Bro Michuzi,

Kwanza hongera kwa kuchaguliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Tegeta (hahahahaha...) ambayo inapatikana siku kama ya leo tu!!!, Pia napenda nikupongeze kwa kazi nzuri sana unayofanya ya kutuhabarisha na siku uliyonikosha sana ni pale bunge liliposoma ripoti ya Rich-Mond, kwani mwenyekiti alipomaliza tu nasi tukawa tumeipata kwenye blog hii ya kipekee.

Sasa narudi kwenye issue yenyewe. Mimi ni kati ya wadau tuliohudhuria fainali za BSS pale Pearl Blue hotel na napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza waandaaji wa shindano hilo na waendelee na kazi yao nzuri sana.
Binafsi nakubaliana nao kwa asilimia mia moja juu ya mshindi wa mwaka huu dada anaimba si mchezo.
Kilichonichukiza bro Michuzi niwahudumu wa hoteli kubwa kama ile kuwabambikia wateja wao bei za vyakula na vinywaji utadhani bar za vichochoroni. Sitarajii kwa levo ya hoteli ile mteja awe na wasiwasi na ukweli wa bei hii ni aibu kubwa na sielewi nchi hii ina laana gani.
Mimi niliuziwa viazi vya kukaanga na kipande cha kuku (wao wiliita chipsi kuku) ambavyo quality yake haitofautiani na tunavyopata manzese kwa shilingi Elfu kumi (10,000/=) na bia ya kopo Ndovu kwa shilling elfu nne na mia tano (4,500/=) kilichonisikitisha ni pale nilipokuja kufahamu bei halisi ambayo ni elfu tano na mia tano (5,500/=) kwa chakula na elfu tatu (3,000/=) kwa bia.
Sasa hapa nashindwa kuelewa tatizo, ni mishahara midogo au ndio vifisadi vidogo ambavyo vipo kuwakamua wateja wao wasio na hatia.
Naomba Bro Michuzi iingize hii kwenye blog yako wadau wawe macho wanapokwenda kwenye tafrija kwenye hizi zinazoitwa eti HOTEL KUBWA.


Mdau

Henry Michael

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. kaka pole sana hiyo ndio bongo kila kitu inabidi uhakiki kabla ya kilipa hakuna cha hoteli kubwa na dogo panga kama kazi watu wapiga panga kanisani misikitini itakua hotelini hii ndio bogno kaka

    ReplyDelete
  2. Vyombo Vya habari na njia nyingine za kufikia jamii si sehemu tu ya kusemea bali ya kurekebishia matatizo ya jamii haswa jambo kama hili la BluePearl Hotel. Ila Kosa letu kubwa waDanganyika ni 'Documentation' ambayo inapelekea 'Validation' (hiLi hatuna kabisa utamaduni nalo hata ktk matumizi ya fedha, Henry naomba rejea blog hii ile ishu ya Pauper March 19
    Ulichokifanya ni sahihi huna tofauti na aliyesema 'CCM wezi sana' bila kutaJa CCM Mwanachama yupi. Inabakia stori zilezileeee za tangu enzi hizo. Kwa suala lako wewe umejaribiwa kuibiwa, huna budi kutaja mwizi na ashughulikiwe, Mmiliki wa Hotel huenda hajui hili, je UNAONAJE UNGEDOCUMENT NAMBA YA MHUDUMU HUYO NA KUIFIKISHIA MENEJIMENT YA HOTEL HIYO? kila mtu angewaka kutaka kusikia mhudumu huyo No. X ameadhibiwaje na tungeona jii tungeweka makala kila siku hapa Blogini adi kieleweke...au Pia km bei siku hiyo ilikuwa kubwa kwa sababu ya Tukio (DEMAND LAWS) si kosa kulinganisha na bei ya leo ambapo hakuna tukio, kama hii si sababu basi kuna kosa, vinginevyo stori yako inaishia hewani tu kama anayepayuka 'Cuf Wadini''Wachaga wezi' 'Wahaya Wapenda chini' 'Wakurya wakali' 'Wachalinze Wachawi' 'Wakenya Matapeli' kwa kidhungu thithi tunaita 'Stereotype' Ahsanteni wadau

    TAMKO LA KATAO (Disclaimer)
    Mimi Active X kwa namna yoyote ile sihusiki (hata kuingia sijawahi) na Hotel ya Lulu BluePearl, nimetumia tu elimu yangu kufafanua mrengo sahihi wa kufikia utatuzi, hii yangu isitumike km mbadala 'alternative' ya Kauli ya Hotel, nategemea watatoa tamko lao kutegemea na taratibu zao za kumaliza.
    Michu km kawa Kamua kaka!

    ReplyDelete
  3. Bongo tambararee!

    ReplyDelete
  4. Tatizo wabongo wenyewe ndo mnaendekeza, nikikuuliza una risiti utasema huna wala hukuomba...

    Lakini pia sometimes, tukio linaweza badilisha bei... Maybe bei ilibadilika siku ile cuz of BSS.

    ReplyDelete
  5. Wadau niko nje ya Tizii mwaka wa kumi na moja , ina maana shilingi ya Tanzania imeshuka kiasi hicho?Mwaka 1997 nilipoondoka bei ya bia ilikuwa mia tano.
    Mdau , Sterling, VA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...