Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, akizungumza na Mkuu wa Manyara, Henry Shekifu pamoja na Meneja Uhusiano wa NMB, Shy-Rose Bhanji baada ya NMB kukabidhi hundi ya sh milioni 10 kwa ajili ya kusaidia mfuko wa maafa, kufuatia vifo wa wachimbaji wadogo wapatao 75 huko mererani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mahesabu ya chap chap,

    10M ni sawa na 133,333-Laki na thalathini na tatu elfu kwa kila familia ya mfiwa kati ya familia 75 wanaosadikiwa kufariki, hii itasaidia familia ya waliyofiwa kununua jeneza na gharama nyengine ndogo ndogo kama itakuwepo pesa ya akiba. Kama maiti haikupatikana, pesa yote wataweza kutumia kwa wiki mbili tatu, wakifikiria jinsi gani ya kuweza kupata mapato ya kuhudumia mahitaji ya familia kila siku. hii yote ni solution ya hivi sasa, pointi kubwa ambayo ninataka kuiongele ni hii.

    Wote tunaelewa hii ni mara ya pili haya maafa kutokea ambapo yangeweza kuzuilika, kama kungekuwepo na njia nzuri za kuwasaidia hawa wachimbaji wadogo wadogo, misaada kama vifaa, elimu ya uchimbaji bora wenye kuzingatia usalama, na yote siyo bure. Jinsi gani serikali wataweza kurudisha fedha zao, serikali itumie financial institution kama banks kununua madini yao kwa bei nzuri. Hapa inajengeka hoja Serikali itaweza kuingiza pesa na vile vile inakua na uwezo mkubwa kucontrol the whole market ya Tanzanite. price iwe nzuri.

    ReplyDelete
  2. Bhanji anapenda publicity za siasa sana. Lakini ndo hivyo asante NMB kwa msaada

    ReplyDelete
  3. Mheshiwa Malima kijana makini sana, alistahili kuwa waziri kamili.

    ReplyDelete
  4. Hongera NMB kwa msaada huo. Lakini mimi nina wazo tofauti. Kama Milioni hizo 10 zingetolewa kwao wakiwa hai nadhani wangeweza kuambiwa waunde kikundi wakapewa pesa hizo ili wanunuwe vitendea kazi ambavyo pengine vingewaepusha na mazingira hayo hatarishi.
    Mimi nashauri makampuni yote walioweka pesa zao wakisubiri maafa ndiyo wazitowe wawahimize vijana wakiwa hai waungane ili wawape wanunuwe vitendea kazi, bure, siyo mkopo. Hii itasaidi kuepusha vifo kama hivi vya kwenye mashimo. Kwa nini mtu akiwa hai anakopeshwa halafu akifa anapewa bure? Kama uwezekano wa kugawa pesa namna hiyo upo ni vyema wakazigawa kwa watu waliohai ili kunusuru hali kama hii.

    Ni kama hadithi ya kijana aliyekuwa anaomna mchango wa kwenda shule lakini hakuna aliyetowa. Kijana kaenda mjini kutafuta vibarua,kagongwa na gari kafa. Cha ajabu mamilioni ya pesa yalitolewa kwenye msiba na wale wale waliogoma kuchanga kwa ajili ya masomo akiwa hai.
    Nawashanuri wadau wa maendeleo tuwekeze kwenye MAISHA na si MAAFA.

    ReplyDelete
  5. Natowa pole sana kwa familia zilizofiwa nashauri serikali wajitahidi sana kutatua tatizo kabla ya maafa. pokezi kwa benki yetu NMB kwakuwa mstari wa mbele kusaidia mchango wao natumaini hizo hela zikitenda kazi ipasavyo itakuwa imesaidia haya maafa yanayoikumba hao ndugu zetu MUNGU AZIKE ROHO ZAO MAHALI PEMA AMINA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...