leo nilienda library nilivoperuzi guess what i found... siyo kwa nyanja za utalii tu wenzetu wako speed ya roket wanaanza kubrain wash watu wa huku tangu utoto imagine hii ni library ya shule ya msingi.


huu ni ukurasa wa tatu; wa pili waneelezea juu ya bendera , population na currency then ukifungua wa tatu Bang!!! ilivyochomekwa ni kiaina.


TAHADHARI KAMA UNATAFUTA MAHALI PAHALI PALIKOANDIKWA MLIMA HUU UKO KENYA USISOME.


Mdau jd

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. box kali hadi sikumbuki tena kama atlas huwa zinawatunzi,kama zinao tupatie jina la mtunzi...
    Can Lawyers do something???

    ReplyDelete
  2. nakupongeza sana we mtu ni mdadisi sana wa mambo, yaani hawa watu wanataka kutunyakulia kabisa mlima wetu wahojiwa ili waeleze walikuwa na maana gani.

    ReplyDelete
  3. wadau asante michuzi hii imetulia, tuwakemee wakenya popote pale walipo kuwa huu mlima uko tanzania, na pia tuachane na vyama vya wakenya sisi watanzania havituhusu, nini tunataka uko kenya.

    ReplyDelete
  4. So What?If I may ask,'Watanzania na nyie mmekua mkifanya nini kuitangaza nchi yenu na maliasili yake?Kazi hiyo mnasubiri nani awafanyie?Nani aliyewazuia msiifanye kwa manufaa ya nchi yenu?Kazi kulalamika tu,BUT NOTHING DOING!ukiwa nchini Kenya mlima Kilimanjaro unaonekana pia tena at close range kwasababu mlima huo upo mpakani kabisa mwa Tanzania na Kenya.Tuache mdomo mrefu tutumie akili zetu kuleta msukumo mpya katika maendeleo ya nchi yetu.Hivi ulikuwa unajua kwamba watalii wengi wanaokuja Afrika Mashariki malipo yote ya Dola na Pound yanafanyika nje ya nchi yetu na hapa wanaingia na pesa ya Kenya au ya kwetu baada ya kutumia sana wakiwa Kenya ambako walitangulia kufika katika safari yao?Waulize Shirika la Utalii Tanzania wamekuwa wakifanya kazi gani katika kukabiliana na ushindani huu wa kibiashara?Hata tangazo moja la kuvutia watalii katika televisheni ya CNN au BBC au SKYNEWS linatushinda?Halafu unalalamika,unamlalamikia nani?Iwapo wewe ungali kijana nakushauri fikiria kuanzisha Kampuni yako binafsi kuendeleza utalii hapa nyumbani.Kama ulifikiria kuna mtu anayeifanya kazi hiyo,umekosea,mtu huyo hayupo.Angekuwepo ungeshaona matokeo yake.Waliopo ni WABABAISHAJI NA WASANII WATUPU ndugu yangu.Pole sana.Hata sie wenzio tunasikia uchungu kama huo wa kwako lakini tufanyeje.Usukani umeshikiliwa na Kuli,unatarajia nini?

    ReplyDelete
  5. LOL!!! sio wajinga hivyo hawa...unfourtunately you cant copyright a view from another country!!!...hata wangesema "welcome to kenya and Africa, the land of kilimanjaro" lakini why do we complain so much it is not as if we are too serious about leveraging of our natural resources..might as well allow our jiranis to do so....

    ReplyDelete
  6. Nyie Watani/majirani zetu vipi? Ningeshauri muhamishe huo mlima utoke kabisa karibu na mpaka wa nchi yetu na uwe katikati ya nchi yenu. Au jengeni ukuta muzuie usionekane tukiwa kwetu. Kwa taarifa yenu mlima Kilimanjaro unaonekana vyema zaidi ukiwa upande wa Kenya. Sasa tusipige hata picha!? Basi na Mungu naye angetunyima jua, mwezi, anga na nyota!

    ReplyDelete
  7. THE POINT IS NOT THAT WHERE IS KILIMANJARO LOCATED AT,THE POINT IS IF I GO TO KENYA WILL I BE ABLE TO SEE KILIMANJARO? IF I WOULNT BE ABLE TO SEE KILIMANJARO THEN THEY WILL BE DOING FALSE ADVERTISING AND U CAN SUE THEM.AND IF I WANT TO CLIMB IT THERE IS NO WAY I WILL DO IT IN KENYA IF KILIMANJARO IS IN TANZANIA ,THAT MEANS I WILL HAVE TO TRAVEL TO TANZANIA AND TANZANIA WILL BENEFIT FROM THE SAME ARTICLE.SO U SHOULD THANKS KENYA BIG TIME FOR HELPING ADVERTISE MT.KILIMANJARO MORE THAN YOUR DUMMY LEADERS WHO THINK ABOUT THEMSELVES 24/7 TILL LAST YEAR WHEN THEY WOKE UP AND REALISE WE R THE LAND OF KILIMANJARO AFTER ALL THOSE YEARS.

    ReplyDelete
  8. KWA USHAURI WANGU MIMI NAONA NI BORA UINGIE HIZO MAKTABA ZOTE HALAFU VICHUKUE HIVYO VITABU KISHA VICHANE CHANE AU VITIE MOTO

    ReplyDelete
  9. So what?? mlima Kilimanjaro huonekana tokea Kenya pia!!! Ndivo wasemavyo. Kumbukeni usemi wa Jomo Kenyatta " Ukiona mitu imelala chukua mali yake, hapana amsa yeye!!". Nyie mlie tu, si rais wenu Mkapa alishasema ku mu wavivu wa kufikiri?? Kazi yenu kulalalma tu. Fanyeni na nyie vitu vyenu, si NONDO mnazo? Kwa nini mnazifungia???

    ReplyDelete
  10. kaka JD una usongo!!vipi wamekuibia mke nini? box saa ngapi na library saangapi? au ndo dinner man /lady au kp?kitchen porter?gas uk

    ReplyDelete
  11. Great lesson, fantastic marketing! Watanzania badala ya kulalamika sasa umefika wakati wa kujifunza kutoka kwa wakenya kwenye kutangaza utalii. Njia mojawapo ni kuingia kwenye networking kwa makampuni ya kiutalii katika East africa. Watanzania tupate ujuzi kwenye hizi network na kuutumia kupiga bao kilaini.
    Pia watanzania tujenge culture ya ujasirimali ambapo moja ya mambo muhimu kimafanikio ni kujifunza kila wakati mbinu za kufanya biashara, kujituma na kuitangaza biashara yako kwa nguvu na sio kulalamika tu kila siku. Anyway moto umeanza kuwaka!

    ReplyDelete
  12. Mdau mmoja hapo umetoa maoni mazuri nilitaka kukuambia tayari JK kaanza kuweka matangazo kuanzia mwaka jana cnn na yale ya Uk nampa pongezi kwa hilo manake hela nyingio ilikuwa inachezewa vibaya akati kuna mambo kama haya yanaweza kutusaidia.Watu wanawalaumu wakenya bure tu bila kujiulizia inakuwaje tuwe na vitu vingi ambavyo ni mvuto kwa watalii kuliko kenya lakini wakenya wao ndio wana pata faida nyingi kwenye soko la utalii kushinda sisi? Jibu nndio hilo hapoo "MATANGAZO". viongozi wetu ni ma mbumbu nao wako affected pia na elimu yetu ya kukariri.tungekuwa tunasoma kwa kuelewa tungeweza kuapply mambo mengi katika maishayetu ya kila siku lakini leo una kiongoZi anakubali kuongwa million 10 huku mtu akitia hasara taifa la bilioni.Mnalia sana na kilimanjaro,mbona tanzanite inachimbwa tanzania tu lakini wahindi wamelikamata soko la tanzanite kushinda sisi? VIONGOI WETU NDIO VICHWA VYA WENDAWAZIMU SIO RAIA.najua watu watasema mbona tunawachagua bado,hapana mchezo mchafu ndio unawapa uongozi.mtu unakula mlo mmoja kwa siku na unafamilia je mtu akikupa 10000 umpigie kura utamnyima? Inakuwa vigumu kwao kukataa rushwa kwani dhiki imewakabili kupita kiasi.sisi watanzania sio wajinga kuongozwa na ccm kila wakati ni kwamba wana nguvu ya kila kitu SASA TUNACHOOMBA NI UADILIFU KUTOKA KWWA HAO WALIOJIPACHIKA KUONGOZA NCHI KWA NJIA CHAFU/kuna nakala moja ya padri nilipenda sana maneno yake kwenye hotuba yake ya pasaka kawauliza mafisadi ni viwanja vingapi mnataka hili muweze kujenga mahekalu yenu mkatosheka? Ni magari mangapi ya kifahari mnataka hili msafiri vizuri? Na vingine vingi tu.viongozi wadini inabidi wajaribu kuwakumbusha viongozi wetu inaonesha imani kwa Mungu zimewatoka kutokana na Pesa .

    ReplyDelete
  13. Kwa hili jamaa wanastahili sifa. Sie viongozi wa kuleta maendeleo bado hawajazaliwa. Tunao wapenda madaraka tu. Ndio maana leo hii hata ikiwa ni wewe sasa umepata uongozi watu watasema fulani kapata ulaji!. Huu mtizamo wetu ndio hasa adui yetu namba 1. Tukiweza kuondoa huu mtazamo maendeleo yatakuja,kwani hatutokua na hulka za kuchangamkia ulaji,bali tutaanza kuzingatia maslahi ya Taifa.
    Ni majuzi tu waendesha kampuni za kitalii nchini wakitoa kilio chao juu ya uzembe na rushwa zilizokithiri huko maliasili kiasi kwamba wageni wanatumia udhaifu huo kufungua kampuni zao na kuziendesha hukohuko Ulaya,wakipokea pesa toka kwa watalii na kisha kuwaleta na kuwatembeza nchini huku sie tukiambulia madafu tu. Maliasili wao hawana presha saana kwani mshahara wanapata na deals kibao zipo njenje,waangaike ili iweje?
    Tatizo letu tupo tayari kupewa sifa na wageni lakini si kumuona mtized mwenzetu anafanikiwa au anakua na maisha bora,tulichoweka mbele sie ni maslahi yetu binafsi na ndio maana ufisadi hautokoma nchi hii labda tubadilike,nafikiri kwa kuweka utawala mpya serikalini maana 40 years now lakini hatujajua namna ya kutumia rasilimali zetu kujitegemea.
    Fikilia tuna madini yanaitwa "TANZANITE" halafu wauzaji wakubwa duniani ni RSA na Kenya! wakati hata dalili tu za kua na mgodi hawana.
    "Kweli zidumu fikra za mwenyekiti"

    ReplyDelete
  14. Hawa watani wa jadi kwa kuchukua majina yetu, wamezidi sasa. Hata jina Kilimanjaro wanatumia, angalia www.kilimanjaroentertainment.com Lini wamesikia waTanzania wamechukua majina yao. Yaani hawana majina yao wenyewe kutumia kama milima waliyonayo huko kwao. These people like to copy and take everything we do!

    ReplyDelete
  15. nawafahamu baadhi ya watanzania wanaoshabikia vyama vya wakenya, sijui wanajidai east africa, wala hawajui hata source yake, na pia vinajihusisha sana sana na kenya, hatari sana watanzania ughaibuni achaneni na vitu vya wakenya kama hamvijui hao watu ni hatari sana, kama hamjui watawaletea matatizo baadae tafadhani chukueni tahadhari haraka sana.

    ReplyDelete
  16. Hivi kwani ukishuka upande wa nyuma chini ya huo mlima ni still uchaggani au ni Kenya???...Naona hii issue inakua big deal lakini ukweli hatuujui...

    1. mlima tunao tumeshindwa kuutangaza...Kama sio hawa wakenya kuutangaza huu mlima sidhani kama ungekua unajualikana hata kidogo mpaka leo kama unavyojulikana kwa sasa...

    Ni vitu vingapi vya kuvutia na kujivunia kuliko huu mlima tunavyo bongo na hatujavitangaza mpaka leo....tumekalia mlima mlima mlima mlima????????

    Kwanza hebu uliza kama huu mlima ni that so important t us ni watu wangapi watanzania wameshauona tu ...acha kuupanda...kwenda kuuangalia tu na kujua historia yake, urefu wake, miji inayouweka huu mlima...very few...ndio maana kwa vile fact hatuzijui kutekalia kulala mika tu...Haitatusaidia chochote kama hatujui ukweli....

    Je kuna mtu anaweza kuniambia ni vijiji gani huu mlima umekalia kwa mbele na nyumba...na hao wenye vijiji wananufaika kwa vipi kwa huu mlima kuwa hapo...je hela za utalii zikipatikana kuna sehemu ya mapato wanagawiwa hivi vijiji ili kujiendeleza?

    2. Kama wakenya wanaweza kuupanda huu mlima bila kuingia TZ (VISA) basi ni sisi wenyewe tu wajinga kwa kuacha hili na wana kila haki ya kusema ni mlima wao...

    Kuna mambo mengi ya kuanza kuangalia kwa sisi wenyewe kabla hajujaanza kuwalaumu wakenya kwa kutumia huo mlima kuuza vitu vyao...

    ReplyDelete
  17. Jamani tunawalaumu bure wakenya!!mie naona ni wajanja sana,,bodi ya mali halisi na utalii imelala sana,kwa hivi sasa serekali ya norway ilitoa msaada kwa ajili ya mali asili na mlima kilimanjaro,utafiti umefanyika ikaonekana hela yote imeliwa na sasa serekali ya norway inataka hela zao zirudi..si unaona bwana kwahiyo acheni wakenya wadvitizi mlima kilimanjaro maana watanzania tunashindwa kwa ajili ya matumbo ya watu wachache...mdau kyekue

    ReplyDelete
  18. Tunahitaji kuitangaza sana Tanzania, mimi nimeshaanza kupakazia kuwa Obama ni Mtanzania. Huu Mlima tukiupigia sana kelele na kuwaambia watu kuwa hauko Kenya, kitaeleweka, wao Wakenya hawawezi kufuta haya mambo, ni wezi wa asili hawa. Ukweli ni kwamba ingawa ukiwa Kenya unauona, lakini picha anayopaya mtu hapa ni kwamba ukienda Kenya utafika kwenye mlima huu, hivyo Wakenya wanapata fedha zaidi kuliko sisi kwa mtalii kukaa kwao, gharama ya kuupanda ni ndogo mno. Tunaumia tu hapo. Rais Kikwete alipokuwepo hapa Washington DC Desemba 2007, aliweka wazi hii kitu mbele ya maelfu ya watu, kwamba mlima hauko Kenya bali uko Tanzania. Tukipiga debe sana duniani Kenya wataishiwa nguvu. Mimi nadhani hata mali zao zingine zinapaswa kutangazwa kama zetu, mfano mbuga ya Masai ni kisehemu kidogo tu cha Serengeti lakini inajulikana zaidi ya Serengeti. Kwa nini tusiseme njoo Tanzania uone wanyama kwenye mbuga ya Serengeti mkoani Mara au wanaozungukazunguka Masai Mara na kuishi Serengeti, kwa sababu ni kweli pia. Pia tunaweza tukatangaza Wamasai kwenye kila picha zetu, achana na sindimba, kwa sababu Wamasai wana ujiko zaidi kwenye utalii. Nani atawaona Wamakonde (samahani Chinga wote) akitembelea mbuga zetu? Pia Ziwa Victoria tunashindwa nini kuliita Ziwa Kubwa Tanzania na Afrika? Tunashindwa nini kusema Pitishia Mizigo Yako Dar es Salaam, achana na bandari zenye vita vya kikabila?
    NAWASILISHA.

    ReplyDelete
  19. ni aje? nyinyi watz mbona hamufikiri? kama roho zenu zaumia mno, basi mka-borrow curtain kuubwa mui-hang pale kwa mpaka wa tz na kenya so that tukikwenda Amboseli National Park hatutaeza kuchukua snap za hicho kilima chenu! shikeni kazi kuji-advertise, otherwise sisi tutaadvertise.

    ReplyDelete
  20. Hivi Mnajua Historia Ya Kilimanjaro Au Kupiga Kelele Tu?? Huo Mlima Ni Wa kenya Sema Malkia Alipewa Zawadi sasa Kaondoka Basi Wenyewe Waacheni Wautumie... Kwanza Tangu Tupewe Hatujafaidi chochote Na Tuwapeni Mlima Wao Tu hatuuhitaji.Mdau Ungepiga Kelele za Tanzanite Kuuzwa sana Kenya Hapo Ningekuelewa.....( KAKA RASHIDI CHIKILIN NIPIGIE SIMU 0767099032 NINA MZIGO WAKOOOO MZEE WA KUNAWA)

    ReplyDelete
  21. Mi naona hamna cha kulaumu Kenya hapo, kama Tourism Officers wanaoajiriwa na Wizara ya mali asili ni watu wa Bcom saa ngapi wanajua kama kuna Mlima kilimanjaro na vivutio vingine?? Mimi kwakweli huwa nashangaa sana kwanini msiwaajiri watu waliosoma mambo ya Tourism na wanyama pori na kuwa maofficer Utalii wenu hao watu wa Bcom waachieni sehemu zinazowahusu. Bila kubadilika tutaishia kulalamika kila siku.

    ReplyDelete
  22. nyie wakenya mnaojidai kuponda watanzania mkome kabisa. hii sio blog ya wakenya, kwahiyo tuacheni watanzania tulalamike tutakavyo kwenye blog yetu kaka ya michuzi. na nyie anzisheni ya kwenu ili mtoe mada zinazoihusu nchi yenu.

    ReplyDelete
  23. Nyangau katupiga kanzu tena,1977 alizipora ndege zetu za East African Airways...2008 anataka kutuibia mlima wetu...JWTZ hebu rudini kutoka Comoro kwani mnahitajika Namanga Arusha!!!

    ReplyDelete
  24. ASILIMIA KUBWA HUMU GLOBUNI NI WAJINGA HUU MLIMA UPO KWELI TANZANIA NA UNAITWA MLIMA KILIMANJARO NA PIA UPO KENYA UNAITWA MLIMA KENYA. KAMA ILIVYO LAKE NYASA TANZANIA NA LAKE MALAWI THE SAME LAKE TWO DIFFERENT NAMES HAKUNA MAKOSA YOYOTE MLIMA HUU UKO BORDER. ACHENI USHAMBA NENDENI SHULE BOX TUUUUUUU SHULE MMMMMMM KINA MAIMUNA WENGI SANA BLOG HIIIII!

    ReplyDelete
  25. mi nimesikitika sana kwa jambo hilo. ila cha muhim ni sisi watz tuamke na tuanze kujitangaza nje.nahisi tunazo ofisi nyingi sana za utalii hapa tz(tour & travel agency)but still hatutoki kwa nini? au hatujajua target za wenzetu?
    mlima kilimanjaro upo tz ila na kenya unaonekana ingawa si wao,na wakiusnep na kujiadvitise ni wao hilo si kosa lao inabidi na sisi tufanye kwa upande wetu.big up sana michuzi.
    mi mdau mpya ritha.

    ReplyDelete
  26. Keep it up Kenyans! I really like it.'USIMWAMSHE ALIYELALA,UKIMWASHA UTALALA WEWE!'.Nyie si mahodari wa kuunda Tume kuichunguza Tume nyingine kabla hata haijatoa matokeo ya uchunguzi.Sasa undeni Tume itembee Duniani kote kuulizia Mlima Kilimanjaro unajulikana kiasi gani.Bajeti yake inaweza kuwa kiasi cha Shs.Bilioni Kumi hivi.Pesa kidogo sana kwa utajiri wa Tanzania!Mwisho itafikia hatua ya kufikiria kujenga ukuta ndani ya maji ya ziwa ya Victoria ili Wakenya wasinywe maji ya ziwa yanayotoka upande wetu kuelekea Kenya!HUU NI UJINGA ULIOJE ULIOKOSA HATA CHEMBE YA BUSARA ZA KIBINADAMU!Mimi naanza kuingiwa na wasiwasi kwamba hawa wanaoleta mijadala ya aina hii katika Blog hii ya Michuzi ni Watanzania wenzetu kweli au ni Mamluki waliotumwa kuja kutuchokonoa ili tukosane na Wakenya?Kwa bahati nzuri Wakenya ni watu wenye akili sana na wenye upeo mkubwa wa kupambanua mambo!Kuna tatizo gani kuutumia mlima Kilimanjaro ambao unaonekana hata ukiwa nchini Kenya kuutumia ili ku PROMOTE utalii nchini Kenya?Tusiwe wajinga kiasi hicho ndugu zangu watanzania.WAKE UP!Tuna rasilimali ngapi hapa nchini?Tuna Vivutio vingapi vya Utalii hapa nchini?Nani anaye nufaika na mapato yatokanayo na vivutio hivyo?Watanzania wangapi wanao fahamu kwamba kuna picha za filamu za kibiashara zilizowahi kupigwa katika vivutio vyetu mbalimbali vya utalii hapa nchini huko miaka ya nyuma lakini watanzania wenyewe walio wengi hawajapata kuziona hizo filamu japo hata mara moja?Hoja zinazo tolewa katika Blog hii kuhusu masuala kama haya ya mlima Kilimanjaro yana faida moja kubwa kwamba yametuwezesha kutambua ni kiasi gani Watanzania baadhi yao walivyo wajinga na mbumbumbu wa kutupa katika masuala ya biashara siyo ya utalii tu peke yake bali katika mambo mengi zaidi!Kuna huyu aliye ng'ang'ania kwamba Tanzania imekuwa ikitoa tangazo la kuvutia watalii katika televisheni ya CCN!Ningependa kumuuliza hayo matangazo yalitoka mwaka gani,mwaka 1856?Maana sisi wengine tunalala na televisheni mabegani mwetu usiku kucha!Or Was it a GHOST ADVERTISEMENT MEANT FOR THE BLIND? Hebu ona aibu kidogo kwa kusema uongo,wewe ni mtu mzima na mcha Mungu siyo?Kwanini uwageuze Watanzania wote ni wajinga kama ulivyo wewe.Pleeeeeeeeeeeeaaaassee!

    ReplyDelete
  27. Habari zenu wazalendo! Mimi nadhani ishu hapa ni kwamba mlima upo wapi na sio kwamba mlima unaonekana kutoka wapi. Hao waliotoa pointi kwamba eti watanzania hatujafanya kazi nzuri ya kuutangaza ndio maana wenzetu wa Kenya wanafanya hivyo sidhani kwamba ni sahihi; Mfano hai huu>> Mimi nina sehemu za siri, kwa sababu sijazitangaza haimaanishi sina, swala ni kwamba ni za kwangu; na wewe huwezi kutangaza ni zako wakati zipo mwilini mwangu...wadau nadhani mmenipata. jamani nimekosa mfano hai kuzidi huo. Hiki kitendo cha wakenya kusema mlima kilimanjaro upo kwao siyo shware ila wanaweza kusema ukikaa kona fulani kule kwao unauona vizuri.

    Ahsanteni!

    ReplyDelete
  28. WEWE UNAESEMA MATANGAZO CNN UONGO YAPO YANAONESHWA NI KWELI YAMEANZA MWAKA JANA 2007.WEWE MDAU MWENYE MFANO WA MLIMA KILIMANJARO KAMA SEHEMU ZAKO ZA SIRI NAH UR WRONG SEHEMU ZAKO ZA SIRI FANANISHA NA TANZANITE KWA VILE ZIKO ARDHINI CHINI NA BADO WAKENYA WANAKUPIGA BAO ,ALAFU KILIMANJARO FANANISHA NA SHARUBU ZAKO AU CHOO CHA USWAHILINI WATU WANAKULA CHABO WAKATI WA KUOGA.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 08, 2008

    MDAU MMOJA AMESEMA UPANDE WA PILI MLIMA HUU UNAITWA MLIMA KENYA HUO NI UONGO MKUBWA, MLIMA KENYA UPO MBALI SANA NA MPAKANI KAMA SIKOSEI UPO KATIKATI YA KENYA, GEOGRAPHY HAIPANDI NINI!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...