Wewe Michuzi aka mtu wa bwawa la main unachotakiwa kufanya nikutupongeza sisi Gunners sio eti tumeona mwezi, wakati sisi tuna shabaha tena bonge la shabaha.
Uncle michuzi tumekuonyesha ulichotakiwa kufanya kwenye fainali dhidi ya hawa watu sio kurukaruka.
Naomba utoe pongezi bila kejeli sawa jitahidi hata kwa leo tuu ni haki yetu jamani na leo kweli hanywi maji mtu.

Wengers Daughter!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tupo pamoja Wenger's Daughter. Baeleze hiyo mutu ya Bwawa la Maini....leo tunategemea watapita kwenye UCL.....waombe tuu wasipangwe na sisi...KUDADADEKI..


    GUNNER NUMBER ONE

    ReplyDelete
  2. Kwanza kabisa napenda kuwapongeza washika bunduki wa imarati kwa mpira safi na uburudishao. Mimi ni kama kaka Michuzi ni mshabiki wa bwawa la maini, lakini soka wanalotandaza washika bunduki huwa linaniburudisha sana. Kama liverpool hawatachukua champions league basi nitafurahi tu vile vile kama Arsenal watalichukua ingawa inabidi waombe wasikutane na mashetani wekundu maana inaonekana Anderson ana uwezo wa kumnyamazisha fabulous fabrigas kama ilivoshuhudiwa kwenye mechi zao mbili ambazo washacheza (premier league na Fa cup). Sasa sisi wa bwawa la maini tunaenda kumalizia shughuli walioianza wanaimarati pale san siro tar 11. Bring it on!!!!

    ReplyDelete
  3. Jamani mimi ni Manchester united for life lakini kwa mara ya kwanza nilifurahi Arsenal kwa kuwatandika Ac milan maana ni kwa haki kabisa!timu maana sasa hivi ni barcelona tu tunaowagopa ,this time kombe linarudi england bila wasi wasi!timu 4 kati ya 8 ni england si mchezo! Jumamosi Portsmouth tuwamalize tuchukuwe treble

    Will

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...