Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Wanakijiji, nimejaribu kupata maana ya katuni hii nimeshindwa. Naomba nisaidiwe. Najua ni mambo ya mwafaka wa CUF na CCM, lakini huyo aliyesimama golini ni nani na huyo anayepiga penati ni nani?

    ReplyDelete
  2. Tatizo sio kocha kupiga penati, KP.Tatizo ni Je,mpigaji penati ana uhakika wa kucheka na nyavu? Isije kuwa akapaisha,akagonga besela,ama hata golikipa mwenyewe kuicheza penati hiyo. Yote yanawezekana japo shauku ya mashabiki wengi jukwaani ni kuona nyavu zinatingisika.Maana najua wako mashabiki wengi tu wameshikilia naniiiii! zao wakati mpiga penati huyu anajindaa kupiga penati hiyo ndani ya Butiama Village Stadium, ama nakosea mtalaam Michuzi! Ni shughuli pevu kweli kweli!!

    ReplyDelete
  3. Nadhani golini kasimama Rais wa Zanzibar,mpiga penalt ni chama chake amabcho kinakaribia kuchukua maamuzi ambayo kwa mujibu wa katuni golikipa hayapendi

    ReplyDelete
  4. Huyo golini ni mhe nanihii wa kule visiwa vya karafuu, na huyo mpiga penalti ni shingo ya ccm au neck kwa jina lingine ingawa wenyewe wameondoa hiyo k. katika neck. Na huo mpira ni muafaka

    ReplyDelete
  5. Msaada kwa anon wa kwanza hapo juu (jaribuni kutumia majina yenu jamani.. hata kama ni a.k.a zenu, ili kuleta urahisi wa kuwareference) ok tuendelee katika mada...

    Huyo aliye golini ni Rais wa Zenj (angalia huo mustachi na hako kakipara ka ushikaji) ambae anashangaa kama chama yake inaweza kuunda serikali mseto na hivyo kupunguza maakuli kwake... pamoja na maumaarufu na misifa

    Ignorant,
    Jeremani

    ReplyDelete
  6. teh teh teh teh!

    KP amekuacha siyo anon wa kwanza hapo juu?

    ni kweli kabisa katuni hii inazungumzia muafaka wa ccm na cuf
    na hapo aliyegolini ni Rais wa zanzibar Abeid Aman Karume(ccm visiwani),na anayetaka kupiga huo mpira ni ccm bara.

    akistaajabu kuwa ccm bara ndiyo waliomfundisha yeye mbinu zote hadi akashinda ushindi wa sunami au wa hila na sasa wanasimamia muafaka karume hapo hanashindwa kuelewa hawa wenzie wa ccm bara wanamtakia nini?

    ReplyDelete
  7. Wadau mimi ni anon wa kwanza hapo juu. Nashukuru kwa kunielimisha. Somo limeeleweka. Asanteni sana.

    ReplyDelete
  8. NA HUU MUAFAKA WA 3 HAUTOTEKELEZWA KAMA WALIVYOKUBALIANA, YANGU MACHO, NA NYIE PIA MUTAONA!!!!MSETO NI BAADA YA MZEE KUMALIZA MUDA WAK --- mwanamapinduzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...