Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Ali Mohamrd Shein akifuatilia kwa makini mkutano wa makamishna wa Tume ya Afrika iliyoundwa Serikali ya Denmark. Mkutano huo unazungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano kati ya Denmark na Afrika pamoja na kutafuta njia ya kuongeza ajira kwa Afrika na maendeleo kwa jumla uliofanyika leo mjini Copenhagen Denmark. Kushoto ni Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mh. Dk. Asha Rose Migiro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hao ndio wawekezaji sio Wadosi!

    ReplyDelete
  2. Body language of VP inanipa wasiwasi.Kama vile mtahiniwa aliyechemsha paper na anaona pepa imeandikwa kiarabu.hahahahahahaha

    ReplyDelete
  3. Kweli Tnzania na Afrika kwa ujumla tunakoelekea hakujulikani, maana kila mtu anataka atugeuze kichwa cha wendawazimu. Mara China, mara India,mara Denmark, mara Marekani, mara Uingereza, mara Ujerumani. Ya kwangu ni macho ila kwa kila kitu kinachokubaliwa na viongozi wetu, sidhani kama kina manufaa kwetu. Hat siku moja watanzania wanatakiwa kujua kuwa mzungu au mhindi au mtu yeyote hawezi kukusaidia hivi hivi, kutakuwa na kitu anatafuta hata kwama ni kwa miaka kumi ijayo.Tatizo la viongozi wetu wa Afrika ni kufikiria mambo ya mwaka mmoja mbel, wenzao wanafikiri hata miaka hamsini mbele.

    ReplyDelete
  4. T:Unasikia Mzee,sisi matatizo yetu makubwa kule Bongo ni kuhusu hivi Visenti.Mkitusaidia Vijisenti Kidogo aaaaaaaahhhhh mbona shida zetu nyingi zitaishaaaaaa!Siunajua mwaka huu vijana wetu wamejitahidi sana lakini Mvua tena ikatibua kila kitu.Aaaaaaagh mwaka huu ilikuwa tuvune Mpunga na Mahindi kibao unafikiri mchezo nini!
    V:Simple,Vijisenti vingapi vile mlikuwa mnahitaji kwa mwaka huu mheshimiwa?Maana sisi kwenye suala la visenti kwetu siyo tatizo,si unajua Denmark bwana pesa njenje.Isitoshe Tanzania is a very beautifull country,good policies,plenty of peace,ndugu kila mtu ndugu you see!
    T:eeeeh Mze hatutaki tukupe hesabu ya kubahatisha.Itabidi wakati wa mapumziko ya chai mimim na wenzangu tukae chini tupige hesabu kwelikweli ili tukupe exact amount.Si unajua lile li nchi likubwa sana!Kuna Matumbo ya kulisha kama milioni 47 kwa hesabu za haraka haraka.Lakini watu kama KUMI HIVI ndiyo watakao tusumbua sana.Si unajua kila kitu kule kwetu ni Politics tu Mze!Aaaah wenzetu huku mna raha eeeeeii!Hivi mihela yote hii mnaitoaga wapi?Mwanangu aje asomee haya maarifa.Mwaka huu Mafuriko,basi ujue Mwakani tutakumbwa na Ukame tu maana hili Jua linatuchezea kwelikweli Mze!
    V:tehe tehe tehe tehe,Tanzania iko muzuri sana!This time tutawapatia kabisa Mtambo wenyewe wa Kuchapishia Manoti,you see!You will never go broke my friend.You be Rich like Us in Denmark,like it my friend?
    T:Lakini sisi tulitaka zilezile mlizozichapisha wenyewe.Mkileta Mtambo kwetu 'Utaibiwa na Mafisadi!'. tehe tehe tehe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...