Jumuiya Ya Watanzania Uingereza inasikitika kutangaza kifo cha mwanajumuiya wa Kitanzania Bi. Mwajuma Ibrahim Seif , kilichotokea katika hospitali ya Royal Berkshire Hospital, Reading, Kifo cha Bi. Mwajuma kimesababishwa na ugonjwa wa Meningitis.

Bi. Mwajuma alizaliwa tarehe 11 Machi 1977 Dar-Es-Salaam, alikuwa akisoma katika chuo cha Lead Academy London ambapo alikuwa akisomea mafunzo ya Biashara.

Ili kufanikisha kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Tanzania kwa ajili ya mazishi, Watanzania na marafiki wa Tanzania wanaombwa kutoa mchango wa hali na mali ili kufanikisha kusafirisha mwili wa Marehemu. Kuchanga kwako ndipo kufanikisha kusafirisha mwili wa marehemu.

Msiba upo Reading anuani :
12 Trevor House,
Colliers Way,
Tilehurst,
Reading,
Berkshire.
UK

Unaweza kutoa mchango wako kwa kuweka fedha katika akaunti:
Bank Name: Nationwide Bank
Account Name: Mrs. H S Salum
Sort Code: 07-44-56
Account Number: 03020879
Pia unaweza kuwasiliana na Diego: +447733318081
Pia simu : +447733318081

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Natuma salamu zangu za rambirambi kwa wana ndugu wa dada yetu mpendwa Mwajuma, poleni sana kwa msiba huu mlio upata.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana ndugu na marafiki.

    ReplyDelete
  3. ooh too young to die.poleni sana wafiwa.RIP mwajuma

    ReplyDelete
  4. maskini,

    Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi amina.- Robert

    ReplyDelete
  5. duh! Ua limechunwa kabla ya kuchanua. Poleni. Gas uk

    ReplyDelete
  6. Poleni sana Watanzania wote hapo London na Uingereza kwa ujumla kwa msiba huo mkubwa.Rambirambi ziwafikie ndugu na marafiki wa karibu wa marehemu.Ni vigumu kuelezea majonzi yetu.Lakini tutakuwa nanyi katika kipindi hichi chote cha majonzi makubwa.Tutajumuika nanyi pindi mwili wa marehemu utakapo wasili hapa nyumbani Bongo.Mwenyezi Mungu kampenda zaidi.Ndiye Muumba na sasa Katwaa!Kazi ya Mungu Ihimidiwe.Akapumzike Peponi milele amina.

    ReplyDelete
  7. Inalilah wa ina ilahi lajuun! huyu si ni Mwajuma aliekuwa matroni wa Hadija Kondo! na si ni yule mke wa Edibily Lunyamila, na si ni mama mtoto mmoja Lulu! kaenda lini London!
    Ama hakika kila nafsi itaonja mauti, yaani alivyokuwaga na usongo na maisha huyu dada! na alivyokuwa mwema! du! namkumbuka enzi za Uhazili 1994-1996. M/Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amen

    Familia tufahamishane juua kuwasili wa mwili wa mpendwa Mwajuma na shughuli za mazishi tafadhali.

    ReplyDelete
  8. Rest in peace dada, hope ur in a better place, pray for us who are suffering in this worl full of problems. May almight GOD grant you eternal peace.

    ReplyDelete
  9. jamani mwajuma aliyekuwa mke wa EdIbily Lunyamila!jamani nakukumbuka sana ulikuwa unaishi Ngokolo shinyanga!Mama Nyendo pole sana mama kwa kumpoteza binti yako!na dada NYENDO nakupa pole sana my dear!
    mimi Hollo mjukuu wa Mzee Mwandu!
    Shinyanga Uzunguni!

    ReplyDelete
  10. Mungu amlaze mahali pema peponi. Bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana liimidiwe. Pole kwa familia ya marehemu na mvumilie wakati huu mgumu na mfarijike kwa kuwa ndugu yenu ameenda kupumzika mahali pema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...