Tarehe 17 Machi, 2008, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama Cha Wananchi (CUF) lilifanya kikao chake mjini Zanzibar ambapo lilipokea na kuridhia makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya CCM na CUF ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Siku hiyo hiyo, CUF iliwatangazia wanachama wake na Watanzania kwa jumla matokeo ya kikao hicho cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia, mjini Zanzibar.
Hiyo ilikuwa ni hatua kubwa na muhimu kutekelezwa na upande wa CUF baada ya vyama vyetu viwili kukubaliana kuwa viwasilishe makubaliano hayo kwa vikao vya juu vya maamuzi vya vyama vyetu ili kuyaridhia kabla ya kutiwa saini. Baada ya CUF kutekeleza wajibu wake, yalikuwa matarajio na imani yetu kwamba na upande wa CCM nao ungefanya wajibu wake.
Kwa mshangao na masikitiko makubwa, jana tumepokea Tamko la Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuhusiana na mazungumzo ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar ambalo kimsingi limeyakataa makubaliano yaliyofikiwa na Kamati zetu mbili.
CCM imeamua kufanya usanii wa kisiasa kwa kutumia lugha ya mzunguko, ya ubabaishaji na ya upotoshaji kwa lengo la ama kuendelea kurefusha muda hadi mwaka 2010 au kuyakataa makubaliano ambayo wajumbe wake wameshiriki kuyaandaa katika miezi 14 ya mazungumzo kati ya vyama vyetu viwili.
Hali hiyo iko wazi kwa sababu mbili kuu zifuatazo:
CCM imetamka ‘kuyakubali kimsingi’ mapendekezo yaliyowasilishwa na Kamati ya chama hicho inayoshiriki mazungumzo lakini wakati huo huo inazungumzia marekebisho ambayo inataka yafanywe na hivyo kuiagiza Kamati yake kukutana na wajumbe wa CUF ili kuyajadili marekebisho hayo.
Kwanza, CCM haikutaja ni maeneo gani inataka yafanyiwe marekebisho. Pili, hoja hii inashangaza kwa sababu wajumbe wa Kamati ya Mazungumzo kutoka upande wa CCM walikuwa wakiwaarifu wajumbe wa Kamati kutoka upande wa CUF kwamba wao walikuwa wakiwasilisha taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vikao vya chama vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa na pia kwa viongozi wao wa juu, Rais Jakaya Kikwete na Mheshimiwa Amani Karume, na kupata maelekezo na miongozo inayohitajika. Hata taarifa ya karibuni kabisa ya CCM iliyokuwa ikikanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba Mheshimiwa Amani Karume si kikwazo cha kufikiwa makubaliano ya muafaka iliweka mkazo na msisitizo kwamba katika kila hatua, viongozi hao wameshauriwa ipasavyo. Hatua hii ya mwisho ilikusudiwa kubariki makubaliano hayo yaliyokuwa yakifikiwa hatua kwa hatua na siyo kufungua mjadala mpya kupitia duru mpya ya mazungumzo.
CCM imekuja na hoja mpya kwamba iwapo mapendekezo haya yatakubaliwa, yatakuwa yanaleta mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala katika Zanzibar na hivyo yanapaswa kuridhiwa na wananchi wenyewe kwa njia ya kura ya maoni.
CCM kuleta hoja hii ni kulifanyia mzaha jambo kubwa linalohitaji umakini wa hali ya juu kwani linagusa mustakbali wa taifa letu. Muda wote wa mazungumzo ambayo yamechukua miezi 14 na yakiwa yamehusisha vikao 21, wajumbe wa Kamati ya CCM wanaoshiriki mazungumzo hawakuleta hoja hii ya kura ya maoni. Kinachosikitisha zaidi ni kuwa tofauti na ilivyoelezwa, pendekezo la kutaka kura ya maoni halikuwa limeibuliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM bali lilikuwemo katika Taarifa ya Kamati ya CCM inayoshiriki mazungumzo likiwa ni pendekezo walilotaka liridhiwe na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa. Hivyo, ni wazi liliandaliwa mapema kutokana na kile Kamati hiyo ya CCM ilichokiita “kuipiku CUF katika ubunifu wa kujenga”. Kitendo cha Kamati ya CCM kuwasilisha kitu kipya nje ya makubaliano yaliyofikiwa ni upotoshaji mkubwa wenye lengo la kulifanyia usanii wa kisiasa suala kubwa kama hili linalogusa maslahi ya taifa na watu wake moja kwa moja. Na iwapo pendekezo hilo lina nia njema ya kuwashirikisha wananchi, kwa nini wajumbe wa Kamati ya CCM wasiliwasilishe katika vikao vya mazungumzo na badala yake wakaamua kuliingiza kama mtego wa kisiasa wenye lengo la “kuipiku CUF”?
Hoja nyengine ni kwamba kura ya maoni hiyo itaendeshwa na chombo kipi na kwa utaratibu upi hasa ikitiliwa maanani tayari CCM na CUF wamekubaliana kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura vina matatizo ya msingi ambayo yanahitaji kurekebishwa? Ni vipi basi Tume hiyo chini ya Daftari bovu liliopo itaweza kuendesha kura ya maoni ambayo itakuwa huru na ya haki?
Sisi tunaona suala hilo ni mbinu chafu tu yenye lengo la kuendelea kupoteza muda ili makubaliano yaliyofikiwa yasiweze kutiwa saini na utekelezaji kuanza. Kwa lugha yao CCM waliyoandika katika waraka wao ni njia ya “kuipiku CUF” na kamwe haikusudiwi kupata maoni ya wananchi.
Kwa msingi huo CUF haikubaliani na hoja hizo zote mbili.
Ni lazima tukiri kuwa tumeshtushwa sana na kiwango hiki cha CCM kulifanyia usanii wa kisiasa suala kubwa kama hili. Lakini pia tumepata faraja kuwa Watanzania sasa wameweza kujua ni nani kati ya CCM na CUF asiyeitakia mema nchi hii. Wamejua ni nani kati ya CCM na CUF asiyetaka amani na utulivu katika nchi hii. Wamejua ni nani kati ya CCM na CUF asiyetaka siasa za maelewano na mashirikiano katika nchi hii.
Sasa ni wazi kwamba CCM iliingia katika mazungumzo haya ikiwa haina dhamira ya kweli na ya dhati ya kuupatia ufumbuzi wa kweli mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Inaonekana lengo pekee la CCM katika mazungumzo haya lilikuwa ni kuwahadaa Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwa kujidanganya kwamba wangeweza kuidhibiti kisiasa CUF kupitia utaratibu wa kuwapa matumaini ya uongo (strategic engagement) na kuyarefusha mazungumzo hayo kadiri inavyowezekana hadi kipindi kinachokaribia uchaguzi mkuu ujao pasina kuchukua hatua zozote za maana zenye kulenga kutoa ufumbuzi wa kweli wa mpasuko uliopo. CCM imeonesha wazi wazi kuwa haiitakii mema Tanzania yetu na wala haitaki kuona umoja wa kitaifa na utulivu wa kudumu vinapatikana Zanzibar ambayo ni sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano.
Kwa upande mwengine, Watanzania wote na jumuiya ya kimataifa ni mashahidi kuwa CUF imefanya kila liliomo katika uwezo wake kuinusuru hali tete ya kisiasa Zanzibar isichafuke. CUF imechukua kila juhudi kuona mazungumzo haya yanafanikiwa. Imetoa kila ushirikiano unaohitajika kwa CCM na hata kuachia madai yake makuu (kutoa ‘concessions’) ili kuyanusuru mazungumzo hayo na kuyafanikisha.
CUF imeonesha ustahamilivu, ustaarabu na uelewa mkubwa katika mazungumzo haya. Tumeweza kukubaliana na CCM kwa kila hatua tuliyoombwa tuwe na subira ili kupisha mambo kadhaa ya kisiasa yapite. Mara nyengine, hata bila ya kutuomba, sisi wenyewe tumeonyesha uelewa na kuwapa nafasi pale yalipoibuka matukio ya kisiasa ambayo hayakutarajiwa na ambayo tulihisi yanahitaji tuwape muda wenzetu. CCM haionekani kujali au kuthamini juhudi hizo na imeamua kuzipiga teke.
Kama tulivyowahi kusema, hatukufanya hivyo kwa sababu CUF ni dhaifu kisiasa kama ambavyo CCM wangependa kujidanganya. Tulifanya yote hayo kwa sababu tunaongozwa na dhamira njema ya kuhakikisha nchi yetu inabaki katika hali ya amani na utulivu huku tukiamini kwa dhati kwamba mazungumzo ndiyo njia pekee ya kistaarabu ya kumaliza tofauti au migogoro ya kisiasa na kijamii. Lakini ni lazima tusisitize kuwa mazungumzo yenye lengo hilo ni lazima yawe mazungumzo makini yanayoongozwa na utashi wa kweli wa kisiasa uliojengeka juu ya nia njema na kuheshimiana baina ya pande zinazohusika. Hilo limekosekana kwa upande wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Kufuatia misukosuko iliyoyakumba mazungumzo haya mwaka jana, Rais Kikwete, alitoa taarifa kwa umma tarehe 14 Agosti, 2007 akiuomba upande wa CUF ukubali kuendelea na mazungumzo na akiwahakikishia Watanzania kuwa angechukua hatua kuona yanakamilishwa na yanafanikishwa. Wakati akiwahutubia Mabalozi wa nchi za nje wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya, mapema mwaka huu, Rais Kikwete aliwaeleza kwamba mazungumzo yamefikia ukingoni na kwamba karibu suala la mpasuko wa kisiasa Zanzibar litakuwa historia. Kauli hiyo ilipokewa kwa matumaini makubwa na wananchi ambao wamekuwa wakifuatilia kwa makini kila hatua ya mazungumzo yetu. Ni bahati mbaya kwamba Rais Kikwete ameyaangusha matumaini hayo ya Watanzania kama ambavyo ameyaangusha matumaini yao katika masuala mengine yote aliyowaahidi wakati anaomba kura na anaingia madarakani.
CUF imevunjwa moyo sana na Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM. Imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa nchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa imetetereka sana. Kitendo cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM chini ya Uenyekiti wake kukataa kupitisha makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya CCM na CUF na badala yake kuja na hoja mpya za ajabu ajabu zenye lengo la “kuipiku CUF” kisiasa kunamwonyesha Rais Kikwete ama hakuwa mkweli na mwaminifu tokea mwanzoni na kwamba alikuwa akifanya usanii wa kisiasa wakati alipotangaza kuwa anasononeshwa sana na mpasuko wa kisiasa Zanzibar au ni kiongozi dhaifu asiye na udhibiti wa chama anachokiongoza. Yote mawili hayampi sifa za kiongozi ambaye nchi inamhitaji inapopita katika vipindi vigumu.
Kama tulivyofanya mwaka jana, ni vyema tumkumbushe tena Mheshimiwa Jakaya Kikwete kauli yake mwenyewe aliyoitoa wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 16 Septemba, 2003 wakati anafungua Mkutano wa Kumi na Moja wa Hali ya Siasa Tanzania ambao ulihusu ‘Udhibiti na Utatuzi wa Migogoro’, pale aliposema:
“…[N]aelewa kuwa utaratibu wa kung’amua dalili za migogoro hauwezi kuwa na manufaa kama haukuambatana na vitendo vya haraka. Taarifa za dalili za uendelezaji wa migogoro zinapopatikana zitakuwa hazina manufaa katika uzuiaji wa migogoro hiyo kama zitashughulikiwa kwa njia ya mlolongo wa uamuzi wa kirasimu ambao unaweza kuchelewesha utekelezaji hadi migogoro inapotokea. Kwa hiyo ni wazi kuwa upatikanaji wa taarifa za dalili za migogoro unakuwa wa maana katika uzuiaji wa migogoro kama mara zipatikanapo, zinatafsiriwa kwa vitendo. Mtiririko wa hoja hapa unapaswa kuwa “dalili za mwanzo kujumlisha na vitendo halisi ni sawa sawa na uzuiaji wa migogoro.” Ili haya yatokee unahitaji kuharakisha au kurekebisha utaratibu wa utoaji wa maamuzi ili dalili za mwanzo ziweze kutafsirika kwa vitendo haraka iwezekanavyo.”
Maamuzi ya Chama chake kupitia kikao alichokiongoza yeye mwenyewe akiwa Mwenyekiti wake hayaonyeshi kuwa anayazingatia haya aliyowaasa wenzake mwaka 2003 maana maamuzi ya Halmshauri Kuu ya Taifa yanawakilisha hasa “mlolongo wa maamuzi ya kirasimu” ambayo kama alivyosema hayawezi kuwa msingi wa utatuzi wa mgogoro. Inasikitisha zaidi kwa Rais Kikwete kuwatangazia Watanzania na ulimwengu kuwa amefanikiwa kuwakutanisha Rais Mwai Kibaki na Mheshimiwa Raila Odinga wa Kenya na kufanikisha kufikiwa kwa makubaliano kati ya ODM na PNU nchini humo lakini anashindwa kulifanikisha hilo nchini mwake ndani ya chama anachokiongoza mwenyewe na kati ya CCM na CUF. Rais Kikwete anaona fakhari kuwa Tanzania imeongoza Jeshi la Umoja wa Afrika (AU) katika operesheni ya kijeshi iliyopewa jina la “Operesheni Demokrasia” kisiwani Anjouan, nchini Comoro lakini ameshindwa kuongoza operesheni ya kisiasa ya kusimamisha demokrasia visiwani Zanzibar.
Rais anapaswa ajue kuwa heshima ya ofisi yake na uadilifu wake binafsi ameutia doa kubwa kutokana na kushindwa kusimamia kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa kwa Watanzania kupitia hotuba yake ya Desemba 30, 2005 Bungeni na pia ahadi aliyoitoa na kuirejea mara kadhaa kwa marafiki wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa katika ziara zake za nje ya nchi kila mara pale alipoulizwa kuhusiana na mgogoro wa muda mrefu wa kisiasa Zanzibar.
MSIMAMO WETU:
Chama Cha Wananchi (CUF) hakiko tayari kushirikiana na CCM kuwafanyia Watanzania usanii wa kisiasa. Huu sio utaratibu wa CUF katika uendeshaji wa siasa. Kwa CUF, siasa si proaganda zilizopitwa na wakati bali ni utumishi wa dhati na uliotukuka kwa umma uliowaamini viongozi wake. Kwa msingi huo, CUF haitakubali kurejea katika mazungumzo kwa utaratibu inaoutaka CCM.
CUF kinakitaka CCM kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya vyama vyetu viwili na endapo kweli Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho “ imeyakubali kimsingi” makubaliano yaliyofikishwa kwake kama ilivyosema taarifa yake, basi kikubali kutia saini makubaliano hayo na utekelezaji wa yaliyokubaliwa uanze mara moja.
Kinyume na hayo, CUF inatoa wito kwa marafiki wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti, za uhakika na za haraka kuingilia kati suala hili ili kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa yanatiwa saini. Baada ya Tanzania yenyewe kushindwa katika utatuzi wa mgogoro wake huu wa muda mrefu, sasa ni wakati muafaka kwa Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati kwa kuchagua Mpatanishi wa Kimataifa anayeheshimika kuja kuyasimamia hadi kuyafikisha ukingoni kwa kuhakikisha makubaliano ya dhati yanafikiwa yatakayotoa ufumbuzi wa kweli na wa haki wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar.
CUF inatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuepuka fedheha iliyoipata katika nchi nyengine za Kiafrika ambazo iliziachia hadi hali ikachafuka na ndipo ikaingilia kati. Hali ya Zanzibar ni mbaya. Ilitulia kwa sababu ya matumaini ya Wazanzibari na Watanzania kwamba mazungumzo ya CCM na CUF yataleta suluhisho la utulivu na umoja. Makubaliano yaliyofikiwa yanapokosa uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuyakamilisha, yanahitaji kuona jumuiya ya kimataifa inaingilia kati kwa hatua za wazi na madhubuti kuinusuru Zanzibar na Tanzania isitumbukie kule nchi nyengine za Kiafrika zilipotumbukia.
Wakati tunawashukuru kwa dhati viongozi wa vyama vyengine vya siasa, viongozi wa dini, taasisi na jumuiya za kijamii, mabalozi wa nchi za nje wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania na vyombo vya habari hususan magazeti huru kwa mchango wao mkubwa walioutoa na ambao ulisaidia kuyafikisha mazungumzo hadi hatua ya kukamilishwa, CUF tunatoa wito tena kwao kuendelea kutoa ushirikiano wao na kutimiza wajibu wao kuona mgogoro huu unamalizwa kwa njia za amani na za haki.
CUF inawataka wanachama na wapenzi wake pamoja na Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki wakijua kuwa CUF iko upande wa amani, ukweli na haki na siku zote upande wa amani, ukweli na haki utashinda.
Kwa jinsi inavyoyachezea masuala mazito yanayohusu maslahi ya taifa kama ilivyodhihirika kwa mambo yote makubwa yaliyojitokeza hivi karibuni, ni wazi kuwa CCM imepoteza uhalali wa kuongoza nchi na wakati sasa umefika wa Watanzania kuchagua chama makini kitakachoipa Tanzania uongozi makini unaohitajika.
HAKI SAWA KWA WOTE
SEIF SHARIF HAMAD
KATIBU MKUU – CUF
Dar es Salaam
01 Aprili, 2008
Madaraka ni matamu sana.
ReplyDeleteAh mie si mwanasiasa, lakini mazingira nliokulia yananifanya niijue siasa, haswa siasa ya visiwa vya zanzibar! "Kule Pemba wanasema usipoiingia siasa basi siasa itakuingia wewe..." Kwa hiyo nathubutu kujiita gwiji wa siasa ya zanzibar tu. Kwa kweli binafsi nashindwa kumuelewa Maalim seif, sababu bila shaka yeye ni mweledi wa siasa kuliko mimi..!Siasa ya zanzibar ni siasa ya inayaoendeshwa kwa historia, ni siasa ya walionyimwa maendeleo na fursa ya utawala (wapemba)ambao wengi asili yao ni wamanga wa oman na pesria na waliona maendeleo na utawala waunguja ambao wengi asili yao ni bara!Ndio! Kilichopo zanzibar hivi sasa ni matunda ya mbegu ya chuki iliyopandwa tangu 1964, sasa watu wanavuna walichokipanda! Ndio aliyeko madarakani amefanya mengi yamadhila na uovu juu ya huyo anaetaka madaraka sasa. Jee unafkiri atakuwa tayari ampe nafasi ili naye alipiziwe! Thubutu nanikasema mkuki kwa binaadamu... siku zote mkuki kwa nguruwe tu! Sasa basi siasa ya zanzibar imebaki kuwa ni chuki na visasi, na katika hali hiyo kamwe hakuwezi kuwa na muafaka, hakuna tofauti kwa muhutu na mtusi, muizrail na mpalestina, hata ukiona kumetulia ujuwe ni moshi wa kifuu wakati wowote moto utawaka!
ReplyDeleteKinachonifanya nisimuelewe maalim, ni kujifanya anakili za kuku, yaani kuku unaweza kumfukuza sasa hivi asile mpunga wako uliouanika, lakini baada ya dk 5 kashasahau anakuja tena! Sasa seif hajifunzi kutokana na historia, kwani ni miafaka mingapi imefikiwa, tena na mengine kutiwa sign mbele ya wawakilishi wa umoja wa mataifa (Chief Anyauku), halafu mwishowe ikaishia wapi? HIvi hakumbuki si ni mwaka juzi tu au?
CCM zanzibar inaendeshwa kwa kiburi na jeuri! Siku zote mwenye kiburi na jeuri hana muafaka na mtu, sababu kwenye muafaka lazima kila mtu akubali kupungukiwa, Kanuni ya mtu mwenye jeuri na kiburi huwa simwenye kukubali kupungukiwa hata chembe juu ya yule anaeshindana nae! Seif alitakiwa alijue hilo kabla ya kwenda kwenye muafaka.
Seif ilitosha kuamini kwamba muafaka wa serkali ya mseto ni ndoto tena ndoto ya ya mchana wajuwa kali, kanuni inaonyesha yoyote mwenye kiburi na jeuri ´huwa hakubali kulipinda aliloahidi au kulisema, CCM zanzibar walisema kitaambo "...tangu lini mawe na mchele vikapikwa mseto..." wakaendelea kusema "...watasema mpaka watachoka kelele za chura tu hizo, hakuna mseto wala msambwija"
(msambwija ni mchanganyo wa muhogo na ndizi au tuite mseto wa muhongo na ndizi)
Sasa mimi binafsi si mlaumu kikwete, huenda Rais alikuwa na nia mzuri, au anania mzuri, lakini lazima tukubali CCM sio ya kikwete, yeye mwenyewe amewekwa anaendeshwa na waliomueka, na kwakweli ambae si mzanzibar ni vigumu kuijuwa siasa ya zanzibar kiundani! Wanasema siri ya mtungi...!Sasa kwa kutokuijuwa kwake siasa ya zanzibar kikwete alidhani inaweza kutatulika kwa muafaka! Lakini ilipokuja ishu sirias amewaona mahafidhina kutoka zanzibar kule Butiama, bilashaka walikuwa tayari wote kurudisha kadi za chama kama Kikwete angekubali muafaka wa serkali ya mseto, sikuwa kwenye kikao lakini akili yangu yaniambia hilo! Sababu wanaogopa huenda walichokifanya na wao watafanyiwa...! Ndio! kanuni inavyonyesha mtendaji siku zote hujihadhari kutendewa
Kwa maoni yangu CUF bora waaamuwe yaishe tu, wasirudi kwenye meza ya mazungumzo kwani CCM wana "bytime" zaidi CUF watakuwa wanajipotezea muda wakuandaa mikakati ya 2010. Lakini pia CUF wasithubutu kuwaambia wananchi (wazaznibar) waandamane eti kuipinga CCM kwani nnachojuwa ni kuwataftia wananchi matatizo ya kuumizwa na kuuliwa bure kwa risasi, na mwisho wa siku hakuna linalopatikana, CCM wamejiandaa kwa hilo wako "very proactive" huwa hawaandiki moja mpaka wajuwe 2 na 3 zinakaaje! Ndo maana wamepeleka jeshi commoro nisehemu ya mazoezi.
Kilicho baki CUF na wapinzani kwa ujumla ni kupanga mikakati ya 2010, wananchi kujitaftia riziki zetu, wapemba jueni hakuna marefu yasiyo na ncha hata kama si wewe basi japo mjukuu wako atakujaishi wakati CCM haipo tena madarakani!
"ROME HAIKUJENGWA SIKU MOJA"
Bablii
Waheshimiwa tumewasikia,mkae mkijua kuwa tuna akili za kutosha kuchambua pumba ni zipi na mchele ni upi.Tunataka pia kusikia kutoka kwa CCM, ni mpaka lini wako tayari kutufanya kama hamnazo namna hi ??
ReplyDeletehongera baba tangaza mkwanja sie tutie timu mpaka Kofi aje na kwetu.Tumechoka kuburuzwa.
ReplyDeleteHaya UK hiii ndi CCM yenu tuelezane jamani kuliko kufungua matawi. Uduwanzi huu hauko USA.
ReplyDeleteCCM chupi imebana.
ReplyDeleteJe tumuite Koffi Annan au Thabo Mbeki. Lakini nadhani Mwai Kibaki atasuluhisha vizura kwani anajua fadhila za CCM pale chupi ilimpombana si siku nyingi.
Kwa upande mwingine msuluhishi mzuri nadhani ni rais wa Comoro kwani pia anatoka visiwani. Kama wote hawafai wanitafute mimi kwani kila mtu anataka ulaji wa kuwa katika kamati ya mwafaka kwani posho yake ni njenje na wanalipwa kwa dola.
Holla at yoyr boy JK najua Ndevu kakulia kidedea.
michuzi hili sio gazeti.. bwana mihabari mirefu hivyo .inatumalizia nafasi ,tunataka picha..bwana
ReplyDeleteToo long to read, watu wapo busy, go straight kwenye point. weka in bullet form, haya ndio mapendekezo bang bang
ReplyDeleteUkianza na adisa za baba na rosa wakaenda, watu wanaskip na kusema another politician. I hope kwanza Maalim ataawaachia wenzie wagombanie sababu technical ameshashindwa more than 3 times.
Kauli mbiu ya CUF ni "Haki sawa kwa wote" kama walivyomalizia kwenye hili tamko.
ReplyDeleteKauli hii ina maana ya haki sawa kwa CUF,CCM na Wananchi wote wa Zanzibar.
CCM na CUF wameshapata haki yao ya kujadili na kukubali huo muafaka.Ili kukamilisha mduara wa haki sawa kwa wote sasa ni zamu ya wananchi kuukubali au kuukataa huo muafaka wa serikali ya mseto kwa njia ya kura za maoni.
Kuwakatalia wananchi wasipate fursa ya kura ya maoni haitakuwa "Haki sawa kwa wote" bali itakuwa haki sawa kwa CCM na CUF peke yao! Na nchi hii sio yao peke yao! kuna wananchi wenye nchi!
CUF iache porojo isimamie suala la haki sawa kwa wote liwafikie pia wananchi kwa kuwapa nafasi ya kupiga kura ya maoni.Tamko la CUF naliona kama porojo tu za mpiga filimbi wa hamelini zisizosikika vizuri kwenye spika za demokrasia.
Koloboi@yahoo.com
CUF kuweni na subira, Zanzibar siyo ya CUF na CCM pekee yao. Umakini wa hali ya juu unhitajika ili kupunguza malalamiko kama yale yaliyopo kwenye muungano ambao ninyi wenyewe mnadai ni wa Karume na Nyerere.
ReplyDeleteSerikali ya umoja Zanzibar ni lazima ili kuundoa unyanyapaa uliopo kati ya waaunguja na wapemba ila ni vivuri ukatafuta umoja ulio imara utakaodumu bial kuvunja sheria. Tulizeni mzuka, mtaingia tu madarakani
CCM imechemsha big time...
ReplyDeleteKama ilivyotokea hoja ya BUZWAGI, RICHMOND NA EPA, hapa pia yatawakuta yale yale yaliyowapata.
Ni wakati wa kuanza kufikiria kwa kutumia utashi walio nao, si kushabikia tu chama bila kufikiria.
Hivi kupeleka maamuzi ya muafaka kwa wananchi ndio hoja waliokua wanaijadili kwa miezi 14 na ndo maamuzi waliyofikia?? hawa wa heshimiwa? mimi ningeshauri wafanye kile walichokubaliana au vipi Maalim na makamba?????????????
ReplyDeleteKoloboi@yahoo.com bin kibatari na kibatari hakifanyi kazi bila kibiriti (Chibiriti) wewe unaposema Tamko la cuf ni sawa na kelele za mpigafilimbi wa hemelini, kumbuka mpigafilimbi huyo aliishiaje hivyo uwe mwangalifu na kejeli zako kwani mzarau biru hubiruka yeye.
ReplyDeletemi CCm nawajua fika,
ReplyDeleteHapo kama ni mpira unarudishwa kwa wananchi,
Halafu wananchi wakipiga KURA ZA MAONI yanakua yale yale ya mwaka 1995, 2000 na 2005,
CCM wana uwezo mkubwa wa ku-manipulate figures za kura,
Hata Karume alivyoshinda??!!2005(kama ni kweli), alidai "ELECTION IS A GAME OF NUMBER".
Hapo hata jamaa zangu wa zanzibar wakipiga kura za maoni, tutegemee matokeo yataingiliwa tu na kina KIVUITU wa Bongo,
Cha msingi muafaka ufikiwe mapema tu, na tamko liwekwe wazi,
Kwenye kura za maoni tutaibiana tu,
Nimewasilisha,
Pliiiiiz Michuzi usiibanie hii
CCM is employing ''delaying tactics'' ... Wanajua fika kuwa hiyo referendum itachukua kama miaka miwili na hiyo itakuwa 2010 na tayari Uchaguzi mwingine....
ReplyDeletekaka misupu unatuboa na long story za ujinga sisi tunataka picha sio habari wakasome kwenye site zao za ccm na cuf huko weka picha bwana,bongo tambarare
ReplyDeleteWe have to agree that we do have a 'Constitutional Crisis' in this country.I am not sure if there s anything like an Independent Constitutional Court in this country,tofauti kabisa na hizi mahakama zingine!An Independent Electoral Commission?Hapa CCM imechemsha wazee.Vijana maamuma wasidandie siasa wasizozijua malengo yake.Kaa pembeni jifunze kisha tafakari.Mgogoro uliopo hapa ni unahusu mgawanyo wa madaraka baina ya vyama viwili vya siasa vilivyo shiriki uchaguzi mkuu na kupata ushindi mkubwa kwa kupata wabunge wengi zaidi.Kwa hiyo wananchi walishatamka katika uchaguzi huo watapendwa waongozwe na chama kipi cha siasa.Itakapo tokea vyama viwili vikapata ushindi sawa au uliokaribiana sana ni juu ya viongozi wa vyama hivyo kukubaliana kuhusu muundo na mfumo wa mgawanyo wa madaraka katika kuiendesha nchi kupitia serikali itakayo undwa na pande zote mbili.Kwasababu upande mmoja tu haukupata nguvu ya kura za wananchi kuweza kuunda serikali peke yake,lazima pawepo na mseto.Kuweko kwa serikali ya mseto ni moja tu ya suluhu ya mgogoro wa Zanzibar.Yamekuwepo malalamiko kuhusu kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi pamoja na Daftari la wapiga kura hai lililo hakikiwa na vyama vyote viwili vya siasa.Pamoja na utaratibu mzima wa kuendesha uchaguzi ulio wazi na jinsi ya kutangaza matokeo ya uchaguzi bila kupika matokeo ya kugushi.Kwenda kutafuta kura ya maoni kuhusu mgogoro huo wakati huu baada ya vikao chungu nzima katika kipindi kisicho pungua miezi 14 na katika kila hatua maafikiano yalifikiwa kabla ya kwenda hatua ya mbele zaidi,TUNASEMA HIVI KWAMBA HIYO NI JANJA YA NYANI.NA KWA BAHATI MBAYA SANA KATIKA SUALA HILI LA ZANZIBAR KILA MTU NI NYANI.Walikolala wao ndiko sie tulikoamkia jana yake.Tusigeuzane watoto wadogo.Serikali ya Mseto imeshindikana CUF wafanye kila liwezekanalo kupitia Umoja wa Mataifa na Balozi za Nje ili kusudi,ama yaliyokubalika katika muafaka pande zote mbili zitiliane saini mbele ya Mpatanishi wa Kimataifa mwenye baraka ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,na yaliyobakia yaachiwe Uchaguzi Mkuu uamue AU Uchaguzi Mkuu uitishwe mara moja bila ya kusubiri 2010 ili wananchi wa Zanzibar waweze kuchagua viongozi wao kwa njia ya kura halali na siyo ya kupikwa kwa kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Daftari la Wapiga Kura lililo hakikiwa na pande zote mbili,na kuwepo na utaratibu ulio wazi,huru na wa haki katika kusimamia uchaguzi wenyewe pamoja na kutangaza matokeo ya uchaguzi, AU Kura ya maoni ifanyike kuhusu suala zima la Muungano na Mfumo wake.Ieleweke hapa hakuna anayepinga kuwepo kwa Muungano.Hoja hapa ni Muungano gani utakao leta tija na maendeleo haraka zaidi kwa pande zote mbili.Ikineemeka Zanzibar,Bara nayo pia itaneemeka.Ikineemeka Bara,Visiwani nako pia wataneemeka.Sisi sote ni kitu kimoja.Lazima tukubali kwamba Mfumo tulionao hivi sasa haufai.Kama ulifaa mwaka 1964 katika hali ya dharura,lakini siyo sasa mwaka 2008 wakati nchi ikiwa imetulia na ina fuata utawala wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa.Kamati za CCM zisijisahau zikachukua na kufanya MAJUKUMU YA BUNGE!Wakati huo umekwisha.Hata katika Bunge ambalo litakuwa na wabunge wengi zaidi kutoka CCM maamuzi yote nyeti kitaifa lazima yafanyike kwa KURA YA SIRI YA KILA MBUNGE BILA YA KUSHINIKIZWA KICHAMA!Lazima kila Mbunge atangulize UTAIFA WAKE KWANZA ndipo tutaslimika kitaifa na vyama pia vitasalimika.ACHENI SIASA ZA KITOTO.CUF msimamo ni uleule tuone CCM itafanya nini!Marekebisho katika KATIBA,Tume Huru ya Uchaguzi,Daftari jipya la Wapiga kura lililo hakikiwa na Vyama vyote vya siasa au wawakilishi wao VINGINEVYO Uchaguzi wa 2010 NI NDOTO!tujue moja tu kwamba CCM itatawala milele.
ReplyDeleteMichuzi hebu tuambie is it true that Zanzibar hali ni mbaya kiasi hicho?
ReplyDeleteThe whole shit seems to be very intimidating... CUF watisheni CCM. Angalieni tu isiwaguse raia wa kawaida....
Wasiwasi wangu hatuchelewi kuwaona CUF huku ughaibuni wakishinikiza Tanzania isipate misaada, ilhali wanaoumia ni wabongo wakawaida. Ndo upinzani wa bongo huo...
Ila CCM nao wamezidi.... Washajiona miungu watu na kwamba wao tu ndo wateule wa kuitawala Tanzania....
tumeshachoka na siasa ya vyama vingi haina mpango zaid ni ugomvi,chuki, mauaji na majungu na kutuzidisha umaskini ,kuleta maendeleo sio kukaa madarakani tu mnaweza kuchangia kwa kuingia bungeni,baraza la wakilishi kwa kutoa hoja zenu kujadiliana kwa kushindana ktk kuleta maendeleo ya nchi,na pia kushirikiana na jumia za mataifa au nchi tofauti ambazo wanataka kuisaidia nchi yetu sasa nyie mngelikuwa mnashindana kwa kuleta maendeleo ya nchi yenu,kwa mfano ccm wameengeza mshahara 90% na nyie cuf mnajitangaza kuwa mnatengeneza barabara,kwani hata ukiingia cuf madarakani ukawa rais hakuna geni umaskin uko palepale na chuki kuzidi,kikubwa kueni wamoja kwa kujadiliana na kushindana kwa kuleta maendeleo ya nchi. kila chama kinaomba msaada wake kwa jinala chama chake hapo ndio kushinda kwa kuleta maendeleo ya nchi,sio kugoma na kuzuia misaada na kutukanana wewe mpemba weee na wee muunguja hio sio siasa kwani ukiangalia zaid mpemba nani na muunguja nani mtanganyika nani sote ni ndugu na tukamatane,tupendanekwa kuleta maendeleo ,tunachokitaka nyie ccm na cuf au kwa ujumla vyama vyote vya upinzani ni maendeleo ya nchi yetu ,amani, utulivu na furaha sio fujo.
ReplyDeleteSeif Sharif ni vyema utambue kuwa ni vigumu kwetu kuelewa kama malalamiko yako yana msingi iwapo wewe utaendelea kukubaliana na Makamba kuwa mapendekezo ya muafaka huo yawe siri. Sasa hatujui kama wajumbe wa NEC wako sahihi kuyafanyia marekebisho mapendekezo hayo au lah.Tuwekeeni hadharani mapendekezo hayo,yanatuhusu watanzania wote.
ReplyDeleteHalafu Seif unapomtupia lawama Rais Kikwete unakuwa "too political",sasa wewe ulitaka Kikwete afanye nini zaidi ya kuyapeleka mapendekezo hayo NEC kama katiba ya chama chake CCM inavyotaka.Au unamshauri asiheshimu katiba ya CCM?
MI SI MWANA CCM WALA CUF ILA WOTE HAWANA JIPYA CUF WANA NJAA CCM MAFISADI,HAKUNA MUAFAKA KATI YA MTU NYEWE NJAA NA FISADI
ReplyDeleteZEMARCOPOLO,
ReplyDeleteUNAJUA TATIZO HAPA KWA CUF NI UBINAFSI, HIYO TAARIFA YA CUF NI IMEJAA MAWAZO BINAFSI YA MAALIM SEIF AMBAYE HUPENDA KULAZOMISHA KILA JAMBO ALISEMA KUWA NI LACUF WOTE NA HATA MAAMUZI. SASA ANADHANI NA KIKWETE NAYE ATAKUWA ANAJIFANYIA MAAMUZI KAMA ANAVYOFANYA YEYE.
JAMBO LINGINE SISI WAZANZIBAR WENGINE TUSIOKUWA CUF WA CCM TUMEFARIJIKA SANA KUONA KUWA HILI JAMBO LINARUDISHWA KWA MAAMUZI YA MWISHO KWA KUWASHIRIKISHA WANANCHI WOTE BILA YA KUWA NA UBAGUZI WA VYAMA VIWILI TU. SIE TUSIOKUWA CUF WALA CCM TUMEPIGA KELELE SANA KUWA TUSHIRIKISHWE KWENYE MUAFAKA LAKINI CUF HAWAKUTAKA KUSIKIA KILIO CHETU KWA UROHO WAO WA MADARAKA, WALITAKA WAO TU WAPEWE NAFASI NA WALA SI VYAMA VINGINE.
TUNAYAPONGEZA MAAMUZI YA BUTIAMA KWAMBA NI KIHISTORIA NA YAMEJALI KILA MZANZIBARI BILA YA KUJALI NI CHAMA GANI.
WAZANZIBARI WENZANGU SASA TUKAE TUFIKIRIE JINSI YA KUTUMIA NAFASI HII YA KIDEMOKRASIA KUWA MUSTAKABALI WETU SISI WEMYEWE NA WALA SIO MAWAKALA WETU YAANI VYAMA VYA SIASA.
Nimesoma hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa Diamond na halafu nikafananisha na maelezo ya Maalim Seif, kwa kweli huenda CUF au Maalim Seif alipandwa na jazba. Tamko lake halioneshi hata chembe ukweli wa Kikwete.
ReplyDeleteNinamshauri Maalim asihamaki kwani yeye ndiyo CUF na ndiyo kila kitu, wengine wote wasindikizaji, akae chini afikirie kama alikuwa haja ni madaraka ya serikalini tu nadhani atakuwa anajishushia hadhi yake.
Mimi kwa maoni yangu ni kuwa maamuzi ya CCM ni sehemu tu ya maelekezo ya kawaida ya mazungumzo ya muafaka kwa wajumbe wake. Na kuhusu kuwashirikisha wazanzibari wote kuamua na kufikia muafaka na dhani CCM wamekubaliana na sera za CUF za HAKI SAWA KWA WOTE sasa tatizo liko wapi?
Mimi sio mwanasiasa lakini naomba kuuliza jamani mbona huyu SEIF na LIPUMBA wapo tuu tangu hiyo CAF sijui CUF ianze au hii inakuwaje kwani hakuna viongozi wengine?si ndio udikteta huu?na mkipewa nchi si ndo mnang'ang'ania kabisa.Kustaafu kumo wazee.
ReplyDeleteTUKO PAMOJA NA WEWE MAALIM SIF ,HEKO HEKO
ReplyDelete