waislamu wa dar na wanaharakati wameandamana leo mara tu baada ya sala ya ijumaa kupinga ujio wa rais wa marekani george bush ambaye katika ziara yake ya siku 7 nchini siku nne atakuwa bongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 67 mpaka sasa

  1. unamaana gani kusema katika ziara yake ya siku saba nchini siku nne atakuwa bongo? Bongo unamaana Dar-es-salaam

    ReplyDelete
  2. mbona kikwete alipoenda marekani hamkuandamana? watanzania acheni unafki.uvunjaji wa haki za binadamu upo tanzania kupitia mikataba feki inayowanyima watanzania kufaidi rasilimali zao. hilo hamlioni? ondoeni kibanzi kilichomo machoni mwenu kabla ya boriti iliyopo kwa wenzenu. unafki hautatufikisha popote.

    ReplyDelete
  3. Ukimkamata mmojawapo akutafsirie hayo mabango yaliyoandikwa kwa Kiinglishi mnaweza kukesha.

    ReplyDelete
  4. HALAFU NDO IWEJE?????????

    ReplyDelete
  5. Mmmmm kazi kweli kweli mtu anakuja kwa ajili ya maslahi ya Taifa na si mambo ya kidini, mmmm kazi ipo watanzania!!

    ReplyDelete
  6. Bush anakuja Tz kwa ziara ya Kiserikali na siyo kwa masuala ya kidini. Ninashindwa kuwaelewa hawa Waislamu wanaandamana nini. Huku ni kukosa uelewa na kufanya mambo kwa jazba. Tanzania haiongozwi kidini na wala serikali haina dini bali wananchi wake wanadini. Si waislamu tu ndio wanaujua marekani ni wavunjaji wa haki za binadamu.

    ReplyDelete
  7. Bush haji, bado hajaaambiwa tu?

    ReplyDelete
  8. Nje ya Topic lakini mbona hukutujulisha baraza la mawaziri la wapinzani?

    KIONGOZI wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamedi, ametangaza Baraza la Mawaziri Kivuli linalojumuisha wabunge wa upinzani

    Aliwataja mawaziri vivuli kwamba, yeye ataongoza Wizara ya Mipango na Fedha, akisaidiwa na Fatma Fereji.


    Waziri Kivuli wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Dk Willibrod Slaa, naibu wake Ania Chaurembo, wakati Sera, Uratibu na Bunge unashikwa na Halima Mdee.


    Shoka Khamis Juma anakuwa Waziri Kivuli wa Nchi, Utawala Bora na Waziri wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ni Grace Kiwelu.


    Wengine Waziri Kivuli wa Muungano ni Riziki Omar Juma, Waziri wa Mazingira, Chacha Wangwe, Afya ni Dk Ali Tarab Ali na naibu wake ni Omar Ali Mzee, Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni John Cheyo akisaidiwa na Ali Said Salim.


    Waziri Kivuli Elimu na Mafunzo ya Ufund ni Susan Lyimo, Naibu wake atakuwa Nuru Awadh Bafadhil na Waziri Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Said Amour Arfi.


    Zitto Kabwe ataongoza Wizara ya Miundombinu na atasaidiwa na Bakari Shamis Faki, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ni Mwanawetu Zarafi na Naibu wake ni Mohamed Ali Said na wakati Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Salim Abdulla Khalfani.


    Mhonga Ruhwanya, amepewa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Naibu wake, Mkiwa Adam Kiwanga, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imeenda kwa Salim Hemed Khamis akisaidiwa na Juma Said Omar.


    Waziri Kivuli Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto itakuwa chini ya Maulidah Anna Komu, wakati Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi itaongozwa na Mwadini Abbas Jecha na Naibu wake ni Ali Khamis Seif.


    Waziri Kivuli Maliasili na Utalii, Magdalena Sakaya, Mambo ya Ndani, Mohamed Ibrahim Sanya, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Khalifa S Khalifa, Nishati na Madini, Mohamed Habib Mnyaa, naibu wake na Savelina Mwijagwe.


    Wengine ni Waziri Kivuli Katiba na Sheria, Fatma Maghimbi, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Masoud Abdulla Salim, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Abuubakary Khamis Bakari, Viwanda, Biashara na Masoko, Lucy Owenya akisaidiwa na Khadija Salum Alli.

    ReplyDelete
  9. Waafrika ujinga tutaacha lini? Waarabu wakipigwa Palestina,Iraq,Iran,Afghhanstan n.k Waarabu dunia nzima huandamana na kuhamasisha waislamu dunia nzima ikiwemo Waislamu wa Tanzania wawaunge mkono.

    Waafrika wenzetu wakipigwa na Waarabu kule Sudan kusini,au Darfur huoni nchi za kiarabu zikitoa hata tamko la kulaani utawala wa waarabu wa Sudan na Janjaweed wa kiarabu wasiwaonee waafrika ngozi nyeusi wenzetu.

    Mfano Darfur ni Waislamu l weusi kama jaluo.Janjaweed ni waarabu na wanasaidiwa na Mwarabu Raisi wa Sudan lakini huoni tawala za kiarabu zikiandamana kwa niaba ya watu weusi wa Darfur na kuwatetea.Sana sana Marekani ndio unaona inainuka na kupeleka misaada ya kibinadamu kule.

    Pia hakuna haja ya kuilaani Marekani kwani watumwa weusi waliochukuliwa Marekani wakati wa Biashara vizazi vyao viko hadi leo (Afro Americans) walihifadhiwa hai na Marekani na wako hadi leo na ukiwauliza hadi nchi wanazotoka watakwambia lakini mamilioni ya waafrika weusi waliopelekwa Uarabuni wakati wa biashara ya utumwa wako wapi? Mbona hatuoni vizazi vyao kama wapo kwa mamilioni kama ambavyo Marekani bado wapo?

    Naogopa kuunga mkono Iraq,Iran,Afghastan n.k kwa sababu kama wao walifiwa kwa vita na marekani na sisi mamilioni ya bibi zetu waliteketezwa wakati wa utumwa huko uarabuni. Kila mtu alie msiba wake. Nimewakumbuka babu na bibi zako mamilioni waliofia Uarabuni waliouawa na waarabu.

    Nashukuru Marekani kwamba pamoja na kuendesha biashara ya utumwa walihifadhi hai hadi leo babu na bibi zetu weusi na tunao ndugu zetu weusi Marekani.

    KARIBU TANZANIA GEORGE BUSH MTU AMBAYE NCHI YAKO ILIWEKA HAI BABU NA BIBI ZETU TOFAUTI NA WAARABU WALIOWATEKETEZA VIZAZI VYETU WAKATI WA BIASHARA YA UTUMWA.

    TUPELEKEE SALAMU ZA ASANTE KWA WAMAREKANI WAAMBIE KUWA TUNASHUKURU KWA KUJALI UHAI NA KUWAWEKA HAI VIZAZI VYA BABU NA BIBI ZETU (AFRO AMERICANS).

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  10. DEMO.....SHOW'S WE IN RIGHT STEP TOWARD'S DEMOCRATIC COUNTRY......

    ReplyDelete
  11. Kingereza/Kizungu,

    Yani nafikiri watanzania wanaomba KiEnglish kingekuwa maji ya kunywa, basi kila mtu angekunywa halafu ingekuwa ni mtelemko tuu kila mtu ana flow,

    katika pitapita zangu nimekutana na hii, ni baadhi ya post za kwenye topic ya yule kaka wa Sydney alietoa pongezi kwa JK,

    sasa hichi ni kizungu au huyu mtu alifanya makusudi, siuandike kiswahili jamani.

    Tarehe Monday, February 11, 2008 7:32:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

    Mdau wa Sydney, you has got a point. Kikwete is vely hadwoking. Kikwete is the only people who can help us walking hard in bongo. Kikwete is vely hadwoking than anybody.

    I agree with you 100% that Kikwete is vely wisdom. Since he has been a president in this country we have seen kwite a gret development.

    My ferrow Tanzanians, lets walk hardest to build our national.

    Mimi Mdau Namba wani kutoka TIGO

    (Jiunge na TIGO. Tutawaletea poromosheni mpya nest wiek)

    NB. halafu ni mfanyakazi wa ofisini huyuu, yani mambo ya aibuu

    ReplyDelete
  12. 1.wengi pale hawajui wanapinga nini wanachokifanya ni kubebwa kwenye mkumbo ambao unanufaisha masheikh wachache wanaopata fedha kutoka nje
    2.Bush is coming for this country 4 all citizens uwe muslim o christian ametanguliza dola mil 700 akifika atasign millenium challenge goals funds
    3.ugomvi wa waarabu na bush ni wao sio wa waislam wote hao walishatufanya watumwa long tym all we need is an oportunity to exploit them
    4.Kikwete is a little bit soft labda tumwite liberal amewaachia watu watumie akili zao sio kupelekwapelekwa ndio maana kawaacha waandamane
    5.na wakristu wakiandamana kupinga ujio wa marais wakiarabu sijui ndio itakuwaje
    6.Bush amekuja kutembelea pia migodi yake kama barrick
    7.kiutalii tutapeta maana sasa hivi ukicheck cnn tangazo letu linaapper sana
    8.Kikwete nampongeza kwa kuwafanya watu akili zikue na kutoa mianya ya kufikiri na uexercise ujuzi wako ingawa maisha sasa yanakuwa magumu kwa sababu watu wanatumiwa

    ReplyDelete
  13. Wanachopinga ni nini hasa? Kwani Bush amesema anakuja kutembelea Waislam? Vipi, na wale wanaopenda aje nao waandamane na mabango yao?

    Kweli foreign policy ya Bush haifagiliwi hata na wamarekani walio wengi, lakini nadhani tuna matatizo mengi ya kutatua (including ya ufisadi) kuliko foreigh policy ya marekani, which is about to be changed by Americans this November anyway!

    Tuache kupoteza muda bila sababu za msingi na tuhimize watu (waumini) wetu kujishughulisha kwenye shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma. Hizo ndio zitakuza uchumi wao binafsi na wa nchi kwa ujumla. Sio maandamano ya kumpinga Bush!

    ReplyDelete
  14. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  15. ALLAHUAKBAR...INSHAALAH...GOOD SHALL TRIUMPH OVER EVIL...

    ReplyDelete
  16. kha!!jamani mi nawashauri hata kama mnaandamana lakini msikatae misaada yake.kama hamuamini cheki zimbabwe ilivyo sasa hivi.

    ReplyDelete
  17. Nadhani sasa tunaona jinsi siasa za bongo zilivyokolea..kikwete kasafisha serikali ili apate ulaji wa dollar billon 1 za marekani ona sasa watu aliowatoa wanavyotaka kumbania ULAJI..Tutaona mengi mwaka huu...hawa waislamu wasingeenda mtaani bila go ahead kutoka watu fulani fulani waliomwangwa...kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  18. HALAHALA MICHUZI NAOMBA UREBISHE USEMI WAKO!!!! USISEME WAISLAMU WA DAR... SEMA BAADHI YA WAISLAM UKISEMA WAISLAMU WA DAR SHEIKH WANGU NA WE ULIKUWEPO PIA?

    Wabillah Tawfiq

    ReplyDelete
  19. MR.MICHUZI
    RAISI WA MAREKANI GEORGE BUSH,KISHA HAIRISHA SAFARI YAKE YA TANZANIA.

    PIA NAOMBA UIONDOEE HII PICHA KWANI INAONYESHA PICHA MBAYA YA WAISLAMU WA TANZANIA.SIO WOTE NI WASHENZI,HAWA WATU WENGI WANAONEKANA SIO WASOMI KABISA.

    JAKAYA KIKWETE NI MUISLAMU LAKINI HAJAMZUIA BUSH KUJA INCHINI.
    INAKUWAJE HAWA WATU WANAANDAMANA???

    HII PICHA ITASABABISHA WATALII WA KIMAREKANI WASITEMBELEE TANZANIA.

    HAWA WATU WATAFANYA UCHUMI WA TANZANIA URUDI NYUMA.

    HII PICHA INAWEZA KULETA BALAA DUNIANI

    USIPOIONDOA MAPEMA WAANDISHI WA HABARI WAKIIONA WATAIKOPI NA KUITANGAZA TANZANIA VIBAYA SANA

    TAFADHALI SANA,HII BLOGU INATEMBELEWA NA FBI PAMOJA NA CIA

    KWA HIYO NAKUOMBA SANA KWA NIABA YA WATANZANIA WOTE DUNIANI,UIONDOE HII PICHA AHSANTE.

    ZEROOO

    ReplyDelete
  20. Mi naona hawa mtazamo wao tofauti,mbona hawakuandamana pesa zilivyokuja Tz kutoka Marekani?Huku ndo tunaita kujichanganya.

    ReplyDelete
  21. Mhh watanzania jamani mbona tunakuwa ivyoooo,Tujirekebishe ndio tutakuwa na maendeleo.

    ReplyDelete
  22. Sasa Bush hasipokuja Bongo nani ata-loose? Pili alialikwa na Rais JK!!! Hizi siasa za kuiga hazitatusidia bali zitaturudisha nyuma kiuchumi!!

    ReplyDelete
  23. watanzania muw emnaendelea mambo ya uswahilina ni mbaya sana, sasa mnaandamana kwa sababu gani, kuweni wastaarabu yaani kikwete ameshindwa kabisa kuwakataza waislamu wenzake kutoandamana??? acheni mambo ya udini watanzania.

    ReplyDelete
  24. Nafikiri hii nguvu ya umma imeelekezwa sehemu ambako hakuna manufaa ya moja kwa moja kwa Mtanzania bali ni kuunga mkono tu jitihada za wanaharakati wa kimataifa. Kwa mtazamo wangu haya mambo ya ubovu wa kiutendaji na matukio ya ufisadi kwenye nchi yetu tulipaswa kuyapigia kelele kwa nguvu zote.Hivi sasa sote tunafahamu madhara yaliyoletwa na ongezeko la bei ya umeme,bajeti ya mama Meghi je ni nani aliyeingia barabarani kupinga hili au kugomea Tanesco kuhusu upandishaji bei ya umeme? Ufike wakati tupate ujasiri kama huu kwa kutetea mambo ya msingi yanayogusa maisha ya hata hawa wanaoandamana kupinga ziara ya Bush. Kuna wabaya zaidi ya Bush tunao humuhumu na wanaitafuna vilivyo nchi yetu na wala hatupigi kelele.

    ReplyDelete
  25. wakristu haandamani kwa mambo ya siasa, sasa nyie nani anawaruhusu kuandamana, kwa kweli inasikitisha sana, mpokeeni mgeni anakuja kutembelea tanzania, mtazishangaza hata nchi zingine, kwa mambo haya ya ajabu.

    ReplyDelete
  26. niambie kama Bush alisaini mkataba wa Richmond, niambie kama Bush alisaini IPTL, niambie kama Bush alisaini mkataba wa ATC, niambie Bush kama alisema Bunge la sasa litakuwa la 'speed na viwango' na baadaye kukandamiza wapinzani, niambie kama Bush alisema alsiuburi World Bank ije kujenga CHOO Manzese [ wadau someni gazeti la Alasiri leo}, niambie kama Bush anaisifia PCB, niambie kama Bush aliwapa Kharafi ujenzi wa barabara ya kusini na kula hela zote, niambie kama Bush hajatoa takribani sh bilioni 800 KWETU SISI. kama ni kweli hata mimi nitaandamana mpaka lyamba, lakini otherwise PLEASE NENDENI KAZINI MKAJENGE TAIFA, kama hamna kazi NENDENI SHULE mkaongeze ujuzi. pia USHAURI WA BURE, naungana na mdau hapo juu, toa boriti kwenye jicho lako kwanza.

    ReplyDelete
  27. Wapinga haya maandamano wote juu, kwanza muwe munaangalia Waislamu wameandamana kwa sababu gani. Na si mara ya kwanza kwa waandamanaji kupinga ujio wa Rais fulani. Bush kapingwa nchi kibao alizoandamana duniani, hata wakati wa mkutano wa jumuiya ya madola, kwa mfano kuna walioandamana kumpinga Malkia wa Uingereza. Marekani inajulikana inaua watu kibao Iraq, Afghanistan n.k. Sasa anayeumia na hayo ataandamana, sio mpaka huyo ajaye awe kaja kidini. Sasa mlitaka hasira za waislamu kwa Bush ziwe wakati gani?. Aje kiserikali ama kibinafsi wanaotaka ruhusa kuandamana. Hata UDAS na DARUSO walikuwa waandamane j1, siku ambayo Bush anakuja, nao wanapinga hayo hayo ambayo Waislamu wameyasema na mengineyo. Na hawa mnasemaje?.

    ReplyDelete
  28. Kukosa kujua mambo sasa mnaandamana ili iweje na nini bush kawafanyia nyie.....Nendeni shule....Haji kwa ajili ya dini anakuja kiserikali....

    JK kila kila akienda huko mbona hamuandamani????

    Kila siku mko ubalozini kuomba visa...sasa si unafiki huo.....


    Elimikeni...mambo msioyajua msiyavalie njuga....


    kesho nyie nyie mtakaa njiani kutaka kumwona ....

    ReplyDelete
  29. Mzee Michuzi ,HATA MIMI NINAMUUNGA MKONO ANONYM WA FRIDAY;FEBRUARY 15,7:46 PM;EAT. TAFADHALI ONDOA HIYO PICHA:SISI WATANZANIA TUMESOTA KWA MIAKA MINGI,SASA MAMBO YANAANZA KUNYOOKA KIDOGO HALAFU WATU WENYE UJEURI WA KIJINGA WANALETA BALAA.WAARABU WANA MAFUTA,SASA SISI TUNA NINI!.TAFADHALI ONDOA HIYO PICHA KWA NIABA YA WATANZANIA WENGI AMBAO HAWANA UWEZO WA KUTETEA RIZIKI YAO:WATALII WANAIKIMBIA KENYA,WACHENI TUFUNGUE MILANGO NA KUONYESHA INTERNATIONAL STANDARD.MIMI NINAHESHIMU DINI YA KILA MTU LAKINI TATIZO LANGU NI WAKATI DINI INAVYOANZA KUTUPA KIPOFU.SASA HATA NYERERE ALIWAKATALIA WALE MAPADRI WALIOMWAMBIA KUWA KUGOMBEA UHURU SI NJIA TAKATIFU YA MUNGU.MJANJA NI YULE ANAETAFUTA CHAKULA NA MJINGA NI YULE ANAYENGOJEA.MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.MUNGU AMBARIKI KIKWETE AMBAE MPAKA SASA NI RAIS KABAMBE UKILINGANISHA NA WENGI WA AFRIKA:

    ReplyDelete
  30. yaani wewe anon wa 15feb 5.42 pm
    nakufagilia sanaaaa
    hivi jamani mmeona lini waarabu wakaaandamana kwaajili ya waislamu wenzao weusi wa huko Sudan?
    jamani waislamu wa Tanzania mnatakiwa kuamka
    acheni kuiga kasumba za mataifa mengine.
    Na huyo bush haji kwa ajili yenu tu
    leo nyie mkiwa na shida, hakuna mwarabu atakaye nyanyuka kuwasaidia

    mdau canada

    ReplyDelete
  31. Nimeona bango la kumsifia inasema BUSH GREAT CRUSADER! Ni kweli amecrusade mpaka kumwangusha Saddam Hussein na kufanya Iraq colony!

    ReplyDelete
  32. WATU WALIVYOSIKIA BUSH ANAKUJA BONGO NAKUMBUKA HUMU HUMU KWENYE BLOGU WATU KIBAO WALIKUWA WANAPINGA UJIO WA BUSH TZ. NA WENGI WAKASHAURI APOKELEWE KWA MAANDAMANO UWANJA WA NDEGE. NA NINAWEZA KURUDI HUKO NIKATAFUTA HIZO COMMENT ZENU. SASA WATU WAMEHAMASIKA WANAANDAMANA MNALALAMA? AU KWA KUWA WANAOANDAMANA NI WAISLAMU?
    HUYO ANAYESEMA KUHUSU WAARABU WA AFGHANISTAN SI WAARABU NA HATA HAO WA IRANI SI WAARABU NA SIKU AKIAMUA ANATAKA KUVAMIA TZ ATAVAMIA BILA KUANGALIA HUMO NDANI KUNA WAKRISTO AU WAISLAMU WATUPU.

    HUU UNAFIKI WA WATU ULIKUWEPO HATA WAKATI WA KUDAI UHURU. KUNA MTU HUMU ALITUMA MAKALA NDEFU AKIMSHUTUMU JK ANAIUZA NCHI KWA AJILI YA KAMBI YA KIJESHI, LEO HUYO MTU YUMO HUMU ANAWASHUTUMU WAISLAM WANAOANDAMANA KUPINGA UJIO WA BUSH. HIVI HUU UNAFIKI UTAWAISHA LINI? NA KUHUSU SUALA LA UARABU NA HAKI ZA KIBANADAMA HILO WALA SI LA MSINGI KWA SABABU TUNAONA HIZO NCHI ZA KIARABU NDIO MARAFIKI WAKUBWA WA US NA NDIO WANAOCHANGIA KWA HALI NA MALI KATIKA VITA YA IRAQ ILI KULINDA MASALAHI YAO.

    HAO WANAONDAMANA KWA MTAZAMO WAO WANAUDHIWA NA SERA ZA MAREKANI NA HAYO SI MAANDAMANO YA KWANZA, HATA KUHUSU DARFUR, NA PALESTINA PIA WALIANDAMANA.

    WAKATI WAISLAM WANADAI UHURU KWA KUANDAMANA NA KUFANYA MIKUTANO SIE TULIJICHA MAKANISANI KUOGOPA KUFUKUZWA AU KUMUUDHI BWANA MKUBWA NA NDICHO HICHO KINACHOTOKEA SASA. NA WATU WOTE WANAONDAMANA KUPINGA SERA ZA BUSH DUNIANI SI WAISLAM PEKE YAO ILA NI WOTE WENYE COURAGE NA WASIO NA WOGA NA UNAFIKI WA KUONYESHA HISIA ZAO.

    KAMA NI MISAADA ASILIMIA KUBWA YA MISAADA INATOKA EUROPE NA SI US. TENA HIYO SAFARI YAKE INA MASLAHI KWAKE ZAIDI NA WALA SI KWA WATANZANIA.

    ReplyDelete
  33. kaka michuzi kunawatu hapo juu wanajifanya wanaelimu kumbe mambumbuu wanafanya kazi ile ile ya utumwa kama mababuzetu huku ughaibuni.Eleweni hii dunıa ya sasa si kama ile kıla mtu anao uhuru wa kutoa dukuduku.Nashangaa hao wabebe mizigo wa ulaya wanavyo warukıa WAİSLAM wanonekana upeo waoni mdogo kwa kubabaikia watu.ETI MSAADA achani ujınga nyini watu.

    ReplyDelete
  34. hawa sio watu pekee/wakwanza kuandamana duniani dhidi ya GW Bush kutembelea nchi yao, hata UINGEREZA ambao wana apparent 'special relationship' na Marekani pia watu waliandamana Bush alivyokuja kwenye state visit yake. Na sio tu waislamu kwa ajili ya mambo yanaotendeka Iraq etc, pia watu wa climate change issues etc. Kwahiyo sijui mnaoshangaa kuona maandamano mnashangaa nini. Maandamano dhidi ya huyo raisi siyo ya kidini tu.

    ReplyDelete
  35. Jamani kumbukeni usemi unaosema "DEBE TUPU HALIACHI KUVUMA"

    ReplyDelete
  36. hawa watu kila pembe ya dunia watakapokuwepo hivi ndio vijimambo vyao hamjazoea tu haka kautamaduni?. hata watalii wameshawazoea. hii ni mila na desturi.
    Binadamu wote matatizo tunayaelewa ila tunatofautiana jinsi ya kuyakabili.
    watanzania chapeni kazi kujenga taifa.

    ReplyDelete
  37. Mweeh kumbe Watanzania tuna safari ndefu. Hebu ona hapo juu!!! Watu hawaelewi uhuru wa mawazo hata ukiw apeke yako hukubaliani na wazo una uhuru wa kutoa dukuduku na kama kuna asiyekubali naye anaweza kuwa sambamba kukupinga. Kama kuna anayeona hao waislamu wanaandamana kwa sababu hawajasoma basi yeye ndio mbumbumbu.

    ReplyDelete
  38. inshaallah utaala haki itakuja lakini tuwe na subira kwasababu subira ni ufunguo wa peponi

    ReplyDelete
  39. hawa sio watu pekee/wakwanza kuandamana duniani dhidi ya GW Bush kutembelea nchi yao, hata UINGEREZA ambao wana apparent 'special relationship' na Marekani pia watu waliandamana Bush alivyokuja kwenye state visit yake. Na sio tu waislamu kwa ajili ya mambo yanaotendeka Iraq etc, pia watu wa climate change issues etc. Kwahiyo sijui mnaoshangaa kuona maandamano mnashangaa nini. Maandamano dhidi ya huyo raisi siyo ya kidini tu.

    ReplyDelete
  40. hao jamaa wamekosa cha kufanya. Au walitaka kuingi kwenye news??? mi sidhani kama walifikri kabla ya kuandamana, inasikitisha kuona watu hawajui ni nini wanataka, mbona hamkuandamana wakati wa 9/11? Au walikufa ilikuwa halali yao? Je mbona hamuandamani kupinga watu wanaochomwa moto kwa uwizi pengine wa kusingiziwa wa simu? na hawapewi muda wa kujieleza. Mbona hamuandamani kumshinikiza mzee wa kiwira ajieleze? Na vipi kuhusu watanzania wanaokufa kila siku kwa kukosa vituo vya afya karibu? Pia kwa nini hamuandamani kuishinikiza serikali ishuhulikie swala la usalama barabarani kikamilifu?

    Naomba wanounga mkono maandamano hay wafikirie wanjiweka katika picha gani na kuwaweka waislamu wenzao wa tanzania katika picha gani? vyombo vya habari vya kimataifa havitasema baadhi ya waislamu wa dar vitasema waislamu wa tanzania....
    Mnachotakiwa kufanya ni kusali na kuendelea na shuhuli zenu.

    ReplyDelete
  41. kwa huo muonekano i bet kama kuna mwenye gamba la KUHITIMU kidato cha nne panapoeleweka ukiacha tu KUMALIZA jabal hira,kinondoni muslim and the likes.
    kaaazi kwelikweli!

    ReplyDelete
  42. Sio lazima tuige kila wanachofanya mataifa mengine. Ingekuwa hivyo hata Tanzania ingekuwa kama UK ama US, maana tungeiga kila wanachofanya na uchumi wetu ukama kama wao.

    Sasa kwa vile hilo hatuwezi, ina maana tusiige yale yasiyo na manufaa kwetu.

    Tuache unafiki, waislam wangapi wako US na wengine wanalala ubalozini kuomba visa. Mbona hatujasikia Waislam wa TZ wakiwaamuru watoke huko, sababu hawaipendi US na Bush wake. Mbona hawaandamani kila siku JK anapokuwa kiguu na njia Marekani? Mbona hawaandamani marekani inapoleta mabilioni ya misaada bongo?

    Kweli, kila mtu ana uhuru wa kuonesha hisia zake na kusema anachotaka. Lakini mbona hao waandamanaji hatujawaona mitaani kulani ufisadi na wizi wa mali za umma? Au hilo haligusi hisia za 'Waislamu wa Dar'?

    ReplyDelete
  43. Kuandamana ni haki ya kikatiba kwa kila Mtanzania. Bora hao waislamu wa Tanzania wameandamana kwa Amani, kuna nchi nyingine Bush akienda Maandamano yanaambatana na fujo kibao na mpaka wakati mwingine wanamtupia Mayai Viza. Unajua tatizo la watanzania ni Uoga na Ujinga wa hali ya juu mpaka mnafikia kuwasakama hawa waislamu walioandamana. Kama hamjui hiyo ndio inaitwa Demokrasia. Kwa hiyo watu acheni kupayuka na kutapika kama mashimo ya vyoo vya Uwanja wa Fisi mkiwalaumu waislamu maana inaonekana wengi wenu ni mambumbumbu. Kuandamana ni kitu cha kawaida na katiba inaruhusu. Hongera Waislamu kwa kutoa dukuduku lenu.

    ReplyDelete
  44. watanzania ama hakika inashangaza kuona kuwa warabu ndio waliofanya utumwa kumbe hata historia hamjui nendeni mkasomome shule na hivyo vitabu vilivyoandikwa na babu yenu mbritish.

    waarabu walifanya utumwa ni sehemu ndogo sana tena ni sawa na tone la maji kwenye bahari ukilinganisha na waammerika.

    waamerika unazungumzia west afrika yote karibu kawaulize liberia siyo mnapiga kulele tu.

    halafu amerika kuchukuwi siyo sababu ya waarabu mzee angalikuwepo baba wa taifa ndio ungaliweza kupata jibu.

    afrika kusini yote yaani nimibia, angola na kadhalika wakati wa upaniaji uhuru kawauliza nani alikuwa akimsaidia kaburu.

    inafaa watanzania mkamuulize mandela ni nani aliyemtia jela miaka 27 wakatia akigombani haki ya mwafarika na siyo mwarabu.


    HAYA NANI ALIYEMPINDUA UGANDA WAKATI WA OBOTE JAMANI SOMENI NA KUFAHAMU.

    HAYA NANI ALIYEPINDIA SERIKALI YA KONGO YA KUCHAGULIWA NA KUMPA MADARAKA MABUTO SESEKO JAMANI NI HATARI WATANZANIA HATA HISTORIA HATUJUI BALI KULIPUKA KAMA TAA MBOVU.

    haya nendeni Mkamuulize raisi mugabe na huyo mugabe pia siyo mwarabu wala mwislam.

    watanzania ndio maana nakumbuka mzee kinaya alimwamabia baba wa taifa unatawala mijitu isiyo jua mbele wala nyuma.

    nahii inasikitisha hadi leo kazi waarabu na kadhalika wakati maji safi na hata mengi mnategemea misaada kama watoto yatima.

    kazi ubaguzi na majungu badala ya kuchapa kazi na ndiyo maana hata inafikia watu kufanya ufisadi wa hali ya juu kabisa kutokana na upunbavu usiokuwa na maana.
    waarabu wameoa watanzania kibao na kuzaa watoto nao leo unapiga kelele gani.

    waislamu wanapinga kutokana na msimamo wa amerika badala ya kufuata haki yeye hufanya atakavyo kwa kila tiafa na siyo waarabu tu.

    nenda amerika ukaone sehemu wanayokaa waafrika halafu ndio mzungumze.

    ikiwa mimi mtanzania alini inanikera kuona tungalia tuko nyuma kimawazo tunapewa milion 700 eti tunyamaze nchi yetu ingalikuwa inaendeshwa kwa huruma basi sisi tungalisaidia nchi zingine mana tuna utajiri mkubwa. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    kila mmoja nahakia ya kutoa maelezo yake ila mara nyingi wazungu husema nusu elimu huwa ni sumu.

    jambo usilojuwa ni usiku wa giza.

    wasalamu msomi

    ReplyDelete
  45. Michu, Kwanza nataka kujua kama kuna mtu aliyechunguza 100% kwamba hilo kindi zima ni kweli waislamu. Pili kama kweli wanayo imani kwanini wasisome maandishi ya Kuruhani kupinga?

    Walogwe wajitokeze basi hapo airport wakione cha moto. manake kuna Mr Jack Bauer kibao wamesha mwagwa...

    ReplyDelete
  46. ANONY WA Tarehe Friday, February 15, 2008 5:42:00 PM EAT,

    UNAAKILI SANA

    ReplyDelete
  47. KWELI WABONGO WENGI WAPUMBAVU YAANI HAWAJUI KUWA KUANDAMANA NI KITU CHA KAWAIDA. BUSH ALIKUJA HAPA NILIPO WATU ZAIDI YA MILIONI MOJA WALIANDAMANA KUPINGA ZIARA YAKE. TENA HAO NI WAZUNGU WENZAKE AU KAMA WANAVYOJULIKANA KWA JINA LA ANGLO-SAXONS. TENA BUSH AKISIKIA WATU WAMEANDAMANA KUPINGA ZIARA YAKE ATAKWAMBIA HIYO NDIO DEMOCRACY

    ReplyDelete
  48. We anonymous 16 Feb (7:29 am) acha kufagilia ujinga. hawa watu wetu wanatakiwa wakaelimike, then wajue wanaanamana kwa ajili gani. inavyoonekana hapa wengi wameandamanishwa kwa mwamvuli wa dini. Maana waelewa wengi hawaoni mantiki. kwahiyo demokrasia yako unayoifagilia ni kuandamana tu hata kama kitu hakina mantiki, kweli tumahitaji somo kubwa la demokrasia. sasa waweza walinganisha kwa kipi na hao Anglo- saxons unaowatolea mfano? MKWELI

    ReplyDelete
  49. Waislam wa kitanzania ndo maana hamuendeli, kazi mmekalia kushadadia visivyowahusu. Badala kuangalia mtapeleka vipi watoto wenu shule mnaishia kubeba mabango ya kiingereza mshichokielewa na kuozesha mabinti zenu pindi wamalizapo darasa la saba.

    Masheikh wa kisaudia wamewachapishia mabango na kuwabebesha kama puppets...

    Huyo mtu wa evil empire si ndo huyo anakuja na $700M kuwalisheni au sio? Hao waliwapa mabango wamewapeni bei gani?

    Na mtaishia kuwa miaka 400 nyuma milele na kuvaa matambala yenu.

    ReplyDelete
  50. Hapa just watu wasioupenda uislam na waislam wamepata la kusema na kusahau kwamba kuandama ni haki ya kikatiba la msingi ni kuandama kwa amani.Sioni sababu yoyote ya kuwalaumu hawa na kuwatukana waislam wote kwa jumla wakati watu wanatekeleza haki yao ya kikatiba na hata serikali inalijua vyema hilo ndio maana ikawaruhusu, nyie mnaopinga ndio vichwa maji na mna ajenda zenu za siri na upeo mdogo wa kuweza kufikiri pamoja na nidhamu za woga.

    ReplyDelete
  51. Anyno 2:16

    Mi si mwislam lakini nimesoma Quran, one of the finest written pieces of text/literature. Wanaoifuatisha bwana, weeeeh! Si shabiki wa Bush wala Israel

    Sijapinga kuandamana, ila waandamane vitu vyenye msingi na vinavyowahusu. Kwani Bush anakuja Tanzania kuongelea Palestina/Israel? Iraq, Iran? Na wala si missionary. Mtu anakuja kuwaletea chakula mnawaka.

    Mbona hatuoni viongozi wa dini zingine wakiandamana kama hiyo misaada anayoleta ni mibaya hivyo?

    ReplyDelete
  52. NANI KAWAAMBIA KUWA MAANDAMANO DHIDI YA BUSH HATA KAMA YAMEKUWA ORGANISED NA WAISLAMU NI KWA AJILI YA UISLAM????????? WATU WENGI DUNIANI WANAANDAMANA DHIDI YA HUYU MJINGA KWA MAMBO MENGI, I.E FOREIGN POLICY ETC, KAMA HAPA ARFICA ANATAKA KUWEKA MILITARY BASES ZISIZOKUWA NA MPANGO. WALIOHUDHURIA HAYO MAANDAMANO TANZANIA KWA TAARIFA YENU WALIKUWA SI WAISLAM PEKE YAO- THAT IS A FACT

    ReplyDelete
  53. Viongozi wa dini nyingine watandamana vipi kumpinga bwana mkubwa wakati masinagogi yao yanategemea misaada kwa ili kujiendesha kutoka kwa bwana mkubwa? Hawawezi na wala hawatathubutu kunadamana kumpinga Bush na kuna wakati hata Mchungaji Mtikila katika moja ya hotuba zake alisifia siasa za Bush za Palestine, Iraq, Afghanistan na kwingineko. Akandye akale jalalani? Akale wapi jamani?

    Na huyo anayesema ni waislam wa TZ ndio aliyenadama aingie kwenye website aangalie moto unavyowaka huko Venezuela kati ya Rais wa huko na G Bush. Kweli elimu ya mjinga ni majungu!

    ReplyDelete
  54. nyie wabeba makasha ulaya au wala benefit au wasukuma mapram acheni hizo bongo tambarare mtu ana uhuru sio nyie mnaishi kwa uwoga wa makaratasi kila siku tokeni zenu nyoo.

    ReplyDelete
  55. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  56. Pointless kabisa!!!

    ReplyDelete
  57. Kinachoonekana hapa ni chuki za kidini tu. Any way! ndio maisha yalivyo, wacha yaendelee.

    ReplyDelete
  58. Waislamu, tatizo si Bush

    Salehe Mohamed


    ‘BANIANI mbaya kiatu chake dawa na mtumikie kafiri upate mradi wako ni misemo ya Kiswahili ambayo kwa namna moja au nyingine inamhamasisha mtu kufanya kazi bila kuangalia kasoro za majiri wake.

    Kwa maneno rahisi ni afadhali ukafanya kazi kwa mtu usiyempenda au kuelewana naye ilimradi maisha yako yanakwenda vizuri, kuliko kukaa nyumbani au vijiweni bila ya kuwa na kazi.

    Misemo hii imerithiwa tangu enzi na enzi na ina mantiki makubwa kwa watu wenye nia ya kufanya kazi kwa bidii na wenye kiu na maendeleo ya familia zao na taifa lao kwa ujumla.

    Linapofika suala la kazi au kutaka msaada wa maendeleo, mtu hapaswi kuweka mbele tofauti zake na anayempatia msaada, kwani akifanya hivyo kuna kila dalili za kukosa msaada husika na atakayepata hasara zaidi ni yule aliyekuwa akitarajia kupata msaada.

    Marekani ni miongoni mwa mataifa machache makubwa yenye kujiweza kiuchumi na inaaminika kuwa ni taifa linalopenda kuingilia mambo ya mataifa mengine, bila ridhaa ya taifa husika au umoja wa mataifa.

    Miongoni mwa mambo ambayo hadi hivi sasa yanalaumiwa na jumuiya mbalimbali ni kitendo cha kujiingiza katika vita ya Iraq bila baraka za Umoja wa Mataifa.

    Kutokana na vitendo vyake hivyo hasa kwa mataifa ya Kiislamu, baadhi ya Waislamu wanatafsiri kuwa taifa hilo halitaki kuona Uislamu unaendelea.

    Matokeo ya sera za nje za Marekani yamechangia zaidi raia wa nchi hiyo kutokuwa na amani wapokuwa katika mataifa mengine, kiasi cha kushambuliwa mara kwa mara na kupoteza maisha yao.

    Maadui wa Marekani hivi sasa wapo kila kona na kila kukicha kuna taarifa za kukamatwa kwa kundi fulani kwa kufanya uhalifu dhidi ya raia wa Marekani, kiufupi hali si shwari kwa raia wa Marekani.

    Kesho Rais wa Marekani George Bush anatarajia kuanza ziara ya siku nne hapa nchini ziara iliyoelezewa kuwa ni kwa ajili ya kusaidia Tanzania kifedha, ili kufikia malengo ya melinia, kupambana na ukimwi na malaria.

    Ziara hiyo imeanza kupata wakati mgumu baada ya jumuiya mbalimbali za Kiislamu kujitokeza na kudai zitafanya maandamano kuipinga, kwa madai Rais Bush amekuwa kinara wa kuua Waislamu katika nchi zenye mrengo wa dini hiyo.

    Kumekuwa na mivutano ya kutofautiana katika jumuiya hizo ilimradi kila mtu anasimamia upande wake na kutoa hisia zake bila kutathmini kwa umakini ni kwa kiwango gani Tanzania itanufaika na ziara hiyo.

    Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa bin Shaaban Simba, alisema Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kama msemaji mkuu wa Waislamu wanaunga mkono ziara hiyo, kwani itakuwa na manufaa zaidi kwa Watanzania na ni ya kiserikali, hivyo si vema watu wakichanganya na dini.

    Kimsingi maneno ya Mufti Simba yana mantiki ndani yake, kwani huu si muda wa kuanza kuangalia matatizo yanayosababishwa na Marekani katika nchi nyingine, bali kuangalia matatizo ya Tanzania.

    Ukweli siku zote unauma, lakini ni lazima usemwe ili kama kuna mkosaji aweze kujisahihisha kwa lengo la kuleta ufanisi ndani na nje ya dini hiyo au sekta husika.

    Waislamu hapa nchini wana matatizo mengi tu ambayo wao hawajaweza kukaa na kuyatafutia ufumbuzi kwa lengo la kuendeleza dini yao na maendeleo kwa ujumla.

    Migogoro ya kugombea madaraka kila kukicha haishi. Mara leo msikiti huu mara kesho msikiti ule ilimradi watu wanaoanzisha migogoro hiyo wapate kile wanachohitaji.

    Migogoro hiyo kwa kiasi kikubwa imewarudisha nyuma sana kimaendeleo Waislamu hasa katika suala zima la elimu dunia ambayo ndiyo ufunguo wa maisha.

    Hivi sasa unapoamua kutafuta shule na vyuo vya Kiislamu hapa nchini ni vichache sana kulinganisha na madhehebu mengine ambayo kila kukicha shule au vyuo vyao vinasikika kwa kutoa matokeo mazuri katika mitihani.

    Hata shule za Kiislamu zilizopo hazina walimu wazuri, kwani hata maslahi yao ni duni hivyo walimu wazuri huamua kuzikimbia na kwenda kufundisha kule kwenye maslahi manono.

    Tatizo la Waislamu hapa si Bush, bali ni wao wenyewe kushindwa kujipanga vema, ili kufikia malengo waliyojiwekea ili kuleta tija na ufanisi katika familia zao na taifa kwa ujumla.

    Ni aibu leo hii kumpeleka mgeni katika makao makuu ya Bakwata na kuanza kumtambulisha kuwa hizo ndizo ofisi za baraza hilo, ambalo ndiyo chombo kikuu cha kusimamia mambo ya Kiislamu.

    Shule, msikiti na majengo mengine ya Bakwata hayapendezi hata kidogo machoni mwa watu, lakini hilo wahusika hawalioni. Wao wanafikiria kubeba mabango siku ya ujio wa Bush.

    La watoto yatima kukosa ada za kuwasomesha kwa sababu ya kukosekana mfuko maalumu wa kuwasidia, halionekani bali hili la Bush ambaye anakuja kutembea hapa kwa siku nne ndilo linaonekana na rahisi kulitekeleza.

    Hao wanaopinga ziara hiyo kwa nguvu hiyo hiyo wangeanzisha harambee angalau kila mtu atoe sh 500 kwa ajili ya ujenzi wa shule za Kiislamu au kuwasaidia yatima, ingekuwa bora zaidi kuliko walichokifikiria.

    Ni kitegauchumi gani ambacho watu hao wamekianzisha na leo hii unaweza kusema hiki kilitokana na nguvu za jumuiya fulani ya Kiislamu ambayo iliguswa na matatizo ya wananchi.

    Kitabu cha Qur’an hakitaki mtu mwongo, mnafiki au watu kugombania madaraka misikitini, kisa kutaka maslahi binafsi au sifa ya kukalia uongozi.

    Leo hii hapa Tanzania ugonjwa wa malaria ndiyo unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi vya watoto wachanga na watu wazima kila kukicha na serikali imekuwa ikijitadi kupambana na ugonjwa huo kwa kadri iwezavyo, lakini tatizo kubwa ni uwezo mdogo wa kifedha.

    Ugonjwa wa ukimwi kila siku unazidi kumaliza watu na hauangalii huu ni Mwislamu au Mkristo. Ukimwi leo hii msaada kwa ajili ya kupambana nao unakuja watu wanaanza kuuwekea vikwazo.

    Katika nchi hii kuna watu wanapata mlo mmoja kwa siku kwa sababu ya ugumu wa maisha, msaada unakuja watu wanatanguliza siasa za nje zisizo na maslahi kwa taifa na watu wake.

    Maji, nishati ni tatizo kubwa sana hapa Tanzania kwani ni asilimia kubwa ya Watanzania hawapati huduma hizo sababu kubwa ikiwa ni uwezo mdogo wa serikali katika kutoa huduma hizo.

    Miongoni mwa maeneo ambayo Rais Bush anatarajia kuja kuidhinisha fedha ni maji na nishati, hivyo ni vema Watanzania wakawa watulivu katika ziara hii ili wanufaike.

    Kimsingi yapo mambo mengi ambayo wahusika kama watafuatilia kwa makini, wanaweza wakawa na jibu sahihi na sababu kamili za kufanya au kutokufanya maandamano ya kupinga ujio wa Bush.

    Mambo ya kutumiwa na watu kufanya mambo yalishapitwa na wakati na kamwe hayawezi kuikwamua nchi katika lindi la umaskini ambao unazidi kuongezeka siku hadi siku.

    Rais Bush na taifa lake la Marekani wana madhambi mengi wanayoyafanya, na Tanzania ikiwa kama nchi inayojali ubinadamu, lazima ikemee hali hiyo kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu ili isije kujiingiza katika matatizo yatakayoiathiri yenyewe.

    Ni fedheha kwa taifa changa kama la Tanzania linalotafuta nafasi ya kuonekana na kusaidia kimataifa kuanza kuwa na sifa mbaya ya kuwazomea au kuwapokea kwa maandamano viongozi wa kimataifa.

    Matatizo ya Tanzania au Waislamu hayakusababishwa na Bush au nchi yake, bali yalisababishwa na Watanzania wenyewe, hivyo ni vema yakatatuliwa na wenyewe bila kuwashirikisha watu wengine.

    Mwisho, ni busara kwa Waislamu wakakaa pamoja na kuangalia walipojikwaa, ili waweze kurekebisha hali waliyonayo bila ya kufanya shinikizo kwa watu wasiohusika na hali waliyonayo.

    ReplyDelete
  59. Wasomi UDSM wapinga ujio wa Rais Bush wa Marekani
    Na Kizitto Noya

    UMOJA wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), kwa kushirikiano na taasisi mbalimbali za kijamii na za Kutetea Haki za Binadamu, umepinga ziara ya Rais George Bush wa Marekani aliyewasili jana nchini.


    Umoja huo ulieleza kutoridhika kwake na ziara ya rais huyo jana katika mdahalo wao ulioandaliwa kwa kushirikiana na wanaharakati hao kwenye Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.


    Akisoma tamko la pamoja, Mwenyekiti wa UDASA, Datmas Nyaoro, alisema Umoja wa Wanataaluma chuoni hapo unaamini kuwa kidemokrasia Tanzania haina jambo lolote jema la kujifunza kutokana na kuwa rafiki wa karibu wa rais huyo wa Marekani.


    "Hii inatokana na ukweli kwamba, chini ya utawala wa Rais Bush, haki za Wamarekani weusi zimeendelea kuvunjwa, idadi ya wafungwa kutoka katika jamii za Wamarekani weusi imeongezeka huku huduma za kijamii hasa afya na elimu zikidorora," alisema.


    Kwa mujibu wa UDASA, Tanzania haiwezi kuendelea kwa kutegemea ufadhili kutoka nchi zinazotoa misaada yenye masharti kandamizi kama Marekani, hivyo mkataba wa dola za Marekani 608 milioni unaotarajiwa kusainiwa kati ya Rais Bush na Tanzania akiwa nchini, hauna maana yoyote zaidi ya kuendeleza ukandamizaji huo.


    "Tunaamini pia katika kujitegemea na kujitawala wenyewe. Kuongezeka kwa kiwango cha misaada kutoka Marekani katika kipindi hiki ambacho uchumi wake umedhoofika na upinzani dhidi ya ubabe wake umeongezeka, kunatufanya tuamini kwamba ufadhili huu una agenda ya siri ambayo ni Africom," aliendelea kusema Nyaoro.


    UDASA ilitoa wito kwa Watanzania kulinda misingi ya uhuru na utaifa, kulinda na kutetea utu, haki, usawa, amani na umoja wa Afrika badala ya kuendelea kuikumbatia Marekani na kupoteza misingi iliyojengwa tangu enzi za mababu.


    Awali wakizungumza katika mdahalo huo, baadhi ya wanaharakati na wawakilishi wa taasisi za kijamii walisema kuwa ziara ya Rais Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania isipokuwa kwake binafsi na taifa lake la Marekani.


    Kwa upande wake, Amiri wa Shura ya Maimam, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema ziara ya Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania zaidi ya taifa kujitengenezea maadui kwa kuunga mkono sera ya ugaidi.


    Alisema sheria ya ugaidi nchini inapaswa kuangaliwa upya kwani inapingana na sheria za nchi na ndiyo inayosababisha mapigano katika mataifa mengi duniani.


    Hussein Mmasi wa Chama cha Wananchi (CUF), alisema Bush hana utaratibu wa kufanya ziara zenye manufaa kwa nchi wenyeji na kuwa ziara hii ni mwendelezo wa utaratibu huo wenye misingi ya kuzinyonya nchi maskini.


    Profesa Azaveli Lwaitama, Mhadhiri wa UDSM, aliitaka serikali kuchagua marafiki wa kweli wanaoweza kutoa ushauri wa haki kuhusu maendeleo yake badala ya marafiki wanafiki kama taifa la Marekani.


    Alisema Rais Bush amekuja nchini kwa kivuli cha misaada, lakini ukweli ni kwamba ana agenda kubwa yenye masilahi binafsi na taifa lake.


    Ndani ya ukumbi kulikofanyika mdahalo huo kulikuwa na mabango kadhaa yaliyoelezea hisia za wanaharakati hao juu ya ziara ya kiongozi huyo wa taifa kubwa duniani.


    Baadhi ya mabango hayo yalisomeka 'Mfumo tulionao wa demokrasia wakilishi haufai, tunadai demokrasia shirikishi... Bush sitisha vita Iraq, Amani na Haki siyo vita.

    ReplyDelete
  60. Wewe anon wa 9:27pm,naona una contradictions nyingi kwenye maelezo yako mareeeefu.Ikiwa kama unakiri kuwa bush na taifa lake wana madhambi mengi vipi watu wasiandamane,si kila siku Bush ana kuja Tanzania,inabidi watu waandamane wakati huu akiwa nchini.Unasema tatizo la waisilamu si Bush,ukweli ni kwamba tatizo la nchi nyingi za kiisilamu ni Bush na wenzie,hatusikii USA na rafiki zao kwenda kumpiga Mugabe wakati Mugabe ana maliza wananchi wake na ulimwengu unaangalia,lakini angalia interest zake ziko wapi?Iraq na Iran na popote pale mwislamu anapoongoza akijua kuna maslahi yoyote kwa nchi yake analeta utemi.Gaddafi ni mtemi mwenzao kwahiyo hawamuwezi.
    Tatizo si kuandamana tatizo ni kwamba watu hawapendi waislamu waji involve na chochote,kama Bakwata iko disorganised basi hata serikali yetu iko disorganised hivyohivyo,misaada haija anza leo wala jana miaka nenda miaka rudi Nordic countries zimekua zikitoa misaada lakini kwa ufisadi wa viongozi wetu wananchi hawafaidiki,vipi iwe ajabu kwa waislamu kua disorganised.Lakini kama wana feel the need to rally why not.
    Haya maandamano yame highlight dharau ya asilimia kubwa ya watanzania juu ya waislamu,yangefanywa na dini nyingine nafikiri ingekua OK,lakini vile ni waislamu wameonekana ni wajinga na hawajui wanachokifanya(a rebel without a cause).Na kwa vile sisi wafrika tumezoea utumwa tuendeleze kutumiwa kwa kisingizio tuna saidiwa,tusitumie misamiati iliyo pitwa na wakati kwa ajili yaku justify injustice za huyu mgeni wetu,ndio wamarekani wanasaidia na ndio mabaya wanayoyafanya yakemewe. Nafikiri walio andamana wana more guts and courage and bravery kuliko sisi tulio kaa nyumbani tuna subiri kutoa maoni,katiba ya nchi ina waruhusu kuandamana so why not them,kusudio la kuandamana is to be noticed,nafikiri mme note mabango yao na wengine wamepata kutoa hasira zao humu ndani juu ya waislamu.Hii dharau mngeiacha,waislamu wana akili kama watu wengine if their action doesn't make sense to you,it makes sense to others.
    Nafikiri makanisa mengi yanapata misaada toka nje hawawezi toka na mabango wakati misaada yao inatokea kwa hao wamarekani,kama waislamu wana toka na mabango wanamshambulia bush dhidi ya uonevu unao endelea Iraq na nchi nyingi za warabu ni kwa sababu wafadhili wengi wa waislamu ni hizo nchi za warabu vipi wasiandamane ikiwa kama wafadhili wao wanamalizwa na vita?
    Magonjwa uliyo yatolea mfano yako ndani ya uwezo wetu watanzania na afrika nzima kwa ujumla endapo hatutotaka kubadili maisha yetu hakuna msaada wa aina yoyote utakao tusaidia.Dawa ya malaria inataka ujue source ya malaria halafu utafute ufumbuzi.
    Vipi mbu hawaishi nchini kwetu?Vipi mbu wanazaliana kwa wingi?
    Kwanini serikali haitengenezi drainage system ambayo itasaidia ku eradicate malaria completely,tunajua madimbwi yanaongeza kuzaana kwa mbu kwanini serikali hailazimishi kila mwananchi achimbe mtaro uliofunikwa(maana mitaro inatengenezwa sasa hivi humo barabarani inachekesha barabara nzuri lakini mitaro pembeni yake iko wazi where is health and safety)utakao wezesha maji yatumikayo kwenye nyumba yaingie kwenye main drainage itakayo chukua maji na uchafu mwingine kwa ajili ya disposal.Nakumbuka kuliwahi kuja zoezi la kila mwenye duka ajenge baraza mbele serikali ilikazania wengi wakafanya hivyo kwahiyo na amini na hili wakilitaka wananchi watakua hawana namna ila kutenda.Kwa swala la ukimwi nafikiri dawa sote tunaijua,ila tunajitia pamba za masikio,zaidi sisi watu weusi.Angalia statistics za ukimwi dunia uone statistics za Africans and African Americans,kiwango kiko juu sana kwa sababu ya sexual activity zetu mpaka tubadilike hakuna amount of help katika hii dunia itakayo tusaidia.Unless misaada hiyo inayo semwa tunapewa iwe inahusiana na surgical condoms nikiwa na maana kua wanatuletea condoms za kushonewa ili mtu awe hana haja ya kuitoa ili tujikinge na ukimwi na malaria tunaletewa suti special za kuvaa wakati tukilala hazileti joto na vilevile tunajikinga na kuumwa mbu.

    ReplyDelete
  61. Hao wasomi wa UDSM wanaosema african-americans wameongezeka tangia Bush aingie madarakani,hizo statistics wamezipata wapi?Wakiitwa wasomi UCHWARA wataanza kupanua midomo kama bakuli.Unatoa hoja bila utafiti wa kutosha halafu unajiita msomi,shame on you all!!
    Anony hapo juu,swala moja tu-tunataka wagomapo wakue sababu zinazowafanya wagome,siyo kufuata mkumbo tu.Matokeo yake watakapohojiwa watashindwa kujieleza.ANGALIA MAHOJIANO YA SHEKH Bahtazar na al jazira ni kichekesho ndugu yangu!
    Kingine-kila mtu anajua american foreign policy-Kwako ni uonevu kwa america kuvamia Iraq,na Saddam alipokuwa anaua wa kurdi??Mbona waislam wa tanzania hawaandamani kupinga mauaji ya waisla wenzao na waarab haohao kule DaRFUL?Kama hamumtaki Bush na sera zake,mbona akiwaalika kwenye futari mnakwenda?Mbona akitoa misaada bakwata mnapokea??Masikini wa kutupa kama Wewe unapewa bango uandamane wakati hujui jioni utakula nini,na hujui sababu ya kuandamana na wala huelewi kilichoandikwa kwenye bango,kama siyo upuuzi ni nini?Mngemshinikiza basi na Kikwete asimlete kama mnaweza!Nyinyi andamanane,potezeni muda wenu lakini Bush ameshakuja,ataondoka na policy yake kwa magaidi itakuwa hivyo mpaka anaondoka madarakani.
    VIVA BUSH,VIVA KIKWETE.

    ReplyDelete
  62. Ahsante cherry,feb 17,2008 2:15 umeongea point ya maana ni kweli watu humu wamezidi dharau dhidi ya waislamu taireni jamani hata hamuwezi kuficha hata kucha zenu loh.

    ReplyDelete
  63. Assalaam Alaykum Mabibi na Mabwana. Mimi ni muislam na najivunia Uislamu wangu. Nafurahi kuona hawa waandamanaji wameachiwa waandamane maana hiyo ndio tunaita demokrasia. Ninachohofu ni kuwa majority ya hao waandamanaji hawajui hata mabango waliyobeba yana maana gani. Mimi ningekuwa mtu wa media ningemfuata mtu aliyebeba bango la kiingereza na kumhoji kimombo uone jicho litakavyomtoka... Hivi hawa watu hawana kazi mpaka wanaandamana mchana wa jua? ningekuwa bosi huko na kama mfanyakazi wangu yuko maandamanoni mchana akirudi anakuta barua "YOU ARE FIRED!!"

    Mdau - Boston, US

    ReplyDelete
  64. HEBU ACHENI KUWASIMANGA WALIONDAMANA. MBONA ULAYA KIBAO WALIANDAMANA ALIVYOKUJA BUSH KUANDAMANA TANZANIA IMEKUWAWA NONGWA. SHAME ON YOU ALL WHO ARE MAKING BIG DEALS OUT OF NOTHING. IKOWAPI FREEDOM OF SPEECH!!! LET PEOPLE EXPRESS THEIR FEELINGS AFTER ALL NI MAANDAMANO YA AMANI

    ReplyDelete
  65. hivi huyu Dr.Azavel Lwaitama ni mzima kweli?msomi mzima anaenda kuungana nae layman(mbumbu wasiojua dunia inakokwenda eti kuandamana kupinga ujio/ziara ya bush nchini Tanzania!
    hivi msomi kama yeye amekosa njia nyingine ama forum ya kuexpress his feling about america!
    ni mara ngapi anahuduhuria makongamano ulaya na marekani mbona asitumie hiyzo fursa au ndo ushabiki?
    very stupid?
    hii nchi haifunagamani na upande wowote,wapuuzi ninyi,sisi ni maskini tunahitaji misaada toka kwa yeyote,ndiyo maana viongozi wahasisi wa taifa hili walianzisha kiti kinachoitwa Non Align Movement(NAM),namaanisha nchi zisizofungamana na upande wowote.
    ni kwasababu walijua maskini(taifa) uwezi kupambana na mataifa (tajiri)

    hivyo mnaoandamana kwa kufuata mkumbo muwe manajua maswala ya kuandamana kuyapinga!
    mlitakiwa kuanadamana dhidi ya kashfa za BOT-EPA,RICHMOND,BUZWAGI ,IMPORT SUPPORT,TICKS nk hizi ndiyo zinatesa na kuwaumiza watanzania kila siku na kupunguza umri wa mtanzania wa kuishi.

    ReplyDelete
  66. kwanza KB nadhani una faili mirembe, waislamu hawajaanza kudharuliwa/kupuuzwa leo imeanza toka enzi za wajerumani,waingereza na huyo mtakatifu wenu nyerere. ukitazama waislamu hali ilikuwa ngumu sana zamani lakini yote wamepita, utakuta waislamu vibaraka kama kikwete,amepewa biblia saba na wakristo wajinga,sasa usishangae leo jk kumsujudia/kumlamba bush, jk ni kibaraka mkubwa ndio maana kawa rais wa bongo. kuhusu bush , ni mnafiki mkubwa, watu wa katrina wengi bado hawana nyumba za kuishi, wengi wao wamatumbi kama sisi halafu anawapa pesa bongo!!!wazungu/wakoloni wanasema "charity begins at home"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...