MH. ZITTO KABWE NAYE AMEUNGA MKONO UTEUZI WA JK KUMCHAGUA MH. MIZENGO PINDA KUWA WAZIRI MKUU MPYA. AMETAJA HILI LIBENEKE KUWA KAMA CHANGAMOTO YA KIKATIBA AMBAYO AMESEMA INGEKUWA NCHI INGINE SAA HIZI BAKOLA TU. KAMSIFIA MH. PINDA KAMA THABITI NA KUUNGA MKONO HOJA HIYO.
WA MWISHO KUJADILI HOJA HIYO NI MZE SAMWEL MALECELA AMBAYE PIA ANATOA MAKSI ZOTE, BADA YA KUTOA FALSAFA YA TANZANIA KISIASA. NA PIA AKAONGELEA NGUVU ZA WANANCHI KWAMBA MWENYEZI MUNGU HUWA NYUMA YA WANANCHI WENGI KATIKA KUTOA UTASHI WAKE.
MH. MALECELA AMEUNGA MKONO HOJA HIYO.
SPIKA SASA ANAMWOMBA WAZIRI MKUU MTEULE MIZENGO PINDA AONGEE NA WABUNGE. KILA MTU ANASHANGILIA
Ninakupongeza sana Michuzi kutupa habari motomoto jinsi zinavyotokea, utafikiri na sisi tuko huko Bungeni. Hongera sana na Mwenyezi Mungu akuzidishie uhai ili uendelee kutupa habari kama hizi hasa sisi tulio mbali na nyumbani, asante sana.
ReplyDeleteZito alishanunuliwa.
ReplyDeleteUsicheze na siasa wewe kijana na wakati wowote by next election utakuwa tayari ndani ya CCM.
Hela ilifanya mwana wa Adamu akasogezewa kwa nguvu Sifongo Siki