

dawa ya mbu yenye kutumia teknolojia ya kisasa na ambayo ni salama imeingia bongo tayari na wenye nia ya kupiga vita wadudu hao wauwaji wakae mkao wa kula.
dawa hii ni balbu yenye miali maalumu ambayo mbu akikumbana nayo anatoka unyoya mwenyewe, na harudi. yaani ukiiwasha ndani unafungua madirisha ili mbu wakimbie, sio kufunga madirisha na milango ili mbu asiingie.
kama sikosei hiyo hapo juu ndo tafsiri ya maelezo ya hiyo dawa hapo chini. kama sio kunradhi, maana mie inglishi izi kuishia ugokoni bikozi of zee umandezzz
-----------------------------------------
The work principle of product is like this: As we know, insect vision is very different from human’s, The study indicate that insects are attracted to light in the UV part of the spectrum, in opposite way, they should feel uncomfortable in certain part base on this, Scientist made out a yellow luminous pigment which is coated on the inner of the glass bulb can filtrates the UV radiation when it turns on, and in the meantime a special light source of an illuminating wavelength was given off to drive mosquitoes away.
Harmless, non-toxic, non-radiation, protecting the environment Complies with International safe standards IEC, CE, TUV and ISO 9400.
What you need to do is keep door and Windows open
Make sure the windows and doors are open when you use it in the room so that the mosquitoes could find a way to fly out
Ensure to turn off the other lamps while using Peace light mosquito repeller.
For more Information Contact
Dar Es Salaam; Dr Chum on 0784-333860
E-mail; allynoti@aol.com
Harmless, non-toxic, non-radiation, protecting the environment Complies with International safe standards IEC, CE, TUV and ISO 9400.
What you need to do is keep door and Windows open
Make sure the windows and doors are open when you use it in the room so that the mosquitoes could find a way to fly out
Ensure to turn off the other lamps while using Peace light mosquito repeller.
For more Information Contact
Dar Es Salaam; Dr Chum on 0784-333860
E-mail; allynoti@aol.com
What a GREAT news!
ReplyDeleteMichuzi thank you for breaking it to us.
I DEEPLY KNOW THAT, WE ARE GOING TO WIN THIS WAR.
A war worth fighting till we get the VACCINE, and that will be a start of the END of the MALARIA.
By Mchangiaji
Brother wataalamu wa uchumi wanasemaga kila kitu kina uzuri wake na ubaya wake.
ReplyDeleteSasa hiyo MIONZI pamoja na kufanya kazi nzuri ya kuwafukuza hao m-mbu, haina MADHARA kwa BINAADAMU kweli!?!
kwakweli naona mtakuwa mmetusaidia sana kwa swala hili,kwani tunapata shida sana hasa sie wamabondeni,basi hizo bei zenu ziwe za wote sio za wa masaki,mikocheni na wale kwa mjomba oysterbay.
ReplyDeleteSounds so good to be true. Wataalamu mwasemaje? Au kama kuna aliyetumia na akaona matokeo yake atufahamishe. Ila anonymous msiingie. Otherwise, kama ni kweli, basi hongera. Tulie na Tanesco tu.
ReplyDeleteBlackmpingo
ni jambo zuri kutendeka katika jamii yetu.SASA HAPA KUNA MAMBO MAWILI MATATU NATAKA KUHOJI?
ReplyDelete1.JE HIZI BULB ZITATOLEWA BURE KWA WANANCHI KWA KUPITIA MISAADA YA FEDHA YA NJE YA NCHI KWENYE MFUKO WA MALARIA KAMA INAVYOFANYWA VYANDARUA AU WANANCHI WATATAKIWA KUNUNUA? sio mbaya wenye uweo wakinunua lakini je wale walengwa wanao shindwa kununua vyandarua waliokuwa na maiasha ya chini je watapewa bure?
2.Kutokana na tatizo kubwa la umeme linalokabili nchi yetu je watu ambao hawewezi kumudu gharama za umeme na wale wasiokuwa na umeme kabisa itakuwaje?
mdau mzawa
Wazushi nyie. Eti mi na akili zangu niache madirisha wazi eti kuruhusu mbu wakimbie baada ya kumulikwa na kataa kenu? Na midudu mingine je? Kama sasa hivi mvua inanyesha kuna midudu kibao usiku, kumbi kumbi, kumba kumba, mende, kereng'ede, ladybirds (vile vidudu viduchu vyeusi vinanukaa), n.k.
ReplyDeleteSasa hao wote watatolewa baru na hivyo vitaa??
Dawa ni Rungu tu! Milango madirisha yanafungwa, RUNGU linapulizwa babaake halafu tuone huyo mdudu atakayebaki.
Mtoa Maoni: Mdau,Tarehe Thursday, March 27, 2008 6:48:00 PM EAT,
ReplyDeleteNime pendezwa na maoni yako, ha ha ha!! Lakini ndugu yangu ndiyo kusema akili yako haina akili.Ama ndiyo lugha maimuna!!! Kutokana na kiingereza changu cha ze (the ) na and, na kasayansi kangu kadogo ka mambo ya Ultraviolent waves< nimeng'amua ya kuwa miale itolewayo na taa hiyo hufukuza wadudu.Sasa ifikirishe akili yako kuhusiana na tafsiri ya wadudu.Je ulivyokuwa unapitia kule kwa mzee wa kaamiba hukujifunza sifa za wadudu na makundi yake.Je majina uliyoyataja hayajumuishwi kwenye nasaba ya wadudu. Am confused
Dr.Confusion
Jamani kumbukeni ule msemo kwamba safari moja huanzisha nyingine au hakuna kizuri kisicho na kasoro. Heunda hizo bulb ni suluhu ya mbu lakini kitendo cha kuacha wazi madirisha na milango muda wote wa usiku (kwa sababu mbu hukumbizwa na mwanga)hamuoni kwamba kitaingiza mibaka katika vyumba vyetu? Unafukuza mbu na kuingiza vibaka!!Kwa sisi wa uswahilini nadhani other methods zitakuwa better kuliko hizi bulb. Ni mtazamo wangu wadau msikonde wala nini akaona nawabania wafanyabiashara. Kama kuna maelezo ya ziada kuhusu matumizi mnaweza kunipatia
ReplyDeleteBwana michuzi honger SANA HII TAA MIMI NITITUMIA KWA MIAKA MIWILI SASA NA HAKUNA TATIZO LOLOTE YAAN HATA CHANDARUA TUMETOA VYUMBANI THEY ARE VERY GOOD TO BE HONEST
ReplyDeleteDAh iyo dawa ni bomba kweli, sio watu tunaacha cd zetu zile zenye moshi wenye kubembeleza halafu zikajakutuzingua izo taa za rangi?
ReplyDeleteKiniga-unguja
Kwa umeme wa mgao hapo mbu ameula.
ReplyDeleteKaka Michu pamoja na habari hizi nzuri hapo juu, lakini nina wasiwasi na habari nilizozikia/nilizosoma kuwa hizo bulb zimetengenezwa na mercury, hivyo inapoungua inabibidi kuwa mwangalifu ili isivunjike. Inapoungua, basi ifunge ndani ya mfuko wa nylon na uitupe.
ReplyDeleteVita ya kweli ya malaria ni kuua mbu au kupata chanjo.
ReplyDeleteHizi harakati za katikati ni jitihada za kupunguza tu maambukizo na sio kutokomeza malaria.
Naona shortcommings nyngi kuliko mafanikio katika kutumia hizi taa kwa sababu jinsi maelezo mafupi yanavyosema ni kwamba taa inabidi iwake ili mbu waondoke.
Hii ni kusema kuwa watu walale huku taa ikiwa inawaka, tatizo hapa sio tu bei ya umeme bali pia ni uwezekano wa kutokupata usingizi mzuri na madhara yanayofuatia kukosekana kwa usingizi mzuri wa kutosha.
Swala la kufungua dirisha sio tatizo kwa sababu kinachohitajika ni kuondoa nyavu tu.
Matumizi ya taa hizi hayataweza kukubalika in large scale kama njia muhimu ya kupinga malaria kwa sababu asilimia 80 ya watu walio katika hatari ya maambikizo ya malaria wanaishi katika mazingira ambayo hakuna umeme!
tukitengeneza computer model ya kitakachotokea baada ya njia hii kutumika kwa muda mrefu,itakuwa very interesting - natarajia ionyeshe kuwa maambukizo katika maeneo yenye umeme yamepungua kidogo wakati katika maeneo yasiyo na umeme yameongezeka kwa sababu mbu wataadapt zaidi katika maeneo hayo.itafanana kidogo na kutumia chandarua zisizo na dawa ya kuua mbu.
bottomline: jitihada walizozifanya wataalamu hawa zinahitaji pongezi na shukurani,hata hivyo bado wametuacha na changamoto ya kutafuta njia sahihi zaidi za kumuangamiza vector wa malaria au kutengeneza chanjo dhidi ya complex antigen structure of plasmodia...zemarcopolo.
Hapa, kwa wale ambao hatuna umeme itakuwaje?
ReplyDeleteKumaliza tatizo la Malaria Tanzania na nchi nyingine zote ni kutumia DDT kama wenzetu wa nchi zilizoendelea walivyotumia wakamaliza mbu wote hadi leo.
Mungu atusaidie sie masikini.
Wadau,
ReplyDeleteMbu wakijificha chini ya mivungu itakuwaje? Mnajua tena nyumba zetu za uswazi.....
Michuzi madirisha yatafunguka vipi wakati nyumba zetu tutundika nyavu , za kajungio.. kogapa mbu .. sasa inabidi tuingia hasara kubadilisha madirisha..
ReplyDeleteHIZI ZOTE BIASHARA TU: KAMA KWELI WANA UCHUNGU NA MAISHA YA WATANZANIA KUFA KWA MALARIA MBONA HAWALETI DAWA ZA KUNYUNYIZIA KWENYE MAZALIA YA MBU ILI KUWATOKOMEZA? WANALETA BISHARA TU MBU WAENDELEE KUZALIANA NA SISI TUENDELEE KUNUNUA BIDHAA USIPOINUNUA UFE KWA MALARIA:
ReplyDeleteSERIKALI MKO WAPI KUSAIDIANA NA WANANCHI KUTOKOMEZA MAZALIA YA MBU SIO KUINGIZA BIASHARA KUTOKANA NA MALARIA:
WANANCHI NUNUENI TAA ZINAZOUA MBU AMBAZO ZIKONYINGI MADUKANI NA SIO ZINAZOFUKUZA KWANI TUNATAKIWA KUWAPUNGUZA. MIMI NI MTUMIAJI WA CHANDARUA CHA NGAO NILICHONUNUA TOKA KWENYE BANDA LA NGAO SABASABA LAKINI HAKIJAWAHI KUUA HATA MBU MMOJA, ETI HAO HAWANA VIJIDUDU VYA MALARIA! SWEET BIASHARA IMEZUIA MADAWA YA KUUA MBU YASILETWE NCHINI.
ReplyDeleteWadau habari zenu!
ReplyDeleteNapenda kuwafahamisha kuwa hii Tech ipo na huwa inafanya kazi fresh, hapa sio kuwa unaacha milango na madirisha usiku kucha.(kwani Rungu huwa unaspray usiku kucha?? no). Unawasha taa wadudu wanakuwa disturbed na huo mwanga halafu wanakimbia.
Nimeshawahi kufanya project kama hii ila mimi nilitumia sound. Kwa wale wanaojua mambo ya sauti kuna sauti ambazo hazisikiki kwa binadamu ila wanyama wanazisikia.
Sasa project yangu ilikuwa inatoa sauti ambayo ilikuwa kero kwa wadudu hivyo huwa wanakimbia. Binadamu huwezi kusikia kabisa.
Hii haikuwa kwa biashara ila ni mambo ya kuwa udadisi wa kujaribu vitu.
Tuache ubishi ila tuwe wadadisi sio kubisha bila kuwa na POINT.
Mimi naomba kumjibu Annon 12.41 hapo juu kuhusu kuharibu mazalia ya mbu
ReplyDeleteNjia nzuri ya kuharibu mazalia ya mbu ni usafi kama utatumia dawa yeyote ni kuharibu mazingira au kuweka sumu kweny vijito ambopo si njia nzuri
Napenda kumuelewesha mdau hapo juu kuhusu maisha ya Mbu
ReplyDeleteDini zote Duniani zinakataza KUUA KUUA ni dhambi kubwa sana kwa hiy hata mbu anayo haki ya kuishi
Ukisoma kwenye sifa za mbu Their life expectancy is only three days so whatever you do to them it won't help you RATHER THAN POINON YOURSELF
NINAVYOFAHAMU JINSI MBU ANAVYOCHUKIWA NA BINADANU KWA SASA ANGEKUWA KWENYE DANGEROUS SPECIES LIKE RHINOS OR GIANT PANDA
Kama utaitumia hii taa mbu wataweza kukuacha chumba au ukumbi wako baada ya siku tatu atajifia mwenyewe na sio kubeba zambi za ukatili
Kama kuna kitu cha kusaidia tatizo letu ni bora kukijaribu na kukiboresha
Naomba kumjibu mdao hapo juu Zemarcopolo
ReplyDeleteSio kwamba uache milango au madirisha muda wote kwani unapofungua mlango na madirisha ni kuwahurumia hao mbu and other INSECTA KINGDOM wasiumie macho yao baada ya saa moja hivi unaweza kufunga ila itabidi uwe mwangalifu kwani wengine nearest exit itakuwa chini ya uvungu hao wataweza kukushambulia ukizima taa
Tunashukuru kwa dawa hii ya kisasa.
ReplyDeletelakini kabla ya kuanza kutumiwa ufanyike upembuzi yakinifu kuhusu madhara ya mwanga wa taa hizo kwa viumbe wasio mbu. ili tupime faida na hasara. pili kutolewe elimu ya utambuzi ili kujua ipi feki ipi harisi maana bongo vitu feki kibao.mtu unaweza acha madirisha wazi ukiamini una dawa kumbe bulbu imepakwa rangi tu. na mbu watakushughulikia kama kawa
Thom.frm kinoshamba bongo.
Ningependa kumueleza mdau hapo juu Mbu ni living organism like human being with their characteristics
ReplyDeletena anadhibitiwa na charcteristics zake hivyo kwa sasa ni harufu sauti na mwanga
Kuua sasa hiyo ni mipango ya mungu hawezi kufa kibwege atajaribu kujiokoa.
kwa mfano ukipiga rungu chumbani kutokana na harufu mbu atakimbia kama atashindwa kukimbia ndipo atateseka hadi kufa sasa hizi taa zinaumiza macho yao hivyo itabidi wakimbie tuu
Askofu mkuu kweli we mkali, kuna mdau hapa ananiambia kuwa inawezekana wewe ndio unaoleta hizi taa. Mimi nimemwambia sidhani kama wewe ndio unaoleta taa ila nadhani wewe ni chibiriti umeamua kujiita askofu.
ReplyDeleteMdau uliofafanua kuhusu "nearest exit" nakushukuru...
Jamani, swala la mbu ni tata na ufumbuzi wake unahitaji fikra na maamuzi sahihi na sio hizi njia tunazoletewa zikiwa na nia ya kuneemesha watu wachache. Kinachotakiwa ni kuwatokomeza mbu na sio kuwakumbiza,nje tutakuwa tunatembea na hizo taa au?, Mazalio ya mbu ndio lazima yapewe kipaumbele, na sidhani kama kuwauwa mbu ni dhambi kama alivyonena anayejiita askofu mkuu hapo juu, maana hata vitabu vyasema 'viumbe wote wapo chini yetu' na tunaweza amua jinsi ya kuvitenda. any way Kila mtu atajiju!!!!
ReplyDeleteVipi kuhusu sisi unaokesha kwenye kilaji? maana mbu huko si mchezo
ReplyDeletesasa huyu mdau hapo juu anonekana amechanganyikiwa kwani unafahu mazalia ya mbu yalivyo sasa hiyo ni kazi ya halmashauri ya jiji si unalipa kodi ya ya jiji inabidi waboreshe huduma nje ikiwa kondoa mazalia ya mbu
ReplyDeleteKwa kifupi mazalia ya mbu ni uchafu kama utaweka nyumba yako na eno karibu safi utapunguza mazalia ya mbu
aaah nimekumbuka physics ya form 2 enzi zile
ReplyDeletedispersion of colour in spectrum ukichanganya na themionic emission au thermionic diode
Harmful colour to human being is Black spectrum and Luminous white
same as welding light
Je ni nani anaweza kuvumilia moto wa welding
R -red
o- orange
Y- yellow
G - green
B - Blue
I - indigo
V- Violet
Hiki kweli ni kipande cha sayansi na tekenolojia yake
Hongera mdau
Wadau kweli bwan zinafanya kazi nimenunua na hali jana haikuwa mbaya yaani mbu wengi sana wamepungua
ReplyDeleteHawa wasomi wasitake kududanganya kwa biashara zao.. Mbu wa Bongo hata siku moja hawafuati mwanga wa taa,hujitokeza pindi taa zinapozimwa. Dawa ya vita hii ni kufukia mashimo yote ya maji yaliyosimama yakitanguliwa na ujenzi wa mitaro ya maji machafu (sewerage system)ambayo haipo ktk miji yetu. Miundo mbinu mibovu ndio sababu kubwa ya maradhi haya pamoja na Kipindupindu. Haya yote ni maradhi ya kujitakia, tupo radhi kupokea viandarua milioni 5 vyenye thamani zaidi ya dollar millioni 50 wakati tunalewa wazi kuwa Maleria haipatokani na kulala kitandani. Tunaacha ku deal na source ya maradhi haya badala yake tunazidi kuwatunza mbu utadhani ni pet majumbani mwetu...
ReplyDeleteUpuuzi mtupu.
Mdau hapo juu unasema umetumia na kweli mbu wamepungua tunataka kujua wameenda wapi swala sio kupungua tu umewafukuzia kwa jirani mwenye watoto na hana umeme? tunataka dawa za kuua mazalio ya mbu watokomee sio kufukuza.
ReplyDeletenaomba kumjibu mdau hapo juu sasa mimi nimenunua kama jirani akioa wanazidi kwake nae atanunua kwani huku kwetu tabata mbu ni wa kupangusa siku ambayo hawakukeri ni siku umelala nazo kuanzia bia nne na kuendelea na sio mbili sasa watoto jee hiyo rungu 4500 na siku mbili tuu imeisha
ReplyDeletesamahani kidogo wahusika kuna email nimeona hapo allynoti jee huyo allynoti anauhusiano wowote na allynoti songambele? nilisomanae miaka mingi bongo
ReplyDeleteBwana hizi taa ni kiboko zinafukuza mbu kweli hao wanaopiga kelele wapo Marekani na hawajui adha tunayopata
ReplyDeleteMimi mwenyewe nimetumia
Hivi kwanza wanajua hadi chloroquin imedata kwa ajili ya malaria ?