Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Hivi pesa manake nini, hivi utajiri manake ni kuwa na pesa nyingi? Hapo mimi hujanishawishi, nahisi kuna ulakini, kama utakuwa na pesa nyingi halafu ukazilundika tu benki.
    Lakini hata hivyo mbona mafisadi imekuwa nyimbo isiyo na mwitikaji. Nani amefisadishwa baada ya kuwa fisadi?
    Hapo kapo kamchezo ka siasa!
    m3

    ReplyDelete
  2. Wadau jana niliumia sana baada ya kumsikia Chenge kupitia BBC radio akisema kwamba bil.1/= ni vijisenti. Binafsi nitamshangaa JK kama ataendelee kumuweka madarakani huyu jamaa kwani inaonekana hana huruma na watanzania anaowaongoza. JK aliopoingia madarakani alisema kwamba atataka akumbukwe kwa kuwasaidia watanzania ili waondokane na umasikini lakini kwa kuwa na watu wenye kiburi kama huyu Chenge sidhani kama atatimiza lengo lake. Bwana Chenge hebu fikiria hizo pesa zingeweza kuokoa na/au kuboresha maisha ya watanzania wangapi halafu wewe eti unaziita vijisenti? Nadhani sasa huu ni wakati wa wananchi kuonyesha hasira zao kwa viongozi wasio na hekima kama huyu jamaa. Mimi nadhani ni hapa sasa watanzani tunahitaji mshikamano wa kuishinikiza serikali ili imng'oe huyu fisadi ili aweze kuchunguzwa vizuri kwani kama hizo anaziita vijisenti huenda anazo nyingi zaidi ya hizo. Mlalahoi

    ReplyDelete
  3. Heheheheheheheeeeeee!!!!!!!! Duh!! hii hatari tena na wala sio balaa !!!!!!!!!!
    Hata wakiweka ufunguni, tutawafuata hukohuko. Nakumbuka mzee mmoja 1982 Sokoine akiwa Wazri mkuu alizifukia kwenye zizi la ngombe washikaji wakazigagua hukohuko.

    Masaai Halisi

    ReplyDelete
  4. Viongozi wa kiafrika huwa wananishangazi kitu kimoja, kwanini hizo fedha wanazoziiba wasiwekeze kwenye nchi zao na badala yake zinakwenda kuzalisha ajira kwa wazungu? Tatizo ni nini? Hivi wale waliopigana na wakoloni wangekuwa na roho kama za viongozi wa sasa leo tungesema nini kuhusu Tanzania? Hivi Chenge angewekea japo milion 200 tu jimboni kwake angetoa ajira ngapi kwa wapiga kura wake? Mimi nadhani sas ni wakati wa serikali kuzitafuta pesa zetu zilizoibwa popote zilipofichwa na wahusika washughulikiwe kwani haiwezekani wengine waishi peponi kwa jasho letu na wengine tuishi motoni hapa duniani. Ni lini viongozi wataacha ile dhana ya kwamba hili ni mali ya serikali hivyo wewe iache iliwe!! Chenge step down kwani huna sifa za kuwa kiongoni na ni wewe uliyeipeleka nchi hapa ilipo kwa kusaini mikataba mibovu. Historia itakuhukumu

    ReplyDelete
  5. Sawa kabisa KP, watazificha mpk kwenye NTUNGI, sabb hivi sasa Benki hazina maana hata kdg, ukiweka tu lazima zibumbuluke.

    N`dau toka NCHUMBIJI.

    ReplyDelete
  6. KP kweli wewe umepinda.Hizo hela si zitaoza?Au utazima frijii?????

    2Ladies.

    ReplyDelete
  7. KP wewe kiboko, ila jamani cha msingi ni kumuomba JK afanye mikakati ya kudhibiti mianya yote ya RUSHWA angalau kwa 85% ndio tuanza kuulizana hawa wengine walizipataje hizo mi EPA kuliko kwa njia hii sijui kama tutafika ni kutiana machungu tuuuuuu uona kunamijitu kumbe inaifisadi nchi hii bila huruma.
    JK awaambie kama kuna MTZ yeyote ambaye inasadikia anamiEPA arudishe angalau zije kny BANK za hapa nchini ziwezwe hata kukopeshwa kwa watz kwa riba nafuuu kwa miijili hiyo awape miezi kama sita ataeshidwa kufanya hivyo wanafreeze accounts na mali zao zinakuwa za serikali kwa mipango mengine. nahisi hii itakuwa injia ya kuwafanya watu hata wakiiba wazitumie hapahapa ili hata serikali ipate kodi na watz wapate ajira

    ReplyDelete
  8. Mzee hizo pesa hata ukienda zifutika North Pole madhali ni haramu na bado ungali katika siasa zitajulikana tu!Adui yako hayuko mbali sana na wewe,Ni Ulimi wako mwenyewe!Si unajua pesa zikiwa nyingi sana mikono haiishi kuwasha!Koonooooooooooooooooooooooooooooooz

    ReplyDelete
  9. HONGERA sana Kipanya ujumbe umefika
    M3

    ReplyDelete
  10. SIMCHEZO ANAFICHA VIJISENTI SIO KWENYE FRIJI HE HE HE.JAMAA WAKO KWENYE NCHI MOJA DUNIANI AMBAYO KUIBA HELA ZA UMA KUNA RAHA YAKE KUBWA SANA.MANAKE UNACHOTA TU KAMA KISIMA HAKUNA ANAYE KUULIZA WALA KUKUSUMBUA.
    chonde chonde lakini siku hio kipofu atapewa nafasi ya kuona na bubu akapewa nafasi ya kuongea hapatakalika waheshimiwa SIRIKALI.

    ReplyDelete
  11. Nashangaa kwanini JK kamrudisha Chenge nyumbani badala ya kwenda nae huko UK alikoziweka hizo hela ili wakatanue vizuri na kufungua matawi ya CCM.
    kaka Michuzi I bet you ukimkoromea Chenge lazima atakaka kidogodogo. Zusha tu mjadala kwenye blog yako mambo yatakuwa safi.

    ReplyDelete
  12. Money talks and bulshit walks. Amakweli huu ni msemo wa kweli Chenge ana mihela mpaka JK kaogopa na kumrudisha madarakani. Wengine wote waliojiuzulu kumbe wana vijisenti kwani Chenge kila mkataba alikuwa anaondoka na dolali milioni moja taratibu. je ni mikataba mingapi imepita mkononi mwake.
    Tulipofika hivi sasa wala sikasiriki tene mtu akiiba ilimradi iwe sura mpya kuliko walewale. Kesho nikisikia mzee Michuzi kala hesabu fulani ya Tageta mimi ntasema sawasawa kwani hiyo ni timu mpya.

    ReplyDelete
  13. LISTI yao kubwa na inaanza na kaka yao mwenyewe. Kinachoniuma mimi ni kwamba hawa watu wataishia kuachishwa nafasi zao za uwaziri tu, ubunge watabaki nao, uhuru watabaki nao, pesa watabaki nazo na dharau wataongeza.

    ReplyDelete
  14. nina uhakika kuwa idadi ya viongozi waliothbitishwa kua ni mafisadi ni ndogo kuliko ya wale waliokuwa hawajathibitishwa!
    hapa namanisha kua hawa wa style hii ya kuficha mabilioni nje wapo wengi tu ila ndo hawajakamatwa...
    wadanganyika amkeni!

    ReplyDelete
  15. MAKARATASI SIO ULAYA TU,HATA BONGO..(From mwananchi,17/04/2008
    Raia wa Wakenya, Uganda watimuliwa kwa kuishi,kufanya kazi Tanza
    Na Samson Chacha, Tarime

    IDARA ya Uhamiaji Wilaya ya Tarime mkoani Mara, imewatimua raia wa Kenya na Uganda wapatao 50 kwa kosa la kuishi na kufanya kazi nchini bila ya kuwa na vibali.


    Raia hao, wametimuliwa baada ya kubainika kuwa, walikuwa ni wahamiaji haramu tangu walipoingia wilayani hapa, tangu Januari mwaka huu.


    Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Uhamiaji wa Wilaya za Tarime na Rorya, Mamti Sehewa, alisema raia hao walikamatwa hivi karibuni na kubainika kuwa walikuwa wamekiuka taratibu za kuishi nchini na kufanya kazi au shughuli nyingine, ikiwamo ya uganga wa jadi.


    Sehewa alisema kuwa, raia hao, walikuwa wakiishi na wengine kufanya kazi katika eneo la mgodi wa dhahabu Nyamongo kinyume na sheria.


    Alisema mmoja wao, mkazi wa Kumumwamu nchini Kenya, Alex Thomas aliyekuwa anajifanya mganga wa jadi katika Kijiji cha Tagota, alikamatwa na Polisi, kisha kukabidhiwa kwa Uhamiaji, kwa hatua zaidi za kisheria, kisha kufikishwa mahakamani na kwamba, amekuwa akiwatishia mashahidi wa upande wa mashitaka kutoa ushahidi dhidi yake.


    Aliyataja maeneo ambayo yamekithiri kwa wahamiaji hao haramu kuwa ni ya miji ya Sirari, Borega na Kibiterere


    Naye Zulfa Mfinanga anaripoti kutoka Shinyanya kuwa, Uhamiaji imekiri kuwapo kwa wahamiaji haramu kutoka nchi za Rwanda na Burundi.


    Afisa Uhamiaji wa mkoani hapa, George Nakenya alisema kuwa, imekwisha kuwarejesha katika nchi walikotoka, wahamiaji haramu 191 katika kipindi cha mwaka jana.


    Wengi wa wahamiaji hao walikutwa katika mashamba wakifanya kazi za vibarua, wengi wao, wakitumia fursa hiyo kuoa watoto wa waajiri wao, kwa imani kuwa ndio kibali cha kupata uraia.


    "Wengi tuliowakamata walidai kuwa wameoa Tanzania hivyo wana haki ya kuishi na kuwa raia halali ya Tanzania, yaani wakitumia mwanya wa kuoa kwa waajiri wao wakidhani kuwa ndio suluhisho la kuwa raia wa Watanzania," alisema

    ReplyDelete
  16. Mnaojua contexts za "lugha" ya Kiswahili, mtusaidie:

    Kuwa na visenti
    ni heli ya utajiri
    kuliko kuwa
    na utitiri vijisenti!

    Dharau!

    "Kwa nini mwanigusa mimi na hali watu wanazo zaidi ya milioni mia mara milioni?"

    ReplyDelete
  17. I have been following the EPA scandals for some time, and other allegations such as this old one –BAE system- that have been leveled to our party leaders, government officials, member of our parliament and other private and local officials for some time now. I have come to conclusion that it’s the right time now that we run our country on truth by following the laws that have been made to both- people in high offices and those that are supposed to be served by.
    Recently I was reading a British newspaper which cited Mr. Chenge as having (billions –equivalent of our local) money in one of the banks here in UK. Britons take it too serious on any offshore money accounts to its citizens on the basis of tax and legitimacy. The whole point is to ensure that it account all their incomes also -knowing how all its bank are handling money transaction inside and outside their country. Back to what I read, Mr. Chenge, will have to answer all those questions on how he got all that amount of money at the first place and if- that money was also obtained from an illegal practices. It has been okay for some times now to see that people who hold big offices can go away with any allegations. It’s the high time for Members of the parliament or Government officials to either save our country or leave their position and decide to run their business, on which, this will help them be free from problems of interest if not conflict of interest. Let me be straight here, I am not condemning or saying that Mr. Chenge is now guilty ,that’s why earlier I used the word "also", on the second allegations because , people who hold these top position seems to think that the laws applies for them in the way addressed on the books. What we have been seeing is that, to them -they are innocent until proven guilty, but vice versa to other citizens who don’t hold high offices or positions, its assumed that they are guilty until proven innocent. T
    What I know now is Chenge would still be in China on that trip with the president and would never come home if these allegations were to be reported by our local newspaper. If I am not mistaken, what we do know now is these allegations were written or generated from a newspaper in Britain, and that’s why- not to paint the picture bad, Mr. Chenge was forced to return home to answers those allegations. I am sure he would still be in China if those allegations were addressed or were coming from a newspaper let’s say Majira, or Nipashe , both would be stories or rumors that would let go away. Thanks God the Britons did not let this issue go away, no matter how long it would take, but all the info would have to be known later . To me, this is one of many opened and continuation or follow up to come on their side on allegations’. This allegation involved both -their companies, our members of parliament, Gorvment official and a sizeable number of cru-pious and greedy Tanzanian businesses personal on dealing with these Radar issue.
    What I am thinking on my side or view concerning this allegation is to suggest Mr. Chenge, to resign immediately, waiting for his innocence or guilt to be proven by the court of law as he is entitled too. But, also should give a way on the pure and non interfered process to take way. I have been wondering for so long now, why other Ministers who also were engaged in greedy issue like Msabaha and the others are not resigning on their MP's positions. The Prime Minister need to let people know that once a Minister resign on a ministerial position due to their blunder etc, will also be required to resign there second positions as Members of the parliament. The notions that they are elected by Wananchi’s, and therefore are entitled to remain as Member of their constituency , despite them doing blunder is wrong. The problems they have caused are Wananchi's problem and not only ministerial problems and the notion of giving them another chance to be heard or listened is to give them a chance to feel that they are superior to others and can still do anything. We are more than 30 millions Tanzanian who among us we have talent -educated, experienced and well groomed citizens who can run our country right. I do understand that It’s expensive to re-run the MP’S election but, its worthy to let anyone who has been elected by citizens to understand that they are there to save them, and not playing with them. Let people who need to have money offshore have them as business people and not as government official who use their power to collide or force with other greedy business men and cite a conflict of interest.

    ReplyDelete
  18. Hawa waheshimiwa wote wanaohusika na ufisadi tusiwalaumu hata chembe kwani bosi wao JK anawalinda kwa kutwambia kwamba wamepata ajali ya kisiasa kama vile alivyopata Lowasa. Kwa hivyo kamchezo na kaendelee tu lakini iko siku nguvu za uma zitawahukumu "You can fool some people sometimes, but you can not fool all the people all the time" Tumesha shituka nyote viongozi lenu moja nalo ni kula jasho la wananchi. Ole wenu dhuluma haishindi haki !!

    ReplyDelete
  19. Duuuuu coment za leo kila ukifika kipengele cha verification password unakutana na neno FSAD au FISD au EPAPHOBIA au RCHMONDSIS au UFISD au FISDI na mengine mengi kama hayo. Wadau jaribuni hii sijui imekaaje nisaidieni hii komputa inajuaje tunacoment juu ya ufisadi????

    ReplyDelete
  20. TATIZO LA MAWAZIRI WETU NI KUWA NA NYUMBA NDOGO NYINGI SASA KUZIUDUMIA NDIO TATIZO HADI UNAKUWA JAMBAZI. KWANI KUWAJENGEA NYUMBA WOTE LAZIMA HUWE JAMBAZI.MTU UNADIRIKI KUSEMA NI VISENTI NILIKUWA NAJUA SIKU NYINGI WEWE UNA TATIZO. MAJIBU YAKO NI MACHAFU. JK NIKO CHINI YA MIGUU YAKO NAOMBA UMTOE TUMGOMBANIE KAMA MPIRA WA KONA.NA HUYU SIO KWAMBA HAPIME NA KUAMUA NI KUMFUKUZIA MBALI.

    ReplyDelete
  21. tatizo sio wao kua na fedha kp,inshu ni vp wamezipata.

    ReplyDelete
  22. Well KP, nafikiri umefikiria sana hadi ukafika hapo,ila nauliza huo ufisadi ni "fasheni" au ni "mbadala" wa propaganda iliyotangulia uchaguzi ulopita? maaana sasa ari, kasi na nguvu vimefukiwa na tunasikia UFISADI usiokuwa na mwenyewe wa kuushughulikia.....zile nguvu na kasi isiyokuwa na mwendo sasa vimejiidhiirisha kaka Misupu

    Maana yangu ni kuwa hakuna hata mmoja amabaye tumesikia amechukuliwa hatua yoyote kuhusiana na haya mambo...ndugu zangu nahisi tunapoteza muda, kwani mpaka jamaa anasema ni "vijisenti tu" sasa kumeota mizizi... hakuna kitu hapo

    Nyaningedere

    ReplyDelete
  23. Actually ni vijisenti tu. IoI unafaa kupigwa mawe wewe kama yule dada wa Nigeria hauna aibu!!! Loh!

    ReplyDelete
  24. Huenda kweli kwake yeye ni vijisenti, ikiwa na maana hizo mlizogundua ni sawa na senti katika mashilingi! Vijisenti...

    Tanzania hii wapo matajiri, na utajiri wao walivyoupata wakiambiwa wauelezee sio rahisi. Kwasababu njia nzima ya kuupata huo utajiri ni `ufisadi'. Kama kweli serikali itaamua kufichua hutaamini!
    m3

    ReplyDelete
  25. mnajifanya mna hasira mtaishia kuandika comment mpaka mkome!!!! hehe, kama una uchungu na ufisadi mnafanya nini nyie!!!!! mtaishia kuwa wenyeviti wa vikao vya harusi. kamna mna hasira ingineimitaanai comment za nmana hii nao ni ufisadi, mnataka nani aingie mtaani, weni wanafiki tu humu, mmkiambiwa twende maandamano hamjitokezi walalahoi waiotoa comment humu ndiyo wanaenda.
    heri tujisahaulishe maumivi yetu ya woga na kuhujumiwa kwa vichekesho.

    kitendawili??? tega

    Karuka kajipanua

    chenge!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  26. WAKATI UMEFIKA RAIA WACHUKUE HATUA MKONONI.WALALAHOI WENZETU TUNAWACHOMA MOTO KWA WIZI WA "VIJIKUKU" SASA HAWA WANAOIBA "VIJISENTI" MBONA WANAPETA?

    ReplyDelete
  27. KIKWETE unatuyeyushaaaaaaa,
    tumechoka kuibiwaa mnatukamua kodi kubwa mno mpaka slip hazitizamiki

    mtuuze kabisa tujue sisi ni watumwa ,bora tukafie ulaya kwenye haki naukweli

    tumechoka
    tumechoka
    tumechoka jamani

    hakuna hata action inayochukuliwa juu ya ubadhilifu,ipo siku mtavilipa kama ni jasho la mtu linaliwa,wote tutakufa hata uwe na mijihela unayoita vijisent

    nchi inanika rushwa kabisa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...