
Ni kweli yawezekana kuwa kujiuzulu Uwaziri kumepokelewa kwa furaha na wengi (mimi mmoja wao). Yawezekana kwa kufanya hivyo uchunguzi utakuwa huru (sidhani alikuwa anazuia uchunguzi anyway); yawezekana kujiuzulu kwake kumekuwa ni kitulizo cha kelele dhidi ya ufisadi; Yawezekana kujiuzulu kwake kumeonesha ufisadi wa viongozi wa serikali ya JK na hivyo kumuondoa kumeonesha jitihada za kusafisha serikali hiyo;
Hata hivyo, hadi hivi sasa CCM haijalipa gharama yoyote ya viongozi wake kuhusishwa na ufisadi na hakuna wakati hadi hivi sasa ambao wao kama CCM wamechukua hatua za viongozi wa serikali waliofanya vitendo vya ufisadi wakiwa ni wanachama wake. Ni kwa sababu hiyo basi naamini kujiuzulu kwa Chenge toka serikalini hakutoshi bali lazima kufuatiwe na kujiuzulu toka Ubunge.
Kwanini?
a. Kiasi cha fedha anachodaiwa kukutwa nacho kingeweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watu wa Jimbo lake lakini aliwaficha wapiga kura wake.
b. Kwa kukiita kiasi hicho "vijisenti" kwa kisingizio cha "usukuma wake" ni tusi kwa wasukuma wengine ambao hawajui maana ya "vijisenti" hasa baada ya yeye mwenyewe kuelezea kuwa "kila mtu ana kiwango chake".
c. Mwakilishi wa wananchi anapotajwa na kuhusishwa na kitendo cha matumizi mabaya ya nafasi yake, nafasi ambayo imetokana na kuchaguliwa na wananchi hao, basi anapojiuzulu nafasi yake basi hana budi kuachia kiti chake ili ampishe mtu mwingine kushika nafasi hiyo.
Bw. Chenge amewaangusha wapiga kura wake, na amekiletea aibu kubwa chama chake. Kati ya wote walioatajwa katika tuhuma za ufisadi ni yeye pekee ambaye tunajua angalau kiasi gani che fedha kimefichwa huko Jersey.
Kwa sababu hiyo basi Chenge siyo tu ajiuzulu Uwaziri kama alivyofanya bali pia ajiuzulu Ubunge wake na Uwakilishi wake ili mwana CCM au mtu mwingine aweze kuwawakilisha wananchi wa Bariadi Magharibi.
JIUZULU UBUNGE BW. CHENGE, UMEKUWA AIBU YA TAIFA LETU!
Title: KLH News Episode: Kujiuzulu Uwaziri kwa Chenge, usiwe mwisho wa kuwajibika
Enjoy!
Duu!mithupu we noma,ckutegemea kukuta habar ya kujiuzuru kwa chenge imeandikwa namna hii kwenye blogu yako.lkn kiukwel kujiuzuru tu hakutoshi anatakiwa achukuliwe hatua zaid
ReplyDeleteKuanza taratibu kurudisha imani na matumaini ya Watanzania kwa serikali nashauri Raisi Kikwete amrudishe Magufuli kwenye hiyo wizara ya Miundombinu alipokuwa Chenge ambaye kajiuzulu kwa sababu ya kashfa tuhumiwa.
ReplyDeletekoloboi@yahoo.com
UFISADI + HASARA + AIBU = JELA full stop
ReplyDeletemmeona domo lake
ReplyDeleteSASA CCM NI CHAMA CHA MAFISADI?? MAANA LOWASSA, KARAMAGI,CHENGE, MRAMBA, MKAPA, YONA, SUMAYE, MSABAHA WOTE NI WANA CCM NA NI WAJUMBE WA KAMATI KUU. INGETAKIWA ILI KURUDISHA IMANI KWA WANANCHI, THEN HAO MAFISADI WAONDOLEWE KWENYE CHAMA (WAFUKUZWE UANACHAMA)THEN WASHTAKIWE NA KUFILISIWA ILI UWE MFANO KWA WANASIASA WENGINE WENYE TAMAA. RAIS KIKWETE BADO ANAWAKUMBATIA HAWA JAMAA MPAKA LINI? KWA NINI HAJARUHUSU BALALI KULETWA NCHINI? US WALISHATOA TAARIFA KUWA WANAWEZA KUMLETA, KWA NINI RAIS ANAZUIA?MIMI NADHANI HATA RAIS ANATAKIWA AJIUZULU AACHIE NGAZI
ReplyDeletevisent vyangu
tusidanganyane kuwa "vijisenti" ni kisukuma. kwetu sisi wasukuma tunasema majihela
ReplyDeleteMichuzi hii ni aibu sio kwa hao mawaziri tuu, bali ni kwa Taifa na hata sisi wengine tunaonekana kama hiyo ndiyo mila yetu. Nashangaa kwanini kashfa kama hizi zinapotokea kamati kuu ya CCM haiwanyangà nyi watu hawa kadi zake za CCM ili kuwatoa katika chama. Suala na dogo tu chukua kadi muone watakaribishwa wapi tena kufanya ufisadi wao. Kwani kunyanganya mtu kadi ya chama kunahitaji fedha za kigeni jamani. Mtoto ukimpa kitumbua akakitia mchanga si unakitupa na kumueleza huwa hatuchafui chakula hii aIBU itaisha lini jamani.
ReplyDeleteAisee Koloboi umesema kweli na wala ujadanganya. Mimi nataka nimpigia JK simu nimpe hii life kabisa. Afadhali hili lifisadi tulichome moto tu mbona jamani vibaka wanachomwa moto? Lione wala halioni haya. Hilooooooooooo!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteWewe anonym wa Apr 21,@10:51am hiyo Recycling ya Viongozi ndiyo iliyotuangamiza nchi hii tukafikia hapa tulipo.Tunao Watanzania wengi tu wenye sifa za kujaza nafasi hiyo ya Chenge isiwe kila siku ni Magufuli tu!Sisi wengine bado tunamkumbuka kwa jinsi alivyohusika katika zoezi zima la Uuzaji wa Nyumba za Serikali yeye akiwa Waziri Mhusika!Wengine tuliishi katika nyumba hizo hizo kwa zaidi ya miaka 20 tukiwa watumishi waadilifu serikalini.Hivi sasa ukituona ni Masikini wa Kutupa huwezi kuamini kwamba mtu huyo alikuwa ofisa wa serikali tena University Graduate aliyeanza utumishi kwa mshahara wa shilingi 900/= kwa mwezi.Na nyumba hizo leo zije ziuziwe watu ambao hawajui hata machungu yake!What a shame!Kwa hiyo ndugu yangu usizungumzie habari za Magufuli kabisa inatutia simanzi sisi tulioikokota serikali hii hadi ikafikia hapo ambapo wenzetu wajanja wakatugeuza sisi tuliotangulia nyuma kama vile hatukuwa na akili timamu.Sisi wakati wetu tungeamua tuuziane zile nyumba za serikali wao wangekuta nyumba gani za kuuziana?Msifanye mambo bila kufikiria athari zake.Wale watu wangeweza kupewa mikopo wakajenge nyumba zao mpya kabisa lakini siyo kutaifisha/kubinafsisha kidogo kilichopo ili wengine wakose kabisa!ULAFI WA MADARAKA NDIO HUO UKIAMBIWA!hiyo wizara inaweza ikabaki na naibu waziri tu mpaka uchaguzi ujao na mambo yakaenda bila matatizo.Msituongezee gharama nyinginezo zisizo na faida yoyote katika jamii ya watanzania.Pleeease.
ReplyDeleteNdo imetoka hiyo! mtamsahau sasa hivi. Anaenda kujilia alivyohifadhi ndani ya "firiji".
ReplyDeleteHapo imakaa vizuri sana sasa kinachofuata angekwenda segerea hata miaka 30 tu hivi inatosha na mshiko urudishwe home haraka sana
ReplyDeleteKatika CCM wasafi ni wachache au hakuna kabisa! Hata huyo Magufuli unayosema arudishwe hakuwa msafi. Alihonga nyumba ya serikali kwa kimada huku akijua kwamba huyo kimada hakuwa mfanyakazi wa serikali na hivyo hakustahili kuuziwa nyumba. Pia naye anauchafu wake mwingine ambao wakati ukifika ataanikwa tu. Hiyo wizara apewe mtu ambaye hana damu ya ufisadi kwani ni kati ya wizara zinazopokea pesa nyingi sana za serikali kwa ajili ya miundombinu
ReplyDeleteAnonymous wa pili hapo juu ungejua, au ukifunuliwa ya magufuli alipokua ujenzi ungetaka asipewe tena hata ukuu wa wilaya. Nchi inatia huruma jamani,sijui msafi ni nani! May be kizazi kipya kije kiiokoe.
ReplyDeleteNadhani ni muda muafaka kwa Mh. Pombe Magufuli kurudi katika wizara hiyo ili amalizie vision yake ya CORRIDORS. Yaani kuwa na barabara za kiwango cha Lami katika kila kanda.
ReplyDeleteKorido za Magufuli nikizikumbuka,Kibiti - Lindi, Mtwara-Mbamba Bay, Tunduma-Mpanda, Kigoma - Kagera, Kagera - Mara via Mwanza, Arusha- Iringa Via Dodoma, Kigoma-Dodoma.
Kujiuzuru pekee yake haitoshi warudishe hizo pesa walizokwiba
Moja kati ya kitu ambacho masikio yangu hayatamani kusikia ni kuhusiana na na watu kujiadhibu wenyewe. eti amejiuzulu.hivi licha ya kuwa tunataka maendeleo lakini nani asiyejua kuwa tunahangaika kwa ajili ya matumbo yenu.leo hii umeshapata pesa bilionea kwa nini usijiuzulu, yani umeshakuwa bilionea halafu bado unahangaika kuwaongoza watu kwa lipi hasa? umekuwa ndio mchezo wa hawa viongozi. palikuwa na haja ya watu hawa kufungwa na kufilisiwa mali zao leo ukinambaia kujiuzulu wameona sio ishu ndio mana wanajiadhibu wenyewe,hawa vipi? mnavyotwambia mmejiuzulu mnamaana sisi tufurahi yani tufurahi kwa kuwa mmeachana na majukumu sasa mnakula kuku,what!s the meaning of the neno kujiuzulu.
ReplyDeletemh, wasiojua maumivu watafurahi kusikia kujiuzulu, what the meaning of the neno kujiuzulu,ha umeona wapi mtu kujiadhibu mwenyewe? kwani umesikia sisi tuianataka uendelee kupata shida? kutuongoza amini usiamni kazi ya kweli ni ya kanisa na misikiti faida kwa mungu but katika uongozi huu haman kujituma bali unafanya ili upate pesa na umeshapata umekuwa bilionea vipi leo usiseme kujiuzulu, kwani kuongoza watu ni raha au shida? tunaongoza coz tunataka hela umeshapata sasa kwa nini usijiuzulu ili uzitumie kwa nafasi,dawa yako wewe ni bora ufilisiwe mali zako then uende jela miaka isiyojulikana,hapo angalau but inskuwaje mtu anaefisadi badala ya kupewa adhabu kali leo anataka kupumzika. kweli haki iko mbinguni duniani ni sheria, katuibia halafu leo anakwenda kupumzika tunafurahia,mwacheni afanye kazi kama punda bila mshahara wala marupu rupu tena kama vipi awe mjumbe wa mtaa. hakuna kupumzika mtu hapa nenda kalime segerea, unapumzika? unajiuzulu? unajipa adhabu mwenyewe? kweli tanzania kichwa cha mwenda wazimu
ReplyDeleteJamani hivi tunaelekea wapi ? Nchi yetu inazidi kudidimia . Sasa huyu kajiuzulu , anachukuliwa hatua gani? Lowasa vimeisha hivi hivi .. Ujumbe wanaotoa hapa ni kwamba ni sawa kuwaibia wananchi ukikamatwa jiuluzu ?? Serekali yetu hii...ni lini itatupigania sisi walala hoi . Maana viongozi wengi wanaingia kwenye madaraka na wamechoka wakikaa muda wanakuwa na "VIJISENTI" . Tumechoka sisi hatua sichukuliwe hapa ..
ReplyDeleteMimi sina imani na mawaziri wote waliopo, kama ingeliwezekana waziri kutoka nje ya hawo waliopo ingekuwa bora!
ReplyDeleteWapo watu wazuri, viongozi safi ambao hawapo kabisa kwenye hiyo `system'. Sijui tufanyeje ili waweze kuliokoa taifa hili.
Nawaambia ukweli, kama Kikwete ataendelea kuwapa hawa jamaa waliomzunguka, atakuwa anaendelea kuwanufaisha mafisadi.
Ni wakati mzuri wa kuweka damu changa, asiangalie tena `majina/umaarufu', kwani wote hawo wapo kwa ajili ya nafsi zao, na akiendelea hivyo... watazidi kumchafulia jina!
m3
Jamani kwanza nini maana neno fisadi! mimi nadhani hii itakuwa tabia viongozi watakuwa wanaiba weeeeeeee kashfa zao zikitoka au zikijulikana wanajiuzulu, naona ishakua mchezo, JK Sasa nyonga, hakuna cha jela wala kufilisiwa mmoja akiwa mfano wengine wote watarudisha pesa wenyewe!
ReplyDeleteWakati wa CCM kusambaratika/ mpasuko umefika. Kama kweli JK anataka kuisafishia CCM mbele ya umma itabidi mkondo wa sheria ufuatwe bila woga au hujuma kwani ni wengi wako katika list ya mafisadi na wanashikilia vyeo aya juu ndani ya CCM, kamati kuu.
ReplyDeleteCCM wote si mafisadi na wakati umefika wa kujisafisha aidha uchagizi ujao itakuwa kama Kenya.
Wananchi wamechoshwa na scandals za viongozi wabovu na macho na masikio yao yako wazi kuona mtendaji wao mkuu waliompa dhamana ya nchi, Rais JK, anachuikua hatua kali zaidi za kurejesha imani na serikali ya CCM.
KUJIUZULU KWAKE SIO KWA AJILI YA WATANZANIA, KAJIUZULU KWA SABABU YA KUWAONESHA WADHAMINI WA BAJETI YA NCHI KWAMBA JAKAYA ANAFANYA KAZI YA KUZUIA CORRUPTION NCHINI HILI WADHAMINI WAENDELEE KUCHANGIA FEDHA KWENYE BAJETI YA NCHI PAMOJA NA MISAADA MINGINE.NDIO KAMA WAKINA LOWASA NA WENZAKE WOTE HILE KUWARIDHISHA WADHAMINI SIO WATANZANIA.KAMA INGEKUWA KWA AJILI YA WATANZANIA HAO WATU WOTE HAWAPASWI KUWA WABUNGE MPAKA LEO WALITAKIWA KUJIUZULU NA UBUNGE PIA KWANI WAMEWAHUJUMU MPAKA WAPIGA KURA WAO NA SIONI KAMA KUNA RAIA ANAWEZA KUMPIGIA KURA KIONGOZI FISADI.KWAHIO TUSISHANGILIE SANA KWA DANGANYA TOTO HIO KAMA RICHMOND INAENDELEA KULIPWA MPAKA LEO SITAWEZA KUSHANGAA HAO WOTE WALIOJIUZULU WANAENDELEA KUPATA "VIJISENTI" VYAO KAMA KAWAIDA.LAKINI NINACHOFURAHI KUHUSU SWALA LA CHENGE UCHUNGUZI UNAFANYWA PIA NA WAINGEREZA KWAHIO UKWELI UTAPATIKANA KUTOKA PANDE MOJA YAPO.
ReplyDeleteKaka michuzi sioni sababu ya wewe kubania haya maoni kwani post hii pia imeongea ukweli ndio maana nimechangia manake huwa unabania maoni mengi sana ya ukweli.nakutakia kazi njema.
Mdau mzawa
JK ampe Adam Malima hiyo wizara. Ni kijana na hausiki na ufisadi na ni mwenye mtazamo wa karne 21.
ReplyDeletekama kweli wabunge wa CCM wapo kwa maslahi ya wanachi wanaweza kujiunga na wapinzani na kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali. Hii inamaanisha JK lazima atavunja baraza la mawaziri na wabunge itabidi warudi kwa waliowapigia kura kama wanataka tena huo ubunge. Kama kweli wabunge wa CCM wana ujasiri na kukerwa na ufisadi wanaweza kuonyesha uzalendo wao kwa nchi yao.
ReplyDeletelIONE DOMU LAKE,NINGEKUWA KARIBU NINGEMUWASHA KIBAO CHA USO PWAAAAA!!LIPELEKENI JELA MOJA KWA MOJA..DAWA SIO KUJIUZULU DAWA KURUDISHA HELA NA KWENDA JELA,MIAKA KUMI,AKITOKA JELA ACHAPWE VIBOKOVYA MAKALIONI 15 AKAMWONYESHE MKEWE AKIRUDI NYUMBANI...MDAU KYEKUU..MICHUZI MICHUZI TOA HII COMMENT YANGU
ReplyDeleteHii inadhihirisha kauli yangu ya zamani sana kwamba, wabongo bado wana uwezo mdogo sana wa kuelewa siasa. Kuanzia Balali, Lowasa na huyu Karamagi, hii inatosha kabisa kuvunja serikali na kuita uchaguzi. Lakini kutokana na upumbavu na uzembe wa kufikiri, bado mnasubiri mpaka uchaguzi ujao mwaka 2010.
ReplyDeleteWewe anony hapo juu kama bado una imani na kikwete mwenyewe, basi wewe una ugonjwa wa "dementia"
ReplyDeleteKujiuzulu kwa Bw. Chenge na mawaziri wengine kunaonyesha udhaifu wa rais wetu JK. Ili kujiletea heshima yake na kuweka footprints zake kwenye baraza, serikali na kwa baadhi ya wanaoona kuwa 'vigogo' ni budi rais awe akiwaondoa/fukuza katika baraza na serikali watu kama hawa yeye mwenyewe!!!
ReplyDeleteTATIZO LA TANZANIA KESI ZA NYANI ZINAHUKUMIWA NA TUMBILI.
ReplyDeleteMdau mwenye jazba
Three days ago when I was in London enroute to Canada I wrote about the importance of this guy (Mr. Chenge) to resign both his ministerial and member of the parliament positions. I am confident that he has done one of the two asked, and to make me have sympathy with him, I would like him under no pressure to resign the second position left, which is, his constituency post. To me -from that point we (me as mwanachi too) can cut a deal with him to have a lesser case to answer in the high court or appeal court if necessary. What we will need from him –is to offer or give a swift and vivid cooperation with all parties and prosecution side a valid information -on how he got that money in the first place. In either case if it will be revealed that he did obtain it from illegal means, then he will be required to return the money that has already been secured. We as wananchi can ask or persuade the President to pardon Mr. Chenge if he will snitch the names of other greedy citizens who were in that deal, when he was an Attorney General.
ReplyDeleteIf Mr. Chenge thinks he can argue to keep the second position on the grounds that ,Bariadi wananchi were the one who elected him and they will be the one who will decide if he has to be thrown under the bus, then he will be very dead wrong. There will be no means of cutting any deal with him and therefore he will be left to answer the allegations with the high court or court of appeal and very important is either his case has to be summoned in UK where he will be found guilty. I am not sure that Tanzania court will found him guilty, because they are all the same in “Kulindana”; he (Mr. Chenge) will provide dubious documents showing stocks purchases and business profits that nobody will make a follow up of its legality and with no any balance and check he will be left free and roaming in Dar-Es-Salaam streets, like nothing did happen to him at first place. If you don’t believe my words then read today’s IPP media on the comment that Mr. Venance Ngula the then deputy Finance Minister said about Mr. Chenge, which to me shows it was chain of many dignitary people who were involved in this deal. Mr. Venance went on saying that “nothing can be done by wananchi concerning this issue”. To me this shows that’s the reason despite all “makelele” from wananchi not to buy this radar at the first place the government and its officials went all the way and bought it anyway. The perfect place that will conduct this case fairly will be UK, I have read the Tanzania law concerning this and Mr. Chenge can face British court if Tanzania prosecutors can obtain a permit to file this case overseas. I am sure like any smart guys, him being a former AG, will hire the best lawyers in town and eventually win this case if conducted in Tanzania and with the help of former Judges whom many he helped appoint, will pay back the favor.
I wonder why Mr. Chenge who is catholic and a former seminarian at Makoko and Nyegezi seminaries, with a first degree from UDSM and a Harvard graduate degree ,who also once happened to be a highly respected leader changed to be one among the arrogant leaders that our country now have. I am astonished why at least he would not follow the “nyayo” of Judge Warioba, who at least is saying loudly something -about what is going on in the country - and is now engaging in business that can allow him to have or put money anywhere and “at least clean” money. I remember some days back when I was in Tanzania Mr. Chenge was once quoted and said to Prof Lamwai that although “he (Mr. Chenge) does not have a PHD/JD in law like Dr. Lamwai, his (Chenge) LLM degree from Harvard University is greater that any PHD/JD offered by UDSM. To me the way I see, that was an insult and with addition of “vijisenti” comments it’s like adding a fire
My advice to Chenge and all others who hold public and high offices- it’s now time to come clean and show to us how honest and truth you guys are. Concerning, the money and businesses that both of you operate or hold locally and offshore, we need to see within an open format either at official Government gazette or at other channels how much ya, all worth. Please, do me a favor; resign the Member of the parliament position of Bariadi west, and that will send a clear message or signal to Lowassa, Msabaha, Karamagi, Mramba, and Yona to follow the suit and do the same.
Michuzi unakumbuka huu msemo wa miaka ya nyuma kabla ya taarifa ya habari RTD
ReplyDelete"Lione linavyojitafunatafuna.
Limekula mali ya umma.
Wewe wacha kuiba mali ya umma"
At least miaka hiyo redio ya serikali ilikuwa inakemea maovu lakini miaka hii ndio kwanza vyombo vya serikali vinatumika kukingia kifua viongozi wabovu.
Mbona Abdu Jumbe alivuliwa uongozi Dodoma wakati JK Nyerere alivyokuwa kiongozi wa nchi. waulize kina Fundikira, Kasanga Tumbo, Kasela Bantu, Malecela nk watakueleza fagio la chuma la Nyerere lilivyokuwa na makali.
Viongozi wote walikuwa wanaogopa rushwa kama ukoma na wanavaa chonglai na safari buti. Siku hizi wanapiga masuti ya $ 3000 kama vile mchezo.
Jamani hii ni aibu! Nguvu za wananchi zinaishia kwa hawa mafisadi! Hawa ndo wanaosababisha wananchi kuishi maisha ya kimasikini. Jamani tunahitaji kukataa mambo kama haya! Mambo mengi Tanzania hali yake ni ya kusikitisha shauri ya mafisadi.
ReplyDeleteKikwete huna muda wa kuendelea kutabasamu kwa mambo kama haya, ni muda wa kuwashughulikia mafisadi kisheria, warudishe jasho la wananchi! Hizo hela zitaleta mabadiliko makubwa badala ya kuendelea kuombaomba kwa nchi za watu watusaidie huku sisi wenyewe hatuko serious kutoka kwenye huo umasikini. Watanzania tunatakiwa kusema hapana na tunataka hiki na kile. Muda wa kudanganywa kuwa tuna amani haupo kwani kama hatuwezi tena kuamini kuwa viongozi waliopo kwenye public sector kazi yao ni kutumikia wananchi hatuna amani na hatuna imani nao. Mafisadi wote inabidi watolewe kwenye shughuli zote za chama na serikali na kusulubishwa!
Tumechoka na mafisadi mnatuaibisha! Hakuna raha tena ya kusema eti mi ni mtanzania! Nchi imeoza!
Huyu nae katuaibisha wasukuma!!!
ReplyDeleteanyway lenye mwanzo lina mwisho. Ukificha moto moshi utakuumbua
Acheni uzandiki jamani hasa huyo anayesema eti "akijiuzulu waziri na JK ajiuzulu"kWA KOSA LIPI???Makosa ya wengine ajiuzulu Rais wapi na wapi?Mbona enzi za JK Nyerere-RIP alijiuzulu Nwinyi pekeyake??Na hamkupiga kelele.Leo JK kawapa freedom kila kijijambo oooh Rais ajiuzulu.Mbona kipindi cha Nkapa maneno hayakuwapo???Na kulikuwa na uvundo wa kutisha?Msimuonee JK nina uhakika yeye ni msafi.
ReplyDeleteKingine huku ughaibuni - Ukerewe walijiuzulu mawaziri kibao enzi ya Tony Blair lakini yeye wala hakuguswa wala kujiuzulu hata USA wamejiuzulu mtu kibao za CIA mbona Kichaka hakujiuzulu???msipende kuosha vinywa just because mmepewa uhuru huo.
Keep it Up! JK,safisha mafisadi Tunakuaminia babaake "NA KAZI IENDELEE".
Upinzani bongo hamna,wapinzani wenyewe ni MAFISADI ORIGINAL.
Cha Chandu - UK
Anon wa April 21 9.15 p.m hapo ju umenikumbusha msemo wa Mazungumzo Baada ya Habari RTD enzi hizo. Msemo huo naukumbuka hadi leo ulikuwa unasema hivi:
ReplyDelete"MWENZETU HUYU ANAUMWA. TENA ANAUMWA SANA. MUDA MFUPI TU ULIOPITA ALICHUKUA KISU AKAJIKATAKATA MWENYEWE HUKU ANATABASAMU! MWIZI WA MALI YA UMMA NI SAWA NA PUNGUANI. AKILI ZAKE ZIMEHAMA. MALI YA UMMA UNAYOSITIRI UHAI WAKE NA UHAI WA JAMII NZIMA, INAITAFUNA, ANAIMEZA. IKIMALIZIKA NA YEYE ATAMALIZIKA!"
Kweli enzi zile viongozi walikuwa wanaogopa kuiba. Walioiba anangalau zilikuwepo dalili kuonyesha kuwa walishughulikiwa. Lakini leo, Mh! Labda kwa kuwa Bwana Bulicheka naye ni mmoja wa watuhumiwa.
MIMI NINAWASHANGAA SANA WAANDISHI WETU WA TANZANIA WANAVALIA NJUGA KITU HALAFU HAWAKIMALIZII. INAELEKEA WANACHUNGUZA WAKISHAPATA JAMBO MTU AKIJIUZULU BASI WANARIDHIKA, ANGALIA YA LOWASA, KARAMAGI, MRAMBA SASA HIVI KIMNYA HATA USIKII WAKIFUATILIA KWAMBA BAADA YA HAO KUJIUZULU WHAT NEXT. NA HUYO MH. RAIS ANASUBIRI MPAKA MAFISADI WATAJWE NDIO WAJIUZULU INA MAANA YEYE ALIKUWA HAWAJUI MPAKA WATU WA NJE WAWATAJE NDIO TATIZO LA KUPEANA MADARAKA KISHKAJI NA MARAFIKI ZAKE ONA SASA INAVYOMKOST ANAONEKANA HAJATULIA
ReplyDeleteJk ana kazi kweli,huu uozo mwingi tunaoona sasa ni kipindi cha uongozi wa MKAPA lakini zahama yote inamkuta yeye madarakani,jitahidi JK kadiri uwezavyo kuwashughulikia hao mafisadi.
ReplyDeleteDah!! mimi naona hawa viongozi wetu wote wameshaona kuwa cha kufanya wakiwa kwenye madaraka yao ni ufisadi tu, hivi hakuna wa kuwauliza wanawezaje kuwa na mapesa yote hayo,watuonyeshe walizalishaje hizo pesa kama ni kwa kazi mbili na overtime, wahesabiwe na kilichobaki kijengewe angalau shule za msingi nzuri kwa taifa la kesho.Tanzania nchi ya ajabu sana,unaiba mali za nchi na wananchi kisha unajiuzuru na wananchi wanashangilia na ndio imetoka hiyo. Mungu ibariki Tanzania, wabariki ...
ReplyDeleteMHESHIMIWA SPIKA!! TUNAOMBA PESA ZETU SISI WALALA HOI ZIRUDISHWE HARAKA SANA SIO TU KUJIUZULU!!
ReplyDeleteJe umewahi kusikia msemo kuwa a flap of butterflys wing in Brazil setting off a tornado in Texas, kila nikisoma juu ya mizozo ya misappropriation of public funds in Tanzania naogopa sana kuwa sasa ni flapping of wings of kipepeo lakini kesho mambo hayo yasipoangaliwa vizuri yatatuletea matatizo na misiba balaa.Bila shaka wakina nanihii waliokuwa na nafasi serikalini na kwenye chama walidokoa kidogo kutoka chungu wa wananchi,they picked our pockets its now payback time, lakini wengi wao bado wana meno na huweza wakatuuma tukiwanyanganya mifupa yao. Wadau mwaonaje kama tukiomba serikali iappoint commission a bishop Tutu commission to deal with this in public na wakosefu wasamehewe au watiwe bakora au a few years free parking in Ukonga
ReplyDeleteTHis is none sense...Utafukuza wangapi??? watu wanahela miaka na miaka...zikizidi tu ati Ufisadi. Sasa wangapi watajiuzulu? na baraza litavunjwa mara ngapi? Mbona mambo mengine ni ujinga tu. Kikwete amewapa power wapinzani hii ndio matokeo yake na asipoangalia watakuja kumvaa kila mtu. Ushauri wa bure, since serekali inadosari ni vyema rais awe anawachia ngazi bila ya kashfa. What if hizo hela alizonanazo hakupata kwa ufisadi, whats next?
ReplyDeleteNamhala watugwisha gete mahela gose ayo?
ReplyDeleteMdau UK
Huyu Nchenge au nchuzi? Nchuzi pia nchenge!!!
ReplyDeletemmmhh....
ReplyDeletejamani, viongozi wana tutia aibu watanzania tulio huku nnje...
tunashindwa hata kujivunia nnchi yetu, unadhani nani atakuwa kifua mbele kujitambulisha "mimi ni mfisadi", natoka nnchi ya mafisadi....
tunakosa pride na Tanzania, na hadhi ya nnchi inashuka vibaya mmno...
big up michuzi kwa kutu update na nyeti za bongo..
SISI WASUKUMA TUNASEMA MAPESA! KAMA ALIVYOSEMA MH CHEYO MOMOSE TANGU MIAKA HIYOOO! HILI LA VIJISENTI NI DHARAU ZA CHENGE TU! IN SHORT, AREJESHE 'VIJISENTI' VYETU VITAOKOA MAISHA YA AKINAMAMA WANAOKUFA KWA UZAZI KWA KUKOSA GLOVES ZA SH. 500/- KWA AJILI YA MANESI WANAOWAZALISHA!
ReplyDelete