mdau wa waja leo, waenda leo katuletea hizi kutufahamisha kwamba baadhi ya vituo vidogo vya polisi vimetelekezwa sehemu za kwaminchi (juu) na amboni. vituo hivi vilijengwa enzi za mh. augustino lyatonga mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani. huenda bila shaka aidha uhalifu umepungua ama umetokomea sehemu hizo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. huyo jamaa wa kwanza mwenye blue mikono mifupi anafanana na magonera yuko finland je ni yeye au, alikuwa musoma na alikuwa arusha,samahani wadau namtafuta sana,
    mdau USA,masai@jid.sio,us

    ReplyDelete
  2. VITUO VINGI VYA POLISI VILIVYOJENGWA WAKATI WA MHE. MREMA VILITELEKEZWA KWA AGIZO LA KISIASA, HII IKO KATIKA MIJI YOTE IKIWA NI PAMOJA NA DAR. BAADHI YA VITUO HIVYO HAVIPO TENA KANI VILIBOMOLEWA. HIZI NDIZO SIASA ZA TANZANIA HIVI SASA, SIASA ZA CHUKI BILA KUJALI MASLAHI YA WANANCHI.

    ReplyDelete
  3. NAOMBA HUYO ARIYETUMA PICHA ZA VITUO VYA PORISI AJISARIMISHE HARAKA SANA KWA RIJESHI RETU RA PORISI. NI MARUFUKU KUPIGA PICHA MAENEO YOTE YA JESHI RETU.

    ReplyDelete
  4. Mafisadi wamefanya vitelekezwe, vionekane havina umuhimu ili wajiuzie, kwa mtindo wa kuuza nyumba za serikali.

    ReplyDelete
  5. Huu mfano wa kutelekezwa hivi vituo na tukio la Kibiti wanafunzi walivyo choma mabweni ni baadhi tu ya mifano kuonyesha jinsi serikali na viongozi wake hawapendi kazi zao. Tuseme tu JUMLA ya wafanyakazi wa umma hawana moyo wa kuendeleza nchi yetu. Kwani wao wangesoma enzi zao bila kupewa chakula na serikali eti kwa madai serikali haina pesa wangefanyaje? Au enzi zao kungekuwa hakuna vituo vya usalama kwa uraia wangeisha vipi? Watoto wetu wanasoma katika mazingira magumu magumu sana. Shule hazina chakula, vitabu, walimu hawana moyo wa kufundisha, eti serikali haina pesa. Zamani nchi yetu ilikuwa masikin sana lakini chakula shuleni kilikuwa hakikosekani, japo ugali wa maharage lakini wanafunzi hawakulala njaa. Sasa iweje leo nchi ni tajiri na ina mabilioni ya shillingi serikali ishindwe kutma vyakula mashuleni? Eti serikali haina pesa? Pesa zinaenda wapi? Tufanyeje turudishe mioyo na hawa watu wamuogope Mungu? Tengenezeni mazingira ya wafanyakazi na wanaanchi wafurahi kuishi katika nchi yao jamani, tena kwa usalama na upenda, na AMANI. Punguze ufisadi, hauwezi kuisha kabisa, lakini puguzeni wajameni...

    ReplyDelete
  6. BASI HIVI VITUO BOMBA SAANA TU YAANI. UKIWA NA PAKETI YA SIGARA HUKAI NUSU SAA UKO URAIANI VINUMU HIVI VITUO JAMANI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...