mnyonge, mnyongeni lakini haki yake mpeni. hawa jamaa ni chachu ya vyama vingi bongo. bila kuwepo kwao mambo mengi yangesimama. kutoka shoti ni mwenyekiti wa chadema, mh. freeman mbowe, mwenyekiti wa cuf mh. profesa ibrahim lipumba na mwenyekiti wa tlp mh. augustine lyatonga mrema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Ningependa kutoa masahihihisho sio Muhimbili University College of Health Sciences (MUCHS)Tangu kijitenge na chuo kikuu cha Dar es salaam Sasa hivi kinaitwa
    Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS

    ReplyDelete
  2. BAHATI MBAYA WENGI WETU TUNAONA HAYO NI MATATIZO YAO TU SISI HAYATUHUSU! NDIO MAANA TUNASHUHUDIA WENZETU WANAANDAMANA KUMPONGEZA RICHMONDULI? TENA WAKIWA WAMEVAA JEZI ZA CCM NA WANACCM WENGINE WAKIWA KIMYA. IKIASHIRIA HAWAJAFURAHISHWA UFISADI KUFICHULIWA.

    ReplyDelete
  3. Wametufumbua sana macho, wameibua mambo mengi mno. Mchungaji Mtikila naye ni baadhi ya watu wa mwanzo kusimama kidedea kwenye vyama vingi. Sijamsikia muda sasa....

    ReplyDelete
  4. WANABLOG NISAIDIENI, KAMA KUNA KITU KINANIUMIZA KICHWA BASI NI HIKI:KWA KUWA KISIWA CHA PEMBA KIPO KATIKA HALI MBAYA YA UMASIKINI WA KUTISHA ,UKOSEFU WA AJIRA,NK LAKINI CHA KUSHANGAZA WAPEMBA WENGI NI MOJA KATI YA MATAJIRI NA WAFANYABIASHARA WA KUPINDUKIA WAKIWA WANAWEKEZA MAJENGO MAKUBWA MAKUBWA NA BIASHARA NYINGINE KUBWA KUBWA KAMA KARIAKOO,TANGA,MWANZA,MOROGORO HUKU WENGI WAO HASA ENEO ILALA WAKINUNUA MAJUMBA YA ZAMANI KUVUNJA NA KUJENGA UPYA SASA NINACHOUMIA NI HIKI,KWA KUWA WAPEMBA WENGI NI CUF AMBAO WENGI WAO ASILIMIA ZAIDI YA 95% HAWAUTAKI MUUNGANO WA TANZANIA SASA KWA NINI HAWAWEKEZI PEMBA AMBAKO HALI INATISHA KWA UMASIKINI NAOMBA MNISAIDIE

    ReplyDelete
  5. huyu tino lyatonga mwenye neema na lipumba wananikumbusha ze comedy show mpoki na vengu jinsi wanavyowaigiza sauti zao kisawasawa ,tehe tehe...

    ReplyDelete
  6. Nawapa hongera sana viongozi hawa, tunaweza kuwaita `waanzilishi wa upinzani, au vyama vingi'. Sina maana kuwa wao ndio walianzisha vyama vingi, au vyama vyao, la hasha, maana yangu ni kuwa wao ndio viongozi ambao wapo sasa na bado wapo katika wakati mgumu wa kuwashawishi wananchi ambao bado akili zao zinaamini kuwa vyama vingi ni `fujo, vyama vingi vitaleta vurugu...
    Mimi bado naamini kuwa vyama vingi ni chachu ya maendeleo. Pale penye upinzani wa kweli na ushindani ndipo maendeleo na mabadiliko yanapopatikana. Watu mkibweteka na kile kilichopo, mtakuwa hamuoni tofauti, na matokeo yake ni kuwapa wale wanaliopo wajione `miungu watu' na matokeo yake mnayaona.
    Mifano mingi ipo, angalieni `nyanja ya mawasiliano, na jinsi nyanja hizi zinavyokwenda kasi kwa mabadiliko yenye manufaa kwa watu' Hii ni kwasababu ya ushindani wa kibiashara. Hio ndio halihalisi ambayo pia inatakiwa iwe kwenye siasa. Siasa za ushindani, zenye shabaha moja la kuindeleza nchi, kuleta maendelea na kumsaidia mwananchi, zinajenga mabadiliko ya haraka ya kiuchumi, na kinyume chake ni kudidimia kwa uchumi na wananchi kuteseka ilihali wale waliopo kwenye mtandao wa chama kinachoshika hatamu wananeemeka na kufisidi nchi. Anayeumia ni nani, kama sio wewe mpiga kura!

    Mimi nawaomba wananchi tusiogope kufanya mabadiliko, tujenge taswira njema kuwa upinzani, kuwa upinzani sio fujo, na kama ni fujo tutazianzisha sisi wenyewe, sio vyama vingi. Viongozi tunawachagua wenyewe kwa kura zetu, kwahiyo tuna mamlaka nao.

    Tumuombe Mungu, ipo siku na sisi tutakuwa na ushindani mwema wa vyama, na upinzani wenye manufaa, na hili litakuja kama tutawapa nafasi `upinzani' na wao waonyeshe kile walichokikusudia. Tuwachague wabunge wa upinzani kwa wingi, ile waweze kuleta mabadiliko huko bungeni. Nashangaa wale wanaosema wapinzani wamefanya nini ili tuwachague? Utawajuaje wanafaa au hawafai wakati hawajatawala?

    ReplyDelete
  7. Hivyo vichwa hapo kila kimoja kinaongea yake:-

    wa kwanza anasema KWANI UONGOOO

    wa pili anasema TUTAWABANA MPAKA KIELEWEKE HAPA.

    wa tatu anasema SI NILISEMA MIMI! SASA YANGU MACHO TUUU

    ReplyDelete
  8. Michuzi una akili sana, naona umemuengua Mh Cheyo "Mapesa", ninaamini si kwa bahati mbaya, lipo unalotuambia hapa! Big up bro Michu!

    ReplyDelete
  9. Sijawasikia siku nyingi hawa Wazee.Watu wanasema ukimuona Kobe kainama ujue anatunga sheria!Kimya chao cha muda mrefu sina hakika kama kweli walizama katika Tafakuri Jadidi ya Hali ya Kisiasa hapa nchini na mwelekeo wake.Hususan baada ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiteto.Bila kutafuna maneno ningependa kuwaasa Viongozi hao watatu ambao picha yao inaonekana hapo juu,Mbowe,Lipumba na Mrema haya yafuatayo:Hivi sasa tumabakiwa na takriban miaka miwili tu na ushei kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu Wa 2010.Ukiondoa muda wa maandalizi ya uchaguzi huo utabakiwa na muda wa tuseme Mwaka Mmoja na Nusu.Kipindi hicho ni kifupi sana kuweza kuleta shinikizo ya aina yoyote itakayo zaa mabadiliko yoyote ya maana yatakayo boresha zaidi mazingira ya Uchaguzi Mkuu ujao 2010.Wote tumashahidi kuhusu mapungufu mengi yaliyopo katika Katiba yetu ya sasa hapa nchini ambayo ndiyo nguzo muhimu katika kuhakikisha kwamba uchaguzi katika demokrasia ya vyama vingi vya siasa itaendeshwa kwa haki na usawa,kwa njia iliyo wazi kabisa katika mfumo wa demokrasia ya kweli na utakao simamiwa na taasisi zitakazo kubalika kisheria na vyama vyote vya siasa vitakavy shiriki uchaguzi mkuu ujao.Kwamba muda wa kufanya hayo ninayo yasema kwa hivi sasa ni mfupi mno na haitawezekana kufanya lolote la maana,swali kwa hao wazee ni,Je, sasa Itakuwaje?Hamuwezi kususia uchaguzi katika mazingira yaliyopo sasa.Kwa sababu kwa kufanya hivyo mtaonekana KIOJA katika hadhara ya Kimataifa.Shinikizo hizo za mabadiliko katika Katiba mlipaswa kuzianza vingali mapema.Sasa mmechelewa kufanya hilo,kulikoni?Sitaki kuamini kwamba mmeridhika na hali ilivyo hivi sasa na hali itakayo wakabili katika uchaguzi mkuu ujao.Bila ya Tume Huru ya Uchaguzi.Bila ya Katiba Mpya.Bila ya Mabadiliko katika mfumo wa Utawala na Uendeshaji wa Serikali na Taasisi zake.Bila ya kuwepo mgawanyo wa madaraka ulio bayana baina ya Mihimili Mikuu Ya Utawala:The Executive;The Parliament;The Judiciary;& The Independent and Free Press.Mabadiliko mengine yote yatatokana na mapendekezo mbalimbali kuhusu marekebisho ya mambo hayo ya kimsingi.Wenzetu wa Kenya wamesha onyesha njia.Tusiipuuze.Ni fundisho muhimu sana kwetu Hata sisi tutatakiwa tufuate mfuano wao katika kurekebisha Katiba yetu.Ni muhimu sana kwamba Rais lazima apunguziwe madaraka aliyonayo chini ya Katiba ya sasa inayo mfanya awe kama NUSUMUNGU.Matatizo ya Zanzibar hayatakuwepo tena iwapo mabadiliko hayo ya Katiba yatafanyika hivi sasa.Siyo Kesho.Kwa kuwa na Rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Ceremonial Head of State)na kuruhus Serikali za Tanzania Bara na Visiwani ziendeshwe na MaWaziri Wakuu wawili,mmoja kila upande(Heads of State)wote wakiwa chini ya Rais mmoja ambaye ndiye atakaye kuwa Jemedari Mkuu wa Majeshi pamoja na mengineyo matatizo yote hayo yatayeyuka kama barafu.Yatabakia matatizo yetu ya njaa ya tumbo lakini siyo masuala ya kisiasa.Nimegusia machache sana na kwa kifupi sana kutokana na ufinyu wa nafasi na muda.Wasomaji mna mengi ya maana ya kufanya.Hii ni kama chachandu tu ya mjadala mrefu niliothubutu kuuchokoza.Nafikiri ndugu zangu Mbowe,Lipumba na Mrema wamenisikia.Bila kuwasahau kina Zitto Kabwe, Dr.Slaa na Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao bila kujali yuko Chama gani na ana Itikadi gani ya Kisiasa.Yatakapo kuja masuala ya Kitaifa sote lazima tuwe na kauli moja na msimamo mmoja.Nakushukuru sana kwa kusoma Blogu hii.

    ReplyDelete
  10. Jamani mheshimiwa mrema alikuwaga wapi?yaani hao watu ni machachari kweli!!na wachapa kazi,,haswa hao two chaggas!!

    ReplyDelete
  11. We anon 1:34PM, unawazungumzia wapemba hapa, kwani we wanakuhusu nini? wakiwa maskini kwao siwao, wamekuja kwako kukuomba chumvi? eboo hem acha kumaind maisha ya watu, we kwenu umeekeza? Wao wanajuwa kwanini hawaekezi kwao, get your life... kama hupendi wao wakae bara hama wewe uwende sayari nyengine ukaishi, lakini wapemba watabaki hapa hapa, na maduka makubwa k/koo na kwengineko yatabaki kuwa yao. Wapemba ndo matajiri wetu! Ndo walotufundisha mapishi, mpaka chapati tumefundishwa na wao, sisi wa bara tulikuwa twajuwa kupika ugali tu, sasa twapika mpaka pilau lol. We vipi bwana ubaguzi umeweka mbele! Mbona huwaambi wamakonde wakaekeze kwao mtwara, kule hali ni mbaya kuliko pemba mara 100. Wapemba wanaishi kwa raha zao kwao,hawaekezi mpaka ccm iondoke kule.

    ReplyDelete
  12. Hapa, Mrema kachoka na kuchakaa. Sijui ni jinamizi gani lilimuingia wakati ule Mzee ruksa alimpa uwaziri wa kazi na vijana, akaona amenyang'anywa tonge la unaibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani; hadi kuamua kutoa siri za baraza la mawaziri.

    ReplyDelete
  13. anony 1.34PMBiashara inafuata soko lilipo. Waliopo Pemba hawana nguvu ya kifedha, hivyo kuwekeza huko hizo biashara utakuwa uwenda wazimu. Nasikia pia wanaogopa uchawi tehteh. Ila wewe unaweza kwenda Pemba nawe ukafugua biashara.

    ReplyDelete
  14. Mrema alipanda haraka, na alianguka haraka. Lakini enzi zake mbona wizi na ujangili ulipungua! Mnakumbua SUNGUSUNGU yake?

    ReplyDelete
  15. Mimi nataka kufahamishwa huyu mchaga Mrema huwa ni mwisilamu au hiyo kofia ni fasheni tu,au anau mind uislamu kinamna.Wajuzi nifahamisheni.

    ReplyDelete
  16. Jamani Freeman handsome mpaka basi, moyo unanidunda! Michuzi nipe contacts basi bwana, niko Washington DC hapa. Ngoma imetulia nina uhakika atakuwa impressed.

    ReplyDelete
  17. MREMA NA WENZAKO PAMOJA NA MTIKILA HONGERA ZENU MLIANZA ZAMANI MAMBO YA ..SIKU SABA..NA MENGINEYO MENGI BADO TUNAWAKUMBUKA KWA MAZURI MENGI MLIYOFANYIA ..NJIHII..

    lyatonga njoo tena usa tutakufanyia mpango wapesa kama last time..."..UTAUNGANISHWA NA WASEE.."

    ReplyDelete
  18. we dada uliyemzimia freeman,pole sana!!freeman ana mkewe mzuri sana anaitwa Dr Lillian...umechelewa kutuma application,

    ReplyDelete
  19. Lazima mkubali kwamba kwa udhaifu mlionao CCM kwenu ninyi ni sawa na PWEZA.Silaha yenu kubwa ni UMOJA NA MSHIKAMANO na wala siyo MAPESA!Fitna na Unafiki ndiye adui yenu mkubwa na wala siyo CCM.Muda umeanza kuwatupa mkono.Mkifanya mchezo kwa kuendekeza njaa ya Tumbo wenzenu CCM watazidi kushika Usukani kwa miaka mingine 20 zaidi.Simuoni kati yenu atakaye stahimili dhiki na mikikimiki ya kisiasa katika mazingira duni na ya unyanyasaji yanayo yatakayo wakabili hadi kufikia kipindi hicho.Ni kazi ngumu sana.Amueni kuelekeza nguvu zenu zote katika mambo machache ya kimsingi yatakayo leta tija kwa vijana wenu watakao fuata nyayo zenu hata ikiwa kati yenu hakuna atakaye fanikiwa kuingia Ikulu kabla ya kustaafu siasa!Ukiamua kujenga nyumba huanzi kwa kuezeka Paa kwanza kabla hata hujajenga msingi wenyewe!Ninacho waasa ndugu zangu msikimbilie kupaua au kuezeka Paa kabla hamjajenga msingi wa nyumba.Kama ni kuanza na kushinikiza mabadiliko ya Katiba basi iwe hivyo na muwe na msimamo mmoja.Tumeanza kuonja matunda ya mafanikio yenu Bungeni japo wabunge wa upinzani ni wachache mno.Nawapongezeni sana kwa ujasiri wenu na kwa mafanikio haya machache lakini muhimu sana katika nchi yetu.Mwendo wa Treni huanza polepole,likisha shika moto halishikiki!Shurti ukalingoje stesheni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...