waziri wa habari, utamaduni na michezo mh. george huruma mkuchika amesema serikali itafanya utafiti wa namna ya kupambana na wizi wa haki miliki ambao umeshamiri nchini ambapo wasanii wananyonywa jasho lao na watu wachache wanaoiba hizo kazi bila kuwajali wenye nazo
akijibu swali la globu hii asubuhi hii kwenye kipindi cha michezo redio wani ambapo alikuwa mgeni mwalikwa, amesema tatizo hili lipo dunia nzima na kwamba ufumbuzi wake haupatikani mara moja na unahitaji utafiti wa kina ili kupata ufumbuzi muafaka.
wadau hili limekaaje?
CHONDE michuzi ongea naJK apunguze safari ili pesa zisaidie kupunguza ghalama za Umeme,Mwenzenu nimezidiwa. majilani zangu wanatumia bila kulipa mimi siwezi.
ReplyDeleteNi wazo zuri,Lakini......!Lazima niseme ukweli kwamba hii dhana iliyojengeka serikalini ya kila kukicha utamsikia kiongozi wa juu kabisa serikalini au hata katika chama akitoa tamko kwamba,'SERIKALI ITAFANYA....',siyo kwamba 'Serikali hivi sasa inafanya utafiti ambao karibu utakamilika na matokeo yake yatatolewa wiki ijayo au hivi karibuni ili kubaini ukubwa wa tatizo na jinsi ya kukabiliana nalo.....'.Kwa kweli mimi binafsi nimechoshwa na tabia hiyo ya viongozi ambayo imegeuka kuwa staili ya uongozi wetu hapa nchini.Utamsikia kiongozi akitoa tamko hata pengine jambo lenyewe bado ni wazo tu halijakamilika,proposal still on the drawing board.Kwa mfano,serikali itajenga barabara ya lami ya kilometa 200 toka Mbuyuni hadi Mkengeni na wananchi wakatulizwa kwa kujazwa matumaini makubwa.Kiongozi atapigiwa makofi na kusifiwa huku mwenzetu akiwa kesha ingiza siku.Kumbe ukweli wenyewe ni kwamba ujenzi wa barabara yenyewe utategemea ufadhili wa Marekani kwa mfano.Na Marekani yenyewe hata taarifa ya mradi wenyewe hawana.Pengine taarifa wanayo,lakini ni ombi tu ambalo hawaja litolea majibu.Kwa hiyo msaada huo pengine usipatikane tokana na vigezo mbalimbali.Huu ni mfano tu.Ipo mifano mingi.Ninachotaka kusema hapa ndugu zangu ni kwamba sawa Waziri ana nia njema.Lakini wizi huu wa Hakimiliki(COPYRIGHT THEFTS)ni suala ambalo limekuwa likilalamikiwa toka siku nyingi mno,siyo suala geni.Kama ni tafiti,zimeshafanywa nyingi sana!Waulizeni kina John Kitime na pale Chuo Kikuu kitengo cha Sanaa na Muziki!Kama ni utekelezaji wa hicho kilicho bainishwa na kupendekezwa,hilo lilikuwa liwe limesha anza kutekelezwa JANA!Ukisha sikia kauli za 'serikali ITAFANYA','Tuna mpango wa kuongeza ajira milioni moja','Tutaongeza Madarasa',kauli za kesho kesho ujue ni michoooooosho mitupu.Tubadilike jamani.Likitolewa tamko hadharani basi ujue kitu hicho utekelezaji wake unakaribia kukamilika au umeshakamilika.Tunapo jenga matumaini kupita uwezo wetu kiutendaji tunajipalilia makaa.Mwisho wa siku ni viongozi hao hao watakao kuja onekana wababaishaji na hawafai,kumbe halikuwa kusudio lao!Haya tusubiri huo utafiti tuone.Unamtangazia mwizi kwamba tutakufanyia utafiti ili tujue unaibaje ili tuweze kukudhibiti zaidi ili usiendelee kuiba.Halafu itakuwaje?Jamani Lets Grow Up.Give me a Break Pleeeeeeeeeaaaaaaaaaseeeeeeeeeeeee!
ReplyDeleteMdau wa 9:58 nakushangilia kwa nguvu zote. Mimi nilidhani Mkuchika ana akili kumbe anatembea mule mule kwenye siasa za ... serikali imejidhatiti...serikali itashughulikia...serikali inafahamu kilio chenu... Ukweli ni kuwa tafiti zimefanyika, vitabu vimeandikwa na majarida yametoka kuhusu ufumbuzi wa wizi wa kazi za sanaa kuanzia muziki hadi filamu na hataza nyinginezo.
ReplyDeleteNakumbuka nikiwa Chuo Kikuu Idara ya Sanaa tulizungumza na wadau wengi sana kuhusu ufumbuzi. Tukaandika na hata kuwakilisha mapendekezo wizarani. Ufumbuzi ni kwa TRA kukubali kutoa stamp kama za sigara au pombe kali ili wao wadhibiti mapato na wasanii wadhibiti mauzo.
Stamp zimechapishwa tayari kupitia COSOTA zinaitwa Hakigram. Mpaka leo tatizo ni kumlipa printer ili ziletwe nchini. Ufisadi na tamaa ya 10% ndio inakwamisha. Pia TRA hawaoni faida ya kuingia kukusanya vijisenti vya CD na DVD wakati wanapata mabilioni ya sigara na bia.
Tatizo lingine ni kuwa COSOTA/BRELLA na sanaa viko wizara mbili tofauti na tumeshashauri mpaka sauti zikakauka kuwa mawaziri wakutane waongee, lakini bwiiiii. Tatizo jingine ni uchovu na ukibogoyo wa Baraza la Sanaa (BASATA) na kulindana kulikokithiri
Michuzi mwambie Mkuchika asituchezee wasanii wa sasa tumejanjaruka hatutaki siasa. Tuna akili timamu na tunajua ukweli
ENDAPO SHERIA YA HAKI MILIKI ITATUMIA BASI WASANII WENGI WA BONGO WATAFUNGWA KWANI WENGI WAO NI WAIGAJI WA SANAA ZA WATU WENGINE IKIWA PAMOJA NA WIMBO WETU WA TAIFA AMBAO SINA UHAKIKA KAMA MTUNZI WA TUNI YAKE TULIMLIPA. SASA NA HAWA WAMACHINGA WANAOUZA DVD, CD NA KANDA ZA KUKOPI TUTAWAPELEKA WAPI, SI ITAKUWA BALAA.
ReplyDeleteMkuchika mwanasiasa, hakuna hata waziri mmoja wa utamaduni ambae hajasema neno hilo, kwanza jambo hilo haliko katika wizara yake ye atafanya nini? kuna watu kama kitime wenye uzoefu wa miaka mingi kwa nini serikali haiwapi sapoti, au japo kuwauliza wamfikia wapi? yaani huyu mkuchika anataka afanye utafiti gani. kama msanii nilijua huyu ni mwanamichezo wasanii tutaendelea kupigwa siasa
ReplyDelete