Home
Unlabelled
dudumizi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Daah kweli Udongo unakula watu .. katika watu nilikuwa nawahusudu kwa uimbaji Alikuwa Dudumizi ..nakumbuka kile kibao cha Makulata..na bima lee .enzi hizo akina Shaban Dede, Athuman Momba Ray Bashekanako, Jumbe Batamwanya, Mulenga, .KILITIKISA JIJI MIAKA YA 80..mimi nilikuwa mpenzi mkubwa nilikuwa sikosi pale Mbwisi Bar MANZESE
ReplyDeleteAmani, Heshima na Upendo kwako Kaka na wadau wote.
ReplyDeleteUnapozungumzia sauti za kipekee katika muziki uliokuwa ukiitwa wa dansi nchini hasa miaka ya mwisho ya 80 kuelekea 90 na ambazo kwa bahati mbaya zote zimebaki kusikika tu kwenye rekodi maana wameshatutoka basi huwezi kuweka pembeni sauti za watu kama Jerry Nashon "Dudumizi", Nicodemus Zengekala, Hemed Maneti "Chiriku", Eddie Sheggy "Fast Mover", "TX" Moshi William, Marijani Rajabu "Jabali la Muziki", Othman Momba, Seleman Mbwembwe, Freddie Ndala Kasheba "Maestro", Rahma Shari na wengine wengi ambao nimeshindwa kuvuta kumbukumbu ya majina yao na ni jambo la shukrani muhimu saana kwa wadau kama John Kitime kutupa kumbukumbu ya Taswira ya wadau hawa wakubwa wa muziki wa Dansi na pia bado nikingali na ndoto ya kuungana ama kuunganisha wadau wenye uwezo kuweza kuwa na tuzo na inductions za hawa Hall Of Famers katika muziki wa Dansi nchini. Yeyote aweza kuwapa tuzo, heshima na haki yao hawa wadau kwani wametenda mengi katika muziki wa dansi nchini. Shukrani kaka Michu na Brother Kitime kwa kumbukumbu njema.
Blessings
Ras Twin
Badi bakule anajitahidi lakini wapiii!
ReplyDeleteDuu pilato
ReplyDeleteunanikumbushambaaalisana mamboya mbwisi wakati huo ndio mitaa yetu msufini kwa alibay sfa united na faru united pia kuana sato aaahh we achatu ninakumbuka kibao cha dudumizi pesa zanisumbua
ah mabox kaka
Nilicheza na huyu bwana nikiwa na umri wa miaka 5 to 6 na nakumbuka vema. Nataraji naye alikuwa na umri kama wangu. Alikuwa na kaka zake waliokuwa na gitaa - bali sisi tulikuwa tukitengeneza gari kwa kutumia majani ya katani. Baba yake alikuwa mchunga ng'ombe nje kidogo ya mji wa Musoma karibu na Mara Sekondari - miaka hiyo ikiitwa Musoma College. Tuliachana kwenye umri wa miaka 8 au hapo. Sikuonana naye tena kwa miaka. Baadaye sana nikiwa shule ay bweni Mwanza nilikutana naye akiwa askari magereza - nafikiri kwenye miaka ya mwisho ya sabini au mwanzo mwa themanini. Ama nisingalimjua ila kwa kuambiwa na rafiki yangu mmoja ambaye sasa ni mwandishi wa habari mahiri jijini Dar. Miaka ikapita na kunako miaka ya mwanzo ya tisini (au pengine ya kati ya tisini) tulipanga mimi na rafiki yangu huyo mwandishi twende kumuona akitumbuiza - sikumbuki wapi kwa sababu sikuwa mtu wa sehemu. Katika ile wakoloni wanachoita dilly-dallying - kabla hatujalitimiza hilo akawa amefariki. Hadi leo hukaa nikijiuliza kama utoto ni sehemu ya maisha yetu ni vipi hutokea tukasahauliana na kupishana mitaani hadi ya kwamba tulikuwa tulicheza pamoja, tukila pamoja na kuimba pamoja.
ReplyDeleteNani zaidi ya dudumizi? Huyu jamaa kweli alikuwa tishio na tungo zake zilisisimua kichizi. Kuna anayekumbuka ule wimbo wa Sagha Rhumba uitwao Mtatumaliza? Hapa Jerry alichekesha kwa kulalamika juu ya mademu wa kibongo walivyo wazuri na namna gani wanavyotumaliza. Ama kweli kizuri hakidumu daima.
ReplyDeleteYaani. Nyie wacheni tu.
ReplyDeleteMie namkumbuka kwa ule wimbo wake
"Ndoto yetu ya siku nyingi mwanaa mama, imekuwa kweli.
Ahadi yetu tuloipanga siku nyingi tumeitimza.
Utakumbuka tulikuwa wote siku nyingi, taangu tuko masomoni, rembeee tuliipendana.
Tukapanga tufunge ndoa mimi nawe...."
Mwanawane!