Hallow kaka Michuzi,
Nashukuru sana kwa umahili wako wa blog hii,nakupongeza sana kwa kuliendeleza libeneke.Vyombo ya habari leo asubuhi vimeandika kauli ya Waziri wa TAMISEMI kuwa ujunjaji wa zile nyumba ulikuwa ni wa kimakosa,hii inakwenda sambamba na Ufusadi na maamuzi ya kiimla na yasiyo na tija ya viongozi wa halmashauri ya Ilala.
Serikali imeamua kuwafidia milioni ishilini wenye nyumba waliobomolewa sasa Vipi kuhusu wapangaji waliokuwa wamepanga katika zile nyumba?wao watafidiwa na nani? au maamuzi ya Waziri ni ya Kibaguzi?
Kumbuka kuwa sio wote wakazi wa Tabata Dampo ni nyumba zao halisi zimebomolewa wengine walikuwa wamepanga tuu.
Wito,Chama cha Wapangaji Dar es salaam kitowe tamko halaka iwezekanavyo na vyombo mbalimbali na asasi zisizo za kiserikali zisaidie kwa hili nini hatma ya wapangaji hao!!
Mimi mdau
Godfrey.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. nawewe hujui kutofautisha l na r

    ReplyDelete
  2. Hakuna cha niaje wala viaje, si wafuate sheria inavyosema kuhusu hilo. Iko sheria ya ardhi inayohusiana na masuala ya fidia. Nikuulize swali wewe mtoa hoja, unataka na wapangaji nao walipwe fidia ya viwanja na gharama za kujenga nyumba?

    Nafikiri pia kuna mkataba kati ya mpangaji na mwenye nyumba na hata kama hiyo nyumba ya iliyovunjwa ilikuwa inaishi mpangaji, huyo mpangaji hawezi pewa kiwanja na pesa za kujengea nyumba, maana hapo kama nyumba ina wapangaji 6, ina maana serikali ilipe nyumba sita na viwanja sita au vyumba sita vya wapangaji au kiwanja kimoja na gharama ya nyumba moja?

    Kama ingelikuwa ni shamba, na mwenye shamba mwaka huo hakulima ila alimkodisha mtu alime na akatumia nguvu zake kulima kwa maana akivuna mazao ni yake, basi kama kuna suala la fidia, huyo tenant aliyelima atalipwa thamani ya mazao yaliokutwa hapo shambani na mwenye shamba atalipwa thamani ya ardhi yake kulingana na mahali ilipo.

    Mwisho inachefua kuona mswahili wa Tanzania hajui kiswahili fasaha na hawezi kutofautisha wapi pa kuweka R na L. Au sio mtanzania wewe? Unatoka wapi Rwanda au Burundi?

    ReplyDelete
  3. Wenye nyumba wamelipwa kufidia nyumba zilizobomolewa, wapangaji walipwe nini maana hakuna taarifa ya vitu kupotea? Kwa maoni yangu hata wenye nyumba wamelipwa kwa huruma ya serikali tu na kufidia "uzembe" wa watendaji wakati wa ubomoaji maana walijenga mahali pasiporuhusiwa na bila vibali. Nadhani siasa imetumika zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...