kocha jamhuri kihwelo akiwa akiwapa tizi vijana wake wa simba leo neshno
vijana wa yanga wakisubili wenzao wa simba wamalize tizi ili nao waanze leo. hii ni ishara kwamba kuna haja ya kila timu kuwa na kiwanja chake badala ya kulumangia neshno namna hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Inasikitisha sana kuona timu kubwa kama hizi hazina hata viwanja vya mazoezi. Timu zina zaidi ya miaka sabini sasa lakini hatuoni kiwanja hata kimoja. Yanga ingawa ni timu yangu lakini ule uwanja toka mpewe na CCM cbasi hata ukarabati unawashinda. Simba ndio kabisaa mara leo Chuo Kikuu mara Chuo cha Sayansi basi bugudha tupu. Kwa hali hii mtasikia redioni kuifunga Enyimba.
    Wazo ni kwamba makampuni makubwa ingieni mikataba na timu hizi mzijengee viwanja kwa mikataba maalum. Ndivyo wanavyofanya wenzetu huko Emirets au hata Vodacom cSouth Africa. Mtakaa mnamimina mipesa miss Tanzania kwa ndoto za alinacha kila siku lalalala ggooooo noh kakosah! dah nusu tuchukue miss world!! Hebu wekeza fedha kwenye soka watu tupate raha. Mkishinda miss world undahani watanzania wangapi watafarijika kama sio wakina Lundenga kupata ruhusa vizuri ya kutuharibia wanetu!! haya msije makasema mie sikusema!!

    ReplyDelete
  2. Mdau uliyekuwa wa kwanza kuchangia hii mada umenikuna sana.

    Hivi haya makampuni yanayotumia mamilioni kuwapatia kina Lundenga kutafuta warembo wa miss world wafikirika hawaoni kuwa Soka ni njia pekee ya kujitangaza kuliko hayo mashindano ya mara moja kwa mwaka? Naona wangetumia busara kudhamini hizi timu kwa kuwajengea viwanja na kuwapatia vifaa muhimu kama Emarati walivyofanya kwa Arsenal.

    Pili Vilabu vyenyewe ndo vina matatizo, nadhani hakuna mtu atakayetoa pesa yake kuwekeana mkataba na akina mzimba ama Matunda wakati vilabu ni vya mifukoni havina hata account. Cha msingi kwa vilabu vyetu kama hichi cha mimi na wewe (Yanga)kuanza mageuzi ya kiuendeshaji, vijiendeshe kama makampuni ndipo tutafika mbali la sivyo tubaki kuwa tunasubiriana kufanya mazoezi katika kiwanja kimoja.

    Mkereketwa wa YASC na YNWA

    Mchokolasi Mlaviliwe

    ReplyDelete
  3. Mimi kama Simba, inanisikitisha simba, Club ya Simba tu ni chafu hawawezi kuiweka sawa, itakuwa wawe na uwanja?. Yanga club yao ilikuwa nzuri na kiwanja ila mvuwa ikinyesha inakuwa bwawa la kuogelea. Voda walikuwa wakiwazamini wote hao sasa sijui imeishia wapi watu mvutano wa pesa tamaa na ziki zisizo na msingi, tuwache yote hayo Simba 3 Yanga 1 Issa Michuzi Fundi kasemaje kuhusu ushindi manake siku zile kakwambia liverpool 3 manchester united 0 tumefungwa mwambie aseme Yanga 3 simba 0 ili Simba ishinde.

    ReplyDelete
  4. Mimi sielewi kidogo Bwana Michuzi,Yanga wana uwanja wao wa Kaunda jee umefungwa au vipi na ni uwanja mkongwe.
    Pili kama ni hivyo hata uwanja wa Karume unaomilikiwa an TFF nao unaweza kutumika kwa mazoezi,tatizo liko wapi?

    ReplyDelete
  5. Jamaa aliyeuliza TFF wana Uwanja wa Karume kaongea Point, TFF Kiwanja wanacho usoni, kukitengeneza na kukiweka sawa hawawezi? Aibu tu Uwanja wa Taifa ni wa Taifa. Karume ni uwanja unaotakiwa Ligi za Bongo hata mazoezi msisubiri kutengenezewa uwanja, Toeni Pesa wavute mafundi waliojenga taifa, siwameona wa China walivyowafundisha kujenga? au walikuwa wanajenga akili wakaziwacha pale?. Pan African Oyeeeeeeee. Yanga bakora hazijaanza huko.

    ReplyDelete
  6. Mimi naona sasa haya makampuni yaanzishe football academies kwa sababu wachezaji hawajapata mafunzo mazuri, ukija kwenye mlo ndo kabisa, hebu waangalie jinsi walivyo wadogo kweli tutafika, msimamishe Adebayor na mmoja wao, utaona jinsi gani hatutafanikiwa kufika katika African cup of nations. Hii yote na mengineyo mengi yanatupeleka ktk football academies run by these sponsors ambao wataweza kuwajenga wachezaji kupitia mafunzo, mlo, na kadhalika.

    ReplyDelete
  7. Kwa sisi tuliozaliwa na timu hizi mbili tunaumia zaidi. Yanga wanao uwanja wa Kaunda, kulikoni? Simba zao walikuwa na uwanja wao Jangwani ambao "uliharibiwa" kutokana na ujio wa Papa John Paulo mwaka 1990, basi ndo mpaka leo hakuna kilichofanyika. Mimi kama mshabiki wa Simba, Legacy ya papa john paulo kwetu ni kutufanya tukose Uwanja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...