mwalimu na mzee karume wakipita mitaa ya dar kusherehekea na wananchi siku ya kwanza ya muungano miaka 44 ilopita. sherehe za siku hii zinafanyika jumamosi hii hapa dar kwa gwaride rasmi neshno pamoja na shamrashamra zingine kibao ikiwa ni pamoja na maonesho ya ndege za kivita

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hawa tu ndio viongozi ambao Tz ilikwisha wahi kupata. Kuwapata kama hawa tena hatutokuwepo tena hapa duniani. Hii nchi imekwenda kwa mbwa kama Nyerere alivyosema. Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Africa.

    ReplyDelete
  2. look at those asians that means they have been there since those dark days....born and raised in Tz...poor miss Tz was accused for nuthing...........

    ReplyDelete
  3. ukiangalia kwa undani matatizo mengi ya zanzibar hivi sasa yanachangiwa sana na huu muungano wa tanganyika na zanzibar...
    wazanzibar hatuutaki tumechoka nao...hebu na atokeze mtu anambie hasa huu muungano una faida gani hasa???
    kama ni udugu ulokuwepo baina ya wazanzibar na watanganyika basi udugu unaweza kukuwepo hata baina ya mtanzania na mganda,mtanzania na mkenya,mtanzania na mkongo..etc na hata mzanzibar na mtanganyika bila kukuwepo na muungano wa kiserekali au kichama.umenifahamu???au kama kuna kitu chengine chochote kinachoonekana kama ni faida ya muungano(hamna) basi kinaweza kutekelezwa kama ni hisani na udugu uliodumu baina yetu tu sio lazima kwa kuungana.
    wazanzibar walilazimishwa tu huu muungano bila ya baraka zao sijui kuhusu tanganyika laini nahisi na wao ndo hivo hivo tu..
    umeona muungano gani duniani ukawa na serekali mbili?ya muungano na ya zanzibar??
    maraisi wawili??lakini chama kimoja??
    wazanzibar hawataki muungano bali wanataka amani,maelewano, kutoingiliwa katika maamuzi yao etc..
    udugu kati yetu na utaendelea kuwepo tu bila hata kuunganisha nchi na kufanya sherehe!!

    ReplyDelete
  4. hilo gari bado lipo? mdau kutoka Arizona anauliza

    ReplyDelete
  5. Mdau namba moja umeishiwa busara na inaonekana ama huijui historia ya Tanzania vizuri au ufikiri wako ni mdogo. Karume na Nyerere pia walifanya yao mazuri na mabaya na kama wananchi tungeruhusiwa kuwachambua hawa jamaa kiundani tuengeona madudu yao. Ukiangalia pia wengi wa viongozi wa sasa walifanya kazi na nyerere na walifilisi mashirika ya umma huku nyerere akiwepo na aliishia kuwahamisha kutoka shirika moja kwenda lingine sasa unaposema nchi inakwenda kwa mbwa inamaanisha nini? Nyerere mwenyewe nchi ilimshinda (hali ya uchumi ilikuwa mbaya sana) ndiyo maana akamua aingie mitini mapema. Cha msingi hapa siyo kulalamika ila ni kupapambana na mafisadi paomaja na maisha kwa wakati tulionao kwani hata wangekuwepo nyerere na karume wasingeweza kubadili hii hali kulingana na wakati uliopo. Boresha maisha yako na siyo kukata tamaa na kuanza kukumbuka watu ambao hata wakati wanatawala huenda hukuwepo

    ReplyDelete
  6. Namuunga mkono anony wa 9:32 hapo juu. Tanzania ingekuwa mbali kama Nyerere angeachia ngazi mapema. Kaifilisi nchi na siasa yake ya kijamaa. Watu wamesahau kabisa kuwa walikuwa wanalala na njaa kila siku wakati viongozi wetu wanaiba na kufilisi mali ya umma.

    Nilikuwa mfanyabiashara wakati wa Nyerere na Sokoine. Wananchi walikuwa wananililia dukani kwangu kila siku. Kila kitu kilikuwa kwa ration. Unga, sukari na mchele nilikuwa napewa magunia matano kwa mwezi ili niwauzie wananchi wa mtaa wangu. Ukiwa na dola unawekwa ndani. Kusafiri nje lazima uwe na ruhusa maalumu kutoka serikalini. Kupinga uongozi wake unawekwa ndani. Hamna mtu mwenye akili yake timamu anaweza kusema kuwa uongozi wake umeleta faida yoyote kwa jamii . Nakumbuka kabisa nikiuza sabuni ya Urusi na mchele wa China, ikiwa na mabandiko yake ya kuonyesha kuwa ni bidhaa za misaada. Wananchi wengi waliteseka na serikali yake, najua Watanzania wenzangu wengi ni Wapiga Makofi wa Nyerere, lakini ni muhimu kujua matatizo aliyotuletea pamoja na ufilisaji wa nchi kutokana na siasa yake ambayo pia haijaheshimu haki yoyote ya binadamu. Nawakilisha kama nitachapishwa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2008

    nawaunga mkono hawa jamaa wawili wa mwisho wanasema ukweli, ningeozea kimoja kuhusu huyu baba wa taifa nyerere hakauachia ngazi, aliendelea kuwa mwenyekiti wa chama pekee tanzania,watu wa bara hatuellewi historia kwa sababu tulikuwa tunasikiliza radio tanzania ambayo ilikuwa inamilikiwa na serikali ya nyerere.Nakumbuka mwaka 1980 uchaguzi mkuu, watu walikuwa wanaulizwa kitambulisho cha kura kama huna unatiwa ndani, kumpigia kura nyerere ilikuwa ni lazima kichekesho nyerere alikuwa hana mpinzani,ulikuwa una yes for nyerere au hapana for nobody, halafu tunaambiwa nyerere ameshinda asilimia 95-98 ya kura!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...