hapa kila mtu mbabe. kila mtu anataka apite yeye kwanza. kila mtu hataki mwenzie aende...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kwa akili ya haraka haraka, kama kungekuwa na mistari inayoonyesha direction ya magari. Tatizo hilo lisingetokea!

    ReplyDelete
  2. Kwa staili ya 'mimi kwanza' watz tumijaliwa.
    Picha hii inaonyesha hali halisi ya maisha ya kila siku ya mtz: Nenda kwenye vituo vya daladala, inastaajabisha. (bahati mbaya mzee michuzi siku hizi hutumii dala dala,lakini naaamini hali unaielewa ilivyo). Kila mtu anataka apande yeye kwanza. Wenzetu hapo Kenya tu, achilia mbali sehemu zingine, wanapanga foleni hadi kwenye kupanda dala dala.Lakini wabongo, ee bwana eeh!,hadi nakosa maneno ya kuelezea. Tatizo la foleni Dar linachangiwa sana na hali hii pia. Kweli ni kama senene vile, watu wana'chomekeana', bara barabara zinaziba, halafu wanabaki wametumbubliana macho huku kila mmoja akiwa amekwama.
    Ni kwa spirit hiyo hiyo mtu anapewa uwaziri, akishapewa pesa za kuleta maendeleo ya kwenye huduma za jamii anatia ndani zote, tena kwa kuzipeleka ulaya, wadau wa nchi wanabaki wakipiga miayo!
    YaanimMaisha ya bongo ni kaazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  3. HABARI KUTOKA LEADS..THE GREAT BRITAIN

    MICHUZI BABA SASA SISI TULIO UGHAIBUNI USUSANI LONDON NA BABA LAO NEW YORK USA TUTARUDI VIPI KAMA MAISHA YENYEWE NDIYO HAYA? JUZI JUZI UMETUWEKEA PICHA ZA MAJI YAMEJAA KILA KONA YA JIJI KISA ETI MVUA ZINANYESHA KABLA YA HAPO ULITUAMBIA MASHIMOZZZ KILA PEMBE YA BONGO BARABARANI SASA UMEKUJA NA HII MPYA NA ZINGINE NYINGI TU ZA AJARI BARABARANI MIMI NIMEANGALIA KWA UNDANI NIKA ONA NI HERI NIFE HUKU HUKU KWENYE MAZIWA YA MGANDO NA MKATE KULIKO HUKO KWENYE VUMBI LA PILIPILI SIJUI MWENAZNGU KAKA YETU MICHUZI UNASEMAJE, NINAWEZA KUKUTUMIA MWALIKO UKAJA HUKU TUKAKUTAFUTIA KARATASI NA WEWE UACHANE NA MAISHA MAGUMU NJOO UBEBE BOX HUKU UKIWA NA MAISHA MATAMU NA KULA KUKU WENGI TU. PIA HUKU UTARUHUSIWA KUWA NA CHECK BOOK YAKO MWENYEWE, WATOTO WA KIZUNGU WENGI TU MIKAMERA IMEJAA KAZI KWAKO KUPIGA MIPICHA UIPENDAYO HATA YA UCHI WA MNYAMA KAZI KWAKO. KALIBU SANA LEADS THE GREAT BRITAIN

    ReplyDelete
  4. we mchangiaj wa tatu acha unafiki na kujifagilia,nakufahamu vizuri uish UK,unaish tandale na biashara zako za kubangaiza kariakoo,so ongea mambo ya muhimu,nilijua utatoa maon ya kuweza kusolve tatizo badala yake unaongea vitu vya kujisifu.
    mdau
    Chicago,USA

    ReplyDelete
  5. We mchangiaj wa 3,acha unafiki na kujisifu,nilijua utasaidia kwa maon namna ya kusolve tatizo we unajisifu,unaonekana muongo tu,so ongea vitu
    vya maana siyo kujisifu.
    mdau
    Chicago,USA

    ReplyDelete
  6. wanachojua matrafiki wetu ni kupiga mabao,mahali kama hapa ndio wanatakiwa,sio kukimbizana na vidaladala.Hivi angekuja trafiki mmoja pale akaondoka na leseni za hao jamaa wenye umimi mimi,na hiyo ikawa ndo style ya kuwakomesha wangerudia?

    Mdau,
    Afghanstan

    ReplyDelete
  7. Foleni kama hizi ni kawaida katika miji mikubwa hata huku majuu, msiwazingue wasiojua. Hii ni deadlock na dawa yake ni physical control, yaani kutumia Polisi wa trafiki kudhibiti upitaji wa magari eneo husika. Hutokea mara nyingi Brussel karibu na VUB ( Tiomflaan/General Jacqueslaan) saa za asubuhi ambapo taa hushindwa kudhibiti akili za madereva.

    ReplyDelete
  8. PART 1
    MICHUZI TAFADHALI CHONDE X2 BABA NAOMBA UENDE MWENGE KESHO ASUBUHII KITUO CHA KUENDEA POSTA THEN TULETEE NEPU NDO MJADALA UANZIE HAPO!!! ITS SAD VERY SAD USAARABU HATUNA KABISA WE HAVE TO START FROM SOMEWERE. NILIKUWA KWA HIYO SITE LAST YEAR FEBRUARY NILISHIKWA NA HASIRA SANA. KILICHONIUMA ZAIDI WATU WALOKUWAMO KWENYE HIYO DALADALA 70%WALIKUWA NA SUTI ZAO WANAFANYA KAZI CITY MITAA YA POSTA.SIYO MBURAHATI!! NAJUA MAMBO MENGI NI MAGUMU KUBADILIKA LAKINI HILI CAMON MICHUZI NAJUA LIKO CHINI YA MIGUU YAKO YOU CAN CHANGE JAMII.

    ReplyDelete
  9. part 11
    NILIKUWA VEKESHENI HAPO BONGO NDO MAANA NILIAMUA KUTUMIA DALADALA.PIA IT WAS NICE KUJICHANGANYA NILIFIKA POST MPYA CHA KUSHANGAZA SIKUPATA KADI HATA MOJA YA MJI WA DAR. HATUKO CREATIVE TUNADHANI WATALII WOTE WANAPENDA WANYAMA HOW WRONG?!! ANY WAY NIKAAMBIWA NTAPATA KWENYE DUKA LA POSTA MAMANGU MCHAGA IT WAS BALAA LILE DIRISHA LA NONDO LILIJAA WATU NA MHUDUMU MMOJA NA HAKUNA DISPLAY JASHO LIKANITOKA JUU HAKUNA FOLENI KILA MTU ANA HAKI YA KUHUDUMIWA AT THE SAME TIME. NIKATOKA NJE NIKANUNUA KARIBU ZANZIBAR THEN NIKAANDIKA IWISH YOU WERE HERE!!! NIKAPOST KWA NIWAPENDAO. ITS TRUE STORY NAOMBA UTULETEE HIZI SCENE TAFADHALI

    ReplyDelete
  10. Part 3
    jamani Dar jiji kubwa mtalii siyo lazima atoke nje mkazi wa arusha anaweza kuja bongo kutalii. mwanza na kwingineko. natoa tahadhari juu ya waosha vinywa wawezadai kwenu ni kwenu. yes iknow ndo maana nasema yote haya .tuanze na haya ambayo yako chini ya uwezo wetu kwanza.

    ReplyDelete
  11. Humu naona wadau, ni uk, usa. talebani kwa uchache. Tunataka maoni jamani! au mnaona hapa ndo mahali pa kutangazia mnapoishi. Weka maoni, mbio chomoka mambo ya mdau UK, USA, ni ulimbukeni au mnafikiri ndo tutaona maoni yenu ya maana sana.

    ReplyDelete
  12. we anonymous wa 7.53pm,ujue wadau kusema walipo sio ulimbukeni. ni kumhabarisha bwana misupu kwamba blogi yake ina mvuto na inasomwa pembe zote za sayari hii.
    kwa tarifa yako mimi niko Tobago

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...