MDAU, JE WEWE UNGEKUWA JK UNGEMCHAGUA NANI KUWA WAZIRI MKUU NA KWA SABABU GANI?
CHONDE CHONDE WADAU HILI SI SHINDANO WALA HAPA SI MAHALA PA KUONDOLEA DONGE. TUJADILI KWA KINA BILA YA KUCHAFUA HALI YA HEWA AMA KUMTIA MTU DOLE JICHONI..
NAWASILISHA ILI KUPOTEZA MUDA WAKATI TUKISUBIRI FAINALI...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 80 mpaka sasa

  1. Mizengo Pinda for PM post

    au

    Dr. Harrison Mwakyembe, hiki kichwa nakikubari toka enzi zake za UDSM

    ReplyDelete
  2. Professor Ibrahim Lipumba...in the interest of national unity!!!

    ReplyDelete
  3. Ningekuwa JK ningemchangua Mwandosya kuwa waziri mkuu na Magufuri kuwa waziri wa nishati na madini.

    Mzee wa TBS

    ReplyDelete
  4. Mh Doctor Mch Askofu Mama Getrude Lwakatare:
    SIFA
    1.Ana mvuto
    2.Hajidai
    3.Mcha Mungu
    4.Ana sauti yenye kujaa ushawishi(Kiongozi)
    5.Ni tajiri (hatakuja kuwa fisadi)
    6.Tangu aingie bungeni wabunge wote sasa wanamkumbuka wanamtaja Mungu ( Mfano:-Kilontsi Mporogomyi,Simbachawene,Mama Anne Killango,Maulida Komu,Ndesamburo na hata waliotuhumiwa ufisadi (LOWASSA,KARAMAGI NA MSABAHA)

    Mpendakeroro@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. ningekuwa mimi na kama katiba inaruhusu kufanya hivyo kwa kuteua wapinzani, basi ningempa mpenda nchi mmoja "Dr. Wilbroad Slaa" na madini ningemweka Zitto Zuberi Kabwe! nukta, hao wengine ningefumba macho na kutaja tu, lakini majina yao yote ningeyaandika kwa penseli ili iwe rahisi kuwafuta kazi pasipo kusubiri tume teule kama hivi!

    ReplyDelete
  6. Ningemchagua Mark Mwandosya, nina imani kuwa atasaidia sana katika kuendesha serikali haswa katika kipindi hichi ambapo imekumbwa na matatizo. Na pia atakuwa amesoma kutokana na kilochotokea kwa hivyo atakuwa na tahadhari kubwa.

    ReplyDelete
  7. Duhh!! Hapo kazi ipo... Unaona sasa, Michuzi mimi nilikuuliza kwanini umeenda Zanzibar wakati kama huu! Wewe mdau wetu wa kijiweni, kura tayari zaidi ya mil.3 ungepita tu! au ndo utaunganisha boti mpaka Pemba kwa wajuzi? Sasa na vile spika 6 tena amemwaga hazalani ya kuwa watu wajisafishe mimi naona Mhe Lwakatare maana yeye tayari msafi au vipi, au hata Mhe Kilango-Malecela sababu yeye alikuwa tayari kumtosa hata mumewe kwaajili ya siasa. Nimeona badala ya wewe basi awe mwanamke maana katika ripoti nzima ya Richmonduli hakuna hata mwanamke wa kusingiziwa... Na hivi kule USA atashinda Mama, basi mwaka huu uwe wa wakinamama tu!!!

    Kinamama Oye!!!

    ReplyDelete
  8. Mimi nigekuwa JK ningemteua Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri(TAMISEMI) Mh.Mizengo Kayanda Pinda(MB) kuwa waziri mkuu mpya.Sababu ni hivi zifuatazo.
    1.Kitaaluma ni mwanasheria hivyo naamini anaweza kutumia taaluma yake kubaini mambo mengi ambayo yataonekana kuwa yanakinzana na sheria za nchi na hivyo kuepusha kuliingiza taifa kwenye matatizo yasiyokuwa ya lazima.
    2.Amewahi kuwa afisa mwandamizi wa idara ya usalama wa taifa pale Ikulu kabla ya kwenda kugombea ubunge kwao huo Mpanda mwaka 1995.Kuwa katika idara hii ni imani kutamuweza kuwa upeo mkubwa wa kushushtua dili fekifeki mapema na kuchukua hatua haraka.
    3.Alipochaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya kwanza 1995,Rais Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI chini ya waziri mzee Kingunge.Hapa ndipo wafuatiliaji wa mambo tulipogundua kuwa anaonyesha dalili za kuja kuwa kiongozi makini sana kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao katika kujenga hoja alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge.
    4.Mwaka 2000 aliteuliwa tena kuendelea na nafasi yake hiyo hiyo chini ya Mh.Brig.Ngwilizi.Kwa kuwa tayari alishakuwa na uzoefu wa miaka 5 katika wizara hiyo,Mh.Pinda alizidi kuonyesha uwezo mkubwa sana kiasi ambacho wachambuzi wa siasa tuligundua kuwa alikuwa na uwezo hata kumzidi waziri wake.
    5.2005 Rais JK kwakuwa alikuwa ameshauona uwezo wake kwa kipindi cha miaka 10,kama naibu waziri,akampandisha kuwa waziri kamili.
    6.Sasa hoja yangu ni kwamba kwa wanaojua dhamana ya waziri mkuu katika mfumo wa serikali yetu,ni kwamba yeye ndiye msimamizi mkuu wa sera za serikali.Na sera za serikali zinatekelezwa kwa asilimia 90 na TAMISEMI.Kwa hiyomuhimu sana kuwa na mtu mwenye uzoefu na masuala ya serikali za mitaa na tawala za mikoa.Kwa lugha nyepesi,TAMISEMI ndio serikali yenyewe.Hakuna wizara isiyofanya kazi na TAMISEMIukiondoa,mambo ya nje,Ulinzi,na mambo ya ndani.

    Naomba kuwakilisha,
    Kada-Ohio

    ReplyDelete
  9. Mkuu naona bora tu ampe mama Malecela maana hana mchezo na mafisadi hata kama angekuwa mshua wake mzee kilango angemkaanga..
    Big Up mama zetu.
    Ben Dar

    ReplyDelete
  10. Bro Michu
    Samahani najua hii sio mwake hapa, ila nasikia na Hosea nae kapeleka barua ya kaachia ngazi? Taarifa za kweli hizi?

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli ki haki lilah michu mi simuoni hasa ni nani mana nachelea kwa kuona wote ndo walewale walokunywa uji wa mgonjwa.

    kwa mbaaaali ingekua dr sheni si mgombea mweza ingekua afadhali yake mara kumi na mbili.

    Hili swala ni zitto zitto mr michu kuamua

    ReplyDelete
  12. JOHN MAGUFULI.

    HUYU AMEONYESHA UJASIRI MKUBWA KWENYE WIZARA ILIYOJAA UOZO YA ARDHI. PIA HAOGOPI KUSEMA PALE INAPOTAKIWA KUSEMA. KWA MFANO JUZIJUZI MBELE YA RAIS ALIWA-CHALLENGE MAWAZIRI WENZAKE WA MAJI NA MIUNDOMBINU JINSI AMBAVYO HAWATOI USHIRIKIANO WA KUTOSHA KWENYE UJENZI WA NYUMBA HUKO KARIBU NA CHALINZE

    MAWAZIRI ALIO-WACHALLENGE WALILALAMIKA, LAKINI SISI WANANCHI(AMBAO SI WADANGANYIKA TENA) TULIMUUNGA MKONO NA TUNA MUUNGA MKONO NA TUNATAKA AWE NA UWEZO KAMA WAZIRI MKUU KUWATAKA WAFANYE KAZI KULINUSURU TAIFA LETU.

    MAGUFULI ALL THE WAY....

    ReplyDelete
  13. MIMI namuona MAGUFULI ndiye anayefaa kuwa waziri Mkuu.

    Ni Mchapa kazi, hana kashfa sana kama wengine.

    ReplyDelete
  14. MAGUFULI BABAAKE!

    ReplyDelete
  15. jina jipya kabisa na wala sio kutoka katika cabinet, kwa hiyo liwe jina jipya kabisa.

    ReplyDelete
  16. Mimi kwakweli ningempendekeza Mzee Mizengo Pinda.
    Pamoja na uzoefu, sijasikia kujihusisha au kuhusika kwake katika kashfa yeyote ile.
    Naomba kutoa hoja

    ReplyDelete
  17. HAYA YOTE NI MASKANDAL, YANA BASHASHA ZAKE KATIKA SIASA. akrm

    ReplyDelete
  18. Mie napendekeza waziri mkuu awekwe BALALI sababu ndio kawaida na desturi ya serkali ya CCM anaeharibu wizara hii hupelekwa wizara nyengine!Na bwana Edo (edward lowasa)nae sasa apewe uwaziri wa fedha.

    Michu usibanie, kuna falsa katika hili, na utaona, japo haitakuwa hivyo lakini haitatofautiana na hivyo.

    ReplyDelete
  19. Bernard Membe

    ReplyDelete
  20. Jamani prime minister sio lazima awe mwana siasa awe mtu mwenye experience ya management for over 10 years , i know salim ahmed salim ni mwanasiasa lakini i think he has experience and exposure najua sio mbunge ila anaweza pendekezwa

    Williamtz

    ReplyDelete
  21. kwangu ni Dk. Wilbroad slaa,

    kama mpinzani hatakiwi basi hata Kilango Anne Malecela,

    Ni mama jasiri na asiependa Unyonyaji,

    Wala hana U-CCM zaidi ya kujali maslahi ya wananchi na kuchukia ufisadi.

    Pia Simbachawene nae anafaa

    ReplyDelete
  22. JK hatakua na kazi kubwa sana kama atamfanya MBUNGE WA KUTEULIWA halafu akamvika kofia ya UWAZIRI MKUU.... Mambo yote yatanyooka na kurudi kule ambako tulikwepa naye si mwingine ni Mzee Joseph Butiku.... (dRU)

    ReplyDelete
  23. Mheshimiwa naibu waziri wa bunge letu tukufu anafaa sana kwa nafasi hiyo.

    ReplyDelete
  24. MIMI NINGEMPA BASIL MRAMBA. Sababu ni moja tuu. Tayari ameshashiba kwa hiyo atapenda na nchi nzima washibe.

    Hawa wanaotajwa tajwa yaani Mizengo Pinda, Kimiti, Membe sijua wana historia gani nzuri huko nyuma inayoweza kuwapa uwaziri.

    Mramba ana national interests katika moyo wake, that is why he is more accepted in Mbeya than in Rombo where he was born.

    Waingereza wana msemo usemao kwamba "BETTER THE DEVIL YOU KNOW, THAN THE ANGEL YOU DON'T KNOW.

    ReplyDelete
  25. Ningempa Chibulunje

    ReplyDelete
  26. MIZENGO PINDA,anafaa kwa sababu hana mauchafu ya ufisadi na ameweza kuzibana Halmashauri vizuri

    ReplyDelete
  27. magufuli ndo awekwe hapo.........

    ReplyDelete
  28. KWA UFUPI NI NGUMU SANA.MAY BE ACHAGULIWE MTU AMBAYE HAYUPO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI LILILOPO.COZ WALIOPO WOTE NI HAO HAO, HATUNA IMANI NAO

    ReplyDelete
  29. aaaah hamna wa kuchukua hiyo nafasi labda dr slaa!!!!

    ReplyDelete
  30. Kama ingekuwa mimi ni JK ningemtetua mtu aliye nje kabisa ya hilo Bunge kwa kumteua kama Mbunge kwani bado nina nafasi ya kati ya wabunge kumi. Kisha ndio ningewaambia wananchi huyu hapa niliyemteua kuwa mbunge ndiye atakayekuwa PM.

    1. Mbunge wa kuteuliwa na Rais hana Jimbo hivyo hatakuwa na upendeleo wa jimbo lake la uchaguzi ili asikose kura.
    2. Atakuwa bado hajaingiwa na kirusi kilichowavaa wabunge cha kuanza kutafuta kura kwenye majimbo yao hivyo atafanya kazi zake kwa uhakika
    3.Atakuwa hatoki katika kundi lolote kati ya makundi yaliyopo bungeni, hili kundi la huyu na hili kundi la yule, hivyo basi ataweza kufanya kazi kiuadilifu.
    4. Kwa kuwa ndiye atakuwa anaanza kazi ya uwaziri kwa mara ya kwanza atakuja na utaratibu mpya wa uongozi yaani sitataka kutia mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya. Ataleta changamoto kwa mawaziri wengine kwani kutakuwa hakuna kujuana hapo.
    5. Huyu mtu atakayetoka nje ya hawa wabunge na mawaziri waliopita sitakuwa na wasi wasi wa kuhusika kwake na kashfa ya Buzwagi wala ya BoT ambayo uchunguzi bado unaendelea hivyo nitakuwa nina uhakika yuko Ok.
    6. Wananchi watashangaa sana na uamuzi wangu kwani nitamchagua mtu ambaye hajulikani kabisa na wala hatamtegemea, wakati wakiendelea kushangaa na wapinzani wakiendelea kutafuta kama ana skandali siku hazigandi zinazonga mbele.

    Hayo ndiyo yangekuwa maamuzi yangu kama ningekuwa mie ndie JK.

    Subira

    ReplyDelete
  31. amweke salim ahmed salim

    ReplyDelete
  32. 1. Dr. Harrison Mwakyembe
    2. Magufuli

    Yoyote kati ya hao wanafaa.

    NB: By the way, umetumwa na JK nini?

    ReplyDelete
  33. Would go for Hon John Malecela ama amrudishe Asho Rose Migiro

    ReplyDelete
  34. Hapo bwana wote waliotaja sidhani,

    Ye atafute jamaa tu wa mtaani,
    ampe ubunge na kisha uwaziri.

    Hao kina magufuli ndio wale wale waliuza nyumba za serikali.

    Mi niko tayari hata niwe mimi, maana mi hua simuaminigi kabisa mtu,

    anaingia jamaa saaaafi na kupigiwa kura kibao tu kama Edo lakin then anaharibu baadae,

    hapo hapamfai mtu mwingine zaidi ya mimi tu.

    Zaidi zaidi napatikana Maskani kwangu, K-Nyama,

    email shqeir81@hotmail.com

    ReplyDelete
  35. Kama KATIBA ingeruhusu ningemchagua Asha Rose Migiro.NUKTA!

    ReplyDelete
  36. Mtikila anafaa. Yeye na Lwakatare watafanikiwa kulifanya bunge kuwa kanisa na baadae taifa zima kuwa la kikristo.

    ReplyDelete
  37. Ningependekeza Magufuli kwa sababu ya rekodi yake kiutendaji kuanzia awamu ya tatu.

    ReplyDelete
  38. Mama JOYCE KAFANABO.Afisa ubalozini USA
    -Shule imetulia
    -Makini kuliko unavyodhani.
    -Ana convincing power yya hali ya juu.

    ReplyDelete
  39. Naona anayefaa kwa nafasi hii kabisa ni Wilson Masilingi. huyu bwana ni mchapa kazi sana na si fisadi hata kidogo. Alifanya kazi nzuri sana alipokuwa Waziri wa nchi ofisi ya rais Utawala Bora wakati wa Mkapa, alipambana sana na mafisadi mpaka wakamchukia; hakuwa na simile nao, atafaa sana sehemu hiyo, ni mwanasheria; atahakikisha haipiti mikataba ya kihuni. Madini na Nishati apewe Dr. Mwakyembe halafu Ardhi abaki Magufuli maana bado pana uozo mwingi alioanza kuondoa; aendelee na kumalizia kabisa.

    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  40. Nashauri PM ateuliwe nje ya baraza lililopo sasa manake,baraza lililopo likiundiwa Tume ni aibu hakuna ambaye si fisadi.Maghufuli hafai aliuza nyumba za Serikali

    ReplyDelete
  41. Salim Ahmed SALIM

    ReplyDelete
  42. Tuna tabia ya kuamini kuwa majina ni yale yale. Sasa hivi mtu atasema Malecela. Naungana na wale wanaotaka jina litoke nje ya uozo. Kama mimi ningekuwa natawala dunia - ningetoa ruhusa JK atafute mtu kokote hata kama itabidi kumuomba Barrack Obama akikosa urais wa Amerika aje achukue mkataba wa uwaziri mkuu kwa miaka mitano. Tunataka uzalendo mara unatushinda. Kuna faida gani kuwa na gavana wa benki kama Balali au waziri mkuu kibaka - si bora tukamwomba hata George Weah aje asaidie - siku moja moja atakuwa anaweza kusaidia kufundisha Stars.

    ReplyDelete
  43. KWA UPANDE WANGU MIMI NINGEONA BORA GETRUDE MONGELLA KUNA WA KINA BATILDA NA MWENGINE TU NAWAKIKA HIKI NI KIPINDI SIOCHA KUFANYA MAJARIBIO TENA NI WAKATI WAKUFANYA MABADILIKO SISI WANAWAKE NI WATU WAMSIMAMO SANA TOFAUTI YA WANAUME WAO WANACHUKULIA WAKIPATA AJIRA ITATATUA MATATIZO YA UKOO MZIMA MPAKA NYUMBA NDOGO PIA.KAMA KWELI JK AKIMPA MTU KAMA MAMA MONGELLA SHE WILL DO WONDERS,JK PLS BADILISHA SURA ZOTE ZA WATU WALIOKWENYE CABINNET BILA MANUFAA YOYOTE KAMA KAPUYA NA WENGINE WENGI TU WATU TUNGEPENDA WABAKI MFANO MAGUFULI TULIONA KAZI YAKE NA NDIO TUNATAKA SIO WATU WANAWEKWA WIZARANI KUKAMA PICHA YA ASKARI WA SAMORA AVENUE.MZEE NGOMBALE MWILU MIMI SI MIND AKIPEWO MAANA YULE NI KICHWA SANA KWA SISI BABA ZETU WALIYOKAA SERIKALINI MUDA MREFU TUNAELEWA NADHANI

    ReplyDelete
  44. SALIM AHMED SALIM

    ReplyDelete
  45. Mi naona Salim Ahmend Salim, itakumbukwa alivyokuwa waziri mkuu watu wote walifurahia

    ReplyDelete
  46. MAMA KIKWETE

    ReplyDelete
  47. Magufuli mzee anamaanisha kweli kweli

    ReplyDelete
  48. To restore the Goverment Credibility I do believe the only person who can do good job of which afterall I believe he should be the current prezo is Salim Ahmed Salim. Those people who refused to endorse him in the first place knew exactly what they were after.

    ReplyDelete
  49. Ni ngumu sana ukizingatia uwezo na uadilifu maana mara nyingi haviendi pamoja,lakini kwa kuzingatia msemo wa Kihaya '' Abafu bakilana ukunuka" maana yake ni kuwa hata maiti uzidiana kunuka, so ningempa B. Membe by I. M.K Theonest

    ReplyDelete
  50. Stephen Wassira

    ReplyDelete
  51. Mbona Rostam Aziz hajawajibika???????????????????

    ReplyDelete
  52. Kwakweli hapa ni pagumu kiasi ingawa at the end of the day lazima PM apatikane.
    Kwa sasa mtazamo wangu unaangukia kwa wasomi kuchukua hii nafasi kwa kweli na wawe wenye sifa nzuri kutokana na historia zao. vichwa viko vingi tu bungeni na najua hii itakuwa ni kazi kubwa kwa JK kuchagua kutokana na kuwa vichwa vya maana humo bungeni.PM si lazima awe mtu aliesheheni sifa za kisiasa.Cha muhimu ni uadilifu,mchapa kazi kwa kuzingatia experience aidha kiuongozi,kielimu,kisiasa etc. Hapa pia suala la URAFIKI likiingia tena lazima tutarudi tena kule kule tulipo sasa. Kuna watu kama wakina:

    *Magufuli
    *Mwandosya
    *Mwakyembe
    *Salim Ahmed Salim(ingawa si mbunge ila nafasi 10 hazijajaa bado)
    na wengineo wengi tu ila hao kwa uchache wao tu wangefaa.

    Ila kazi ipo kweli kweli katika hili.....

    Mdau mpenda nchi

    ReplyDelete
  53. Katiba inasema kuwa waziri mkuu lazima atokane miongoni mwa wabunge wa kuchaguliwa na si wa kuteuliwa, yaan lazima atoke jimboni na si vinginevyo. so take note waka tukipendekeza PM mpya

    ReplyDelete
  54. John "Matingas" Maghufuli,
    sababu ameonyesha ujasiri akiwa wizara ya ujenzi na sasa ardhi.

    ReplyDelete
  55. Naomba kuwakumbusha jamani kwa mujibu wa katiba yetu waziri mkuu lazima awe mbunge tena wa kuchaguliwa sio kuteuliwa. So mama Rwakatatre is completely disqualified. Mimi nisingemteua Mizengo Pinda kwani yeye juzi ndio karidhia kuuzwa kwa mwekezaji kwa uwanja wa Nyamagana Mwanza,anaweza kuuza hata ikulu.

    Ningempa UPM.Dr.Shukuru Kawambwa.

    ReplyDelete
  56. MICHUZI ANAFAA

    ReplyDelete
  57. MICHUZI UMETUPATA KWELI YANI KISWALI CHA UZUSHI HALAFU MAONI YASHAFIKA 35, UMETUSHIKA AKILI ZETU NIMEGUNDUA, SASA ITABIDI UANZISHE KANISA KABISA MANAKE WAFUASI WENGI.

    ReplyDelete
  58. Jakaya kama ana busara atamweka Salim ahmed Salim - Kipenzi cha wengi!

    ReplyDelete
  59. Mwandosya pia anafaa

    ReplyDelete
  60. Anna Malecela, MB

    ReplyDelete
  61. Salim Ahmed Salim

    ReplyDelete
  62. Wote naona hamfwatilii "breaking news" za dk chache zilizopita. JK ameshanichagua mimi kuwa Waziri Mkuu nitaapishwa hivi karibuni.

    ReplyDelete
  63. SALIM AHMED SALIM

    Huyu ana uzoefu,
    ana ujuzi,
    anajulikana pote duniani,
    anakubalika na wananchi wote (hata wapinzani),
    ana uchungu na nchi yetu, anaheshimika...unaweza kuendelea mpaka kesho asubuhi....

    Sidhani kama kuna mwingine ana masifa kem kem kama Salim Ahmed Salim!!!

    ReplyDelete
  64. SINA MENGI YA KUSEMA LAKINI NI WAKATI MUHAFAKA WA KUWA NA SERIKALI YA MSETO.

    ReplyDelete
  65. MAGEUZI INABIDI WAKAE HIYO NAFASI..
    MBOWE AU AMUWEKE SALMA MKEWE KABISA.

    ReplyDelete
  66. Naona mzaha umezidi. But n a very serious note Issa Michuzi:

    Waziri Mkuu: Dr. Mwakyambe
    Waziri wa Fedha: Dr. Kimei
    Waziri wa Madini: Dr. Idrisa Rashid
    Waziri wa Ulinzi: Waitara
    Waziri wa Nje: Lukuvi
    Waziri wa Miundombinu: Samson Luhigo
    Waziri wa Sheria: Pr. Othman
    Waziri wa Ardhi: Anne Kilango
    Waziri wa Habari: Jenerali Ulimwengu

    ReplyDelete
  67. Ngwanawane PM ni Magufuli tu nchi hii kama tunataka iende mbele

    ReplyDelete
  68. twende mbele turudi nyuma, kuna mtu mmoja tu anatufaa kama tunataka kuwa na serikari bora, tuombe Mungu J.K atupatie MAGUFULI ili atunyooshee viongozi walio lala huu sio wakati wa kuchagua mtu kuwa P.M kwasababu ya ushabiki na urafiki au muonekano wa sura. Tunataka mtu mwajibikaji, Mtu Huyo ni J. P. Magufuli tu!!!

    ReplyDelete
  69. wadau, naomba m-confirm aliyosema mimi hapo juu. ni kweli kwamba ili kuwa waziri MKUU ni lazima awe mbunge. lakini ni lazima awe mbunge
    wa KUCHAGULIWA na sio wa KUTEULIWA?
    Naomba muongozo....!

    ReplyDelete
  70. MUHIDIN ISSA MICHUZI FOR PRIME MINISTER!!!

    ReplyDelete
  71. Jamani JK kazi anayo, inabidi atulize kichwa kwanza,maana kwa bongo viongozi wengi ni wezi, ni vigumu kumjua kwa uhakika haswa ni yupi mzuri nyupi ni mwizi, Jaribu kubahati labda tutafika.

    ReplyDelete
  72. Plz naomba awe PETER KAYANDA PINDA
    Huyu mtu ana sifa zifuatazo:
    1)Mchapa kazi
    2)Mkweli sana
    3)Mchapa kazi
    4)Analijua bunge vizuri
    5)Ana nidhamu na mtiifu
    6)Mcha Mungu ile mbaya

    ReplyDelete
  73. Tuazime kutoka japani, kuna waziri mmoja kule hana kazi anaitwa KAHARISHA KANAWA, anaweza kutufaa huyu.

    ReplyDelete
  74. Michuzi inabidi utoe zawadi kwa wale waliootea sawia.

    ReplyDelete
  75. Huyuki wa Ngekewa.

    ReplyDelete
  76. Kesha chaguliwa

    ReplyDelete
  77. MIE NAONA BORA ANGEPEWA UWAZIRI ISSAH MICHUZI..ANAFANYA KAZI NZURI SANA HUYU KIJANA..
    MDAU NORWAY

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...