Kwa niaba yangu na kwa niaba ya ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu Abdulhameed Bafagih, napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu zadhati kwa wote walioshiriki kwa njia moja au nyengine katika kukamilisha hitma yetu.
Inshallah Allah SW atakulipeni kwa kila jema mlilofanya.Pia shukrani za dhati ziwafikie wale wote waliohudhuria na pia waleambao walikuwa na nia ya kuhudhuria ila walishindwa kutokana na sababumoja au nyengine. Tunakushkuruni sana.
Tunamuomba Allah SW atutakabalie dua zetu na inshallah Ampumzishemarehemu wetu katika makao mema, amuepushe na adhabu za kaburi naamfufue miongoni mwa waja wema waliobarikiwa pepo na ampe kivuli chakesiku ya hesabu , siku ambayo hakutokuwa na kivuli ila kivuli chake yeye Allah peke yake, ameen
Na sisi Mungu atupe mwisho mwema, ameen.
Tafadhali wafahamisheni wenzetu popote walipo.
Ahsanteni sana.
Katty.NYC.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...