Habari yako Bro. Michuzi pamoja na wadau wote wa Blog yetu ya jamii. Ni matumaini yangu kuwa wote mu wazima na mnaendelea vyema na shughuli za kulijenga Taifa.


Ninaliombea Taifa langu la Tanzania katika kipindi hiki kigumu hasa wakati huu wa Muafaka baina ya CCM na CUF ambapo nimepata taarifa kuwa wajumbe wa kamati kuu ya NEC wametaka hili suala lirudishwe kwa wananchi.

Hivyo ninawaomba ndugu zangu Wazanzibar wafanye maamuzi ya busara ili kufanikisha mshikamano wa kudumu kwa manufaa ya Taifa letu changa.

Mungu Ibariki Tanzania.
Mdau Zainabu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. huyu siulishamtoaga na picha hii hii..una lako jambo!wengine tukitoa picha hapa kapuni

    ReplyDelete
  2. nimekupenda ghafla dada

    ReplyDelete
  3. Things can get NASTY for you Mdau Zainab. The hitting and bashing of ugly comments will wave in from every direction and some good one of course. I hope you will stand the storm, you seems to keep yourself informed of the current political stallment back home, Are you on CCM or CUF side.

    By the way who is MAVIS HARRIS, the name shown at the background ?

    Was that picture meant to be sent to ISSA MICHUZI, private folder ? LOL.. Michuzi, this is just a joke ? don't take it seriously and I hope your wife wont read this ?

    It reminds me of my schools days, would ask for a picture of a girl, and most of the time, and not all the time, you will be given this sort of snap. You all know what I am talking about.

    I truly salute your courage.

    You look beautiful girl, I mean with the white top.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  4. mh! dadangu bado tu unatafuta umaarufu kwa nguvu???!!!pole we ila jitahidi kwani manka kashaupata na chibiliti hadi SR aliwafagilia na ww jitahidi tu....utaukwaa umaarufu!!
    mdau XXXL

    ReplyDelete
  5. michuzi kweli huyu ni zainabu wa kweli, sio wa kulazimisha, hongera zainabu kwa ukarimu.

    ReplyDelete
  6. Nimekupenda ghafla..toa email basi!!

    ReplyDelete
  7. WADAU, SI MUMEONA!!!!!!!!!!, TAFADHALI REJEENI MAONI YANGU KTK KATUNI YA KP (ILE RAIS KARUME ANATAKA KUDAKA PENALTI) NILISEMA HATUKUBALI MSETO MPAKA MZEE AMALIZE MUDA WAKE ULIOBAKIA, mwanamapinduzi

    ReplyDelete
  8. wadau si niliwaambia muafaka hautotekelezwa mpaka mzee amalize miaka yake 2 iliyobakia, rejea coments zangu katika katuni ya kipanya ile ya rais anataka kudaka penalti-- mwanamapinduzi, "sisi ndio wenyewe"

    ReplyDelete
  9. kaka misupu badilika kaka sio kila siku picha za mademu tuu wape nafasi wa blog woto hii blog ni yetu sote wana jamiii sio so watu wote wakitoa picha zibandike kaka

    ReplyDelete
  10. Nimesoma leo kuhusu CUF wanavyosema kupinga hilo suala serikali ya mseto Zanzibar kupelekwa wa wananchi.

    Kama ni kweli CUF hawataki hiyo hoja ipelekwe kwa wananchi ili waamue CUF itakuwa ni chama cha ajabu chenye matatizo makubwa!

    CUF inajiita Chama cha Wananchi sasa kama ni Chama cha Wananchi kweli wanaogopa nini hoja hiyo kupeleka kwa wananchi ili waamue kama wako tayari kutawaliwa na serikali ya mseto?

    CUF waelewe kuwa wananchi wa Zanzibar si wote ni wanachama wa CCM na CUF hivyo kama wameyaongea kivyama hayo ni yao kama vyama wananchi nao wana haki ya kuamua kama hayo waliyoongea wanayakubali au hawataki.

    CUF inataka udikiteta wa vyama kwamba CUF au CCM wakisema basi hiyo ndiyo sauti ya wananchi wote wa Zanzibar!!! ambayo wazanzibari wote inabidi waseme AMINA kwa hao miungu vyama Maalimu CCM na Maalimu CUF!!! Si Kweli CUF amkeni.Sauti ya wananchi ni muhimu nayo isikike kwa kura ya maoni.

    Vyama vya CCM na CUF mmekubaliana kugawana vyeo,posho, magari,maofisi na fursa. Lakini ni vizuri kupata maoni ya walipa kodi kuruhusu huo mgao au kuukataa! na pia kuwapa nafasi wajue hatima zao zitakuwa nini mkishagawana hiyo migao.

    Kuwakatalia fursa hiyo wananchi ni kuingiza udikteta wa vyama katika siasa za Zanzibar kitu ambacho hakikubaliki kwa wanademokrasia.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  11. Dada umependeza lakini hii picha kama vile umeipigia kwenye lobby ya hoteli. Ulikuwa Days Inn nini?

    ReplyDelete
  12. Hivi mara ya kwanza hawakukubeep....toa basi picha nyingine yaani hii ndio the best of the best....!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  13. Mwanamama huo mkao wako uliokaa mmh kuna sehemu zinakua wazi..zile sehemu ambazo..hupita kama hewa hivi ziko waaa..ila kwa pozz unalo..ni hayo tu

    ReplyDelete
  14. Mhhhhh wewe mbona mshamba hivi yaani unaona raha gani kukaa chini na kuweza kutuma picha yako hapo kila mtu aione huoni kama unajishusha hadhi kweli wewe huna mpango au wewe ndio upo katika kundi la kina manka?kwanza mbovu nenda zako huko.

    ReplyDelete
  15. Hii picha alishaitoa huku...sasa nini maanaya pili kuirudia....????Jamani Michuzi hebu tuongee deal tutengeneze site ya kutafuta wachumba manake naona huku tunabanna sasa

    Halafu huo mguu nadhani manka ndio anautafuta...Size 13 ....

    ReplyDelete
  16. Mi nashindwa kuelewa, watu wakiwa wanatafuta wachumba hawaweki picha zao, kutoa maoni tu wanaweka picha, I dont understand, sasa hiyo picha ni ya nini, kama ulitaka tujue nani kachangia maoni, jina na address vinatosha, Au unatafuta mchumba kijanja eeh?

    Big Sam

    ReplyDelete
  17. nakuunga mkono hakuna kitu kikubwa kama kuwa na busara ktk kuleta maendeleo ya nchi na sio ugomvi na mvutano, hayo hayasaidii kitu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...