Hello michuzi naomba kuomba msaada kwenye tutas!!
Mimi bwana michuzi sielewi nini maana ya neno mzungu!kuongea kizungu ndio uitwe mzungu? Je mchina, mhindi awezi kuwa mzungu? kukaa ulaya ndio kuitwa mzungu? na muafrika asilia akiongea kizungu na kujipaka mkorogo anaweza kuitwa mzungu?
asante sana
Mdau Kyekue.
Wazungu wana toka ulaya mfano USA na Australia kuna wazungu ambao asili yao ni ulaya. Michuzi ukimuita mzungu inakuwa kama utani kwa sababu labda ana mambo ya kizungu kizungu (utamaduni)
ReplyDeleteWahindi na Wachina/wajapani n.k wanasimama kama walivyo ingawa nao wana majina kama gabacholi.ingawa wote wako kundi la caucasians.
caucasoid-europeans & asians
negroid-waafrika
mongloid-red indians, maori & chapatians
Austreroid- Aborogians & kiribatians
Katika kufuatilia historia ya neno MZUNGU;inatokana na kitendo cha kuzungukazunguka.
ReplyDeleteWatu weupe wakwanza kufika huku kwetu walikuwa na malengo yao na kwakuwa wenyeji iliwawia vigumu kuelewana nao na kuelewa malengo lao ilinekana kama vile hao wageni wanazunguka zunguka tu katika maeneo yao na hapo ndipo walipowapachika jina la MZUNGU au WAZUNGU kutokana na kuzungukazunguka hapa na pale.Kwa maana nyepesi MZUNGU au WAZUNGU ni mtu yeyote anaezunguka huku na kule kwa lengo la kutalii never mind awe mweupe au mweusi wa blue au manjano.Katika Lugha, hakuna Lugha ya kizungu na wala mtu hawezi kuongea kizungu kwa kuwa Lugha hiyo haipo isipokuwa kuna Kiingereza, na wanaoongea au kuzungumza Kiingereza wanitwa WAINGEREZA.
Mzungu ni watu wanaotoka mabara ya ulaya, inachanganya kiasi chake hata mzungu mtu mweupe pia. mie naona mzungu ni mtu mweupe unaweza kusema mzungu wa kutoka africa au mzaliwa wa africa, anakuwa mwafrica tu kuwa mwafrica si kuwa mtu mweusi. kuna wahindi, waarabu, mchanganyiko. Australia wazungu wakule wengi walikuwa wanatupwa na uwengereza sababu walikuwa wezi walevi majambazi miaka ya zamani. wenyewe wenye Australia ni waborijian. unaweza ukazalia africa ukaambiwa jamaa anatabia za kizungu. wengi wanaona kuwa natabia za kizungu ni nzuri ila nyingi mbaya kuliko nzuri.
ReplyDeleteSawa na Sie watu wa Tanzania Bara, kusema Wamanga koko, Wamanga wanatokea Oman ila tunaona Wamanga ni wote wanaotokea uwarabuni. Wazungu ni Asili wanaotoka Ulaya, wengi wao kuna Wazungu wanatoka Africa vilevile ni Waafrica.
ReplyDeleteTanzania huku Bara tunaita watu wakutoka Pemba, Wapemba wakati Pemba ni Kisiwa si Kabila, Je? Tunaweza kuita Watu kutoka Moshi, Wamoshi Badala ya kuita Wachaga? haiji siunaona mie Swali langu Watu wa Pemba Kabila Lao Nini? Washirazi ni Unguja msichanganye na Chama Chama ni Afro Shirazi.
Asili ya neno 'Mzungu' linatokana na 'Mzunguko'. Wazungu (hasa waingereza na Wajerumani) walipokuja kwetu walikuwa wanafunga vifaa vyao (kama magari) kwa kutumia nati za kuzungusha, matairi yalikuwa ya kuzunguka hata ya gari moshi, walikuwa na taa za mzunguko na vitu vyao vingi vilikuwa vya kuzunguka (kwa kimombo round). Hii ndio asili ya wahenga wetu kupata neno 'MZUNGU'.
ReplyDeleteMzungu vilevile inamaanisha jinsi yaani mbinu au maarifa. Mfano ni methali "mzungu wa kula haufunzwi mwana" ambayo ina maana mtoto hafundishwi jinsi ya kula.
ReplyDeleteWazungu ni watu kutoka Ulaya, badala ya kuwaita waUlaya kama ilivyo kwa watu kutoka Afrika wanavyoitwa WaAfrika, na watu kutoka Amerika wanavyoitwa WaAmerika au watu kutoka Asia wanavyoitwa WaAsia..... Watu kutoka Ulaya huwezi kuwaita waUlaya ndio maana wanaitwa Wazungu...
ReplyDeleteNI USHAMBA TULIONAO WAAFRICA. MTU AKIFANIKIWA, AKITOKA ULAYA, AKIPENDEZA, NGOZI YAKE IKING'ARA, YAANI FULL A/C BONGO WANAMUITA ZUNGU, HASA AKITOKA ULAYA KUUZA MADAWA YA KULEVYA WANAMUITA ZUNGU LA UNGA. WAKATI UKU ULAYA SI TUNAITWA MA NIGGA NA WENYEWE WANAITANA MAJINA YAO VIZURI TU. MI WANANGU AMBAO NI WAJANJA KIMAISHA NAWAITA BAARIYAA, AU MNAONAJE WADAU. AWA JAMAA WASITUTAWALE KIAKILÍ.AINA UKUDA BAALIYA WANGU TUNASONGA MBELE!!!
ReplyDeleteneno mzungu lina present white peolple, na watu kama wahindi,waarabu ,china, vietnam wao wanaitwa kwa uraia wao ama bara watokalo, kawaida yetu wabongo hupenda kuitana majina kutokana na utashi wa mtu either unavyo behave ama jambo unalo fanya usishangae kuitwa mzungu,mara jackchain,muarbu,osama basi ilimradi akuitae aridhike yeye
ReplyDeleteKyekue,
ReplyDeleteUsihangaike sana. Kwa ufupi wewe sio mzungu. Hata ukae Ulaya miaka 20 hautakuwa Mzungu.
Papaa Chibiriti analijua hilo. Japo kasogeza mzungu hana wasi wasi na identity yake kuwa yeye ni Chinga hata awe wapi.
Habari ndio hiyo.
Watu wengi waliotoa maoni hapa inaelekea wanachanganya asili na matumizi ya neno 'mzungu.' Kwanza sidhani kama neno hili asili yake ni nati au matairi ya garimoshi kama mdau mmoja alivyosema hapo juu. Kama alivyosema mdau mwingine, inawezekana neno hili lilitokana na tabia ya wageni wa kwanza wa Ulaya 'kuzunguka-zunguka' walipofika nchini kwetu. Wengi wao walikuja kutafuta malighafi na sehemu zenye rutuba zitazofaa kwa kilimo. Inawezekana walikuwa wakitembelea/wakizunguka sehemu mbalimbali. Hii ndio yaweza kuwa asili ya neno 'mzungu.' Kwa mantiki hii maana ya neno mzungu kwa kiasi fulani imepotoshwa. Hivi leo neno hili linamaanisha mtu mwenye asili ya Ulaya kwa sababu 'wazungu' wa kwanza walikuwa watu wenye asili hiyo. Kuna waafrika weupe wengi ambao bado pia tutawaita wazungu kwa sababu ya asili yao. Kama tunaamini asili ya hili neno, basi kufanya hivi ni makosa. Vile vile kutumia neno 'kizungu' badala ya kiingereza/kijerumani, n.k. ni makosa pia. Inawezekana hapo awali watu walitumia neno 'kizungu' kwa sababu hawakujua lugha mbali mbali za Ulaya zilizozungumzwa na wageni hawa. Haikuwa rahisi kwao kuchanganua tofauti kati ya lugha mbali mbali za Ulaya.
ReplyDeleteNyie wote mnaongopeana.. humjui kwamba kiswahili ni mchanganyiko wa lugha mbali mbali .ikiwewo asilimia kubwa kiarabu .na baadhi ya maneno toka katika lugha za kingerza ,kidachi, kireno na lugha mbalimbali za kibantu....
ReplyDeleteNeno mzungu asili yake ni South Africa
linatoka na Lugha ya kizulu,MLUNGU
yaani watu weupe..ikumbukwe wazungu South Afrika wamefika toka mwaka 1652..Ras of Good Hope
now is known as CAPE TOWN.. hivyo wenyeji wa hapo waliwaita WALUNGU
..nitakupa maneno machache ambayo lugha ya kiswahili inayatumia kutoka makabila ya South Afrika..
Nywele- Ndwele
Mzungu -Mlungu
Mleteni- muleteni
anon mar 30, 3:33 Mimi ntakuita chotara wa kiarabu, zaidi tena ntakuita muoman wa pemba.
ReplyDeleteparagraph yako ya pili imenisuuza pia umelileta wakati muafaka, pale wanapoita watu wa mwambao waswahili hasa wanaotoka zanzibar, tanga na bwagamoyo huitwa waswahili hebu we mswahilina hapo juu, hiyo swahilina kwa maana ya uswahili au swalihina kwa maana ya swali au suali/swahili(waulizaji au wadadisi?)hebu pia tusaidieni enyi wenye kujua .
mzungu ni TABIA na wala siyo rangi.watu kama waingereza ambao wapo mbele sana kwa haki za binadamu ndo wanao onekana wazungu halisi.Mtu kama mpolish,mgiliki na weupe wengine washenziwashenzi na maskini hao huwezi kuwaita wazungu.
ReplyDeleteKumbuka kwamba wazungu kama waingereza na wamarekani ndo waliokataza biashara ya utumwa, kutocha hasa wafungwa, kuondoa madikteta madarakani, UBAGUZI WA RANGI AU JINSIA ili kila mtu ainjoi dunia.Hao ndo wazungu,na wala siyo Rangi unless unataka kuniambia kwamba M'BATA(Mturuki) nae ni mzungu???!!!!.
We anonymous wa 7:03:00 PM EAT sijui unakaa dunia gani. Kwanza elewa kuwa Ashley Cole wa Chelsea au Mike Tyson pamoja na kuwa kwao ni Uingereza na Marekani SIYO WAZUNGU. Michael Schumacher au Vladimir Putin NI WAZUNGU kwa ainisho linaloelweka kwenye lugha yetu ya Kiswahili. Kitu cha pili nashangaa unakuja na historia yenye kuwasifia wamarekani na waingereza kuwa ndio walizuia utumwa. Mbona husemi kuwa wao walishika mstari wa mbele katika biashara hiyo haramu wakiwafuatia Wahispania na Wareno kwa miaka mingi hadi pale walipoona biashara hailipi tena ndipo walipoanza kuwareejsha visiwani na hadi Liberia. Soma historia vizuri.
ReplyDeleteMzungu ni MUNGU kasoro Z unakumbuka hiyo????? Jamani tumetoka mbalii.....alikua akipita mzungu watoto tunashangaa njiani.....au kumfwata nyuma...saa hivii.....
ReplyDeleteAti hata wapanyoro waliotoka south america wanajifanya wazungu
mzungu ni kitabia kinachopatikana kwa watu weupe katika bara la ulaya
ReplyDelete