DAKIKA KUMI ZIMEPITA NA SI YANGA WALA AL AKHDAR YA LIBYA IMEONA LANGO LA MWENZAKE KWENYE MGUU WA PILI WA MPAMBANO WAO HAPA NESHNO.
IKUMBUKWE YANGA WALITOA DROO 1-1 WALIPOCHEZA NAO WIKI MBILI ZILIZOPITA HUKO TRIPOLI NA LEO KUNA KINA DALILI WANA-JANGWANI WATAPETA TU KWANI WAMEANZA KWA KASI, JAPO MVUA KIDOGO ILETE NOMA KWA KUJAZA NESHNO YETU MADIMBWI KIBAO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kaka Michu, Leo Emirates vipi? maana naona 1-1 mpaka dakika hii ya 78:27, Bwala la Maini litakauka leo au?

    ReplyDelete
  2. pamoja na habari za kufurahisha za michezo, habari za dunia zisizotangawa mapema:


    Viongozi wa Tonga, Pakistan, Tanzania, Chile kutembelea Uchina.

    Viongozi hao watafanya ziara zao nchini Uchina, kama ifuatavyo:


    Mfalme wa Tonga Tupou V toka Aprili 9 hadi 15.

    Rais wa Pakistani Pervez Musharraf toka Aprili 10 hadi 15.

    Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete toka Aprili 10 hadi 15.

    Raisi wa Chile Michelle Bachelet Jeria toka Aprili 11 hadi 15.

    ReplyDelete
  3. Tatizo la timu zetu hasa yanga pamoja na mabo mengine ni viongozi kutokuwa makini nadhani si viongozi wa mpira wanachojua wao ni kubwabwaja tu kwenye vyombo vya habari kana kwamba kila mmoja anajipigia kampeni hatulishangai hilo manake inavyoelekea watu wapo hapo kwa ajili ya kujitengenezea njia njia kuelekea kwenye siasa ( angalia Tarimba ambaye kwangu mimi namchukulia kuwa ndiye chanzo kikubwa kilichopelekea yanga kuwa hapo ilipo kwa kuleta wazo lake la kampuni bila maandalizi na kuwavuruga wana yanga kwa kiasi kikubwa kisha akaiacha na kukimbilia kwenye siasa ).Binafsi napata wasiwasi mkubwa na uwezo wa viongozi wetu wa sasa ambao ni wasomi wana uwezo kiasi fulani lakini wanashindwa si tu kuipa mafanikio yanga uwanjani pamoja na kuwa watajitapa kuwa wanaongoza ligi lakini hata kuiendesha klabu kwa maana ya utawala kwa ujumla kiasi kwamba leo hii ukienda pale klabuni kwa hakika utasikitika kuona kile ambacho wazee wetu wlikibuni pamoja na kuwa hawakuwa na elimu ya kutosha kinateketea maskini . Ukiangalia uwanja ambao naamini ungeweza kusaidia kuiingizia mapato klabu unazidi kubomoka . Ivi wenzangu mnaweza kunisaidia kuniambia tofauti ya uongozi wa hawa wasomi wetu na ule wa wazee wetu?au ni kusajili wanamuziki kutoka Congo kila mwaka ambao hawana faida?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...