wadau wameomba kumuona kwa karibu zaidi bingwa wa salamu reedioni toka enzi za ukoloni hadi leo, zakaria ndemfoo wa babati ambaye anasema libeneke la salamu bado anaendelea nalo hadi leo kwa kutuma salamu kupitia redio za ndani na nje ya nchi. hata mie namkumbuka yeye, haruna damladamla wa mtaa wa ukame, issa hassa majeshi wa magereza ukonga, thobias r. mnyani wa uhuru na msimbazi na wengineo. enzi hizo ilikuwa raha kumsikia mtu akisalimiwa na hawa mabingwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. wengine ni mama Fatu Kaisi, Chivalavala M. Chivalavala, Muungwana Zomboko, ah kaazi kwelikweli

    ReplyDelete
  2. Kumbe hao ni watu hai! Kwa kweli tunawakumbuka sana. Umemsahau Juma Ramdhani Kamage wa Tabora..........! Hahahaha walikuwa wanatutia raha sana hawa watu!

    ReplyDelete
  3. Bro Michuzi

    Enzi zangu namkumbuka bingwa wa salaam kutoka Stakishari Ukonga..Nde Mwasandende

    ReplyDelete
  4. Kuna EXAUD NKO au SURA MBILI

    ReplyDelete
  5. Bro Micghuzi asante kwa kutuwekea picha na taarifa kuhusu uzinduzi wa shirika hili jipya la habari. Hata hivyo, pamoja na kutuonyesha picha na kuwataja wadau wote muhimu waliohusiana na wanaohusiana na shirika hilo, umesahau kumweka au kumtaja Mkurugenzi wa kwanza kabisa wa Tanganyika Broadcasting Corporation, miaka hiiiyo ambapo lilikuwa limezinduliwa, Mzee Paul Sozigwa!

    ReplyDelete
  6. Asante kwa picha hii Mkuu! Jamaa huyu namkumbuka tokea utotoni.Sikudhani kuwa naweza kuona picha yake siku moja.

    ReplyDelete
  7. Tumaini Mwanyika akiwa safarini uingereza.

    ReplyDelete
  8. mdau ulietaja nde Mwasandende wa Stakishari Ukonga.Nilifuta naye ujinga mitaa ya Tukuyu MBEYA
    mdau Sterling, VA

    ReplyDelete
  9. Muhidin,

    Wasikilize wadau. Wanakuulizia vipi mbona hawakumuona Mzee Paul Sozigwa? Na Miye nakuuliza mbona hatukuona picha za magwiji hawa kwenye hiyo sherehe David Wakati, Khalid Ponela, Batholomeo Kombwa, Abdallah Mlawa, Salim Mbonde, Sekioni Kitojo, Abdul Ngalawa?

    Naomba uwastue SUK waingize matangazo ya radio mtandaoni. Nina hakika watapata mashabiki kama issamichuzi.blogspot.com

    ReplyDelete
  10. do! huyu jamaa amenikumbusha mabingwa wengine kama dereva abdallah mgeni wa RTC kibaha,Mnemo Bakari Mnemo,Nganda X Nganda wazamani Dua Wajaad fundi,Chivalavala A Chivalavala,Chasakata wa Chasakata,JFC Vigoron wa nampula msumbiji,Fundi viatu Juma Ramadhan Kamage Wa kata ya puge nzega Tabora,Leonald Mwakambonje.

    ReplyDelete
  11. Tusiwasahau pia Chidi Chidi Chitenda wa Victoria, Abdalah Musa Mikoroti na bila kumsahau Chivalavala A. Chivalavala wa cMahuta Shimoni. Hawa jamaa walikuwa butudani tosha!!

    ReplyDelete
  12. Kwa kweli nadhani hata shirika la posta lilipaswa kuwaunga mkono TBC kwa kuthamini mchango wa mabingwa hawa wa salaam kwa muda mrefu.Nasema hivyo kwani nina hakika wamechangia kwa kiasi kikubwa mapato ya shirika la posta kutokana na stempu walizokuwa wakinunua ili kuweza kutuma salam.Maana nilikuwa kuanzia salaam asubuhi njema,mchana mwema,jioni njema,na usiku mwema, kila siku. Kwa kweli nimefurahi sana kumuona mdau huyu aliyebobea katika anga za salaam nchini Tanzania, na wengine wote walitajwa na wadau.Kazi nzuri bwana Tido Mhando.Kwa muda mfupi uliokabidhiwa chombo hicho nyeti cha umma,watanzania tunaona matunda mazuri kutokana na dira uliyonayo ya kuleta mabadiliko ya kisera katika sekta hiyo ya utangazaji nchini.

    ReplyDelete
  13. Mdau wa March 27.03.2007 11:41Hrs Batholomeo Kombwa Aka BART KOMBWA alishafariki dunia miaka ya mwanzoni ya 90 sijui hao wengine...

    ReplyDelete
  14. Pia Spidi Makoroma nae alikuwepo

    ReplyDelete
  15. Naam huyo Muungwana Zimboko kweli alikuwa bingwa wa salaam.

    Katika wadau wa kale waliokusanya mbona sioni picha za fundi mitambo wetu Juma Bungala, na watangazaji Tumbo Tamili Risasi, Ben Mwangonda, Abisai Stevens n.k. je mkurugenzi Nkwabi Ngwanakilala naye hakuwepo?

    ReplyDelete
  16. Kweli nimekubali kwamba kila kazi duniani ina heshima yake mradi uifanye kwa umakini na moyo wako wote!Huyu jamaa ni kiboko ya watuma salaam redioni.Kapoa sana na anaonekana anapata raha moyoni mwake kwa kutuma salaam.Hasukumwi na kitu bali ridhaa yake mwenyewe.Zakaria Ndemfoo kaifundisha jamii mambo mengi sana,kikubwa uvumilivu na kujituma bila ya kusubiri sifa!Nina uhakika yeye ni mtu maarufu zaidi hapa duniani kuliko hata Mbunge wake wa sasa au hata mawaziri kadhaa walopita!Nampongeza sana na nampongeza zaidi Tiddo Mhando kwa kutosahau nyuma alikotoka na kuthamini michango ya wadau kama huyu Mzee wetu Zakaria Ndemfoo ambaye kwa hakika alichangia kwa kiasi kikubwa katika kuifanya Taaluma nzima ya Utumaji Salaam kupitia vyombo vya redio kupata umaarufu na heshima yake.Kama lipo Shirika au Taasisi iliyoguswa na ujasiri wa Mze Zakaria Ndemfoo kwa mchango wake katika Taaluma ya Mawasiliano NAIOMBA impatie Mzee huyo zawadi ya LAPTOP iliyo unganishwa kwenye INTERNET ili aweze kutimiza ndoto yake!Amejitahidi kujiweka katika afya njema ,Mwenyezi Mungu amzidishie uzima na mafanikio tele zaidi katika maisha yake.Salaam azifikishe kwa familia yake na marafiki zake wote walomzunguka!Huyu kweli ni Jemedari wa Kutuma Salaam!Pia Michu kwa kuitundika picha hiyo katika Blog yako.

    ReplyDelete
  17. Michu,
    Vilevile fundi mitambo maarufu RTD wakati wa matangazo ya mpira wa miguu moja kwa moja toka viwanja vya soka ndani na nje ya Tanzania, Mzee Jacob Aimba sasa mstaafu Hanaasif Kinondoni amesahauliwa.
    Mdau
    Ukerewe.

    ReplyDelete
  18. Mdau wa Ukerewe safi sana ila umesahau na gari yao ya matangazo ya kina mzee Aimba ilikuwa wanaiita "obi van" kama sijakosea!

    ReplyDelete
  19. ZAKARIA NDEMFOO WA LAKE BABATI SALAM CLUB

    ReplyDelete
  20. OB VAN , MAFUNDI JUMA HAMISI KENGELE, ALI SAIDI TUNKU NOEL NAMALOWE,

    KAZI NZURI , WAKO WAPI IKHWANI HAWA, ILIKUWA BURUDANI YA KUTOSHA

    ReplyDelete
  21. MICHUZI KAZI NZURI,

    TUNAKUOMBA UTUTAFUTIE PICHA ZA HAO VINARA WA SALAM,
    1. CHIDI CHIDI CHITENDA
    2.CHIVALAVALA M CHIVALAVALA
    3.EXAUDI NNKO
    4.MUUNGWANA ZOMBOKO
    5. NA HUYO FUNDI VIATU.
    NATANGULIZA SHUKRANI

    ReplyDelete
  22. yaaaah longtime....mnamkumbuka hawa..?
    1)kilungi-wa-kilungi-njinjo-kilwa
    2)wajadi fundi
    3)zainab wajadi
    4)dereva abdala mgeni-rtc kibaha

    ReplyDelete
  23. wapi WAJADI FUNDI

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 06, 2008

    Eheee....,Eheeee...Duu..,Bro Michuzi ni noma.,Hawa Jamaa sio mchezo..,kuna huyu Jamaa sijui ndio Chite chite chitenda sijui chidi chidi chitenda ebwana tutafutie picha yake.....,Thobias R. Mnyani nitakutumia Picha yake maana ni Babu yangu huyu....,hupo Gumba kwa sasa Chalinze hapo amepozi anakula Bata

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...