WADAU WA HABARI KUJADILI MAPENDEKEZO JUU YA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA VYOMBO VYA HABARI, 2008
Umoja wa Kutetea Haki ya Kupata Habari Tanzania umeandaa mkutano wa siku moja kujadili mapendekezo ya wadau kuhusu Rasimu ya Muswada wa Sheria Huduma za Vyombo Vya Habari, 2008, utakaofanyika kwenye hoteli ya New Africa, tarehe 16, Aprili 2008 kuanzia saa tatu asubuhi.
Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Jaji Mstaafu, Mark Bomani na pia utahutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Bwana Reginald Mengi. Watakaohudhuria ni pamoja na wasismamizi wa vyombo vya habari, waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu, maafisa wa Serikali na wawakilishi vya vyama visivyokuwa vya kiserikali.
Mapendekezo hayo yanatokana na mchakato wa takriban miezi sita ambapo, umoja huo ulizunguka nchi nzima kukusanya, kupokea na kuchambua maoni ya wananchi na ya asasi mbalimbali kupata sheria itakayokidhi haja ya kuimarisha na kupanua demokrasia na utawala bora.
Wadau wa habari nchini Tanzania wanapendekeza kuwa sheria mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari ijikite katika Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotambua haki ya kila mwananchi ya kupata na kusambaza habari, kujieleza na kutoa maoni bila ya kuingiliwa.
Wadau pia wamependekeza kuwa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ilinde haki ya kuanzisha vyombo vya Habari na kuhakikisha kuwa haki hiyo haiingiliwi na dola. Vilevile wadau wanapendekeza kuwa uhuru wa kitaaluma unalindwa na vilevile vyombo vya habari vya umma havigombei matangazo na vyombo binafsi.
Katika mapendekezo yao, wadau wameainisha sheria takriban 27 ambazo zinakinza uhuru wa vyombo vya habari ambazo wanapendekeza ama zifutwe au zifanyiwe marekebisho. Pia wamependekeza kuzitoa kwenye makosa ya jinai baadhi ya makosa ambayo yana sura ya kisiasa kama vile kashfa ya jinai, uhaini na uchochezi.
Umoja huo wa wadau unaongozwa na Baraza la Habari la Tanzania (MCT); na kuhusisha Taasisi ya Uhuru wa Habari Kusini mwa Afrika (MISA), Tawi la Tanzania MISA-TAN); Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA); Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT); Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS); Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC); Shirika la Elimu ya Sheria Tanzania (TANLET); Shirika la Msaada wa Sheria (nola); na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TNGP).
Katibu Mtendaji
Baraza la Habari Tanzania (MCT)
Aprili 14, 2008

Huyo Reginald Mengi mwenyewe vyombo vyake vinaongoza kubania watu kupata habari.Mfano vyombo vyake vilibania habari zozote kuhusu timu ya simba mpaka viongozi wa simba wakapiga mkwara wa kuhamasisha wanachama na wapenzi wake kususia bidhaa na vyombo vya habari ndipo sasa tunaziona na kuzisikia habari za timu ya simba
ReplyDeleteKipengele cha vyombo vya umma kutogombea matangazo na vyombo binafsi sijakielewa vizuri...
ReplyDeleteWadau naomba msaada wenu wa ufafanuzi.
shukran.
Baadhi ya wenye vyombo binafsi wanapenda kulia lia na kuonewa huruma.Kipengele cha kukataza vyombo vya umma visigombee matangazo kimewekwa na wao tu kwa hila.Tokea TBC iliposhinda haki kiduchu za kuonyesha ligi ya uingereza watu wanalia tu.Cha msingi ni wote wapambane kwani vyombo vya umma vinahitajika vijiendeshe vyenywe huko mbeleni bila ya ruzuku sasa bila matangazo lengo hilo litafikiwa vipi
ReplyDeleteAma kweli uwana habari wa tanzania una mambo ! kama ni kweli huyo mdau hapo juu alivyosema yaani ipp media walibania habari za simba na mpaka pale walipotishiwa kugomewa bidhaa zao ndio wakaanza kuzitoa .duh! kazi kweli hapa nyumbani ,tena siyo ndogo.
ReplyDeleteMimi binafsi nawapongeza na nawasapoti wahusika, specifically the media representatives kwa kuchukua hatua hii ambayo naiona kama ni mwanzo mzuri kuelekea ktk mageuzi na mapinduzi ya kitaaluma na biashara ya uwanahabari hapa nyumbani
Sheria
Ni wazi kabisa (maoni yangu sheria hizo kama zilivytajwa hapao juu ) ni zile zilizokuwa relevant wkt ule wa mfumo wa siasa ya chama kimoja na ukomunisti
Infahamika na wala siyo siri ni jinsi gani ukomunisti na mfumo wa cham kimoja unavyoogopa uwan habri wa uwazi ,kitu kripotiwa kama kilivyo au kama kilivyotokea .serikali za mitazo ya kisiasa kama hii zinatabia ya kuamini ni heri watu wasifahamu ,wasielimike wasifunzwe kwa kigezo cha amani na utulivu wa majority ktk nchi
Lakini ukweli unabaki kwamba kuruhusu mawazo tofauti (provided ni ukweli na uwazi and given within the functional pricipals of journalism) )kuna faida kubwa na nyingi kuliko kuficha ficha . Najaribu kufikia ni kwa kiwango gani labda kuweka wazi sababu ya kifo cha marehemu na kukizungumzia wazi ktk vyombo vya habari na platform zingine kungeweza kuwaokoa wengi waliosalia hapa duniani (vijana zaidi) ) as opposed na hali ya sasa ya utoaji taarifa kwa jamii ambapo lugha ya kupamba na kupooza
makali ,tena siyo hivyo tuu bali hata kusema uongo ,yote haya ktk utoaji habari tanzania kwa maoni yangi ni kawaida sana.ukiachia sababu nyingine, kubwa hapa ni legal limitations .Ni kitu cha kawaida kusikia habari kwamba mtoto wa fulani hasa anapokuwa ni wa mtu mashuhuri (public figure au celebrity au mwanasiasa mkubwa ) au hata watu wa kawaida ,kuambiwa kwamba sababu ya kifo ni kuugua kwa muda mrefu.Wakati huo huo tunjua ya kwamba tuna janga linatukabili la ukimwi njia moja wapo ya kusaidia kupungu za ni kupashana habari unfiltered and indetail without withholding nothing ili kuwasaidia wale wenye masikio na macho ambao wako hai kwa sasa.
Hivyo kwa maoni yangu nasapaoti juhudi hizi waziwazi ili baadhi ya sheria ziweze badilishwa kwa manufaa ya wananchi na serikali yenyewe media ikitumiwa kwa uwazi ni chombo kizuri sana kwa serkali ktk kupata feedback juu ya sera zake na juu ya watendaji wake na mafakio au shida zinzokabili wannchi na mambo mengine mengi tuu ya kijamii yanahitaji attention ya serikali na ile ya wanajamii zinazohusika.
Matangazo
Kwa maoni yangu nafikiri jamani nyie private media houses wacheni kulia lia .huu ndio ushindani wa kibiashara .TBC inahaki na haikatazwi kutafuta masoko (adds) kama vile tv station au hata format yoyote ile ya media.hapa nyumbani .hivi ninyi mngekuwa nchi kama marekani au uingereza sijui mngelia nini ... labda mngecommit suiside so to speak.manake competition ni ya nguvu sana kwenye juhudi za kutafuta matanzano kwa wenzetu ni area moja nyeti na kama tunavyofahamu wote ,adds ndio life line ya any functional private media .hivyo basi kutokan na hilo wenzetu wameamua kuacha kufanya mambo kienyeji ,na wanaajri taaluma na wataalam wa masoko ya media .Siyo mtaalam wa masoko ya nyanya au any other tangible products.wtaalamu hawa wanajua every nuts and bolts za soko la matangazo, bits and tricks zoote.Tena zaidi ni kwamba wako very creative inapokuja kwenye techniques za utafutaji na uvutiaji adds na siyo hapo tuu bali hata kumaintain wateja wao.
Ofcourse ktk hili kitu kimoja ambacho ni wazi na ni muhimi ni lazima kuwa na kanuni za biashara ya matangazo yaani mtu akatazwi kumchukua mteja wako any time lakini kanuni na vijisheria vidogo vya hapa na pale vinapaswa kufuatwa without any preferencial treatment iwe ni media ya serikali au mtu binafsi
Lakini bottom line ni kwamba mchezaji yoyote yule ktk uwanda wa media anahaki ya kupata matangazo kwa yeyote yule privided zile kanauni zimezingatiwa
Maoni yangu hapa ni kwamba hivi sasa ni lazima kuamka Tafuteni wataalamu wa masoko ya media yale mambo ya mtoto wa mjomba na wa marehemu kaka wacheni !tafuteni watu ambao ni prudent ,pragmatic na pia ni dynamic wenye uwezo wa kulisoma soko la matangazo bila kujali ugumu wowote ule uliopo ktk competition ktk muda mfupi na kufanya lile linalopaswa lifanyike.
Kwa kweli kulia huku sasa ndio inanifanya nione kweli kwamba tuna utiri wa vifaa na masteshani ,magazeti na maredio nk lakini wtaalamu yaani media producers,media managers na hasa media sales experts ndio shida zaidi kwa private media houses
any way kaza buti wadau huu ndio ushindani wa kibiashara
Hata hivyo kazi mnayoifanya ni nzito na mpaka hapa mlipofika mnastahili pongezi
ni mimi
Raceznobar