Kwa wanachama wote wa F.C.BONGO,


Ningependa kuwataarifu kuwa mazoezi rasmi ya kujiandaa kwa mashindano ya Prevention Cup 2008 yataanza siku ya jumamosi tarehe 3.5.2008 saa kumi na moja jioni katika uwanja wetu wa kawaida wa Väinämöisenkenttä a.k.a (Vumbi Stadium) Hietsu.


Kabla ya mshindano tutakuwa na mechi za kirafiki na baada ya mashindano pia tutakuwa na mechi zingine za kirafiki ambazo moja wapo ni ya safari ya Tampere na ingine ni safari ya Stockholm Sweden.


Majadiliano na maoni kutoka kwa wanachama wote yatajadiliwa baada ya mazoezi katika wiki tatu za kwanza.


Wanachama wote mnakaribishwa kuchangia mawazo yenu ili kufanikisha mafanikio ya mwaka huu wa 2008. Kwani tumepania mwaka huu kuchukua lile kombe.


Mazoezi ya winter yameenda vizuri sana, wachezaji wengi wamehudhuria na tunategemea tukianza Vumbi stadium wengi zaidi watahudhuria.


Hapo juu ndiyo ratiba kamili ya msimu huu wa summer.


Unaweza kudownload attachement kwa ajili ya kuprint.


Regards:

Ezza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Bongo FC..yaani safari mje kabisa na kagunia kakubebea magoli.

    Ila jina la uwanja wenu wa mazoezi linamvuto..uwanja wa vumbi...aa aaalol..

    pamoja watu..jipangeni sisi tunawasubiri

    ReplyDelete
  2. Sawa Edwin, lakini kumbuka mwaka jana tuliwanywisha manane nyumbani kwenu, na safari hii tunakuja na mtindo wa SEX FOOTBALL sio sexy football.

    ReplyDelete
  3. Bongo FC muwe makini sana na Kilimanjaro ya sweden, wanaloga mno. Mdau -Adam-

    ReplyDelete
  4. Kaka Ezza, siku hizi umekuwa manager wa Timu badala ya U-Dj??? Nawatakia kila la heri mlibebe kombe hilo. Nisalimie akina, Mzee Mataluma, Mzee Bonanza, Kijana Shaaban Bakari, Moddy Bakari, Dj Erick, Na Smart Boy Erick. Mimi

    ReplyDelete
  5. Wewe ndaki kwani umesahau mwaka jana mvua ya magoli ilivyo wanyeshea nyumbani ?

    ReplyDelete
  6. Siku hazigandi..muda si mfupi tutatundika matokeo ya game letu na la kwenu.

    Kwanza tumefanya usajili wa kufa mtu safari hii.

    Time will tell...chwaaap

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...