Home
Unlabelled
mshindi wa bongo star search 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ni kigezo gani kimetumika kumpata huyo mshindi?asanteni
ReplyDeletejapo mvuto mdogo wa sura but naamini ana kipaji maana rita na kundi lake wanafanya kazi ya mchujo fair. Big up BSS
ReplyDeleteMimi mwenyewe najiuliza kwamba walitumia kigezo gani labda sauti kwa sababu maana ya BSS ni mtu mwenye kipaji cha kuimba nadhani alikuwa anastaili Rogers kwa sababu kwanza ni mtunzi halafu anatumia beat yake mwenyewe kwa kupiga gitaa na hapa bongoland wasanii wetu hakuna anayejua hata kupiga gitaa namkubali Rogers
ReplyDeleteKatochi)
MICHUZI SEMA SAMAHANI HUYO WA CHINI SIO MISOJI NI BABY MADAHA ALITOKA KWENYE MCHUJO,
ReplyDeletekigezo ni kura za watanzania
wabongo muwe mnakubali matokeo. nyie kila shindano mnahoji kuhusu mshindi.kha! inaboa sana hiyo.
ReplyDeleteHongera sana Misoji. endeleza kipaji dada na hizo offer nyingine za kupiga book..peace..
BSS, Mashindano yasiyokuwa na vigezo vinavyoeleweka, kila jaji anakuja na lake.
ReplyDeleteRoggers ndiye mshindi halali, kama vile walivyoboronga mwaka jana kumpa Jumanne Iddi badala ya Leah Mudi.
Mwaka huu tena wameboronga kumpa Misoji badala ya Roggers.
Pia nafasi ya Elinema na Yohana hazikutulia... Yohana angetakiwa amtangulie Elinema...
Mwangaza hakustahili hata kuwepo kwenye Tano bora. kama ni issue ya Kuimba she is not good at all!
Hata mimi namkubali Roggers Luca kwa uwezo wake wa kuimba na kupiga chombo cha muziki angalau kimoja(Gitaa),labda waandaaji wameangalia jinsia pia maana mwaka jana alishinda mvulana kwhy mwaka huu nahisi wasichana wamepewa nafasi zaidi ili shindano zima lionekane liko fair ili wasichana wasivunjike moyo kushiriki mwakani.
ReplyDeleteHongera kwa mshindi,ila asiongeze huo mkorogo unatosha!
hivi michuzi unahabari kuwa misoji ni wa jina wako?
ReplyDeletekwa kisukuma misoji ni michuzi.
Majaji mmechemka pale tu muliposimama wote kumshangilia huyo mshindi wenu mara tu alipomaliza kuimba wimbo wa pili , inaonyesha jinsi gani mulivyokuwa mumemtayarisha , inasikitisha hata mzee kuona hata kitine nae alipagawa ,hata kama mshindi alistahili kuwa huyo mliyemtangaza kitendo kile kiliashiria kuwepo kwa mchezo mchafu ndani ya shindano lenu,mwisho nawashauri shindano lijalo kama litakuwepo washiriki watumie nyimbo zao wenyewe badala ya kuiga maana tumeshuhudia baadhi ya majaji wakizikandia baadhi ya tungo za watu,sina uhakika kama huwa mnapata ridhaa ya wenye tungo zao kuzitmia .
ReplyDeletejamani wabongo acheni wivu na kulalamika kwa vitu visivyokuwa na mpango, mshindi alikuwa anapatikana kwa kupigiwa kura na watanzania, hivi nyie mnaolalamika hata kura mlipiga kweli? mngewapigia kura hao watu wenu ili washinde, BIG UP MISOJI unastahili mama, mimi mwenyewe nilikuwa nakupigia kura kwa wingi sana. WENYE WIVU WAJINYONGEEE!!!
ReplyDeletehuyo wa chini ni baby madaha misupu umekosea,hata hivyo ilitakiwa ushindi apewe rogers lucas maana anakipaji cha kutunga nyimbo na kupiga gitaa vizur wengine walikuwa wanaimba nyimbo za wanamuziki wengine sana.anyway yote hayo ni kampeni tu ndo zilimshindisha misoji,rogers u rock
ReplyDeletembona wanaoshinda wote wametokea bagamoyo,mwaka jana jumanne idd alikuwa wa bagamoyo na misoji ni wa bagamoyo,sio bure hao tehe tehe tehe
ReplyDeletemimi simfagilii misoji kabisa,kuimba nyimbo za watu wengine ndo kipaji? kipaji anacho rogers haya mambo ndo kama ya mwaka jana abubakar mzuri kuingia 3 bora alafu anakuja kutoa nyimbo anacopy beats ya 2 face wa nigeria ila anaimba kwa kiswahili wat a shame
ReplyDeleteHiyo Bongo star ni biashara na mambo ya kuiga Western culture..iweje watoto hao wanaiga nyimbo za watu ..na kutunzwa mapesa kibao wakati kuna wanamuziki Kama akina Ngurumo wameanza kuimba hata baba zetu hawajazaliwa..lakini mpaka leo wanasaga vumbi hakuna hata mtu wakuwaandalia..matamasha kama hayo .. leo unaiga wimbo .. Ngurumo ..na kuonekana wewe mahiri ..na kuchukua kibunda kinene wakati mwenyewe mwenye wimbo.. hata nauli ya DALADALA hana ,!!! wenzenu ..America ..wanafanya hivyo ..tayari wanamuziki wao wakongwe wameshaukata hivyo wanatafuta .. chipukizi ..
ReplyDelete...Ombi ni kwamba tusishabikie sana kuwainua watoto wanoimba kwa kukopi nyimbo za watu na kuwasahau wenyewe wenye ..hizo nyimbo ...
kwakeli misoji hajanifuraisha kabisa hata maneno ya i will always love alikua anayataja kamtu ambayo hajui english, kwakweli simuimbaja SHE NEEDED MORE TRAINING.
ReplyDeleteROGGERS WAS TO WIN THE THING
We annon wa mar 31, 8:03 Kumbuka kura yako ndiyo ingeweza kumpitisha mshiriki ambae wewe umemuona bora, hata hao waliotoka awali ni watanzania wenyewe ndio waliyowaangusha,kwa kutowapa kura ingawa walikuwa wanajiweza pia hiyo ni kwa kipindi kile na wimbo aliouchagua na jinsi alivyouwakilisha kwa watazamaji na kama wimbo huo unapendwa au vipi gani. sasa hapa kukaa na kuanza kulaumu kuwa hakufanyiwa haki, ni kwamba na wewe ulichangia, kwanza labda ungejiuliza ulituma msg ngapi kumuokoa huyo mshiriki ulompenda awe mshindi, kisha uanze kutoa lawama kwamba wewe binafsi ulitumia laki moja kutuma msg kumuokoa mshiriki wako hapo naweza kukubaliana nawe, usiwe mlalamishi tu bila kujua biashara yenyewe inaendaje! au kulaumu majaji kuwa walishamuandaa mshindi wakati kura zilishapigwa wiki nzima na zilishasomeka sio uamuzi wa siku ile baba ni kura na wimbo aliouchagua mshiriki na upenzi wa wasikilizaji na watazamaji pia usisahau zile idadi ya kura ambazo ziligarimu hela wakati unampigani amshiriki wako. Ah pole mimi si msemaji wa shindano ni mtazamaji wa kipindi tangu walipoanza na nilikuwa najiskia vibaya kila mshiriki alipotolewa kwa kuwa na kura ndogo, sikuwahi kupiga kura mimi binafsi ila pale watoto wangu walipokuwa wanawashabikia washiriki wao, walikuwa wananiomba simu yangu ili wapige kura hivyo nilikuwa nabaki na salio dogo kila usiku wa j'pili ili waendeleeze ushabiki (mpambano)wao nami napata burudani kutoka kwa watoto wangu pale wanapojitahidi kutoa utabiri wa washindi au nani anaimba vizuri au nani atatoka ni katika kuwafundisha kuelewa mambo ya ushindani na kuwapa uhuru wa kuweza kutoa maoni na kuona kipi kiko sawa na kipi hakiko vema.
ReplyDeleteRita & Salama mko wapi? hebu wape maelezo ya ushindi unakujaje na ya kuwa nani jaji wa mpambano huo kwani naona hapa bado wanaona waamuzi mlikuwa nyie il-khali walikuwa wao wenyewe nyie ni watayarishaji na waongozaji tuuu salama mwenetu wagambile mbiyangu wayaowalioko mbali na wale wanaoona hawakuridhika.
Huhitaji kuwa mtaalam wa muziki kuelewa kwamba vigezo vya mwanamuziki aliyestahili kushinda shindano hilo la BSS, ni (1) kuwa na uwezo wa kuimba kwa ufasaha, (2) kuwa na uwezo wa kutunga nyimbo, hata kama ni kwa mtindo mmoja, lakini kwa umahiri mkubwa (hakuna anayeweza kutunga kwa mitindo mingi kwa umahiri...), (3) kuwa na uwezo wa kupiga chombo, angalau kimoja, kwa umahiri, na (4) kuwa na uwezo wa ku-perform akiwa kwenye stage, ingawa hii si muhimu sana. Wapo wanamuziki kama India Aire ambaye anapiga gitaa na si mchezaji mzuri akiwa kwenye stage... orodha ni ndefu.
ReplyDeleteRogers Lucas aliweza haya yote, na alikuwa kipenzi cha Watanzania wengi na watazamaji wengi. Wote hawa wameshangaa kuona kwamba hakupita.
Misoji alikuwa akiimba nyimbo za wanamuziki wengine, na si kwa umahiri. Wimbo aliouimba siku ya fainali, "I'll Always Love You" ambao ulitungwa mara ya kwanza, na kuimbwa na Dolly Parton, hatimaye Whiteney Houston, haukutendewa haki na Misoji. Whitney Houston anaimba kwenye viwango vya Tenor na Soprano. Kwa wanaoujua muziki watanielewa hapa. Misoji anaimba kwenye kiwango cha Alto, ambacho ni sawa na cha Toni Braxton. Kwa muda wote alipokuwa mshiriki alijaribu kuimba (na kushindwa vibaya) katika kiwango cha Tenor, jambo ambalo ni nje ya uwezo wake.
Yohana alimzidi uwezo mkubwa Elynema, nimeshangaa kuona Yohana akishindwa na Elynema, ambaye alitolewa ufafanuzi na majaji kwamba uwezo wake ni kwenye nyimbo za Injili pekee!
Maangaza, ambaye si mzaliwa wa "pwani" ana uwezo mkubwa wa kuimba nyimbo za Taarab, kwa hiyo alistahili kabisa kupata ushindi wa nafasi ya tano, ingawa siku ya fainali alipata "stage fright", akashindwa kufikia kiwango chake stahili. Watu wengine hupata wasiwasi, hiyo inaeleweka.
Jambo la Misoji kushinda nafasi ya kwanza kwa kweli limevuruga maana halisi ya "kutafuta vipaji", na sidhani kama wadhamini watakuwa tayari kutoa udhamini wao mwaka ujao, iwapo waaandaaji wa shindano hili WATADIRIKI kurudi tena kwao na kuomba udhamini. Ninawashauri watafute jambo lingine la kufanya. Binafsi ninawafahamu Master J (ni rafiki yangu), Ritha (niliwahi kufanya naye kazi... lakini hatukuimaliza), Salama (ninamfahamu vema), Kitime (simfahamu). Kwa hao ninawaowafahamu, nawauliza, "Je, mnaweza kulala usingizi mzuri mkijua mmeshiriki kwenye ufisadi wa kutomtendea haki Rogers?"
Kama kweli kigezo cha ushindi kilikuwa ni kura alizopata mshiriki, mbona kura hizo hazikutangazwa? Mngekuwa mnatangaza kura zinazopatikana kwa kila mshiriki, kila wiki, tungejua kwamba hakukuwa na upendeleo. Lakini inaonekana kwamba mshindi ALIPANGWA kuanzia mwanzo wa shindano, na yale machozi yake aliyoyalia Misoji kwenye ukumbi ule yalikuwa MACHOZI YA MAMBA!
Msitudanganye, sisi si watoto wadogo. Hamna haya?
Michuzi kwanza itoe hiyo picha hapo juu, huyo sio Misoji ni baby Madaha.
ReplyDeleteNi kweli Misoji alishinda na anaimba kweli, ila majaji hawakuwa professional. hawana sifa kabisa ya kuwa majaji, walikuwa wanapayuka hovyo, sijui hata kwanini hawaangalii tamasha zingine majaji wana behave vipi.
Hata madam Rita alisema maneno haya wakati Rogers anaimba "next time ingewezekana basi washindi wangekuwa wanatoka wawili" hiyo ilikuwa ni msg tosha kwa Rogers kuwa hakuwa mshindi katika shindano lile. Sijui Benchmarck Production ilitumia vigezo gani katika kuchagua majaji. Next time itabidi wawe careful.
Asante sana mmetuburudhisha but mmechemsha sana mwishoni.
HAKUNA UBISHI MISOJI ALIKUBALIKA,ACHENI WIVU NA MARUMBANO YASIYO NA MSINGI,WATANZANIA KILA KITU MNABISHA ACHENI HIZO
ReplyDeleteJAMANI WENYE MASIKIO KWANI HAMKUSIKIA? BAADA YA ROGERS KUMALIZA WIMBO WA PILI, MADAME RITTA ALISEMA "ROGERS HONGERA SANA BAHATI MBAYA BSS TUNATAFUTA MSHINDI MMOJA TU, ILA WEWE NI MSHINDI PIA", HIYO INAMAANISHA TAYARI MSHINDI ALIKWISHAPATIKANA NA TAYARI WALISHAKUWA WANAMJUA, MISOJI ZAIDI YA KUTETEMESHA SAUTI HAKUWA NA KITU KINGINE!!! ME KWANGU MSHINDI NI ROGERS TU JAMANI, KWA ELINEEMA KWELI WALICHEKESHA JAMANI KUWA WA 3, LABDA KAMA MAKANISA YOTE YALIMPIGIA KURA!! HA HA HA HAAAAAAA
ReplyDeletehi,BSS woote kwanza nawapongeza sana na majaji wote lakini naomba madam rita watafute ka website ili kupata mawazo ya watu wengine juu ya shindano liliovyokwenda lakini nadhani mshindi alistahili kushinda na hasa baada ya mshindani wake baby madaha kutolewa kwakweli haikuwa haki kwa yule dada kutolewa mapema kwangu mimi ilikuwa ndiye angeyatia msisimko ya kutosha yale mashindano
ReplyDeleteKiukweli kabisa aliyekuwa amestahili kushinda kwa kungalia tangu mwanzo wa mashindano haya mpaka hiyo fainali ni RODGERS LUCAS, the boy is a musician na sio muimbaji tu kama walivyokua washiriki wengi. kwa walichokifanya au kufanya mwaka jana ndio maana washindi wao wanaishia kubahatisha tu wakiingia mitaani. Napenda kuamini kuwa haya maamuzi yamelenga zaidi kwenye kubalansisha gender kwamba mwaka jana kashinda mwanaume basi mwaka huu awe mwanamke. Misoji hongera na wewe kwani unajua kuimba ila hujamzidi Lucas. Lucas is the winner BSS!!!
ReplyDeleteHAYA MASHINDANO NI YA KIUJANJA UJANJA FULANI, MAJAJI HAWAELEWEKI, WAPO WAPO TU KAMA WATU WALIO KURUPUSHWA KIPINDI WAKIWA WANATOA MAWAZO YAO KWA MSANII. NAOMBA WATUMIE KIPINDI HICHI KUJIFUNZA KWA WENZAO WA TUSKER PROJECT FAME- KENYA. INGEKUWA VIZURI PIA MATOKEO YA KURA ZA WATAZAMAJI ZINGEWEKWA HADHARANI PAMOJA NA WATAZAMAJI KUELEZWA NA FASI YA JAJI KWA MSANII NI IPI,ILI WATAZAMAJI WAWEZE KUFAHAMU. SIO HUU MTINDO WA KUPANGA MATOKEO MEZANI. MAJAJI WAMEONYESHA UDHAIFU WAO MKUBWA SANA, TOKA TOP 5 ILIPO PATIKANA.
ReplyDeletef-amo@hotmail.com
Jamanieeem, acheni wivu na roho za kwanini! MISOJI alistahili haswaa kushinda na ndo maana watanzania walio wengi walimpigia kura na kuibuka kidedea! Nyie mnaosema eti Rogers ndo alikuwa kipenzi cha watanzania wengi, mna uhakika gani? Mnaweza ku-prove? Kama ndivyo mbona kura zilimwangusha? Hii inadhihirisha Misoji alikubalika zaidi kwa wapenzi. Acheni wivu na lawama zisizo na msingi. Anzisheni nanyi mashindano yenu muweke vigezo mvitakavyo! Ooh, majaji wamechemsha, ooh wamependelea, mara hivi mara vile, hamna hata aibu, nyie mbona mmeshindwa? Acheni kuwavunja watu moyo wa kusaidia vijana wetu wakati nyie hata hamuwezi, kazi kuponda jitihada za wenzenu, hamna jipya na mshindwe na kulegea na hizo roho zenu za kwanini. Majaji wote nawafagilia, Misoji hongera mama kwa ushindi wala usiwasikilize hao wapayukaji, ni kawaida yao, hata angeshinda huyo Rogers wasingekosa la kuongea, ndo walivyo! ACHANA NAO!
ReplyDeleteJamani hao wanaosema kura zimepigwa na watanzania, tuna uhakika gani kama hizo kura nyingi ni za Misoji? Wanatakiwa wawaonyeshe Watanzania kura zilivyokuwa zikipigwa kama mwaka jana
ReplyDeleteRogers anastahili kuwa mshindi
ReplyDeleteunajua hii bongo star search wapo pale kwa maslahi yao binafsi lakini sidhani kama kweli wana nia hiyo ya kutafuta star.
ReplyDeleteROGERS LUCAS alikuwa na kila sababu ya kushina kwani pale hakuna alieweza kushindana nae kabisa, sasa wao wametufanyia usanii tu kujifanya kumuweka huyo MISOJI wao. misoji zaidi ya msauti wa kutetemeka hana kitu yule kabisa zaidi ya Rogers.
Mungu awaalaani kwa kupanga matokeo yenu na kama ni hivyo ni bora muache tutafanya kampeni hakuna mtu kushiriki ili muwape mnaowataka. hamna lolote nyie Benchmark hasa huyo Madam Rita msanii tu.
majaji wenyewe wote washamba tu hamna mzoefu hata mmoja wala nini nendeni kule. na mwakani muwalete watoto wenu waje washiriki unafikiri nani atashiriki kwa kumsindikiza mwenzie?
be carefully madam Rita, umejishushia hadhi sana kwa matokeo ya majuzi, huna lolote.
ROGERS, usife moyo wala nini wewe ni STAR wa ukweli na Mungu atakujalia utaendelea mbele sana tu achana na hao wasanii wa kupanga matokeo.
Hakuna ubishi misoji kavuta mihela hiyo hongera sana misoji!!!! Hao waliotaka Rogers ashinde wangepiga kura zao za kutosha kumpitisha watu wabahili lakini mnajua kulalamika kama nini!!! lol! sijui Rogers alitakiwa kushinda kama ingekua hivyo basi angeshinda. Anzisheni vitongoji star search na nyie mumpange mnaemtaka. Na hizo picha zote ni za misoji hakuna ya baby madaha hata moja!
ReplyDeleteHongera Misoji, unastahili haswaaaaaaaaaa taji hilo, acha wenye kuosha vinywa waseme watachoka tu. Madam Rita wala usiwajali, maana ni kawaida yao, hawana mpya, wewe endeleza libeneke, nasi wazalendo tupo nyuma yako. Wewe unayesema utaanzisha kampeni ya kumsusia madam umechemsha, tunaomsapoti tupo wengi sana, pole zako.
ReplyDeleteAcheni ubinafsi, Misoji anastahili kabisa kuwa bongo star kuliko wenzake wote alioshindana nao. Nyie mnaompinga ndo mnaonekana wazi kuwa mna ubinafsi,na kwa kuwa tayari mlishajipangia mtu wenu (Rogers) na asifanikiwe ndo maana roho zinawauma! Poleni, lakini ukweli unabaki palepale, mshindi aliyestahili ni Misoji na itabaki kuwa hivyo!
ReplyDeletemajaji hawako professional
ReplyDeletesalama ana mambo ya kihuni sana hata akimjaji mtu unashindwa kuelewa kajaji nini sasa mambo ya doro wengine hatuyaelewi,
pili tungependa kujua kura hadharani na tuonyewshwe kwenye computer idadi
tatu ,kuhusu majaji haohao kama wimbo hawaujui wala hauwavutii walikua wanamkandia wanamjaji mtu kaimba vibaya, huyohuyo salama ana watu wake kama mtu alikua hampendi toka mwanzo hata aimbeje alikua hamsifii mfano( baby madaha, mary banyukwa,mshiriki kutoka mbeya anaitwa ombeni na hata mangaza) alikua akiwapendelea live feisal na misoji na rogers kidogo
yule wa reggae nilijitajidi sana kumpigia kura zangu zilikua haziendi kabisa kutoka no yangu ya tigo niliweka 10,000, na wimbo wake wa ukimwi mi nashangaa waliukandia ila ulikua mzuri eti ni wa mafumbo sana
next time tunaomba maprofessional jurges sio wanaoshushua watu kama mastar j alivyomshushua mangaza kwa mpasuo ,tunaangalia kazi sio mipasuo
asanteni
Bss ni mradi tu,watu wanapiga hela....coz wasanii wengi wanao-run Game hawajapitia BSS na wako vizuri ni mtazamo wangu,ron BUKA
ReplyDelete