jongwe la kike likianza zake baada ya kutolewa mkuku kwa kuchafua hali ya hewa kwenye mkutano wa diaspora leo hapa london.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. Jongwe maana yake nini? Ni kiswahili au lugha gani?

    ReplyDelete
  2. Na limetuletea kizaha zaha kweli na style yake ya nyele ya utajiju IoI
    Londoner

    ReplyDelete
  3. unamaana gani ulivyosema kachafua hali ya hewa?

    ReplyDelete
  4. Lakini message sent and delivered. Najua Shein kaisoma na "it is understood". Mwanamke wa shoka! Looooooooh, tukipata 1,000,000 tu Tanzania yatakemea FISADIS na watatokomea. Jongweeeeeeee!

    ReplyDelete
  5. LAKINI UJUMBE SI UMEFIKA?AU?

    ReplyDelete
  6. ee bwana naona sasa Taasisi ya kiswahili pale Mlimani imezidi kutowashirikisha wazanzibari wenye lugha yao katika kutengeneza misamiati. Hii italeta viswahili viwili siku za mbele kama nilivyokishawahi kusema siku za nyuma. Baada ya muafaka wa siasa tutakua na muafaka wa lugha ya kiswahili
    Naomba niwekewe wazi maana Ya 'Jongwe' na pia alichafua hali ya hewa kivipi hii picha haina maelezo ya kutosha,alijamba au?

    ReplyDelete
  7. Am confused

    Tanzania tunao usemi wa kwamba Tanzania haitakuwa huru hadi Africa nzima imekuwa huru, nadhani huyu dada nia yake ni kuona Tanzania ni moja mwanachama wa SADC na amlengo ya SADC ni "objectives include regional economic integration, poverty alleviation, harmonization and rationalization of policies, and strategies for sustainable development in all areas" Sasa kwa nini na yeye asiweze kuleta matatizo yake ili tuchangie.

    Tatizo ni kwamba siasa na itikadi katika nchi za africa ni kiini macho tu, watu wanalindana, tumeona kuanzia KENYA,sasa ZIM, baadaye RSA .

    Dr Confusion

    ReplyDelete
  8. jongwe ndio nini ?

    ReplyDelete
  9. Eti jongwe la kike linachafua hewa!! HUYO MWANAMKE NI SHUPAVU NA SIO MUOGA WALA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU KAMA SISI WATANZANIA TUNAVYOOGOPA KUHOJI HADHARANI MAOVU YA VIONGOZI WETU NA NDIO MAANA WANATUKEJELI KWA KUITA DOLLAR MILLION MOJA VIJISENTI KWA SABABU WANAJUA WATU WANAOWAONGOZA NI WA HAINA GANI.MIE NAMPOKEZA HUYO MAMA KAJARIBU KUTUMA UJUMBE NA UMEFIKA.

    ReplyDelete
  10. alichafu hali ya hewa kivipi, jee ALIPUMUA au alisema ovyo mbona nawe kwa vijimafumbo michuuuuuu, tuweke wazi sentensi inahang hiyo!!!

    ReplyDelete
  11. salaam aleykum bro michuzi tufafanulie tafadhali jongwe limefanya nini....

    ReplyDelete
  12. oyaa diaspora ndio nini? huu mkutano unahusu nini?

    ReplyDelete
  13. Ebo Michuzi, hebu tuelezee vizuri. Jongwe ndo nini?

    Halafu una maana alijamba, mdomo wake ulikuwa unanuka au alikuwa na kikwapa?

    ReplyDelete
  14. Nadhani alikuja kubahatisha kama ataambulia vijisente vya mafisadi

    ReplyDelete
  15. Huyo ni mama shujaa ,I wish angeongezea hoja ya mafisadi tanzania.
    CCM LAAANA YA MUNGU ITAWAPATA KWA KULA JASHO LA WALALA HOI.
    DAMU YA YESU HAIKUMWAGIKA BURE.

    ReplyDelete
  16. mwanamke washoka nathani ujumbe umefika naomba viongozi wetu wa kiafrika waache mambo yakukumbatiana MUGABE kaaribu nchi sasa anasingizia wazungu hata ningikuwa mimi mambo yanoyo fanyika zimbabwe ningejitokeza kuutoa ujumbe na rais wetu MHE J KIKWETE kama mwenyekiti wa AU anatakiwa kuingilia kati suwala hili

    ReplyDelete
  17. Hey Michuzi what u mean by JONGWEA? plus we need to know more about DIASPORA, is it an organisation? And if it is, what its purpose, mission or vision with Tanzania. Maana these days watu wanaibuka na mbinu mpya kufilisi nchi yetu. More explanation will be helpfully bro Michuzi.....Thanks
    Mdau T-Dot

    ReplyDelete
  18. jamani kwani hamjui jongwe la kila siku ni mugabe? basi jongwe la kike ni mke wa mugabe mbona mna vichwa ngumu? ndio hayo mambo ya rais wa kwanza wa kenya anaitwa kenyata je rais wa kwanza wa tanzania ataitwa nani mtasema tanzaniata! kha wadau

    ReplyDelete
  19. watanzania tuko nyuma ktk mambo mengi miongoni mwao ni ku speak for our rights! sioni sababu ya ku report habari ya huyu dada kama vile kafanya kitu kisicho na maana kabisa! msg yake imefika! si rahisi kumpata mtanzania atakae weza fanya kitu kama hicho! why? cowardice!! we need to learn to speak up!!

    ReplyDelete
  20. Jamani Wadau, maana ya Jongwe nayoilewa mimi ni Jogoo na ni alama ya chama cha ZANU-PF, labda Bro Michu alitaka kututanabahisha kuwa huyu dada atokea nchi hiyo !!..Sijui atutegulie...uchafuzi huo niwa aina gani ?! Tukupe mji Kaka...?!!

    ReplyDelete
  21. Zimbabwe, JONGWE ni JOGOO!

    ReplyDelete
  22. Ingawa njia aliyotumia sio sahihi, lakini ujumbe wake umefika, jamani mkumbuke kwamba JK ni nani Afrika. Halafu nchi yetu inasifika kwa amani kwa hiyo ametumia fursa hiyo ya diaspora kwa sababu hana njia nyingine

    ReplyDelete
  23. Hata mimi hii picha sijaeilewa japo huwa wanasema picha inazungumnza zaidi ya maneno elfu Moja pia mmeongezea na maelezo ndio kabisa nakutana na Mambo ya Jongwe sijui na Huo Mkutano sijui Ziporaa Duhh mi naona kama jina la Kinaijeria Fafanuwa Bro Michuzii Najuwa utajibu labda kama na wewe utakuwa Unavijisent basi hutatiliaa manani

    ReplyDelete
  24. jongwe ni jogoo, mugabe ndio huwa wanamuita jongwe (jogoo). Kuchafua hewa ni kuharibu amani kwa ninavyoelewa mimi

    ReplyDelete
  25. Kweli wadau hata mimi ningependa kujua nini maana ya diaspora

    ReplyDelete
  26. HUYU DADA NAMPONGEZA KWA USHUPAVU WAKE.TUNAHITAJI WATU KAMA HAWA HAPA TZ.WATAKAOSIMAMA KIDETE NA KUWAKEMEA MAFISADI WANAOIBA SH.1.BILION HALAFU WAKIULIZWA WANASEMA KWAMBA HIVI NI VIJISENTI TU.

    ReplyDelete
  27. Mwanamke wa shoka huyo..... watanzania wangapi wana guts za kufanya hivyo...... kikwete amekalia kimya swala Zim na inatia aibu. You go gal

    ReplyDelete
  28. Jamani naomba kueleweshwa maana ya jonhwe, na kama ni kitendo cha huyo dada kuyapaka mafisadi hadharani shida nini? au kwa vile nyie mnaejoy huduma nzuri huko london, tumechoshwa na mafisadi. Cha ajabu serikali haitaki kufadhili watu school of law iliyoanzaishwa mwaka huu, sijui wanafikiri wazazi wetu pia ni mafisadi hadi waweze kulipa hiyo milioni moja na nusu ya ada.
    Vena, Arusha

    ReplyDelete
  29. Huyo atakuwa katumwa na JamboForums. Heheehheeee, hheee! Haya JF member wenu huyo, sio Jongwe wala nini!

    ReplyDelete
  30. Jamani tukumbuke leo kwa mwenzio kesho kwako, naona watu mmelala hii kitu inasogea kidogo kidogo Tanzania, kama majirani zako hawako salama ujue na wewe hauko salama.Jaribuni kufikiria siyo kukashifu.

    ReplyDelete
  31. EH MUNGU TUNAKUOMBA UTUONDOLEE GONJWA HILI LA UJINGA SISI WATANZANIA.YANI HUYU MAMA KAENDA KULILIA HAKI KWENYE NCHI YAKE KWA WATU AMBAO RAISI WAO NDIO MWENYEKITI WA AU ANAONEKANA PUMBAVU,WAKATI KUNA JIBABA ZIMA LA KITANZANIA TAMBI KUBWA LINASHINDWA KUHOJI MABILIONI YANAYOTOWEKA NCHINI MWAKE.

    ReplyDelete
  32. HUYO MAMA ANAJUWA HAKI YAKE NA ANATAMBUA THAMANI YAKE KWA UJUMLA NI SHUPAVU NA JASIRI ! NA ANASTAILI PONGEZI KWA KUTHUBUTU KUWAKILISHA MATATIZO YA KWAO ! NASI TUIGE MFANO WA WENZETU AU TUSUBIRI MPAKA TUUZWEE KABISA !
    Mzushi

    ReplyDelete
  33. Jamani Wadau wa Blog,
    Diaspora kwa tafsiri rahisi ni Mtawanyiko wa watu, kutoka kwenye nchi yao halisi na kutapakaa sehemu nyingine. Hivyo jumuiya inayoundwa na watu wa ainahii huko waliko ina fahamika kama Diaspora. Neno hili lina asili ya kigiriki "Diaspeirein" meaning to spread apart. Pia neno hili lina husishwa na Wayahudi walokuwapo nje ya Israel kuanzia Karne ya sita(6) kabla ya yesu kuzaliwa, wakati walipokuwa ukimbizini Babiloni.
    Hivyo kwa Afrika..."African Diaspora" hata AU imeelezea kwamba ni watu wa Afrika, wenye asili ya Afrika ambao wanaishi nje ya Bara hili, bila ya kujali uraia wao au utaifa wao, ambao wako tayari kuchangia katika kuleta maendeleo ya bara la Afrika na kujenga Umoja wa Afrika. ...na ndio maana na Wazimbabwe walikuwemo.

    Naishia hapo Wadau

    ReplyDelete
  34. watanzania wenzangu huyu dada ni shujaa watanzania tungeiga mfano huu ni kama kuwahazarisha mafisadi wabongo bado tuko nyuma kulalia vibatari na kutoa majina ya kubeza wenzetu wakati sisi ndio tunamatatizo na tunaitwa washambo kwa kuogopa kusema ukweli hazarani mr michuzi naomba usinibanie ukweli huu ni kwamba wabongo maneno mengi kusema ukweli twaogopa huyo dada ni shujaa na kumbukeni wabongo mtakuwa next .tusicheke wenzetu wala kuwabeza ndio maana tumezoea kuliwa na wakubwa zetu wazimbabwe tuwaombeeni mungu na tuchukue mfano toka kwao ni kipindi cha kusikilizana na kusaidiana tukiwa wote ni waafrica mimi ni mpenda amani na nawapenda waafrica wote walio duniani kwani wote tunateseka same mugabe aondoke na ni amesha changanyikiwa miaka tisini alivyoiba havitoshi tuu.

    ReplyDelete
  35. SINA UHAKIKA LAKINI NENO JONGWE HAPA NAONA LIMETUMIKA KAMA VILE NANO KINGUNGE AU VINGUNGE TOKA TANZANIA. INAWEZAKUA KINGUNGE RASHIDI KAWAWA. KINGUNGE SALIM AHMED SALIM OSV...... HII. HI.

    ReplyDelete
  36. Du! Nimem-mind huyu dada ushupavu wake! Hongera Jongwee! :) keep it Up dada! inafurahishwa kuwa uliwachafulia hewa kwa ujasiri wako wa kusema ukweli na ukwaacha hoi hata wakakumind! Hasa kwa kuwa ni mwanamke, mwanamama! Du..umeni-inspire sana sis!Inatia moyo kuona katika blog hii at least ameongelewa mwanamke kwa mtazamo chanya...kwani tumechoka kusikia wanawake wakisagiwa humu ndani katika blog hii inayoonekana ina mtazamo dume! wanawake wanasakamwa tu hata wakijitokeza kwa wema. watanzania acheni mambo ya zamani, inabidi mkubali sasa wanawake nao wana nafasi!Kaka michu nipe basi email yake nataka niwasiliane naye mwenyewe!
    femenist no.1

    ReplyDelete
  37. Hili ni funzo kwa watanzania,na tabia za kubabaikia watu kwa kuwapa
    mialiko ya kuudhuria mikutanoni!
    SASA HUYU BINT KWELI ALIVYOVAA japokuwa huko ulaya mna uhuru wa mavazi!lakini kweli kwenye mkutano kama huo!?hilkuwaje walinzi walimpisha getini kuingia mkutanoni!Jamani huku kubabaikia watu mtawalika mamluki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...