"...refa katuua. we umeona wapi dakika za nyongeza zikazidi dakika tanoo?" anasemaarden (pichani) baada ya bwawa la maini kutoa droo 1-1 na chelsea usiku huu.
hata mie namuunga mkono. marefa wamepania tukose ubingwa. lakini tutaonana darajani... sie twamtaka man u kwenye fainali tuuwe kidomodomo

KAKA MICHU

Mimi bado ninayo matumaini tutatinga fainal ya UEFA champions league Moscow. Ni jambo la kusikitisha sana kuona tumejifunga goli na kuwapa zawadi ya bure CHELSEA hasa katika dakika za majeruhi.
ILIKUWA MECHI TUIMALIZE ZAMANI – TORRES GERRAD AURELIO NA KUYT ingekuwa walizitumia nafasi waliozipata – LAKINI BADO NINA IMANI KUBWA TUTAPITA tu. NA VIPI ITAKUWA FURAHA KUMFUNGA CHELSEA KWAO. LAKINI WAKATI HUO HUO NATAKA KUMWAMBIA RAFA ATAZAME NI KWANINI WACHEZAJIA WETU WANAKUWA WANAJIFUNGA WENYEWE – MECHI YA EVERTON HYPPIA, TOTEHNHAM AURELIO NA RIISE HII NI MARA YA PILI KUJIFUNGA.
Pia kitu kimoja namkumbusha RAFA katika mechi kama hizi asimwache nje HYPPIA – alifanya makosa haya HAYA wakati tulipocheza na MANCS katika ligi – kwani magoil yote mawili waliotufunga Man united angekuwa HYPPIA angeyawahi kuyaokoa kwa kichwa.

Kwa hiyo napenda kuwaaambia hao waliofurahi sisi jana kutoka draw – bado kuna dakika nyengine 90.
na mkumbuke kama LIVERPOOL NI THE MOST SUCCESFUL IN THE WORLD. HAO CHELSEA NI ARTIFICIAL TU – PESA ZA ABROWMOVICH TU. NA HAO MAN UNITED NI WIVU TU KWA LIVERPOOL -

Salim – Muscat

.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. oyaa huyu jamaa vipi na chupa yake ya kilimanjaro,eti refa kawauwa,nyie sio wakuongelea habari ya refa ,refa haohao ndio aliewaleta kwenye semi,we kunywa maji hayo ukalale,usipoangalia utapigwa kichwa kma cha RIIIIIIIIISEEEE, MTANGA

    ReplyDelete
  2. Wacha wee refa alikuwa anasubiri mpira upoe apulize kepenga...RIISE baada ya kumwachia kipa na papala zake kautia mpira kimyani..wala si refa...na goli la ugenini ndio tulikuwa tunalitaka Saaana!

    ReplyDelete
  3. kweli dakika zilizidi kdg lakini pia riise alifanya uzembe sana ule ulikuwa mpira wa chini na angeupiga kwa mguu, alinishangaza kuuinamia kwa kichwa!! ila ndio mpira 2subirie 2nd leg, sijui itakuwaje!!!! mpenzi wa liver

    ReplyDelete
  4. Asiyekubali Kushindwa si Mshindani!
    Ndugu zangu nawashauri mwangalie mbele maana kele hazitawasaidia kabisa!

    Goli mfunge wenyewe kisha mumsingizie refa?

    Wapi na Wapi?

    ReplyDelete
  5. ingawa goli limewaua liverpool,ila nafikiri wana nafasi nzuri ya kuwin game ijayo coz watakuwa hawachezi defensively kulinda goli bali watakuwa wanatafuta goli ili wawe safe zaidi!
    you will never walk alone!

    ReplyDelete
  6. Nimekuambia Michuzi, kaa mkao wa kuchinjwa, sasa subirini darajani muone chenu. Sasa hivi naona kichefuchefu bado hakijaisha, yule mtoto riise mnamuweka sana benchi ndio maana kaona isiwe tabu.

    ReplyDelete
  7. Unaongelea refa kuongeza muda mbona huongelei goli la utata mlilofunga?

    ReplyDelete
  8. Dakika za ziada ni zile zinazofidia wakati mpira umesimama either kutokana na mchezaji kuumia uwanjani au emergency nyingine na siku zote hazipo fixed, sasa malalamishi yasiyo na msingi ya kuwa ooh refa kaongeza dakika yametoka wapi. Nadhani mdau huyu kaanza ushabiki wa mpira kwa kufuata mkumbo,inawezekana hapo awali alikuwa anausikiliza mpira kupitia RTD,maana kama angekuwa anaujua mpira asingekuja na hoja hafifu kama hii hapo juu.

    kwanini tusiwe wastaarabu tu kwa kukubali kuwa ilikuwa mechi iliyokutanisha miamba, matokeo ndio hayo tunaganga yanayokuja mbele, visingizio kama vya mashabiki wa Yanga na Simba vimeshapitwa na wakati. Kila timu bado ina chance ya kupita ingawa chelsea kwa kuwa wapo kwao wana advantage ya uwanja.

    tufikie wakati tubadilike namna ya kutoa maoni na sio ku post utumbo

    ReplyDelete
  9. Michuzi,Kama nakumbuka vizuri, hivi karibuni ulipiga marufuku wadau kutuma picha zetu humu kijijini.Sasa bado tunaendelea kuona watu wakituma picha.Tunaomba ufafanuzi tafadhali.

    ReplyDelete
  10. MICHUZI NILIFIKIRI HII STYLE YA WATU KUTAFUTA WACHUMBA NA PICHA ZAO ULIIPIGA MARUFUKU NA MJADALA ULIFUNGA....SASA MBONA WATU WANAZUNGUKA MBUYU NA KUJA NA STYLE NYINGINE????????

    ReplyDelete
  11. Leo mnasema eti Refa mbona alipokuwa anawabeba na Arsener kwa kuachia penati za wazi hamkusema anawapendelea? Mimi nimefurahi sana Riise kufunga lile goli japo simpenzi wa Chelsea.

    ReplyDelete
  12. hao ndiyo the blues bana presha ile ilikuwa ya gori babaake acha lawama za kijinga kama Ref: Konrad Plautz toka Austria ni FIFA refaree tafuta mchawi mwenyewe tuko juu sisi

    ReplyDelete
  13. Sasa ndio naelewa zaidi maana ya kale lamsemo ka "YOU WILL NEVER WALK ALONE"

    Kwamba hamuwezi ku-survive wenyewe kwenye game bila ya marefa,

    Sasa jana mmepata refa fair, ndo mnaanza kulalamika,

    Kifungo chenu ni pala darajani stamford,

    Mshika-dau

    ReplyDelete
  14. aisee kwakweli hakuna habari ya refa kuwaua, ila pale refa alikuwa hawezi piga kipenga cha mwisho kutokana na kwamba hairuhusiwi kumaliza mpira ulio ndani ya eneo la hatari (sheria ya 14 ya marefa FIFA).
    MIMI mshabiki wa man utd ila jana Liverpool mmenikosha, kweli jamaa wa darajani mliwaonyesha kama mnauweza ila kuhusu THE RED DEVILS, THE FREE SCORING UNITED, THE FERGIE SQUAD, MAN UTD THE EVERYTHING, yaani usipime, usibonyeze na wala usijaribu. ule ni mziki mwingine kabisa.

    ReplyDelete
  15. usiwe na hofu kaka.. pale darajani nina uhakika mtafanya mambo ya maana, hao chelsea mpira wao wala siyo wa kutisha, ni bahati tu jana mmewasaidia goli..
    final man u kwa kweli lazima iwepo, ila mjue kwamba mnapata kichapo kama kawa..

    ReplyDelete
  16. bwawa la midebwedo hilo!!!!!!!!!!!""$$%%$%&^^&^^&&*&%%&&*(&*(&&na darajani watawakomesha mapa mwe ifereji ya maini sasa

    ReplyDelete
  17. Nitakupigeni kichwa kama RIIISEEE nyie mnaochonga kwamba refa kawaua. yaani leo ndo mnajifanya kusahau sheria za soka, dakika za nyongeza zilikuwa nne, ndani ya hizo dakika za nyongeza mkapoteza tena muda, halafu ilipofika dakika ya mwisho mkaruhusu shambulizi, sheria hizo hizo za soka hazimruhusu refa kumaliza mpira wakati jamaa wanashambulia, wakati refa anasubiri mpira upoe apulize kipenga cha mwisho, mkamwachia jamaa ageuke, apige krosi, na libeki lenu badala ya kumwachia kipa adake na kulala nao chini kama kawaida yake akajifanya mjanja, akadaivu yeye, wewe mpira unakuja chini anajifanya kuonyesha madoido kupiga kichwa cha kudaivu, matokeo yake ndo hayo, na kipa wenu alishajipa likizo akijua kazi imeisha. Lakini pia msimlaumu sana refa kwani nyie inawapasa kuwa na shukrani kwa marefa, hii ni nusu fainali ya pili mnafikishwa na hao hao marefa eti leo mnajidai kuwageuka! tehetehetehe, mkuki kwa nguruwe kwa bwawa la maini uchungu enhe??? na nyie onjeni machungu ya kufungwa, kwanza mpira wenu unaboa sana, nyie timu ya msimu ya kombe moja!!! Michuzi hata ukibana najua kaujumbe kamekufikia na kawaambie na wenzio, kwa kocha kama Rafa safari bado mnayo kutwaa premier league!!

    ReplyDelete
  18. Nimefurahia sana kwani michuzi ulisema utavaa jezi ya Livepool wiki nzima.

    Hapo hamna cha refa, mbona huzungumzi kwanini mlikubali kukaribisha presha langoni.

    Msife moyo, fainali ni Man united vs Liverpool. Hao chelsea wanaenda kulizwa darajani.
    Naomba dua zenu wadau Man united tushinde leo.

    Poleni sana wanavijogoo.

    ReplyDelete
  19. kilioo kilioo mtamlilia nani weeeeee! HAYA NI KAWIMBO NATAMANI UJARIBU KUKAIMBA KWA MATARAJIO YAKUPATA KICHAPO DARAJANI.

    ze bluu man!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  20. Sisi washika Bunduki yetu macho.

    ReplyDelete
  21. MALIPO HAPA HAPA DUNIANI.........HAKUNA CHA REFA WALA NINI!

    HAO MAREFA MNAOWAPONDA NDIO WAMEWAFIKISHA SEMI FINAL. SIE ILITUKUWA TUCHEZE NA ARSENAL.

    LILE GOLI ILIKUWA NI POSITIVE PRESSURE FROM CHELSIKI

    WE ARE LOOKING FORWARD FOR A SHOWDOWN IN MOSCOW

    ReplyDelete
  22. nyie bwawa la maini hovyo kabisa timu yenyewe imelegea kama mbilimbi mnashindwa kufunga goli 4 ona sasa wamesawazisha mnatakiwa kufunga 2 kavu. sasa kama chumbani kwenu taa inawaka na mmejikwaa, mkienda chumbani kwa wenzenu na taa imezimwa si mtakata vidole vya miguu kwa kujikwaa? na msipongalia mtapigwa 4. Ingawa najua leo kazi tunayo Man U, lakini si mbaya fainali tunaenda na tutamaliza ubishi._bube

    ReplyDelete
  23. Good afternoon ladies and gentlemen, This is Captain John Terry speaking, on behalf of co pilot Frank Lampard, Chief of Staffs Didier Drogba and the rest of The Blues Crew, welcomes you on board, our destination is MOSCOW via Stamford Bridge. Have a Pleasant Journey.

    ReplyDelete
  24. Bwana Michuzi hawa www.spotistarehe.blogspot.com umewaona? mbona hawajitambulishi, wakirekebisha kidogo watafanya vizuri nawatumia mail inarudi kama wanasoma hapa message sent!
    Ihano KLIA

    ReplyDelete
  25. Kaka Michuzi we si ulisema kutuma picha basi

    Unapendelea eeeh.

    ReplyDelete
  26. Rise alichonga na William Hill akiwa nje,jamaa walimwambia ikiwa Ze Buluu wakiloa wangezawadia watu pesa mingi,sasa jamaa alipoona muda unayoyoma akaamua kutupia nyavuni kwake! Habari ndo hiyo

    ReplyDelete
  27. 93:54 Ashely Cole anarusha mpira kwa Mohammed Kalou.
    94:02 Kalou awazubaisha walinzi wawili na aporomosha krosi kwenye goli la Liverpool.
    94:04 John Anne Riise atikisa nyavu kwenye goli na kumwacha Pepe Reina akiwa kama mwali golini.
    94:06 Chelsea washereheka bao na kurudi kati tayari kuanza kipute kabla ya mchezo kumalizika.
    Refa angeweza kumaliza mchezo huku mpira ukiwa wavuni.
    Tatizo linakuja hivi:-
    Kama angemaliza bila kuweka mpira, watatanishi wa soka wangelihesabu bao la Chelsea hata bila mpira kuwekwa kati?
    Kwa refa kuondoa utata na kutaka mpira umalizike ndiyo apulize filimbi, ilikuwa jambo la busara na wala halihitaji ubishani.
    Kila mmoja anadai bao limefungwa dakika ya 95:00 mbona hawana ushahidi wa kweli kama nilitoa mimi hapo?
    Tatizo vyombo vingi vya habari na hata baadhi ya watangazaji hasa wa UK, wanataka Avram GRANT ang'olewe lakini ukweli halisi jamaa ana rekodi nzuri tangu achukue timu licha ya kwamba bado anabahatisha ushindi hasa kwenye mechi kubwa!
    Tujaribu kuwa wachunguzi wa mambo na siyo kufuata maneno ya waandishi na watangazaji ambao ni binadamu kama wewe. Wa UK wamekuwa WAMBEYA WAKUBWA na wanapigwa vita karibu ULAYA yote kwa uvumishi.

    ReplyDelete
  28. Na HIYO "NDIO HABARI" WANA WA BWAWA NLA MAINI.msikonde sana

    ReplyDelete
  29. SIKUTEGEMEA KAMA LIVERPOOL WATASEMA KUHUSU MAAMUZI YA REFA: HATA MWEZI HAUJAISHA TOKA WABEBWE NA MAREFA WALIPOCHEZA NA ARSENAL TAYARI WAMESAHAU? MNATAKIWA MJIFUNZE SASA KU-WALK ALONE,SI KUBEBWABEBWA.

    ReplyDelete
  30. We kaka mi nimekupenda tafadhali naomba tuwasiliane;
    kiezya@hotmail.com
    tafadhali kaka mich usinibanie post yangu.

    ReplyDelete
  31. HUYU MDAU KASHIKA NINI MAJI?... AAH HAPANA MBONA JICHO NYANYA? ITAKUWA NI MACHOZI YA SIMBA TU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...