wadau ndo naiongia toka nanihii asubuhi hii. nawaomba radhi kwa kwikwi ya masaa 24 ilotokea kwa sababu ya matatizo ya kiufundi pamoja na safari. pia fuolana ilichelewa kukauka hivyo0 sikuweza kutoka kifua wazi kwenda kutafuta mitambo mingine. ila naomba ieleweke mie sio mtu wa visababu hivyo nakiri udhaifu na kuwaomba ra`dhi kwa kukaa kimya na mnivumilie kwa kutowafanyia kazi mnayonituma niwafanyie siku zote. baada ya hapo naahidi kuendeleza libeneke kama kawaida

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. ze fulanazzzz again....
    michu plz...tell us..what is behind that fulanazzz
    sijawahi kucomment, ila uzalendo umenishinda leo, au ndo ukivaa hio inatuvuta wadau kila wakati kuvizit ze blog yako....
    ishindwe kabisa!! nakemea!!

    ReplyDelete
  2. Mmmmm!!!! Aisee kajamaa haka kanasafari mno! Hee ni Kajk kapili nini!? Halafu tangu kawe ka mkuu wa tege ndio safari haziishi. Mzee sema kama unajiandaa kukachukua kauraisi 2015

    ReplyDelete
  3. Ina maana huko London ulipiga picha mbili tuu?
    Hebu tumwagie mapicha ya London humu..nshachoka kusubiri

    ReplyDelete
  4. Poa mzee, welcome back home! mbona hutaki kutuambia namna ya kushiriki bahati nasibu yako?

    ReplyDelete
  5. Yaani mtu maarufu kama wewe hata wakezo akiwemo yule bi mdogo mkeo mganda hakuja kukupokea Airport? Unawasili kama mtoto yatima wa Msimbazi Centre.

    Ningekuwa mimi ningetimua wake wote wakatafute mabwana wengine wa kuwaoa kama wanafikiri kupata mume ni kazi rahisi.Shenzi taipu.

    Kuna maana gani kuoa, wakati mwanamke haji kujitwika kichwani hayo masanduku hadi uishie dume zima kusukuma vitoroli kama msumkuma mkokoteni wa Buguruni kwa Kimbengere?

    ReplyDelete
  6. Mie siku zote hizi nilikuwa na hofu kidogo kwa umaarifu wa hiyo fulana.Leo naona nimepata jibu hiyo fulana yampa Michuzi power na kila akiifua huianika juani kuicharge upya , wasoma bibilia wamkumbuka Samson na nywele zake, na jua ndio hata hapo lipo kwani Samson jina latokea kiarabu alshams au kihebrew shimshon ie like the sun
    QED

    ReplyDelete
  7. pole na safari na karibu tena nyumbani. Oga upumzike, kula vyakula vya kitanzania, cheka na watoto na mama kisha anza kazi tunayoipenda ya kupata habari za nyumbani hasa yaliyojiri jana maana si madogo ati

    ReplyDelete
  8. bro michuzi habari!
    mi nshaomba sanaaa,kuhusu hii fulana unirisishe ila inaonekana unanibania,sasa nikupe akiba ya maneno,naomba uzipige copy kama Jambo forums na sisi wadau tuzipate sheakh!!

    ReplyDelete
  9. Sasa wewe Michuzi unataka wale waliokugawia Fulana mpya wakueleweje? kama sio utovu wa nidhamu na upungufu wa shukrani ni nini??? Ama kweli mfadhili mbuzi... binadamu ataku...

    ReplyDelete
  10. welcome back hani misupu.te teh teh

    ReplyDelete
  11. THE FULANAZZZZZ, TEHETEHETEHETEHEEE

    ReplyDelete
  12. Hi! Kaka Michuzi!
    Tunakuomba safari hingine usirudie kosa ka KUTOWEKA FULANAZII mtandaoni wakati unapokuwa ughaibuni!hii fulanazi lazima hiwe ya mwanzo!maana ndio bendera ya blog ya jamii!
    Tena umenikera sana!nilipokuona umeweka picha ya viwalo vya suti za pande tatu na kuhisahau FULANAZIIII!!!!
    Fulanazii!!ii lazima ipewe kipau mbele halafu ndio picha zingine

    ReplyDelete
  13. Haa Haaaaa !!! Fulanazzzz time.

    Sasa wewe Michuzi, picha za UK ziko wapi ?? Tumekukaribisha Birmingham UK lakini wapi. Naelewa umekuwa bizee sana. I had a new Fulanazzz ready for you my friend. Anyway, nice to see you got back to Dar in one piece.

    Much love.

    UK Michuzi Addict.

    ( I like your fulanazzz )

    ReplyDelete
  14. kwanini?Fulanaziiii!!! ya blog ya jamii ilibaniwa?haikuwekwa mwanzo?
    kitendo hiki cha kiufĂ­sadi dhidi ya
    FULANAZIII!!!!hatukipendi kabisa!kabisa!,fulanaziii!hiwe ya mwanzo
    halafu habari zingine

    ReplyDelete
  15. Haaa kaka acha kubana mbona utuambii Yanga ndio mabingwa na game mbili mkononi yakhe nazo ni breakin'nuuuuuzzzzz atiiii acheni wivu msimbazi jamani kichapo chaja
    Londoner

    ReplyDelete
  16. Kumradhi kaka Michu mbona kale ka post ka jana kenye wifiiiiz umekatoa?Amekupiga mkwara nini?

    ReplyDelete
  17. Misupu vije mechi ya leo? Mimi nilidhani ungesubiri uone Bwawa la Maini linavyolowa maji.

    Kila la heri bana, angalia usije ukakosea tena utabiri maana ndo kombe hilo pekee mlilobaki mnafukuzia mpaka dakika hii. Mkilikosa basi ujue kwamba mwaka umeenda mtupu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...