"TUMIENI KOMPYUTA KUHIFADHI KUMBUKUMBU JAMANI..." ANAONEKANA KUSEMA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI WA UMMA MHE. HAWA GHASIA (PILI SHOTO) WAKATI AKIKAGUA MAFAILI YA WALIMU WA NCHI NZIMA YANAYOHIFADHIWA KWA NJIA YA MWAKA 47 KATIKA OFISI YA TUME ILIYOPO UBUNGO PLAZA MJINI DAR ES SALAAM LEO, AKISHUHUDIWA NA MWENYEJI WAKE KATIBU WA TUME YA UTUMISHI MH. THECLA SHANGALI. HABARI KAMILI CHINI:

Na Mediaworks News Agency
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma Mh. Hawa Ghasia ameiagiza Tume ya Utumishi serikalini kuhakikisha wanakuwa waangalifu katika kutoa huduma zao ili kukabiliana na tatizo linaloelekea kuwa kubwa la watumishi hewa hasa katika idara ya ualimu.
Mh. Ghasia ambaye alikuwa akizungumza na wafanyakazi wa tume ya utumishi ubungo Plaza mjini Dar Es Salaam, amesema alishangazwa alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Dar es salaam ambapo aligundua kuna shule (bila kuitaja) ilikuwa na walimu hewa wanaokaribia 50 kitendo ambacho alisema kinatisha ukizingatia shule kama hizo zipo makao makuu ya serikali na kushangaa hali hiyo ipoje huko mikoani.
Akizungumzia tatizo la kuchelewesha mafao ya walimu kama mishara, kupandishwa cheo au mafao ya kustaafu, waziri alisema wachawi wa suala hilo ni wahasibu wao na wala si serikali kuu na kuwaagiza wawabane wahasibu wao na ikibidi waaonyeshe nakala za fomu zao zinazotumwa utumishi ili kujiridhisha.
Waziri huyo alisema pia amegundua kuwa kuna walimu wengi ambao wamehama kutoka wizara hiyo na kwenda wizara zingine kuhamia wizara hiyo wanaendelea kupokea mishahara miwili kwa kutumia namba moja au namba tofauti na hivyo tume iwe ina hakika shughuli zake na kuachana na tabia ya kutumia taarifa tu.
Katika kukabiliana na hali iliyojitokeza katika sekta ya elimu, Katibu wa tume ya Utumishi serikalini Mrs. Thecla Shangali alimwahidi waziri kuwa tume yake itafanya mkutano wa pamoja na wadau wote wa elimu mkoani Dar es Salaam tarehe 17 mwezi huu ili kuwekana sawa.
Katika ziara hiyo waziri alitembelea sehemu ya kuifadhi mafaili ya walimu nchi nzima na aliagiza kuwa waanze kutumia kompyuta na vilevile kuwa na utunzaji wa mafaili katika kila Kanda ili kupunguza mlundikano Dar na kuongeza ufanisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. michuzi unaonaje kama hao walimu wakianza kuhifahdi kumbukumbu kwa kujenga maktaba kubwa dar es salaam, ili wanafunzi na walimu wakusanyike kuchangia mada za maendeleo ya nchi.

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa Waziri wa utumishi Hawa Ghasia.Nakupongeza kwa kuacha kiti pale ofisini na kuenda kutembelea eneola watendaji wa wizara yako.Inasikitisha kusikia taarifa za wahasibu wa wizara ya elimu kuwa ndio wachawi wa mishahara ya walimu.Pili inasikitisha kuona pesa za walipa kodi zinavyotumika vibaya kwa uzembe tu wa utendaji ambao umepelekea mtu mmoja kulipwa mishahara miwili pamoja na mishahara kulipwa kwa walimu hewa.Ninahakika wizara nyingine ni hayo hayo tu na hasa wizara ya Afya na mambo ya ndani ambako kuna rundo la wafanyakazi.Mheshimiwa waziri vitendo hivi havina tofauti sana na saga ya Richmood kwani mamilioni ya walipa kodi yanapotelea kwa watumishi wachache wanaojiita wajanja na wengine kudiriki kusema pesa ya serikari ni ya kuliwa tu. Wakisahau kuwa si pesa ya serikari bali ya walipa kodi.Naishauri wizara yako iunde kikosi kitakachokuwa kikishughurikia kuzuia wizi wa kijanja na ufujaji wa pesa za Serikali kwa kulipa mishahara hewa.

    ReplyDelete
  3. Ni vizuri wameliona suala hili la utunzaji wa kumbukumbu kwa teknolojia ya mwaka 47. Hata hivyo naamini serikali inafahamu kabisa aina hii ya utunzaji wa kumbukumbu uliopo katika nyingi ya ofisi/taasisi zake. Hiyo picha imenikumbusha hali niliyoikuta ofisi ya vizazi na vifo, hakika inatia uchungu na aibu pia.

    Kwangu mimi nadhani kutotilia maanani umuhimu wa kumbukumbu na hali ya kukaribisha rushwa ni baadhi ya sababu zinazopelekea kuwa na utaratibu mbovu wa utunzaji kumbukumbu.

    Utaratibu huu mbovu unachukuliwa kua mtaji kwa wahudumu wa hizo ofisi. Kuna tabia ya kuchelewesha huduma kwa makusudi kwa kujitetea kua faili hailionekani (ingawa najua kuna ukweli kwa baadhi ya wafanyakazi kulingana na uchakavu na mpangilio mbovu).

    Unaweza aambiwa kama una haraka wakukuruhusu utafute mwenyewe au la utoe chochote wakupe mtaalamu wa kupata mafaili kwa haraka (ambae hautamuona hata kama utatoa pesa).

    Ni mapendekezo yangu kua idara/ofisi zote za serikali zinazohusika na utunzaji wa kumbukumbu zifanyiwe tathmini ya ufanisi wake na kufanyiwa maboresho yanayostahili. Nyingi ya kompyuta katika ofisi hizi zinatumika kwa ajili ya kuchapa barua tu.

    Ignorant,
    Jeremani

    ReplyDelete
  4. I think the government should start spending a lot of money on IT INFRASTRUCTURE on Government sectors and offices.

    Just looking at those piles of files, documents. Surely there is a need of urgent archiving of these documents of every single government teachers in a computer using a special software, there are lot of them off the shelf which can just do the job. All could be zipped up on single disk. That will be of a benefit, cost effective for the government, and they will be properly secured. AND I really mean for all Government sectors and institute.

    In Europe, a country like UK, all the citizens and residents are given a special unique number from the day they are born, called insurance number. For them it makes life easier and make it difficult to forge, You can easily be identified, on any government or private institutes, i.e your work place, in a hospital, can also be used to identify how much tax you pay and how much you earned that year and so on and so forth, ofcourse all independent of each other.

    But all in all it is a great system, which we should envy to posses in future. All these forgeries will swiftly minimized or eliminated all together.

    I personally think the government should work toward that GOAL, but for now just get a SOFTWARE and put database in place, that be the quickest things to do!

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  5. hivi nani anatakiwa kununua kompyuta hizo? Si ni serikali au? Na wakishanunua waajili watu wenye qualification nzuri .na sio hapo tu kumbukumbu bado ziko kwenye vumbi ni ofisi nyingi sana

    ReplyDelete
  6. Mheshimiwa waziri kusema tu baadhi ya watu wanapokea mishahara 2 na wengine wanachukua pesa kupitia wafanyakazi hewa haitoshi. Tunachotaka sasa ni namna gani utawashughulikia wahusika kwani ninaamini ni mamailioni ya shilingi yanapotea kila mwezi kupitia wizi huu. Nadhani huu si wakati wa maneno mengi ila ni wakati wa vitendo ili kulifanya taifa lipige hatua mbele. Ninamini kwamba wizi kama huu upo sehemu nyingine pia na mara nyingi ni dili la wahasibu. WAZIRI tunakusubiri kuona wahusika watachukuliwa hatua gani!!!

    ReplyDelete
  7. Ni kweli kabisa mpaka leo hii walimu ni wengi na bado kazi ni kubwa kupata faili wakati technolojia mpya ipo ya kutengeneza mafaili kwenye computer na haitumiki. Ama wanatarajia kuharakisha maendeleo kwa namna gani? Mwalimu badala ya kufundisha unaenda kusotea kwa masaa au siku moja mpaka mbili kutafutiwa faili manually. Kweli Tz tuamke wenzetu wako mbali mno.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...