
Gozi Spoti ni kijarida cha uchambuzi katika michezo, sanaa, maisha na burudani. Gozi Spoti litasheheni picha pia. Tuna dhamira ya kupanua wigo wa kupata taarifa mbalimbali za michezo, sanaa na burudani.
Katika kufanikisha azma yetu hii, tunafungua milango ya ushirikiano kutoka kwa wadau wa ndani na nje ya Tanzania.
Gozi Spoti litakuwa likitoka kila Jumatano kuanzia Aprili 30, 2008. Litasambazwa nchi nzima. Sisi ni wachanga katika kuendesha biashara ya habari. Tunahitaji ushirikiano kutoka kwa wote wenye nia njema.
Hivyo basi, tunakaribisha pia michango ya kazi za michezo, sanaa, maisha na burudani kutoka kwenu wanakijiji. Mipango iko mbioni kuliweka Gozi Spoti kwenye mtandao. Naam. Habari ndio hiyo!
Maggid
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...