Bohemia presents Soweto String Quartet
(exclusively from South Africa)

Including:Carola Kinasha (Tanzania)
Rhoda Mshana (Tanzania)

VENUE: Sweet Eazy, Oysterbay
DATE: Saturday, 8th March, 2008
TIME: 8:00 pm - 12:30 am

ENTRANCE: Tsh30,000 in advance, Tsh40,000 on night
We invite you to purchase self or bulk corporate tickets for yet another night of quality entertainment.
Limited capacity so purchase early to avoid disappointment
Call 0754 836464 for more details.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Babake!

    Hilo onesho litakuwa la kukata na shoka. Mwaka 2005 niliibamba cd ya Zebra Crossing ya Soweto String Quartet. Baada ya kuisikiliza ilibidi nikubali aliyosema Dr Remmy "Muziki hauna mwenyewe". Hawa Waafrika wanabamiza nyuzi utafikiri wamezigundua wao?! NENDENI wanangu mkasikilize Cello, violin, guitar, double bass, harp jinsi zilivyosilimishwa na hawa jamaa toka uzungu hadi Uafrika.

    Babake, hawa jamaa wanaweza kupiga kwasakwasa kwa kutumia hivyo vyombo na ikatoka kwasakwasa kali kama ya Kanda Bongoman. Wanaweza kukupigia Kwela ikatoka Kwela kali kama ya West Nkosi. Watakupigia Benga itatoka Benga kali kama ya D.O. Misiani na Shirati Jazz. Watakuvurumishia Rhumba litatoka Rhumba kali kama la Franco Luanzo Luambo Makiada. Yaani hawa mabingwa ni noma kinoma, babake.

    Duuh! halafu nikifikiria wanachanganya mavitu yao na Shada nashindwa kupata picha! Maanake Shada nao noma kinoma, Bibie mwenyewe Carola kwenye maikrofoni, Sajura anazurura vyombo vyote na vocals, Teddy anavurumisha bass la nyuzi tano huku anaimba kama anatafuta sifa, Norman anacharaza double neck guitar kama kazaliwa nalo, Mzee mwenyewe Katibu anafumua mingoma hatari tupu.

    Shime vijana kwa wazee waibuke kwenye onyesho wakaburudike na kujifunza kwenye nafasi hii adimu.

    Muhidin, usikose kutuletea mapicha na stori za tukio hili.

    Masalaam.

    ReplyDelete
  2. Anony wa 2:44 muziki unaufahamu. Big up! Tunahitaji watu wachache kama wewe wanaoweza kutofautisha muziki muziki na muziki kuchapia a.k.a muziki makelele

    Soweto String Quartet ni wakali sana hasa wakikolezea Jive na Patapata. Nadhani ndio maana watapiga na Shada

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...