Habari za kazi Ndungu Michuzi, nina chemsha Bongo nyingine kwa Wadau, naomba wadau mumize vichwa kidogo.

Nina chupa tatu, ya:
· Kwanza ina uwezo wa kuchukua lita 3,
· Pili ina uwezo wa kuchukua lita 5.
· Tatu ina uwezo wa kuchukua lita 8 na imejaa maji.

Sasa swali lipo hivi; nataka niyagawe hayo maji kwa lita nne nne kwenye chipa mbili, na lazima yawe sawa sawa. Bila kukisia..

Hizo chupa zote hazina alama ya kuonyesha ni lita ngapi, ila tu inajulikana kuwa ujazo wake ni lita ngapi..

Jibu lenyewe liwe ni maelekezo utapata vipi hizo lita nne nne kamili kwa kutumia hizo chupa tatu?

Ahsanteni

JK-Canada

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. 3+5+8=i6,
    16 ukigwa kwa tatu ni=4 kwa hiyo kila chupa itabidi iwe na lita 4,mbayo 4 mara 3=16 jibu lenyewe umeshatoa kuwa lita 4
    mdau finland

    ReplyDelete
  2. nenda kwa mganga ataagua

    ReplyDelete
  3. 8 -> 5 ... 0/3, 5/5, 3/8
    5 -> 3 ... 3/3, 2/5, 3/8
    3 -> 8 ... 0/3, 2/5, 6/8
    5 -> 3 ... 2/3, 0/5, 6/8
    8 -> 5 ... 2/3, 5/5, 1/8
    5 -> 3 ... 3/3, 4/5, 1/8
    3 -> 8 ... 0/3, 4/5, 4/8

    ReplyDelete
  4. Simple,
    I will answer it step by step,

    bot1 = 3ltrs bottle
    bot2 = 5ltrs bottle
    bot3 = 8ltrs bottle

    1. Fill bot1 with three ltrs of oil, pour oil into bot2, from bot1.

    2. Filled the remaining of bot2, with water, as we all know that oil float on top of water, base on some weird physical facts, pour the oil back into bot1, you will be left with 2ltrs of water in bot 2.

    3. Filled bot3 with the 2ltrs of water from bot2, now you have an empty bot2, bot3 with 2ltrs of water, and bot1 with 3ltrs of oil.

    4. Now repeat step 1 and 2. you now have bot 3 with 4ltrs of Water, an empty bot2, and 3ltrs of oil in bot1. Now this is the tricky part, you need another bottle with 4ltrs.

    5. Get that 4ltrs of water from bot3 and pour it into bot2(5ltrs bottle), now fill the remaining 1ltr with oil, from bot1, now, pour out 1ltr of oil from bot2, pour the water from bot2(4ltrs of water) back into bot3, which was empty at this stage. Now this is what you are left with Bot1=2ltrs of oil, Bot2=Empty, Bot3=4ltrs of water.

    6.Take 2ltrs of oil from Bot1, and pour it onto bot2, and filled the remainder with water, pour back oil into bot1, now you are left with bot1=2ltrs oil, Bot2=3ltrs of water, bot3=4ltrs of water.

    7.Final Step, Fill the remaining of bot1, with 1ltr of water, once you have that done, pour the oil out, and pour the remaining 1ltr of water from bot1, into bot3 to make it 4ltrs, and therefore your are left with bot1=empty, bot2=4ltrs of water, bot3=4ltrs of water.

    And that answer your question.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  5. punguza nusu ya hayo maji kwenye lita nane , ambayo yatakuwa ni lita nne uyaweke kwenye chupa yenye uwezo wa kuchukua lita tano. Kwa hiyo tiyo yenye lita nane itabaki na lita nne na ne zitaenda kwenye ile ta lita tano., nusu kwa nusu !chupa ya lita tatu haitatumika. Samahani lakini naona Hii kazi itafaa ifanywe na mwanamke mana tuna uzoefu wa kupima vipimo kamili kwa kuangalia tu na macho kaka zetu itawawia ngumu, sisi tumezoea kupima kama vile vipimo vya jikoni na kadhalika.

    ReplyDelete
  6. Unachotakiwa kufaqnya ni kuchukua hiyo chupa yenye maji ya ujazo wa lita 8 na kumimina nusu ya hayo maji kwenye chupa ya lita tano coz nusu ya lita nane ni nne sa utakuwa ushapata jibu.

    ivosh

    ReplyDelete
  7. lt8 lt5 lt3
    A B C
    1. 8 0 0 mchezo umeanza

    2. 3 5 0 jaza B toka A

    3. 3 2 3 jaza C toka B

    4. 6 2 0 jaza A toka C

    5. 6 0 2 jaza C toka B

    6. 1 5 2 jaza B toka A

    7. 1 4 3 jaza C toka B

    8. 4 4 0 jaza A toka C

    Umefanikiwa

    ReplyDelete
  8. Fanya kama ifuatavyo

    Lita8 Lita5 Lita3
    8 0 0
    3 5 0
    3 2 3
    6 2 0
    6 0 2
    1 5 2
    1 4 3
    4 4 0


    Hapo jee, puzzle solved

    Kichwa maji

    ReplyDelete
  9. Kama ninaruhusiwa kuweka alama kwenye chupa,
    basi jibu ni kama ifuatavyo:

    1.jaza chupa ya lita 3 kwa maji kutoka chupa ya lita 8.
    maji yatakayo bakia katika chupa ya lita 8 ni lita 5.

    2.weka maji yote kutoka chupa ya lita 3 kwenye chupa ya lita 5.

    3.jaza tena chupa ya lita 3 kwa maji yaliyobakia katika chupa ya lita 8.
    maji yatakayo bakia katika chupa ya lita 8 ni lita 2.

    4.jaza chupa ya lita 5 kwa maji kutoka chupa ya lita 3.
    maji yatakayo bakia katika chupa ya lita 3 ni lita 1.
    weka alama ya kipimo cha lita 1 katika chupa ya lita 3.

    5.weka maji yaliyobakia katika chupa ya lita 3 kwenya chupa ya lita 8.
    chupa ya lita 8 itakuwa na lita 3 za maji.

    6.kutoka katika chupa ya lita 5, weka maji katika chupa ya lita 3 mpaka kufikia alama ya lita 1.
    maji yatakayo bakia katika chupa ya lita 5 ni lita 4.

    7.weka maji kutoka chupa ya lita 3 kwenya chupa ya lita 5.
    chupa ya lita 5 itakuwa na maji lita 4.

    mwisho.
    Robert.

    ReplyDelete
  10. kwanza jaza maji kwenye chupa ya lita 3, yakishajaa yamimine kwenye chupa ya lita 5, rudia tena kumimina maji yalibaki kwenye chupa ya lita 8 kwenye chupa ya lita 3, (hapo ina maana chupa ya lita 8 itakuwa imebaki na lita 2 sasa), ....hayo maji uliyojaza kwenye chupa ya lita 3 mimina tena kwenye chupa ya lita tano (ambayo tayari ulishamimina lita 3 before), hiyo inamaanisha zitaingia lita 2 na lita moja ya maji itabakia kwenye chupa ya lita 3, mimina hiyo lita 1 kwenye moja kati ya chupa unazotaka kujaza maji.

    Chukua chupa ya lita 5(ambayo kwa sasa itakuwa imejaa maji) mimina kwenye lita 3, then mimi maji yaliyojaa chupa ya lita 3 kwenye chupa ambayo ulishamimina lita 1 (1+3=4) hapo unakuwa umeshakamilisha lita 4 za chupa ya kwanza.

    Kama unakumbuka vizuri chupa ya lita 8 ilikuwa imebaki na maji lita 2 (8-3-3=2) na chupa ya lita 5 ilibaki pia na maji lita 2 (5-3=2) sasa mimina maji kutoka kwenye hizi chupa mbili (chupa ya lita 8 na chupa ya lita 5) kwenye chupa nyingine ambayo ni tupu kwa sasa(2+2=4).

    Nadhani waliosoma hesabu kwa makini wamenielewa.

    ReplyDelete
  11. SIMPLE:
    Jaza maji kwenye chupa ya lita tano...mimina maji hayo kwenye chupa ya lita tatu!! utakuwa umebakiwa na lita mbili ...ukirudia hilo zoezi mara mbili tayari utakuwa na lita nne

    ReplyDelete
  12. lita 3 lita 5 lita 8
    (0) 0 0 8
    (1) 3 0 5
    (2) 0 3 5
    (3) 3 3 2
    (4) 1 5 2
    (5) 1 0 7
    (6) 0 1 7
    (7) 3 1 4
    (8) 0 4 4

    ReplyDelete
  13. oK

    1. Mimina hayo maji kwenye lita tano.

    2. toa kwenye lita tano na uyamimine wenye lita 3. hivyo kwenye chupa ya lita tano yatabaki lita 2.

    3.Ile chupa ya lita 8 itakuwa imebakiwa na lita 3.

    4.chukua hayo maji ya lita 3 (yaliyo kwenye chupa ya lita 3) na uyarudishe kwenye chupa ya lita 8. (hiyo chupa itakuwa na lita 6)

    5. mimina tena kwenye chupa ya lita 5. kwenye chupa ya lita nane utabakia na lita 1

    6. hayo maji ya lita tano yamimine kwenye chupa ya lita 3. kwa kuwa tayari ina lita 2 basi itaingia lita 1 tu, na ile ya lita 5 itabakiwa na lita 4.

    7. chukua hayo maji ya lita 3 na uyarudishe kwenye chupa ya lita 8 ambayo ilikuwa imebakia na chupa 1 hivyo kuzifnya pia kuwa lita 4.

    Concl. hivyo chupa ya lita 8 itakuwa na lita 4 na chupa ya lita 5 itakuwa na lita 4 na chupa ya lita 3 haitakuwa na kitu.

    thanx and bye

    ReplyDelete
  14. lita 3 5 8
    0 0 8
    3 0 5
    3 5 0
    0 5 3
    3 2 3
    0 2 6
    2 0 6
    2 5 1
    3 4 1
    4 4 0
    Mdau MAK

    ReplyDelete
  15. Omar you nicked it man SPOT ON, GET IT...

    I thought oil, would be the price.
    By Mchangiaji,

    ReplyDelete
  16. Omar..jiniasi!!!

    ReplyDelete
  17. 1. Chukua lita 8 iliyojaa, jaza chupa ya lita 5.

    2. Lita 8 itabaki na lita 3.

    3. Chukua Lita 5 iliyojaa, tia kwenye chupa ya lita 3.

    4. Lita 5 itabaki na lita 2.

    5. Chukua chupa ya lita 3 iliyojaa na tia kwenye ile chupa ya lita 8 (ambayo sasa ina lita 3)

    6. Chupa ya lita 8 sasa itakuwa na lita 6, na chupa ya lita 3 itakuwa tupu.

    7. Chukua ila chupa ya lita 5 (angalia namba 4), na mimina zile lita 2 kwenye chupa ya lita 3.

    8. Chupa ya lita 3 itakuwa na lita 2, na chupa ya lita 5 itakuwa tupu.

    9. Chukua chupa ya lita 8, ambayo sasa ina lita 6 (angalia namba 6) na jaza chupa yenye lita 5.

    10. Sasa chupa ya lita 8 itakuwa na lita 1, chupa ya lita 5 itakuwa imejaa.

    11. Chukua chupa ya lita 5, jaza chupa ya lita 3 (ambayo awali ilikuwa na lita 2)

    12. Hivyo, chupa ya lita 5 itabaki na lita 4 kamili.

    13. Chukua chupa ya lita 3, ambayo imejaa, mimina kwenye chupa ya lita 8, ambayo ina lita 1.

    14. Sasa chupa ya lita 8, itakuwa na lita 4 kamili.

    15. Mwisho.

    Nimejibu 'for the funny of it'
    Cheers

    ReplyDelete
  18. kama kawaida nitaanza na kuuliza,

    hayo maji ni haya ya kawaida au kuna aina ingine ya maji??

    Inawezekana huyo jamaa alikua kwa mama muuza then anataka agawane na wenzake hiyo gongo,

    kama ndivyo hapo wote mmeliwa, maana ikipata hewa tu inayeyuka,

    kuna uwezekana ukachukua hizo lita 8 lakin katika kuzimimina kwenye chombo cha lita 5 isijae wala nini, ingine ikapotelea hewani,

    Kama ni maji haya ya kawaida basi ni simpo tu, ye ayamimine kwenye chombo cha lita 5 kwa kukisia, then alinganishe, patapozidi apunguzie kwengine,

    wala hata chombo cha lita 3 khakitatumika kabisa

    ReplyDelete
  19. Zemacorpolo umepatia zaidi! Kwasababu wewe ndo ulieanza kutegua.

    Mdau Dejvicka

    ReplyDelete
  20. NAKUPA MJI NENDA MUSOMA

    ReplyDelete
  21. Hizo litaa utazipata kwa kunywa ze castle km nane hivi....

    ReplyDelete
  22. Swali lako ni rahisi sana ..
    Given hints .
    chupa moja iko full with 8Lt of h20
    Chupa moja empty of 5 lt
    Chupa moja empy of 3 lt .
    note
    (5 Lt -3Lt)times 2 = 8 Lt.

    Soln.
    Chukua chupa yenye maji 8 lt
    na mimina maji kwenye chupa ( empty ) ya lita tano
    Chukukua tena chupa yenye maji ya lita tano na mimina ndani ya chupa ( empty )ya lita tatu utapata lita mbili , hvyo ukirudia zaoezi hilo mara mbili basi automatically utakuwa na lita nne , maji yaliyobaki bila kupimwa yatakuwa na ujazo wa lita nne pia .
    Kidumu ..
    Mzumbe boy
    ( Supervisor Hazim Timimi )

    ReplyDelete
  23. I WISH ARCHIMEDES WAS STILL ALIVE.HE COULD HAVE GIVEN ME THE SIMPLEST OF ANSWERS THAN THE ABOVE.HOW CONFUSING CAN YOU GET GUYS.I THOUGHT I KNEW THE ANSWER TO THIS UNTIL I STARTED READING YOUR METHODS.DAMN YOU CANT BE TEACHERS.

    ReplyDelete
  24. Simple,
    I will answer it step by step,

    bot1 = 3ltrs bottle
    bot2 = 5ltrs bottle
    bot3 = 8ltrs bottle

    1. Fill bot1 with three ltrs of oil, pour oil into bot2, from bot1.

    2. Filled the remaining of bot2, with water, as we all know that oil float on top of water, base on some weird physical facts, pour the oil back into bot1, you will be left with 2ltrs of water in bot 2.

    3. Filled bot3 with the 2ltrs of water from bot2, now you have an empty bot2, bot3 with 2ltrs of water, and bot1 with 3ltrs of oil.

    4. Now repeat step 1 and 2. you now have bot 3 with 4ltrs of Water, an empty bot2, and 3ltrs of oil in bot1. Now this is the tricky part, you need another bottle with 4ltrs.

    5. Get that 4ltrs of water from bot3 and pour it into bot2(5ltrs bottle), now fill the remaining 1ltr with oil, from bot1, now, pour out 1ltr of oil from bot2, pour the water from bot2(4ltrs of water) back into bot3, which was empty at this stage. Now this is what you are left with Bot1=2ltrs of oil, Bot2=Empty, Bot3=4ltrs of water.

    6.Take 2ltrs of oil from Bot1, and pour it onto bot2, and filled the remainder with water, pour back oil into bot1, now you are left with bot1=2ltrs oil, Bot2=3ltrs of water, bot3=4ltrs of water.

    7.Final Step, Fill the remaining of bot1, with 1ltr of water, once you have that done, pour the oil out, and pour the remaining 1ltr of water from bot1, into bot3 to make it 4ltrs, and therefore your are left with bot1=empty, bot2=4ltrs of water, bot3=4ltrs of water.

    And that answer your question.

    By Mchangiaji

    OIL UMETOA WAPI WAKATI UMEAMBIWA CHUPA NA MAJI!???

    EMBU ACHA MBWEMBWE HAPA!...Kwanza Umekosa...Umeandika JOurnal...Dah!

    -BooSt3D.

    ReplyDelete
  25. JIBU LA CHEMSHA BONGO KWA MDAU WA CANADA

    1st Chukua chupa ya lita 8 na ujaze chupa ya lita 3 na lita 5

    2nd Chukua maji ya lita 3 na yaweke kwenye chupa ya lita 5

    3rd chukua tena chupa ya lita 8 na ujaze tena maji kwenye lita 3 na hivyo utabaki na lita 2 kwenye chupa ya lita 8

    4th chukua tena yale ya lita 3 na ujazie kwenye ile ya lita 5 ambayo tayari ina lita 3. Hivyo utabakiwa na lita 1 kwenye chupa ya lita tatu.

    5th chukua ile ya lita 5 sasa na yatie kwenye ile ya lita 8 ambayo imebakiwa na lita 2, na hivyo chupa ya lita 8 itakuwa na maji ya lita saba sasa.

    6th Chukua sasa ile lita 1 iliyobaki kwenye ile chupa ya lita 3 na uyaweke kwenye chupa ya lita 5 ambayo itakuwa sasa haina kitu.

    7th Then chukua tena ile chupa ya lita 8 ambayo sasa ina lita 7 za maji na ujaze ile chupa ya lita 3, na hivyo utabakiwa na maji lita 4 kwenye chupa ya lita 8

    8th Baada ya hapo, pumua kidogo (phew!!!!!!!) then chukua yale ya lita 3 na uyajaze kwenye ile chupa ya lita 5 ambayo tayari ina maji lita 1 na hivyo kufanya total ya lita 4

    hivyo basi hadi kufikia hapo utakuwa na maji lita 4 kwenye chupa ya lita 5 na maji lita 4 ktk chupa ya lita 8.

    AHSANTE
    NA NAOMBA KUWASILISHA!

    ReplyDelete
  26. JK wa Canada naona kama umechanganya watu kidogo,kawaida huwa chupa tatu zenye uzito kama hivyo ulivyo toa, halafu unauliza vipi utaweza kupata ujazo wa lita4 kwenye chupa moja kwa kutumia hizo chupa, lakini wewe unataka lita nne kwenye chupa mbili tofauti,i hope utatoa jibu lako au wadau wengine watatoa majibu ambayo rahisi kufahamu ya hapo juu naona yamenichanganya.
    Njia yangu mimi ni ya kujaza chupa moja tu hiyo ya pili naona ni vigumu.
    METHOD
    1)Jaza maji kwenye chupa yenye ujazo lita5,
    2)Mimina kwenye chupa ya lita 3,
    utabaki na lita 2,
    3)Hizo lita 2 mimina kwenye chupa lita 8,
    4)Rudia method 1-3
    5)Hapo utakua umepata lita 4 kwenye chupa ya lita 8

    ReplyDelete
  27. lita3 lita5 lita8
    1.0 0 8
    2.3 5 0
    3.0 5 3
    4.3 2 3
    5.0 2 6
    6.2 5 1
    7.3 4 1
    8.0 4 4

    leteni chemsha bongo za maana bwana michuzi.u call this chemsha bongo hata sijatumia zaidi ya dakika 5.bwana michuzi lete chemsha bongo za kweli bwana.

    ReplyDelete
  28. Ingawa michuzi unazifanyia ufisadi post comment zangu sijui, zinakataliwa na mahafidhina! Lakini naona jibu la fumbo hili bora lipelekwe NEC kule hakuna linaloshindakana, hata kama nikujaza maji lita 10 kwenye chupa ya lita 3 na yasibakie basi wao wanaweza!!!

    ReplyDelete
  29. Mdau wa 2.25 hongera umepatia vizuri sana...michuzi vipi mbona hatujasikia zawadi ya mdau million 4.hata mia inatosha si unajua mambo ya choka mbaya

    ReplyDelete
  30. TATIZO LA KWANZA UMEKOSEA KUULIZA SWALI. UNATAKIWA UWAAMBIE WATU KUWA UNA HIYO CHUPA YA LITA 3 TUPU NA YA 5 TUPU NA YA 8 YENYE KIMIMINIKA. ZOEZI NI KUWEKA LITA NNE KWENYE CHUPA ZINGINE MBILI KUBWA NA NDIPO HAPO KWENYE UGUMU.

    UTAFANYA HIVI:
    WEKA KIMIMINIKA KILICHOMO KWENYE CHUPA YA LITA 8 KWENYE CHUPA YA LITA 5, KISHA MIMINA KWENYE CHUPA YA LITA 3 HADI IJAE. UTABAKI NA LITA 2 KWENYE CHUPA YA LITA 5. SASA ZIMIMINE KWENYE CHUPA TUPU KUBWA, HALAFU RUDIA HILI ZOEZI TENA NA UMIMINE KWENYE HII CHUPA KUBWA YA KWANZA. UTAKUWA UMEWEKA LITA 2 MARA 2, HIVYO KUWA LITA 4. FANYA HIVYO KWENYE CHUPA NYINGINE PIA.

    SHUGHULI IMEKWISHA.

    ReplyDelete
  31. Nenda kwa mganga. Peleka kuku mweupe mwenye doa jeusi shingoni na mkia wa nungunungu.

    ReplyDelete
  32. Chupa kubwa imejaa lita nane za maji. Chupa ya kati ipo tupu ila ina uwezo wa kuchukua lita tano. Chupa ndogo inaweza kuchukua lita tatu.
    Anza kwa kuhamisha maji kutoka kwenye chupa kubwa na kuijaza pomoni chupa ya kati. Chupa kubwa itabaki na lita tatu, chupa ya kati lita tano na ndogo lita sifuri.
    Hamisha maji kutoka kwenye chupa ya kati ili uijaze pomoni chupa ndogo. Chupa kubwa bado itakuwa na lita tatu, ya kati mbili na ndogo lita tatu.
    Hamisha maji yote kutoka kwenye chupa ndogo kwenda kwenye chupa kubwa. Kwa hiyo chupa kubwa sasa itakuwa na lita sita, ya kati mbili na ndogo sifuri.
    Hamisha maji yote kutoka kwenye chupa ya kati kwenda ndogo. Chupa kubwa itabakia na lita sita, ya kati sifuri na ndogo lita mbili.
    Hamisha maji kutoka kwenye chupa kubwa na kuijaza pomoni chupa ya kati. Chupa kubwa itabaki na lita moja, ya kati itakuwa na lita tano na ndogo itabaki na lita mbili.
    Tumia maji ya kwenye chupa ya kati kuijazia chupa ndogo. Chupa kubwa itaendelea kuwa na lita moja, ya kati itabakiwa na lita nne unazozitaka na ndogo itakuwa na lita tatu.
    Ukihamishia maji ya chupa ndogo kwenye kubwa utakuwa na lita nne kwenye chupa kubwa, nne kwenye chupa ya kati na sifuri kwenye chupa ndogo.

    ReplyDelete
  33. jaza chupa ya lita 2 na mimina kwenye chupa ya lita 5. mimina tena maji kwenye chupa ya lita 2 na mimina kwenye lita 5. yatakuwa lita 4 kwenye chupa ya lita 5 na kwenye chupa ya lita 8

    ReplyDelete
  34. Tumepewa: chupa lita 8 ikiwa imejaa maji, chupa lita 5 tupu, chupa lita 3 tupu.

    Kazi: gawa maji yawe lita 4 katika sehemu mbili bila kutumia kifaa kingine zaidi ya chupa hizo tatu.

    Njia:

    Moja, Chukua chupa ilojaa maji ya lita 8, mimina katika chupa tupu ya lita 3. Hapo utabakiwa na lita 5 katika chupa ya lita nane na chupa ya lita 5 ikiwa bado ni tupu.

    Mbili, mimina maji uliyoweka katika chupa ya lita 3 uyaweke katika chupa tupu ya lita 5. Hivyo utakuwa
    na chupa tupu ya lita tatu, chupa ya lita tano itakuwa na maji lita 3 na bado utakuwa na maji lita 5 katika chupa ya lita nane.

    Tatu, mimina maji yaliyomo katika chupa ya lita nane (8) uyatie katika chupa tupu ya lita 3 tena. Utakuwa umebakiwa na maji lita 2 katika chupa ya lita nane (8) na chupa ya lita tano itakuwa bado na maji lita 3.

    Nne, chukua chupa ya lita tatu na umimine maji ukiyatia katika chupa ya lita 5 ambayo tayari ina maji ya lita 3 ndani. Hivyo ni lita mbili pekee zitaingia na kubakiwa na lita moja ya maji katika chupa ya lita 3 wakati chupa ya lita tano itakuwa na maji lita tano na wakati huohuo chupa ya lita tano itakuwa na maji lita 2 tu.

    Tano, chukua chupa ya lita tano na umimine maji yote katika chupa ya lita 8 amabayo tayari ina maji ya lita 2 ndani, hii itafanya, chupa ya lita nane iwe na maji lita saba(7) na ile ya lita tano iwe tupu wakati ya lita 3 bado itakuwa na lita moja ndani.

    Sita, chukua chupa ya lita 3 na umimine maji yote ndani ya chupa ya
    lita tano. Hii itafanya chupa ya lita 3 iliyokuwa na maji lita 1 iwe tupu na ile ya lita tano iliyokuwa tupu iwe na maji lita 1 wakati ile ya lita 8 ina maji lita 7 bado.

    saba, mimina maji yaliyopo katika chupa ya lita 8 yenye lita 7 uyaweke katika chupa ya lita 3 ambayo ni tupu, ambapo ni lita tatu tu zitaingia. hii itafanya ubakiwe na maji lita 4 katika chupa ya lita 8 na uwe na lita tatu za maji katika chupa ya lita 3 na lita moja ya maji katika chupa ya lita tano.

    Nane na mwisho, chukua chupa ya lita 3 umimine maji yote katika chupa ya lita 5. Hapo utakuwa na maji lita 4 katika chupa ya lita 8 na maji lita nne katika chupa ya lita 5 na chupa ya lita 3 ikiwa tupu.

    Salaam kwa wote.

    ReplyDelete
  35. Punguza maji kutoka katika chupa ya lita 8 kwenda kwenye lita 3. Alafu toa maji kutoka katika chupa ya lita 3 kwenda kwa lita 5. Baada ya hapo punguza maji tena kutoka katika 8 kwenda kwa 3 tena. Alafu tena punguza maji lita mbili kutoka kwa 3 na ujaze ile chupa ya lita 5. Chupa ya lita 3 itabaki na lita 1 ya maji. Weka alama ya sehemu maji hayo yalipo komea. Kumbuka kwenye chupa ya lita 8 zimebaki lita 2. Jaziliza maji ya lita moja kutoka katika chupa ya lita 3 kwenda chupa ya lita 8. sasa una lita tatu katika chupa ya lita 8. Punguza maji kutoka katika chupa ya lita 5 kwenda kwenye chupa ya lita 3 na uhakikishe maji yanakomea katika ile alama uliyojiwekea wakati ulipobakiwa na lita moja. Sasa ongeza maji hayo ya lita moja kwenda katika chupa ya lita 8 kufanya ziwe lita nne.

    ahsante mdau kutoka Finland

    ReplyDelete
  36. HAYA NDIO MATATIZO YA WATU WALIOZOWEA KWENDA KWA WAGANGA WAKAPEWA MASHARTI YA KIPUUZI.
    INPRACTIZE MASHART KAMA HAYA HAYALETI MAANA NIBORA UMUAMBIE MGANGA WAKO APOKEE LITATANO NA ATAJUWA MWENYEWE KAMA ATAKUNYA OR ATAMWAGA!

    MBONA CHUPA LITA MOJA KIBAO KWANINI UPOTEZE MUDA UNAGAWA UNAFANYAJE JUST BUY NEW BOTTLE!

    MUNAACHA KUJADILI MAMBO YA MAANA MUNALETA VITANDAWILI VYA DARASA LA KWANZA AND THEN MUNAWAZA MAENDELEO! KAZI IPO.

    G7
    UK

    ReplyDelete
  37. simple !!

    unachukua hiyo chupa ya pili yenye uwezo wa kuchukua lita 5
    unamimina nusu ya maji humo
    unabakiza nusu kwenye hiyo yenye maji
    itakua 4 kwa 4 ( nusu kwa nusu )
    umemaliza mchezo huna haja ya kusumbua akili yako

    Next !!!

    ReplyDelete
  38. punguza maji toka lita 8 na jaza lita 5. hayo ya lita 5 weka kwenye lita 3. hayo maji ya kwenye lita 3 yarudishe kwenye lita 8. zimebaki lta 2 kwenye lita 5. ziweke kwenye lita kwenye chupa ya lita 3.toa maji tena kwenye chupa ya lita 8 ujaze lita 5. punguza tena hayo ya kwenye lita 5 na yaweke kwenye chupa ya lita 3. kwenye chupa ya lita 5 zitabaki lita nne. chukua hayo maji ya kwenye lita 3 yaweke kwenye lita 8. zitakuwa 4 kwa nne.

    mdau wa uholanzi

    ReplyDelete
  39. Litres 8 Litres 5 Litres 3 Total shd be 8 for all btls
    from to volume to be moved A B C

    START 8 0 0 8
    A B 5 3 5 0 8
    B C 3 3 2 3 8
    C A 3 6 2 0 8
    B C 2 6 0 2 8
    A B 5 1 5 2 8
    B C 1 1 4 3 8
    C A 3 4 4 0 8

    ReplyDelete
  40. Mimi hapa nimegwaya, kwasabau umesema chupa ya kwanza inauwezo wa kubeba lita tatu tu. Kwahiyo hii mimi niweka pembeni.
    Chupa ya lita nane ndio kigawo changu. Namimina hayo maji nusu yake lita nne kwenye chupa ya lita 5, simple huoni!
    m3

    ReplyDelete
  41. Jibu nalijua! JK wa Canada angalia movie ya Bruce Wills inaitwa Die Hard 3 utapata jibu sahihi.

    ReplyDelete
  42. Nilipata A kwenye maths nilipokuwa kidato cha sita lakini nimegundua wadau wengi walikimbia namba
    Solution ni kama hivi
    8lts 5lts 3lts
    3 5 0
    3 2 3
    6 0 2
    1 5 2
    1 4 3
    4 4 0

    Hiyo ndio solution utakuta chupa ya lita 8 imebaki na 4 na ya lita 5 inabaki na 4 na ya lita 3 haina kitu, hapo ni sawa kwa sawa bila hata kumwaga tone la maji mathematition tupo pamoja hapo

    ReplyDelete
  43. Mweee kaka misupu nilijua ni mimi tu sijui hesabu ila sasa nimejua kumbe kuna wajinga wa hesabu zaidi yangu. Huyo mtoa coment wa kwanza hasara kwa familia yake na Taifa kwa ujumla. Yaani anasubutu kusema nanukuu kama alivyo andika wadau "3+5+8=i6,
    16 ukigwa kwa tatu ni=4 kwa hiyo kila chupa itabidi iwe na lita 4,mbayo 4 mara 3=16 jibu lenyewe umeshatoa kuwa lita 4" Kweli hii ni hasara.

    ReplyDelete
  44. Simpo....

    Ila tatizo sio letu tatizo la huyo anaehangaika kujaza maji wakati hapa kwetu yamekatika......


    Lita nane zote zitamwagwa kwenye ndoo ya maji ya kunywa ili kutuokoa na janga la kiu....


    Mwisho ulieuliza swali zuri ila bado umekosea jinsi ya kutoa maelezo ya chupa.....


    Huwezi ukawa na chupa moja ya coka ndogo na nyingine ya coka kubwa halafu useme utaweza kugawa maji sawa sawa.....


    Chupa zinatakiwa ziwe uniform ila zikitofautiana ujazo ambapo solution itakuwa;


    Unajaza maji kwenye chupa ya lita 5 kwenye chupa ya lita nane zinabaki tatu....

    halafu unapunguza kwenye lita 5 hadi pale yatakapolevel yote n' u got ur 4 lt each kwa chupa...

    Hizi chemsha bongo msizitoe kama hamkuelewa swali vizuri maana hutakiwi kukosea swali ili kuepusha watu kukuchafulia hewa.....Pamoja

    ReplyDelete
  45. Aise kweli ndo maana watu huwa wanafeli mitihani. Kumbe ni kweli kabisa ukiwatolea mwanafunzi wa chuo kikuu swali kwa mfano, 1+1 ni ngapi kwenye mtihani si ajabu wote wakafeli.

    Chupa ya kwanza ina uwezo wa kuchukua lita 3 TU, inawezekanaje sasa maji yagawanywe lita 4 kila moja. Jamani, mmh kazi kwelikweli!

    ReplyDelete
  46. haya maji wakati nayagawa, nikapatwa ni kiu nikanywa kidogo kama turobo lita hivi...sasa itakuwaje?

    fumbo si limeharibika?
    au hewa imechafuka?
    michuzi samahani wakilisha hii!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...