HABARI KUTOKA MOROGORO ZINASEMA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA TABORA UKIWAONA ATHUMANI DITOPILE AMEFARIKI DUNIA LEO ASUBUHI KATIKA HOTELI MOJA MJINI HUMO.
JUHUDI ZINAFANYWA KUJUA CHANZO CHA MAUTI YAKE. UONGOZI WA HOSPITALI YA MKOA IMETHIBITISHA KIFO HICHO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 64 mpaka sasa

  1. (pichani) wapi?, mbona hakuna picha?

    ReplyDelete
  2. always will remember,you as a good neighbour,mazengo rd,upanga,may the almighty rest your gracious soul in peace.AMEN

    ReplyDelete
  3. Inna lillahi wainna lillah raajiuun!! duh poleni sana!
    Mdau East Texas!

    ReplyDelete
  4. Mungu amulaze mahali pema peponi. Amini

    ReplyDelete
  5. KILICHO ZALIWA HUFA RIP DADY

    ReplyDelete
  6. Mwajumbe and the family Poleni sana.
    Inawezekana msongo wa mawazo ukawa umesababisha kifo chake.
    Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya Marehemu - Amen
    Mdau Kula Lumpur

    ReplyDelete
  7. RIP
    Ni njia yetu sote!

    Familia Mungu awatie nguvu

    ReplyDelete
  8. Jamani, marehemu ndiyo yule baba aliyestakiwa kwa kumuua dreva wa minibus?, or maybe the names yanafanana. Mungu amweke Roho yake peponi pema.

    ReplyDelete
  9. Innallilahi wainaillaihi rajiuna, ndio njia yetu sote, poleni sana wafiwa na Mungu awape moyo wa subira katika huu wakati mgumu kwenu. Pole mama Ditto na watoto wote

    ReplyDelete
  10. Tumejifunza mema mengi toka kwake ktk uhai wake. Mungu awape subira wafiwa. Inna Lillahi wa inna ilaihi rajiuun. Maziko lini na wapi ?

    ReplyDelete
  11. Wewe anon wa kwanza ni mwehu kweli, sasa unataka picha ya nini. Kama ukisikia mtu amefiwa au amekufa na wewe huna la kusema shut up! Ishia zako. Poleni wafiwa jamani katika hiki kipindi kigumu Mwenyezi mungu amuepushe marehemu na adhabu ya kaburi na amuweke mahali pema peponi. Amin

    ReplyDelete
  12. Wakati wa uhai wake, Bwana Ditopile alishika nyadhifa kadhaa serikalini ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi.Pamoja na hayo marehemu atakumbukwa pia kwa kudiscepline madereva daladala, tukio ambalo lilimwondoa ktk nyanja za kisiasa.
    Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

    ReplyDelete
  13. INNA LILLAHI WA INNA ILLAHI RAJI'UN.
    REST IN PEACE MWESHIMIWA

    ReplyDelete
  14. Poleni sana kina Tabia dada Jamilla Dito, Selaji, Tuwazela kaka Sababu, na Abdalla poleni sana kwa kipindi hiki kigumu, RIP kaka Dito, tutakumiss sana kwa ucheshi wako.

    ReplyDelete
  15. inna lilah...

    Maziko ni kesho saa kumi kwa mujibu wa familia ya marehemu.nitawajuza zaidi ishallah kuhusiana na wapi wanazikia

    poleni sana Rama,Sele na mariam pamoja na mama yao...

    ReplyDelete
  16. anon no1 we MSHAMBA unataka picha ya DITO kwani we haumju m2 unaambiwa ameshakufa je we hauamini?bila shaka ni shinikizi la damu kama kawaida pia sikuzake zimeshaFika asitafutwemchawi(QUE DIEU LUI PARDONNE)mdau ALGERIA

    ReplyDelete
  17. NI KWELI AU NI USANII TU?

    ReplyDelete
  18. pole sana Ramadhan,kyembe and all the family members..in god we trust,nda life goes on!keep it up K i know u will make it!

    ReplyDelete
  19. Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi, aliyemuumba Ditopile, hatimaye amemrudisha kwake.
    Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen.

    ReplyDelete
  20. Hivi ni kweli kafa, au ndo mambo ya Inteligensia, kama kwenye Movie ya "The Assignment"! Mtu mwenye soo anakuwa declared kuwa kafa, na pengine hata ushahidi hewa huwa unatolewa kuwa kweli kafa, kumbe anapelekwa mafichoni, kwenye kisiwa flani Ughaibuni, ili kumuepusha na soo. Ni hayo tu. Tena ukizingatia kuwa dini ya "marehemu" public huwa hawaagi mwili! Ndo kabsa, sie akina "Tomaso" inakuwa ngumu kwetu kuamini kuwa kweli kafa. Anyway, Apumzike kwa Amani, huko aliko.

    ReplyDelete
  21. Ndugu Michuzi, kuna wakati fulani kwenye hii blog yako mdau mmoja alikuomba kuwa kwenye habari za msiba usiandike BREKING NYUUUZZZZZZ bali uandike tu BREKING NYUUZ, maana unapoongeza hizo zzzz inaonekana kama ni jambo la kushangilia vile. (haya ni maoni yangu tu, ukiamua kuyabana sawa)
    R.I.P. Brother Ditto.

    ReplyDelete
  22. Wabongo kweli wacha mungu, marehemu aliua tena hadharani, akapewa dhamana, kawa anakula kiulaini home kwake (anyway may be ilikuwa bahati mbaya)wakati wa uhai wake maoni yalikuwa very negative juu ya tukio hilo, leo kafariki maoni yote Mungu aiweke mahala pema roho ya marehemu. Hilo ndo kati ya machache ninayojivunia kuwa mtanzania, uvumilivu, upendo na zaidi kusamehe. Mungu azidi kutubariki. Rest in peace Brother DITO.

    ReplyDelete
  23. Huko alikokuwa Mkuu wa Mkoa tutamkumbuka marehemu kwa ujasiri wake wa kutetea wanyonge, alikuwa hakubali kusaini ma fomu ya LF 3 ya watu wenye kuchukua ardhi ya watu huko vijijini kama hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa wenye ardhi wamelipwa fidia. Kwa hili mafisadi wenye kupora ardhi za watu walimchukia. Watu wa Pwani wameondokewa na mtetezi wao, ni mengi sana amewatetea.

    Huko Lindi madereva waliozoea kujaza abiria mpaka wengine kuwapandisha juu ya carrier walimhara, maana alikuwa akiwafuma, hangojei cha trafiki wala nini trafiki alikuwa yeye mwenyewe. Huko Kigoma nao watamkumbuka kwa yake aliyowafanyia.

    Pamoja na hayo yaliyomkuta wakati akiwa Mkuu wa mkoa wa Tabora, Marehemu Dittopile bado alikuwa mtu wa watu, na kwa ushahidi mtayaona siku ya maziko yake.

    Mungu amlaze mahala pema peponi, Amin

    ReplyDelete
  24. inna lillahi wainna ilayhi raajiun.ewe mola msamehe maiti wetu na umrehemu, muondolee adhabu ya kaburi,umpe kauli thabit,shimo lake liwe la nafasi, mfanyie wepesi huko aliko.familia yake uipe subra kwa wakati huu mgumu.tutakuwa wote kama majirani wema pale mazengo.poleni sana.

    ReplyDelete
  25. “You can shed tears that he is gone,
    or you can smile because he has lived.
    You can close your eyes and pray that he'll come back,
    or you can open your eyes and see all he's left.
    Your heart can be empty because you can't see him,
    or you can be full of the love you shared.
    You can turn your back on tomorrow and live yesterday,
    or you can be happy for tomorrow because of yesterday.
    You can remember him only that he is gone,
    or you can cherish him memory and let it live on.
    You can cry and close your mind,
    be empty and turn your back.
    Or you can do what he'd want:
    smile, open your eyes love and go on.”R.I.P Dittopile athuman ukiwaona mzuzuri.pole sana my dear kyembe may god be with you

    ReplyDelete
  26. Inna Lillahi wa inna ilaihi rajiuun!! Binadamu hatuna la ziada ila nikumwomba mwenyezi mungu amabye yeye ndiyo ajuaye atakapokupangia kwa matendo yako.

    RIP

    ReplyDelete
  27. “The unreal is more powerful than the real, because nothing is as perfect as you can imagine it. because its only intangible ideas, concepts, beliefs, fantasies that last. stone crumbles. wood rots. people, well, they die. but things as fragile as a thought, a dream, a legend, they can go on and on.R.I.P bro Ditto

    ReplyDelete
  28. I know the guy, he was a firebrand politician, he has been in politics arena for so long since the NYERERE the legend, ni kizazi cha akina KIKWETE, LOWASSA ndani ya TANU youth legue, TANU yenyewe hadi CCM, I qoute one of his line when he was accused of going out with a women who was married to someone else, it goes like, I quote, "mwanaume bila kufumaniwa wewe si mwanaume bwana" alitoa hiyo alipokuwa anazongwa na waandishi wa habari, otherwise the guy was good. MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YAKE.

    Ni mimi,
    EDWARD ALEX MKWELELE - LONDON, UK.

    ReplyDelete
  29. inalillahi wainalilahu lajiun!
    pole mama rama na dada Afifa kwamsiba wa shemeji yetu mpenzi mh.Dittopile,mungu amlaze mahali pema peponi Amina.

    songabele family!

    ReplyDelete
  30. WOTE TUTASIMAMA MBELE ZA MUNGU SIKU HIYOO.(ROMANS 14:11)
    KAZI YAKE HAINA MAKOSA,DITOPILE AMETANGULIA.

    ReplyDelete
  31. Wee MISUPU VIPI MBONA HUTUPI HABARI KWAMBA CHENGE KAJIUZURU???????????????????????????????????????????????????????????/

    ReplyDelete
  32. Hilo kubwa wadau tena la kusikitisha sana. Mungu amlaze mahala pema peponi.

    La pili najua Michuzi fununu unazo unangoja ruksa tu ulitoe. Kesho Chenge anaachia ngazi... subiri upate nyepesi kama huamini.

    Usinilaumu jamani siku hizi Tanzania hakuna maadili ya kutunza siri za serikali haya tumeshayapata mapemaaaa!!! Binafsi nakumbuka enzi za Baba wa Taifa ,, mambo sapraizi

    ReplyDelete
  33. OTHER NEWS NI KWAMBA WAZIRI ANDREW CHENGE NAYE AMEJIUZULU!!

    ReplyDelete
  34. chenge naye out. alutaaaaaaa.... kontinua!!!

    ReplyDelete
  35. Kaka Michu najua uko katikati ya chanzo cha habari zote za serikali, je ni kweli hujasikia kuwa MWANANGWA CHENGE KAJIUZURU???

    ReplyDelete
  36. Mapenzi ya Mungu, njia ya wote, ametangulia tuliobaki tu nyuma yake. Rest in Eternal Peace. AMINA

    ReplyDelete
  37. Inna Lillah---

    ambo na mijuzo yote jamaa huyo alofanya hapa ni hadithi hivi sasa iliyopo ni kwamba amefika kwenya Mahakama kuu, tumuombee msamaha kama ana makosa
    Jamaa aliyetaka picha si mwenda wazimu na kama kuomba Michuzi kututilia picha ni dalili ya kuwa gaga basi mia ni mmoja wao kwani jamaa huyo simjui wala sijamsikia
    PS bofya Bongo Celebrity

    ReplyDelete
  38. WADAU KUNRADHI KWA KUPITIA KIBARAZANI KWENU NA PIA KUCHELEWA KUWAPA BREKING NYUZZZZZ KAMA KAWAIDA.

    NI KWAMBA MITAMBO YA BLOGGER IMEKUWA CHINI JIONI YOTE HII NA HADI SASA INAONESHA HAWAJAREKEBISHA MAMBOZ KWENYE SERVER ZAO. HATA HIVYO MSIKONDE, MAMBO YAKIKAA SAWA NITAKUWA HEWANI KAMA KAWAIDA.

    KUHUSU HABARI YA KUJIUZULU KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIUNDOMBINU MH. ANDREW CHENGE NI KWELI, NA JK AMEKUBALI OMBI LAKE LA KUJIUZULU KWA KUMWAMBIA NI UAMUZI WA BUSARA KUCHUKUA IKIZINGATIWA HALI ILVYO KWA SASA.

    HABARI INGINE NI KWAMBA MAZISHI YA MAREHEMU UKIWAONA MZUZURI DITOPILE YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMANNE, KWA MUJIBU WA HABARI ZA KIFAMILIA. MAPEMA LEO JK ALIKWENDA KUTOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU DITOPILE MTAA WA MINDU, UPANGA, DAR.

    SAMAHANI KWA USUMBUFU NA ASANTENI KWA UVUMILIVU. LIBENEKE LITAKUWEPO KAMA KAWA BAADA YA MUDA SI MREFU

    - MICHUZI

    ReplyDelete
  39. HATA MIMI SIAMINI KAMA NI KWELI DITO KAFA MICHUZI NI MTU WA FOOLS DAY SANA MPAKA NIONE PICHA NA HIYO BREAKING NEWS, DITO MZIMA SALIMINI HIZO NI KAMBA TU ZA MICHUZI

    ReplyDelete
  40. Ninachoweza kusema ni kwamba nimezipokea kwa mshituko mkubwa habari za kifo cha Kada Ditopile Mzuzuri.Si rahisi kwa sisi tuliowahi kufanya kazi naye kuelezea namna tulivyoguswa na habari za mauti yake.Hatutousahau wema, ucheshi,uchapakazi na uungwana aliokuwa nao Marehemu Dito katika utumishi na uhai wake ndani ya CCM na ndani ya serikali kwa ujumla.Namkumbuka sana alipokuwa Naibu Katibu Mkuu wetu wa CCM,nami nikiwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Dodoma mjini,aliwahi kunipa mausia ya msingi sana katika mustakabali wangu wa kisiasa kwa siku za usoni.Na kwa kweli sitakuja msahau katika maisha yangu ya kisiasa.Kifupi alikuwa mshauri mzuri sana.Basi,yametokea yaliyotokea tikitambua wazi kuwa hiyo ndiyo njia yetu sote,tunapaswa kuyakubali matokeo.Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi hiki kigumu,Familia,ndugu,jamaa,na watu wote walioguswa na msiba huo.

    ReplyDelete
  41. Kwa wale watoto wa ilala likitajwa jina ditto watu wato wanajua nini maana ya kuwa mtoto wa ilala!!! ashanti watoto wa jiji club iko nyumbani kwa kina ditto

    ReplyDelete
  42. R.I.P brother Ditopile

    ReplyDelete
  43. michuzi hataki kutoa habari za kujiuzulu kwa chenge sababu kuna tume imeundwa kumchunguza michuzi.Muda si mrefu mtasikia Mkuu wa Wilaya ya Tegeta naye kajiuzulu baada ya kugundulika ana akaunti kibao za benki Ukerewe na Ujiji.Nyie mnadhani hizo safari za Ukerewe na Ujiji ni za bure.Michuzi Is very connected guys.
    Halafu hiyo "inna lilla na wainalilah" ndiyo kitu gani.Mnanikumbusha wimbo tuliokuwa tunawaimbia watoto vikojozi.Ha ha ha

    ReplyDelete
  44. Watz fuata upepo jamani, au ni ile kasumba ya kuwa ukishafariki wanakusifia hata kama mwanzoni walikuwa wanakuponda. Hii imenikumbusha kifo cha Chifupa, maana before people hawakumkubali, they even called her names! alipofariki ghafla akageuka kuwa tz princess, maana alifananishwa na Diana.
    Huyu baba si mlimtukana alipomuua dereva na kusema hana utu! Michuzi embu vuta achieves zako apa tuone hoja zinavoji contradict apa, unatukanwa ukiwa hai unasifiwa ukifariki! Wapeni watu sifa zao wakiwa hai, msisubiri wafe jamani! kwa mfano mi nampenda Michuzi kwa kazi zake anazofanya kutuhabarisha apa mambo live.

    ReplyDelete
  45. Duuuuuuuuuuuuuuu! ebwanaeeeeeeeeeeeh! Mungu amlaze Mahali pema- peponi -amen

    ReplyDelete
  46. Tanzanian minister quits office
    Dar Es Salaam Airport, Tanzania
    Tanzania's main airport benefited from the deal

    A Tanzanian politician has resigned amid allegations he took bribes during the controversial purchase of a British radar system seven years ago.

    Reports say more than $1m (£500,000) was found in an offshore account belonging to Infrastructure Minister Andrew Chenge.

    He has denied any wrongdoing and says he will co-operate with investigators.

    UK fraud officials have been investigating the sale of the air traffic control system by BAE Systems.

    Mr Chenge is the fourth Tanzanian minister to leave office over bribery claims in the past two months.

    Government spokesperson Salva Rweyemamu said Mr Chenge's resignation was a sign of political maturity.

    He said: "What we are hearing is mere allegations... the reason why people are taking responsibility is because we have a very mature political system.

    "Probably the best political system in Africa in terms of maturity, in terms of people taking responsibilities when things are not going right."

    ReplyDelete
  47. Mbigiri hujatulia wewe, speakout unalotaka kulisema
    lisikuunguze kifuwani bure! we dua ya kumrahamu marhem we unauita wimbo wa kikojozi?

    Kila nafsi lazima itaonja mauti na baada ya kusikia Khabari yoyote ya msiba si vema kwa muislamu yeyote kusema "maskini weee kafa jamani" na kuomboleza kwa uchungu na kumlaumu mungu,
    kwa kusema hivyo inaonyesha kuwa labda mungu kuchukua roho ya mtu yule hajamtendea haki, wakati tunajua kufa ni lazima kwa kila nafsi ahadi yake inapofika. Ndipo hiyo sentensi hutumika kwa kumtukuza mungu badala ya kukufuru kwa maombolezo ya uchungu yasiyasaidia lolote zaidi ya kuumia na kulizana bila uwezo wa kuirudisha roho iliyoondoka.

    ReplyDelete
  48. MICHUZI ACHA UBAGUZI WAKO NIMEWEKA SALAAMU ZANGU HAPA UKAZITIA KAPUNI..WEWE NI MBAGUZI SANA
    KYEKUE

    ReplyDelete
  49. Namkumbuka brother DITTO kwa uwezo na umahiri wake wa kujieleza.
    Katika mchakato wa kura za maoni ndani ya ccm uchaguzi mkuu wa 2000-2005 alishindwa.
    Alisimama bila woga na moja ya kauli zake zilikua:-
    "mheshimiwa mwenyekiti nimeshindwa kwa hila-watu walikua wanapewa pilau na khanga!naapa sitotoa rushwa,sikumbuki ni lini nimetoa rushwa na kama kuna mtu anao ushahidi kuwa niliwahi kutoa au kupokea rushwa anitangaze"
    Kauli hii ya kishujaa ilichukuliwa kama kiwewe cha kushindwa watu wakampuuza.
    Naomba niulize kuna mtu yoyote ndani ya ccm aliewahi kutoa tamko zito namna hii zaidi ya mizengo kanza peter pinda alieapa mbele ya padre wake kuwa nikila rushwa mungu aniangamize.
    Nadhani tunahitaji watu wa aina hii walau wajitoe hadharni

    ReplyDelete
  50. Mbigiri:Hata kucopy inakusumbua! loh!Ni
    Inna Lillah Wa Inna Ilaih Rajiwn...
    Maana yake ni Sote ni wa MUNGU na kwake tutarejea!
    Umefanya vizuri kuuliza.

    ReplyDelete
  51. KUTOKANA NA HABARI ZA LEO ASUBUHI KUHUSU CHANZO CHA KIFO CHA MH. DITO NIMESIKIA MKUU MMOJA WA MKOA AKISEMA KWAMBA MAREHEMU ALIKUWA NI MTU WAKE WA KARIBU SANA NA KTK MAISHA YAKE HAKUWAHI KUSIKIA WALA KUONA DITO AKISUMBULIWA NA UGONJWA WOWOTE...!!?
    SASA HAPO NDIO NICHOSHANGAA INAKUWAJE MTU ALIEPEWA DHAMANA NA MAHAKAMA KUTOKANA NA KUSUMBULIWA UGONJWA AMBAO HAO HAWEZI KUTIBIWA AKIWA MAHABUSU HALAFU LEO KAFARIKI GHAFLA MNASEMA MAREHEMU ALIKUWA HAUMWI..? WHY..? KWA NINIII.Namalizia kwa kusema
    "MBELE YETU NYUMA YAKE" wote njia ndio hiyohiyo

    ReplyDelete
  52. Hao ndio kina Mbigiri bwana, kwao kila kitu ni dharau na kibri, hivi kwani hujawahi kusikia hata siku moja hata watoto wakisema Wallahi wabillahi katika maisha yako, kwani hujui kuwa waislami maana ya neno llillahi au Allah au unataka kuleta kashfa kwa kusema ni wimbo wa kikojozi? Unajua waislamu wakikujibu hutakawia kusema wanakashifu mungu wako au dini yako. Sometimes kama unahisi umeamka nazo kichwani just shut up! Maana mtu akiamka nazo ulimi wake husema ambacho huja kukijutia baadae na ukazua ya kuzua. Ukome na usirudie tena Mwanahizaya weee!

    ReplyDelete
  53. Namkumbuka Dito kama mtu mu wazi na asemaye papo hapo yanayomkera, japo si wote wliokuwa wakifurahia mtindo wake huo. Na katika yote pale alipomuua dereva wa daladala alijipeleka kwa Tibaigana na kukataa kuitwa mheshimiwa bali aitwe muuaji. Jinsi kesi hiyo ilivyoshughulikiwa na DPP ilikuwa nje ya uwezo wake, na lawama zielekezwe kwa DPP na serikali. Naamini yale aliozungumza kwanza kabisa yalikuwa toba tosha. Mungu amlaze pema peponi

    ReplyDelete
  54. poleni wafiwa, sote ni wa MUNGU na kwake tutarejea. (Anon wa 12:33) kwani mbigiri kafanya nini mpaka unamtunaka hivyo, si ameuliza tuu kwani hiyo lugha iliyotumiwa si wote wanaifahamu ndiyo maana kauliza maana yake, mimi naona wewe ndiyo unataka kuleta issue hapa, mbona anon wa 10:41 amemuelewesha tuu maana ya hilo neno bila matusi, acha hizo wewe haijatulia kabisa ndugu, muelimishe mtu kama hajui maana yake siyo kashfa na kutaka kuleta ligi hapa ya dini, mimi naona wee ndiyo umeamka nazo ndiyo maana una hasira na mbigiri, ni kitu kidogo sana hicho ulichokimind mpaka ukaenda mbali kote huko.

    ReplyDelete
  55. Anon 9:19 Hiyo dharau aliyoitoa mbigiri kufananisha maneno ya mwenyeenzi mungu na wimbo wa kikojozi ndio tatizo si kitu kidogo kama unavyofikiri,kama wengi walivyokwazwa na maneno ya kawaida ya Chenge ya kuita Billion kuwa ni vijisenti kidogo.

    Kwa sisi tunaomuheshimu na kumuogopa mungu wetu tunaemuamini na kumuheshimu, hiyo sentensi yake lazima itakuwa makruh (makwazo) kwa yeyote anaeamini.Pole kwa kuingilia mazungumzo yenu, ila nimelazimika pia kukemea mizaha inayojumuisha na Muumba ambae tunamnyenyekea na kumuheshimu, ili masikio yetu tusijezoeshwa kusikizishwa kila siku upotovu na kuzoea kwa kuona masKhara kwa mungu ni kitu cha kawaida.

    INNA-LILLAH WA INNA-ILLAH RAJIUN. Poleni wafiwa.

    ReplyDelete
  56. RIP BRO DITO, Salua, nafikiri mbigiri asingetoa hiyo dharau kama angefahamu maana ya hilo neno linahusiana na mwenyezi mungu, hiyo lugha iliyotumiwa si kiswahili wala kiingereza, hivyo sidhani kama watu wasiotumia hiyo lugha watafahamu maana yake, ni vizuri kama mtu anapenda kutumia lugha kama hiyo aweke na tafsili kwa nia njema tuu ili kuweza kusaidia wale wasio fahamu wajue maana yake ili isije ikawa tatizo tena, sioni kosa la mbigiri kabisa hapo, nafikiri wenye makosa ni wale walioanza kutumia hiyo lugha bila ya kuweka maana yake kwa lugha ambayo labda mbigiri angeifahamu maana yake na naamini kabisa angeiheshimu hiyo. si wote wanaingia kwenye blog hii wanaifahamu hiyo lugha, hii inatakiwa ieleweke.
    mcha mungu.

    ReplyDelete
  57. Ndugu yangu mcha Mungu,Kwa ufahamu wangu kwa haraka haraka tu,naweza kumsoma mbigiri kwenye sentensi yake hiyo ya huo wimbo wa mtoto kikojozi,haushabihiani (haifanani) kabisa na sentensi ya kuomba rehma ya mungu, labda alikuwa na lengo la kufanya utundu ili atuchekeshe humu kama kawaida yetu tulivyozoea baadhi yetu, ila ucheshi huo ameuweka mahali ambapo hapastahili utani ameenda mbali kidogo.
    Yawezakuwa wewe huoni kosa juu ya hili, na sikulaumu ila kwangu mimi kidogo imenisumbua na kuogopa kidogo, kwani ni sentesi ya mafundisho ya QURAAN suratl Baqara Mwenyeezimungu anasema tunapopata mtihani wowote iwe kufiwa au kupotelewa mali au kitu kinachokupa uchungu, ni vema kusema hiyo sentensi kutoka moyoni na mtu hupata wingi wa rehma ya mwenyezi mungu. Angeuliza tu hii inamaana gani ingetosha kupata msaada juu ya hilo .Uniswameh kama utakuwa hukufurahia niliyoyasema awali, kuna neno linasema kuambiana kupo ila kuskilizana ndo huwa hakupo.

    ReplyDelete
  58. ...yani jamani kuna watu wamepinda kama utumbo...hivi we mbigiri up stairs mzima kweli?? RIP DITO

    ReplyDelete
  59. nyie mnaomtetea mbigiri labda mnamtetea kwa kuwa mnamfahamu. Yeye mbigiri anafahamu sana kuwa waislam ndo wanatumia lugha hiyo tafsiri wanaijua wao wenyewe wanaoitumia. kama ni mtanzania hawezi kusema kuwa aliishi bila kuwa amezunguukwa na waislam au hata alipokuwa anasoma shule lazima alikuwa anakutana na waislam. Alichotakiwa kufanya ni kuuliza tu kama watu wafanyavyo kwenye msaada kwenye tuta badala ya kuingiza mzaha wa kufananisha na vitu vichafu!Ni vema wakt mwingine kufikiri kabla ya kuandika au kurudia unachoandika kuona je kinaleta maana na hakimkwazi yeyote au la! mizaha mingine ya kutaka kufurahisha baraza watu wawe wanaichuja hasa inapokuwa inagusa imani za kiroho za watu wengine! huo niushauri tu kwetu sote.
    Mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu Ditto mahali pema peponi na apumzike kwa amani, amen!

    ReplyDelete
  60. nimekuelewa salua ndugu yangu, pole kwa makwazo yote yaliyokukuta ila tuzidi tuu kumuombea ndugu yetu ili afuate yale mungu anapenda, pia nami binafsi naomba msaada wa maana ya QURAAN suratl Baqara, ni furaha yangu kufahamu maana ya maneno ya mungu kwa lugha nyingine, mbarikiwe wadau wote.
    ni mimi Mcha Mungu.

    ReplyDelete
  61. Mcha mungu nimelazimika kukujibu swali lako ulouliza nini maana QURAAN SURATL BAQARA.Ni kwamba kwenye Qurani tukufu kuna aya ambazo zimewekwa ili kutuongoza katika kutenda mema na haki, na katika aya hizo iko moja inapatikana katika Sura inayoitwa BAQARAH MSTARI WA 156 UNASEMA al-laziina izaaasaabat-hum musiibatun,(ambapo uwapatapo msiba), Qaaluuu (husema) "inaaa lillaahi wa innaaa ilayhi raji-uun. "(hakika sisi ni wa mwenyezimungu, na kwake yeye tutarejea)" atatupa jaza yake.

    Ndugu yangu Mcha Mungu ili furaha yako itimie zaidi kama unapenda kujua maneno mengine kwa lugha ya kiarabu pita hapa uanze alifi na ujiti, (a e i o u )na tafsiri ya maneno ya kiarabu, naamini ukiwa kweli una nia ya kujua arabic utafanikiwa kidogo kupata mwanga

    madinaharabic.com/Arabic_Language_Course/Lessons.

    good luck.

    ReplyDelete
  62. Corrections mcha mungu, adress niliyokupa haikuwa kamili .pitia hii:-http:/www.madinaharabic.com/arabic_Reading_Course/AR_Lesson_001.htm

    Wadau wote mniswameh kwa usumbufu wowote.

    Jaazakka-Allahu (be blessed)

    ReplyDelete
  63. mnaolumbana anon na bablii mmenikumbusha wakati fulani ukiingia kwenye ofisi za watu miaka hiyoo unakuta message mbali mbali kwa njia ya maneno au picha za kuchorwa! Nakumbuka moja ilikuwa imechorwa watu wawili wanaume walikuwa wanazozana na nyuso zimekunjana ukiwaangalia wote wamefanana sana. Na ujumbe ulokuwapo ulikuwa unasema 'dont argue with a fool, people might not notice the difference'. Sina hakika kama nimeunukuu sawa sawa lakini hii ilikuwa inanichekesha kuwaangalia hao madume lakini kila siku ujumbe wake ulikuwa umenikaa moyoni hadi leo!Bifu za nini kwenye mablog ya jamii? After all suala lilikuwa ni kuhusu msiba!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...