ubao wa matangazo wa kisasa
siku staaz ilipocheza na msumbiji

HATIMAYE BAADA YA KUBANA KWA MUDA MREFU SERIKALI IMEAMUA KUUACHIA UWANJA MPYA WA TAIFA JIJINI DAR KWA MATUMIZI YA NYUMBANI.



AKIONGEA LEO HUKO DODOMA WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO KEPTENI MSTAAFU GEORGE MKUCHIKA AMESEMA PAMOJA NA KWAMBA NESHNO HIYO MPYA HAIJAISHA ZAWA SAWA, HASA SEHEMU ZA KUKIMBILIA, HAKUNA JINSI BALI KUUFUNGUA ILI TAIFASTAAZ ICHEZE MICHEZO YAKE YA KIMATAIFA ILIYO MBELE YAKE IKIWA NI DHIDI YA MAURITIUS, CAPE VERDE NA CAMEROUN.

MH. MKUCHIKA AMESEMA UWANJA HUO NDIO PEKEE AMBAO UMEPITISHWA NA FIFA KUWA UNAFAA KWA MECHI ZA KIMATAIFA, HIVYO HAKUNA UJANJA ISIPOKUWA KUUFUNGUA NA KUUTUMIA.

UWANJA HUU, AMBAO UMEJENGWA KWA MSAADA WA JAMHURI YA WATU WA CHINA KWA VIJISENTI TAKRIBAN BILIONI 57, ILIKUWA UFUNGULIWE TOKA JULAI MWAKA JANA, LAKINI KUTOKANA NA KUTOKAMILIKA BAADHI YA UJENZI UKAWA UMEDODA. HABARI NDIYO HIYO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. haya mkaibe mabomba

    ReplyDelete
  2. Huu uwanja ulikuwa uwe umeisha na kuzinduliwa kabla Che Nkapa hajatoka madarakani. Sasa hivi ni miaka miwili na nusu imepita eti wameshindwa kuumalizia. Tatizo ni nini hasa? Mbona hakuna anayetaka kutufafanulia?
    Kwa kasi ya ufisadi tuliyo nayo isije ikawa umekuwa mradi wa watu sasa. Kama uwanja haujaisha basi wanajichotea tu mafungu ya walipa kodi kuendeleza ujasiriamali wao.
    Usemi wa "Time is Money" unahusika hapa. Kwa kuchelewa kuufungua uwekezaji uliotumika hapa unapotea bure, serikali ingekuwa inapata hela kutokana na mapato ya mechi za kirafiki ambazo Stars ilishindwa kucheza kwa sababu uharibifu tulioufanya kwenye uwanja wa zamani unaosababisha uwanja kufurika sasa.

    ReplyDelete
  3. misupu umenikumbusha machungu mwenzio siku tulipofungwa na msumbiji,mweeh kufungwa kubaya lkn watz ni watulivu sana hamna fujo yoyote ilitokea mbali na kuchabangwa nyumbani na wageni.

    ReplyDelete
  4. Lazima vijisenti vingi tu vimeingia mikononi mwa wanaojua matumizi!!!

    ReplyDelete
  5. Ndugu Michuzi,

    Naomba kuwasilisha. Uwanja huu ulikuwa mbovu lakini sasa ni bomba sana. Sababu ni pesa ya Mchina, yule yule anayealika viongozi wetu ili apate dili nzuri ya madini yetu.

    Nashangaa hamna mdau kauliza pesa zilitoka wapi kujenga huu uwanja tunaoringa nao. Mimi mwenyewe nilisoma habari hizi katika The Economist.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...