Pata picha hiyo iliyotoka katika gazeti la leo la NewZimbabwe! Swali la kujiuliza "Je kiatu hicho kinashonwa ili iweje?" kivaliwe tena? Wakati sisi (TZ) note yetu kubwa kuliko zote ni yenye dhamani ya Tsh 10,000/=.


Wiki iliyopita Serikali ya Zimbabwe walitoa note mpya yenye dhamani ya Zim Dollar 50,000,000/= (yaani note yenye dhamani ya Milioni 50). Unaambiwa hiyo note ya Zim Dollar 50,000,000/- hununua mikate minne tu, imekwisha!! Zim Dollar 50,000,000 ni sawa na US $ 2 ama Tsh 2,500/-


Hiyo picha nyingine inaonyesha mtu akiwa bureau de change (huku hawahesabu noti, huwa wanazipima kwa kilo), maana ukisema uhesabu ni mpaka kesho na mate yataisha mdomoni, usisahau zile mashine za kuhesabia hazifanyi kazi kisa hakuna umeme!

Good day!

Mdau kutoka Durban, RSA

please jina na email kapuni!!

Zitto (Not Kabwe!)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hivi mdau uliyeleta habari hii unakidharau hicho kiatu. Hata Tanzania hivyo tunavaa, tembelea hasa vijijiji, UMASIKINI ni mkubwa mno, hata mjini hayo yapo. Kuna watu hata icho hawana. Sababu yote ni SERA mbaya za watawala wetu.

    ReplyDelete
  2. "Ukistaajabu ya mussa, utayaona ya firauni" Naona mdau umenikumbusha kipindi cha radio one "mambo mseto"
    Kama uongo vile lakini ni ukweli lol! Fatma Issa ameimba "..bora adui shetani kama adui kiumbe (biaadamu)..." Na unyama wote huu ulioufanya mugabe bado haoni aibu!Itafika wakati hata pesa itakuwa haitumiki tena huko zimbabwe, itakuwa ukitaka mkate mtowe mwanao...ha ha ha!Ndio, us dola 1 itakuwa na thamani sawa na mtoto wa zimbabwe wa mwaka mmoja n.k! Ndiko anakotaka kuwafikisha wazimbabwe.

    Kwa hali hii sikutegemea kama Mugabe angepata hata kura 1 ya wazimbabwe (hata ya mkewe), lakini mhhh kweli, "shani ya mungu shani beberu kuota ndevu ng'ombe asiote kwani? Na nibora ng'ombe thamani..." Waswahili wasema "kwenye msafara wa mamba na kenge wamo..." Haya twaomba CCM nayo ijiandae yasije yakatufika hayo!

    Na sign off nisijeambiwa mie mpinzani...

    ReplyDelete
  3. MICHUZI, MBONA HUYU JAMAA ANAYESHONA MNAFANANA COPYRIGHT? FUATILIA VIZURI INAWEZEKANA......--Zimbabwe kunatisha lakini. Namshangaa Mugabe.

    ReplyDelete
  4. Tatizo ni viongozi wa Afrika wakikutana na Rais Mugabe wanampongeza tu na kumwambia "hivyo hivyo tuko nyuma yako" hawamwambii ukweli wakati wao hawafanyi hivyo ktk nchi zao. Ushauri anaopata unampotosha na kuiangamiza Zimbabwe.

    ReplyDelete
  5. Ukistaajabu ya Musa utaona ya.... Watanzania tusipoangalia huku ndiko tunakoelekea.Kwani sasa hivi ukienda na noti ya sh.10,000/= sokoni utanunua vitu vingapi?Tena ndugu zangu wa Lindi na mtwara mukae chonjo maana munaweza kubadilisha pesa kwa kutumia kangomba au kopo la bata oili ambalo linatumiwa sasa na walanguzi kununulia zao la korosho na ufuta.(bata oili 1= kilo 2 na nusu) [Eazy]

    ReplyDelete
  6. AAAh bwana msitufanye wajinga. hata kama zimbabwe ni maskini kkiasi hicho ni wazi hii picha imepigwa na kutumwa kikampeni. si kweli huyu bwana alikutwa anashona hiho kiatu abli aliambiwa afanye kama anashona ili apigwe picha. ndo maana alisahau kufichasimu yake ya bei mbaya aliyoning'iniza. wajinga no waliwao.

    ReplyDelete
  7. Mimi naamini Zimbabwe has other people than Mugabe. Mugabe hatawali kwa mtutu. Huchaguliwa kwa kura. Na anawafuasi wake ambao kusherehekea kwa nderemo na vifijo wakati wa kampeni. Kwani wao hawalioni hilo? Au wao wanatumia pesa tofauti na Wazimbabwe wengine?
    Kwa hiyo mimi naona kwamba hali hii imeridhiwa na Wazimbawe. Ingekuwa inawakera wangechaguwa rais mwingine(kama kweli Mugabe ndiyo anasababisha hayo).
    Kuna mdau kasema viongozi wa Afrika wakikutana na Mugabe wanamhimiza kwamba wako nyuma yake: Viongozi wa Africa hawawezi hata kutatuwa matatizo yao hadi waje viongozi toka nje ya Africa.( Tumeona Kenya. Na hii inakera). African leaders are not for their countries and the people they are there for themselves.

    ReplyDelete
  8. Poleni sana ndugu zetu wa Zimbabwe kwa matatizo yote hayo.Nawapongeza kwa Uvumilivu na ujasiri mkubwa.Viongozi wetu wa Afrika wana matatizo makubwa!Lakini Mungu kawasaidia na sasa Mugabe kaonja JOTO YA JIWE.Alijifanya MBUYU usiotikisika na kumjaribu Mungu aliye mwekea binadamu yoyote ukomo wa kufikiri na ukomo wa kuishi duniani.Mwenzetu alifikiri hatazeeka kamwe!Madudu aliyo kuja yafanya baadaye katika Uongozi wake na kugeuka kikaragosi badala ya Jemedari LIWE FUNDISHO KWA VIONGOZI WENGINE WA AFRIKA.Hata hapa Tanzania bado tunao viongozi ambao bado wanajidanganya kwamba bado wana akili zilezile za Ujana na eti ni wajanja kweli kisiasa.Nawashauri wastaafu siasa mara moja aibu kama ya Mugabe isije ikawakuta.Hivi kweli yote hayo ya Zimbabwe ni kwa sababu ya 'Imperialism?'.Au Ulafi wa Madaraka na Ubinafsi Uliokithiri?Nani wa kumpa heshima Mugabe sasa huko Zimbabwe?

    ReplyDelete
  9. na hapo hapo ukute bado wana vote for zanu pf..maajabu kabisa......

    ReplyDelete
  10. cha ufala we unaona noti ya elfu kumi ni sawa wakati Ethiopia noti kubwa zaidi ni ET birr 100 inaonekana wewe unawaza kama mzungu, acha zimbabwe wateseke ipo siku watakuwa sawa kuliko kuwa houseboys kwenye mashamba ya wazungu forever, ehee! we hujui kujitegea inataka kukomaa. We vipi au we mzungu nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...