Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Misupu unaona chama hilo? Hadi raisi wa France na waziri mkuu wa Uk wameenda kulitembelea, next time Bush au Obama akija anaende huko na yeye, bwawa la maini halijulikani

    ReplyDelete
  2. Hivi, what does " Imarati " means? Nimeisoma mara nyingi michuzi na wadau wengine wakiitumia wanapoongelea timu ya Arsenal. Kuna uhusioano gani kati ya neno Imarati na timu ya Arsenal? Na hilo neno ni kwa lugha gani? Kiswahili, kiarabu, etc ?

    Natanguliza Shukrani kwa kuelimishwa juu ya suala hili ambalo limenitatiza kwa muda mrefu.

    Mdau,
    Bay Area( San Fransico)

    ReplyDelete
  3. AISEE, KUMBE WENGER NI 'MVULE' NAMNA HIYO! DUH.. JAMAA KAENDA JUU SEKUNDE..

    ReplyDelete
  4. Kwako Mdau wa Friday, March 28, 2008 6:33:00 AM EAT,

    MAANA ya "IMARATI",

    Ijapo mimi siyo msemaji rasmi lakini, ninavyoelewa ni kwamba hilo neno limetoholewa (upo hapo? "derived from..") kutoka kwenye neno Emirates. Hilo ni kifupi cha jina la uwanja wa nyumbani wa klabu ya arsenal ambao unajulikana kama Arsenal Emirates Stadium. Hii ilitokana sponsor wao kufadhili kwa aina fulani mradi wa ujenzi wa uwanja huo. Na makubaliano ni uwanja kuitwa hivyo( yaani Emirates Stadium) kwa kipindi fulani sina uhakika na muda. Emirates hawa ni hao ambao wanamiliki pia shirika la ndege la Emirates.

    Nadhani nikusadia, Kwa heri

    ReplyDelete
  5. heshima mbele. hiyo siku (jana 27/3/2008)ambapo rais wa Ufaransa na waziri mkuu wa Uingereza walipotembelea Emirates stadium iliitwa Britannique-Francophinie, ni siku ambayo rais Sarko alikuwa anahitimisha ziara yake Uingereza hivyo aliamua kutembelea na kuona wafaransa walioko Uingereza wanafanya nini, sasa kituo kikuu ndo kikawa hapo Emirates kwa mukulu prof. Arsene Wenger (tamka Arsene Venga).
    hiyo inatia moyo sana unapoona rais anapanga ziara kutembelea na kuona kazi zako.
    halafu ukiangalia hiyo picha kwa makini utagundua kwamba hapo Wenger kapewa heshima yake kama bosi wa hapo Emirates ndo maana kasimama kati kati ya hao waheshimiwa ndo kusema sio kila mahala rais atakuwa bosi, kuna sehemu zingine kuna mabosi wake na protokali lazima ifuatwe! (wanasayansi jamii najua mtaanza kuonsha vinywa). tehetehethe.

    ReplyDelete
  6. Anon wa 6:33:00.
    Neno Imarati linatokana na jina Emirates ambalo asili yake ni kiarabu. Neno hili linatokana pia na neno EMIR lenye maana MTAWALA. Kwa hiyo maeneo yote ambayo mtawala huyu anatawala kwa pamoja yanaitwa EMIRATES. Nadhani ukiongezea na maelezo ya mdau hapo juu kuhusu udhamini wa ujenzi wa uwanja wa Arsenal FC unapata kitu kamili.

    ReplyDelete
  7. naungana na mwenzangu hapo juu kuchangia hilo neno emirates lina maana ya mtawala, yaani EMIR kwa kiswahili tunaita AMIRI kama vile ukitaka kusema AMIRI JESHI MKUU, yaani mtawala mkuu wa jeshi. upo hapo?

    ReplyDelete
  8. kweli chama linatisha we si umeona misupu hapo hakuna bwawa wala kisima man wala woman chelsea wala chesa ni kazi tu kwa kanuni ya michezo asie kubali kushindwa si mshindani

    ReplyDelete
  9. hapo ndio utakapojua kuwa arsenal chama kubwa , kwa kuangalia list hiyo hapo, nikisema tu tunaambiwa tunaseam sana, queen naye mpenzi wa arsenal, millband secretary wa foreign affairs wa uk naye arsenal, kwa vyovyote arsenal ni chama kubwa

    ReplyDelete
  10. Kiswahili pia kimechukua neno hili "Emir" kama "Amiri" yaani kiongozi. Mfano amiri jeshi.

    ReplyDelete
  11. Emirates Airline walitoa 100M pounds ili uwanja mpya wa Arsenal uitwe kwa jina lao hapo mwaka 2004. Kabla ya hapo uwanja ulikuwa unaitwa Ashburton Grove (waliita hilo jina wakati wa mipango na ujenzi wa uwanja).Emirates waliwekeana mkataba na Arsenal kwamba uwanja huo utaitwa Emirates kwa miaka 15.

    Julius Kessy, London.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...