUNGA MKONO NA TUNATAKA AWE NA UWEZO KAMA WAZIRI MKUU KUWATAKA WAFANYE KAZI KULINUSURU TAIFA LETU.
MAGUFULI ALL THE WAY....
MIMI namuona MAGUFULI ndiye anayefaa kuwa waziri Mkuu.
ReplyDeleteNi Mchapa kazi, hana kashfa sana kama wengine.
MAGUFULI BABAAKE!
ReplyDeletejina jipya kabisa na wala sio kutoka katika cabinet, kwa hiyo liwe jina jipya kabisa.
ReplyDeleteMimi kwakweli ningempendekeza Mzee Mizengo Pinda.
ReplyDeletePamoja na uzoefu, sijasikia kujihusisha au kuhusika kwake katika kashfa yeyote ile.
Naomba kutoa hoja
HAYA YOTE NI MASKANDAL, YANA BASHASHA ZAKE KATIKA SIASA. akrm
ReplyDeleteMie napendekeza waziri mkuu awekwe BALALI sababu ndio kawaida na desturi ya serkali ya CCM anaeharibu wizara hii hupelekwa wizara nyengine!Na bwana Edo (edward lowasa)nae sasa apewe uwaziri wa fedha.
ReplyDeleteMichu usibanie, kuna falsa katika hili, na utaona, japo haitakuwa hivyo lakini haitatofautiana na hivyo.
Bernard Membe
ReplyDeleteJamani prime minister sio lazima awe mwana siasa awe mtu mwenye experience ya management for over 10 years , i know salim ahmed salim ni mwanasiasa lakini i think he has experience and exposure najua sio mbunge ila anaweza pendekezwa
ReplyDeleteWilliamtz
kwangu ni Dk. Wilbroad slaa,
ReplyDeletekama mpinzani hatakiwi basi hata Kilango Anne Malecela,
Ni mama jasiri na asiependa Unyonyaji,
Wala hana U-CCM zaidi ya kujali maslahi ya wananchi na kuchukia ufisadi.
Pia Simbachawene nae anafaa
JK hatakua na kazi kubwa sana kama atamfanya MBUNGE WA KUTEULIWA halafu akamvika kofia ya UWAZIRI MKUU.... Mambo yote yatanyooka na kurudi kule ambako tulikwepa naye si mwingine ni Mzee Joseph Butiku.... (dRU)
ReplyDeleteMheshimiwa naibu waziri wa bunge letu tukufu anafaa sana kwa nafasi hiyo.
ReplyDeleteMIMI NINGEMPA BASIL MRAMBA. Sababu ni moja tuu. Tayari ameshashiba kwa hiyo atapenda na nchi nzima washibe.
ReplyDeleteHawa wanaotajwa tajwa yaani Mizengo Pinda, Kimiti, Membe sijua wana historia gani nzuri huko nyuma inayoweza kuwapa uwaziri.
Mramba ana national interests katika moyo wake, that is why he is more accepted in Mbeya than in Rombo where he was born.
Waingereza wana msemo usemao kwamba "BETTER THE DEVIL YOU KNOW, THAN THE ANGEL YOU DON'T KNOW.
Ningempa Chibulunje
ReplyDeleteMIZENGO PINDA,anafaa kwa sababu hana mauchafu ya ufisadi na ameweza kuzibana Halmashauri vizuri
ReplyDeletemagufuli ndo awekwe hapo.........
ReplyDeleteKWA UFUPI NI NGUMU SANA.MAY BE ACHAGULIWE MTU AMBAYE HAYUPO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI LILILOPO.COZ WALIOPO WOTE NI HAO HAO, HATUNA IMANI NAO
ReplyDeleteaaaah hamna wa kuchukua hiyo nafasi labda dr slaa!!!!
ReplyDeleteKama ingekuwa mimi ni JK ningemtetua mtu aliye nje kabisa ya hilo Bunge kwa kumteua kama Mbunge kwani bado nina nafasi ya kati ya wabunge kumi. Kisha ndio ningewaambia wananchi huyu hapa niliyemteua kuwa mbunge ndiye atakayekuwa PM.
ReplyDelete1. Mbunge wa kuteuliwa na Rais hana Jimbo hivyo hatakuwa na upendeleo wa jimbo lake la uchaguzi ili asikose kura.
2. Atakuwa bado hajaingiwa na kirusi kilichowavaa wabunge cha kuanza kutafuta kura kwenye majimbo yao hivyo atafanya kazi zake kwa uhakika
3.Atakuwa hatoki katika kundi lolote kati ya makundi yaliyopo bungeni, hili kundi la huyu na hili kundi la yule, hivyo basi ataweza kufanya kazi kiuadilifu.
4. Kwa kuwa ndiye atakuwa anaanza kazi ya uwaziri kwa mara ya kwanza atakuja na utaratibu mpya wa uongozi yaani sitataka kutia mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya. Ataleta changamoto kwa mawaziri wengine kwani kutakuwa hakuna kujuana hapo.
5. Huyu mtu atakayetoka nje ya hawa wabunge na mawaziri waliopita sitakuwa na wasi wasi wa kuhusika kwake na kashfa ya Buzwagi wala ya BoT ambayo uchunguzi bado unaendelea hivyo nitakuwa nina uhakika yuko Ok.
6. Wananchi watashangaa sana na uamuzi wangu kwani nitamchagua mtu ambaye hajulikani kabisa na wala hatamtegemea, wakati wakiendelea kushangaa na wapinzani wakiendelea kutafuta kama ana skandali siku hazigandi zinazonga mbele.
Hayo ndiyo yangekuwa maamuzi yangu kama ningekuwa mie ndie JK.
Subira
amweke salim ahmed salim
ReplyDelete1. Dr. Harrison Mwakyembe
ReplyDelete2. Magufuli
Yoyote kati ya hao wanafaa.
NB: By the way, umetumwa na JK nini?
Would go for Hon John Malecela ama amrudishe Asho Rose Migiro
ReplyDeleteHapo bwana wote waliotaja sidhani,
ReplyDeleteYe atafute jamaa tu wa mtaani,
ampe ubunge na kisha uwaziri.
Hao kina magufuli ndio wale wale waliuza nyumba za serikali.
Mi niko tayari hata niwe mimi, maana mi hua simuaminigi kabisa mtu,
anaingia jamaa saaaafi na kupigiwa kura kibao tu kama Edo lakin then anaharibu baadae,
hapo hapamfai mtu mwingine zaidi ya mimi tu.
Zaidi zaidi napatikana Maskani kwangu, K-Nyama,
email shqeir81@hotmail.com
Kama KATIBA ingeruhusu ningemchagua Asha Rose Migiro.NUKTA!
ReplyDeleteMtikila anafaa. Yeye na Lwakatare watafanikiwa kulifanya bunge kuwa kanisa na baadae taifa zima kuwa la kikristo.
ReplyDeleteNingependekeza Magufuli kwa sababu ya rekodi yake kiutendaji kuanzia awamu ya tatu.
ReplyDeleteMama JOYCE KAFANABO.Afisa ubalozini USA
ReplyDelete-Shule imetulia
-Makini kuliko unavyodhani.
-Ana convincing power yya hali ya juu.
Naona anayefaa kwa nafasi hii kabisa ni Wilson Masilingi. huyu bwana ni mchapa kazi sana na si fisadi hata kidogo. Alifanya kazi nzuri sana alipokuwa Waziri wa nchi ofisi ya rais Utawala Bora wakati wa Mkapa, alipambana sana na mafisadi mpaka wakamchukia; hakuwa na simile nao, atafaa sana sehemu hiyo, ni mwanasheria; atahakikisha haipiti mikataba ya kihuni. Madini na Nishati apewe Dr. Mwakyembe halafu Ardhi abaki Magufuli maana bado pana uozo mwingi alioanza kuondoa; aendelee na kumalizia kabisa.
ReplyDeleteNawakilisha.
Nashauri PM ateuliwe nje ya baraza lililopo sasa manake,baraza lililopo likiundiwa Tume ni aibu hakuna ambaye si fisadi.Maghufuli hafai aliuza nyumba za Serikali
ReplyDeleteSalim Ahmed SALIM
ReplyDeleteTuna tabia ya kuamini kuwa majina ni yale yale. Sasa hivi mtu atasema Malecela. Naungana na wale wanaotaka jina litoke nje ya uozo. Kama mimi ningekuwa natawala dunia - ningetoa ruhusa JK atafute mtu kokote hata kama itabidi kumuomba Barrack Obama akikosa urais wa Amerika aje achukue mkataba wa uwaziri mkuu kwa miaka mitano. Tunataka uzalendo mara unatushinda. Kuna faida gani kuwa na gavana wa benki kama Balali au waziri mkuu kibaka - si bora tukamwomba hata George Weah aje asaidie - siku moja moja atakuwa anaweza kusaidia kufundisha Stars.
ReplyDeleteKWA UPANDE WANGU MIMI NINGEONA BORA GETRUDE MONGELLA KUNA WA KINA BATILDA NA MWENGINE TU NAWAKIKA HIKI NI KIPINDI SIOCHA KUFANYA MAJARIBIO TENA NI WAKATI WAKUFANYA MABADILIKO SISI WANAWAKE NI WATU WAMSIMAMO SANA TOFAUTI YA WANAUME WAO WANACHUKULIA WAKIPATA AJIRA ITATATUA MATATIZO YA UKOO MZIMA MPAKA NYUMBA NDOGO PIA.KAMA KWELI JK AKIMPA MTU KAMA MAMA MONGELLA SHE WILL DO WONDERS,JK PLS BADILISHA SURA ZOTE ZA WATU WALIOKWENYE CABINNET BILA MANUFAA YOYOTE KAMA KAPUYA NA WENGINE WENGI TU WATU TUNGEPENDA WABAKI MFANO MAGUFULI TULIONA KAZI YAKE NA NDIO TUNATAKA SIO WATU WANAWEKWA WIZARANI KUKAMA PICHA YA ASKARI WA SAMORA AVENUE.MZEE NGOMBALE MWILU MIMI SI MIND AKIPEWO MAANA YULE NI KICHWA SANA KWA SISI BABA ZETU WALIYOKAA SERIKALINI MUDA MREFU TUNAELEWA NADHANI
ReplyDeleteSALIM AHMED SALIM
ReplyDeleteMi naona Salim Ahmend Salim, itakumbukwa alivyokuwa waziri mkuu watu wote walifurahia
ReplyDeleteMAMA KIKWETE
ReplyDeleteMagufuli mzee anamaanisha kweli kweli
ReplyDeleteTo restore the Goverment Credibility I do believe the only person who can do good job of which afterall I believe he should be the current prezo is Salim Ahmed Salim. Those people who refused to endorse him in the first place knew exactly what they were after.
ReplyDeleteNi ngumu sana ukizingatia uwezo na uadilifu maana mara nyingi haviendi pamoja,lakini kwa kuzingatia msemo wa Kihaya '' Abafu bakilana ukunuka" maana yake ni kuwa hata maiti uzidiana kunuka, so ningempa B. Membe by I. M.K Theonest
ReplyDeleteMrema
ReplyDeleteStephen Wassira
ReplyDeleteMbona Rostam Aziz hajawajibika???????????????????
ReplyDeleteKwakweli hapa ni pagumu kiasi ingawa at the end of the day lazima PM apatikane.
ReplyDeleteKwa sasa mtazamo wangu unaangukia kwa wasomi kuchukua hii nafasi kwa kweli na wawe wenye sifa nzuri kutokana na historia zao. vichwa viko vingi tu bungeni na najua hii itakuwa ni kazi kubwa kwa JK kuchagua kutokana na kuwa vichwa vya maana humo bungeni.PM si lazima awe mtu aliesheheni sifa za kisiasa.Cha muhimu ni uadilifu,mchapa kazi kwa kuzingatia experience aidha kiuongozi,kielimu,kisiasa etc. Hapa pia suala la URAFIKI likiingia tena lazima tutarudi tena kule kule tulipo sasa. Kuna watu kama wakina:
*Magufuli
*Mwandosya
*Mwakyembe
*Salim Ahmed Salim(ingawa si mbunge ila nafasi 10 hazijajaa bado)
na wengineo wengi tu ila hao kwa uchache wao tu wangefaa.
Ila kazi ipo kweli kweli katika hili.....
Mdau mpenda nchi
Katiba inasema kuwa waziri mkuu lazima atokane miongoni mwa wabunge wa kuchaguliwa na si wa kuteuliwa, yaan lazima atoke jimboni na si vinginevyo. so take note waka tukipendekeza PM mpya
ReplyDeleteJohn "Matingas" Maghufuli,
ReplyDeletesababu ameonyesha ujasiri akiwa wizara ya ujenzi na sasa ardhi.
Naomba kuwakumbusha jamani kwa mujibu wa katiba yetu waziri mkuu lazima awe mbunge tena wa kuchaguliwa sio kuteuliwa. So mama Rwakatatre is completely disqualified. Mimi nisingemteua Mizengo Pinda kwani yeye juzi ndio karidhia kuuzwa kwa mwekezaji kwa uwanja wa Nyamagana Mwanza,anaweza kuuza hata ikulu.
ReplyDeleteNingempa UPM.Dr.Shukuru Kawambwa.
MICHUZI ANAFAA
ReplyDeleteMICHUZI UMETUPATA KWELI YANI KISWALI CHA UZUSHI HALAFU MAONI YASHAFIKA 35, UMETUSHIKA AKILI ZETU NIMEGUNDUA, SASA ITABIDI UANZISHE KANISA KABISA MANAKE WAFUASI WENGI.
ReplyDeleteJakaya kama ana busara atamweka Salim ahmed Salim - Kipenzi cha wengi!
ReplyDeleteMwandosya pia anafaa
ReplyDeleteAnna Malecela, MB
ReplyDeleteSalim Ahmed Salim
ReplyDeleteWote naona hamfwatilii "breaking news" za dk chache zilizopita. JK ameshanichagua mimi kuwa Waziri Mkuu nitaapishwa hivi karibuni.
ReplyDeleteSALIM AHMED SALIM
ReplyDeleteHuyu ana uzoefu,
ana ujuzi,
anajulikana pote duniani,
anakubalika na wananchi wote (hata wapinzani),
ana uchungu na nchi yetu, anaheshimika...unaweza kuendelea mpaka kesho asubuhi....
Sidhani kama kuna mwingine ana masifa kem kem kama Salim Ahmed Salim!!!
SINA MENGI YA KUSEMA LAKINI NI WAKATI MUHAFAKA WA KUWA NA SERIKALI YA MSETO.
ReplyDeleteMAGEUZI INABIDI WAKAE HIYO NAFASI..
ReplyDeleteMBOWE AU AMUWEKE SALMA MKEWE KABISA.
Naona mzaha umezidi. But n a very serious note Issa Michuzi:
ReplyDeleteWaziri Mkuu: Dr. Mwakyambe
Waziri wa Fedha: Dr. Kimei
Waziri wa Madini: Dr. Idrisa Rashid
Waziri wa Ulinzi: Waitara
Waziri wa Nje: Lukuvi
Waziri wa Miundombinu: Samson Luhigo
Waziri wa Sheria: Pr. Othman
Waziri wa Ardhi: Anne Kilango
Waziri wa Habari: Jenerali Ulimwengu
Ngwanawane PM ni Magufuli tu nchi hii kama tunataka iende mbele
ReplyDeletetwende mbele turudi nyuma, kuna mtu mmoja tu anatufaa kama tunataka kuwa na serikari bora, tuombe Mungu J.K atupatie MAGUFULI ili atunyooshee viongozi walio lala huu sio wakati wa kuchagua mtu kuwa P.M kwasababu ya ushabiki na urafiki au muonekano wa sura. Tunataka mtu mwajibikaji, Mtu Huyo ni J. P. Magufuli tu!!!
ReplyDeletewadau, naomba m-confirm aliyosema mimi hapo juu. ni kweli kwamba ili kuwa waziri MKUU ni lazima awe mbunge. lakini ni lazima awe mbunge
ReplyDeletewa KUCHAGULIWA na sio wa KUTEULIWA?
Naomba muongozo....!
MUHIDIN ISSA MICHUZI FOR PRIME MINISTER!!!
ReplyDeleteJamani JK kazi anayo, inabidi atulize kichwa kwanza,maana kwa bongo viongozi wengi ni wezi, ni vigumu kumjua kwa uhakika haswa ni yupi mzuri nyupi ni mwizi, Jaribu kubahati labda tutafika.
ReplyDeletePlz naomba awe PETER KAYANDA PINDA
ReplyDeleteHuyu mtu ana sifa zifuatazo:
1)Mchapa kazi
2)Mkweli sana
3)Mchapa kazi
4)Analijua bunge vizuri
5)Ana nidhamu na mtiifu
6)Mcha Mungu ile mbaya
Tuazime kutoka japani, kuna waziri mmoja kule hana kazi anaitwa KAHARISHA KANAWA, anaweza kutufaa huyu.
ReplyDeleteMichuzi inabidi utoe zawadi kwa wale waliootea sawia.
ReplyDeleteHuyuki wa Ngekewa.
ReplyDeleteKesha chaguliwa
ReplyDeleteMIE NAONA BORA ANGEPEWA UWAZIRI ISSAH MICHUZI..ANAFANYA KAZI NZURI SANA HUYU KIJANA..
ReplyDeleteMDAU NORWAY